Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Aisee! Mumsamehe jamaa, labda atakuja na maelezo kuhusu hili. Binafsi huwa sipendi to jump to conclusion. Tumsubiri kwanza aje huenda akawa na maelezo mazuri ya kujustify hii kitu.
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, Mara yangu ya kwanza kufika Beit Bridge, mpakani mwa Zimbabwe na South Africa, ilikuwa saa nane usiku. Ilikuwa safari ya siku tatu kutoka Dar hadi kufika hapo. Ndani ya bus tulikuwa tumechoka sana. Bus lilikuwa na raia wengi wa Zimbabwe na Zambia, Waburundi, Wakenya. Wabongo tulikuwa 4 tu. Wabongo tulipiga mastori kibao, kama watu tuliofahamiana miaka mingi, kumbe ndo ilikuwa mara yetu ya kwanza kukutana.

Tulijichanganya sana na Waburundi na Wakenya. Wazimbabwe hata lugha yao tulikuwa hatuelewi. Dah ilikuwa moment fulani tamu sana.

Pale border Mbongo mmoja hakuruhusiwa kuingia South Africa. Alikamatwa alitaka kutoa rushwa kwa Afisa wa Uhamiaji (Mkaburu) ili apewe miezi 3 ya kuishi kwa Madiba. Huyu mwenzetu aliyekamatwa yeye ilikuwa sio mara yake ya kwanza kuingia South Africa. Ujuaji mwingi ulimponza.

Sisi wengine tuligongewa muhuri wa mwezi 1 tu kuwepo kwa Madiba. Lakini tuliishi zaidi ya Miaka 6, Sio miezi 6, ni miaka 6. Harakati za mtu Mweusi bhana.

Nakumbuka Wabongo wote tulienda kufikia Pretoria kwa jamaa fulani. Kumbuka wote hapo hatujuani, halafu mfukoni nimebakiwa na kama Elfu 50 tu ya Kibongo.

Kati ya sisi tuliotoka Bongo, kuna mwenzetu mmoja anafamiana na huyo jamaa tuliyefikia kwake. Jamaa wa kuitwa Ibra, alitupokea vizuri sana.

Tulikutana na Wabongo kibao pale Pretoria, walituchukua maelezo, tulikutana mpaka na yule demu video queen wa Matonya, wimbo wa Vailet, demu South Africa bado wanamuita Vailet, bado mrembo sana.

Harakati za kuingia mtaani kusaka mishe ndo zikaanzia hapo.

Nilikaa pale ghetto kwa washkaji kama wiki mbili ivi, ndani ya hizi wiki mbili na jamaa zangu tulikuwa tunaenda sana Johannesburg. Mwenyeji wetu alikuwa na rafiki zake wengi huko. Johannesburg na Pretoria sio mbali sana, kwa daladala ni kama dakika 40 tu.

Basi bhana, katika kwenda kwenda Johannesburg siku mmoja kwenye daladala nikawa nimekaa na demu mmoja mkaliii, nikawa namsemesha semesha mara pap akanipa namba yake ya simu. Washkaji zangu wananichora tu.

Mademu wa South Africa wakitongozwa sio wagumu sana kama Dada zetu wa Sinza, siku ya pili demu akawa demu wangu, fasta tukaanza kupanga maisha. Ha ha ha ha

Demu anafanya kazi Bank FNB, pale Midrand njia kama unataka kuelekea Kalfonteen. Baada ya kama siku 4 toka tufahamiane na yule manzi tukaanza kupiga story za jinsi ndoa yetu itakavyokuwa. Jinsi atakavyokuja Bongo kukutana na ndugu zangu, alivyoleta tu stori zake za siku moja atakuja Bongo kukutana na ndugu zangu, mtu wa kwanza kumuwaza alikuwa Mama Riziki, Muuza Vitumbua, Jirani yetu Buza, atakavyoongea mtaa mzima.

Yaan mimi na yule demu ilikuwa ni full uongo uongo tu mpaka demu akajaa. Akaamini kabisa kama kweli mimi ntamuoa.

Zote hizo ni Harakati za Mtu mweusi katika kutafuta sehemu ya kuanzia. Mara siku akanipigia simu akaniambia kwa Kingereza 'Keagan nataka tuishi wote'

Dah

Wadau itaendelea na nyinyi kama mna mastory yenu wekeni hapa Harakati zenu tujifunze



Hii Stori inafanana na ile na haina Kanya wala Kinyesi

Bs tupu
 
Nakuhakikishia jamaa harudi tena, Mana story ya uongo balaa
Aisee! Mumsamehe jamaa, labda atakuja na maelezo kuhusu hili. Binafsi huwa sipendi to jump to conclusion. Tumsubiri kwanza aje huenda akawa na maelezo mazuri ya kujustify hii kitu.
 
Muulize yeye ameshawahi kuandika story yoyote hapa jukwaani??
Katulisha matango pori angalia link hiyo
[emoji1787][emoji38]
Fungua huo uzi hapo juu
[emoji56][emoji56][emoji56]
 
Aisee! Mumsamehe jamaa, labda atakuja na maelezo kuhusu hili. Binafsi huwa sipendi to jump to conclusion. Tumsubiri kwanza aje huenda akawa na maelezo mazuri ya kujustify hii kitu.
Anatufanya Watoto bhana anatunnywesha Chai huku anaringa.
 
Kamalizie hii simulizi yako
 
....
 
Huyu mleta uzi,kumbe muongo, inaonesha kweli amewahi kwenda lakini ukilinganisha story yake hiyo iliyofukunyuliwa na wadau, na hii ya sasa inaonesha wazi baadhi anatupanga si kweli kabisa.
 
Na ametuweza kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…