Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Ni kweli hii mbinu inasaidia na imewatoa wengi wanaume kwa wanawake. Maana kutoka hivi hivi shughuli pevu. Jamaa ni kama alishushwa na Mungu. Alinikubali na kunipenda na unyonge wangu wote. Akawakubali na watoto wangu. Mtu sina mbele wala nyuma naishi kwa watu na ni muhamiaji sina kitu. Jamaa bosi yuko vizuri financially bado akanichagua. Niliamini mwanaume akimpenda mwanamke hakuna kinachoweza kumzuia
Sahihi utapewa kila unachostahili
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Niliishi pale kwa jamaa kama Wiki mbili hivi, Story zao zote ni kuhusu Dawa tu. Aisee nilichoka. Nikasema hapa lazima nitoke. Sijajilipua kuja South kuja kuuza Dawa, Nikasema hata nyumbani wakisikia nimekamatwa kwa kesi ya dawa watanishangaa sana. Kama nimeweza kutoka Bongo mpaka South, Sasa nishindwe nini kutoka hapa kwa Washkaji kwenda sehemu nyengine.

Basi taratibu nilipanga kutafuta Marafiki wengine ambao sio wabongo. Niliona labda nikibadilisha watu nitasikia story nyengine tofauti na Madawa. Nikawa muda mwingi najichanganya na watu wengine. Ukiwa South halafu ukianza kufanya mambo tofauti na wengine lazima wabongo wenzio watachukia. Lakini nilijilipua tena kwa Mara ya pili. Liwalo na Liwe, wakichukia poa tu.

Niseme ukweli wakati natoka Bongo, Kichwani nilikuwa na Mipango miwili ya namna ya kupata Mchongo kwa urahisi. Mpango wa kwanza lilikuwa endapo nitachelewa kupata Mchongo basi niende nikajisalimishe kwenye Kanisa lolote. Ukweli nilipanga kwamba endapo nitakosa watu sahihi wa kunisaidia kufikia malengo yangu basi niwe mtu wa kwenda sana Kanisani ili kupata watu sahihi huko. Nilipanga kujisogeza kwa washua wale wa Makanisani. Nilijua washua wengi wenye Biashara zao Halali au Taasisi zao nitawapata huko.

Mpango wangu wa Pili ilikuwa kama nitachelewa kupata Mchongo basi nitafute Mrembo mwenye Kazi yake, nimpe mapenzi kama yote mpaka anipende na kunisaidia kupata Mchongo. Mjumbe hauwawi ndo yalikuwa mawazo yangu.

Nikaanza na hili la Kwanza la kutafuta Kanisa la Washua. Kumbuka Safari hii nilifanya Karibia na Sherehe za X-Mass na Mwaka Mpya, Nilifanya Karibia tarehe hizo Makusudi. Nilijua kwenye Mikesha ya Kanisani, Mkesha wa X-Mass na Mwaka Mpya lazima nitapata mtu wa kunisaidia. Basi tarehe zikasogea mpaka X-Mass ikafika. Niliwaaga wale jamaa zangu kuwa naenda kwenye Mkesha. Jamaa walinishangaa sana kwa sababu wao hawanaga mambo hayo. Tena siku niliyowaambia kuwa nakwenda kwenye Mkesha tulikuwa tumetoka wote kutembea Mitaa ya Midrand Gauteng. Midrand ipo Katikati ya Pretoria na Joberg. Ni kama dakika 20 kutoka Pretoria. Kuna Umbali kidogo sema wenzetu kwa kuwa Barabara zao nzuri ndo unatumia dakika hizi 20, Ingekuwa hapa kwetu ni umbali wa Kama kutoka Tegeta mpaka Magomeni.

Tukiwa huko Midrand ndo niliwaambia hivyo, Wakati wakuondoka wenyewe wakaondoka Mimi wakaniacha pale Midrand. Nikaanza kuzurura zangu Mitaani nauliza watu wapi nitapata Kanisa kubwa. Nilikuwa natafuta Kanisa ambalo ukiliona tu kwa nje unajua hili ni Kanisa la Washua. Sikutaka haya Makanisa Madogo Madogo.

Nilifanya yote haya ili kujiepusha na Biashara ya Dawa, ilibidi niangaike sana pale. Unajua Wabongo wengi wanajikuta wakiingia kwenye Biashara za Dawa kwa Mtindo kama huu, Yan ukifika ukakutana na Wabongo wenzio hawakupi nafasi ya kujipambania zaidi. Sasa kama wewe ni kichwa panzi basi unaishia kwenye biashara hiyo.

Mimi nilisema nitapambana mpaka dakika ya mwisho, swala la Kibali cha Kazi nitajua mbele kwa Mbele.

Basi nikafika mpaka pale Kanisani. Kuliona tu kwa nje nikajisemea hili ndo nilikuwa nalitafuta. Parking ilikuwa na Gari za Kifahari Kibao. Nikauliza Muda wa kuanza Ibada ya Mkesha wakaniambia kuwa ni saa moja usiku watu ndo wanaanza kuingia Kanisani. Washua Kibao walikuwa wamewahi pale, wamesimama kwa nje wakipiga story zao. Mimi nikasoma mazingira kisha nikatoka, nikazunguka zunguka pale Mitaani mpaka saa moja jioni ilivyofika nikarudi tena. Nikatimba zangu ndani.

Kama ilivyokawaida ya Makanisa mengi, mtu ukifika kwa Mara ya kwanza inabidi ujitambulishe. Tulisimama pale Kanisani kama wageni 50 hivi ndo ilikuwa Mara etu ya kwanza kufika pale. Baada ya kusimama na kujitambulisha kisha tulikaa. Wahudumu wa Kanisa wakawa wanapita kwenye kila Mstari kuchukua maelezo yetu. Nakumbuka kwangu alipita Msichana Mrembo hivi. Nilipomwambia kuwa Mimi ni Mtanzania na ndo nimefika south kwa Mara ya kwanza, alifurahi. Kwenye ile form yao nilijaza namba yangu ya simu. Wakuu kwa upande wa Lugha ya Kizungu siko vibaya sana. Naweza kujitetea kiasi chake.

Utaratibu mwengine wa lile Kanisa kwa mtu aliyefika Mara ya kwanza, wakati unajaza ile form yao wanakuuliza "Je kwenye hili Kanisa letu wewe utatusaidia upande upi?" Wakiwa na Maana Kama utaweza kujitolea mfano kufanya upande wa Media, Yan walikuwa wana Camera za kutosha mle ndani, Kanisa lilikuwa linaruka LIVE kwenye Mitandao ya Kijamii. Pia walikuwa wanataka kujua kama utajitolea kwenye upande wa Muziki sababu walikuwa na Kwaya yao na vyombo vyote vya Mziki. Kama wewe ulikuwa mtaalamu wa Maswala hayo ya Mziki basi utapangiwa huko.

Kwa hiyo ndani ya Kanisa Idara zilikuwa nyingi. Nikaona hapa nitumie fursa vizuri, Kwa kuwa Mimi nina taaluma Fulani ya Mambo ya Camera nikasema Mimi nitajitolea kwenye eneo hili. Yule Mrembo alifurahi kusikia hivyo. Akaniandikisha pale kisha akaondoka.

Ukweli Kanisa lilikuwa la Kishua na limechangamka sana. Kanisa lilikuwa na Gari la kwenda kuwachukua na kuwarudisha waumini wake.
Alleluiya Ministry International kwa Alph Lukau
 
Yani mtu lazima kujilipua. Kitendo cha kupata visa na watoto ulikuwa ni muujiza kwangu. Nikajisemea kama tumepata visa basi Mungu ana mpango mwema nami. Ila haikuwa rahisi mwanzoni. Mtu aliyenipokea alinipa wakati mgumu sana. Manyanyaso kama yote na kumbuka hapo nina watoto. Dah sitasahau. Nilikuja kukutana na mwanaume mwenye pesa yake ndefu akanipenda kufa maana nami ni mzuri si haba, akachanganyikiwa na penzi la mtoto wa kitanga
basi kata taratibu kii.. ray van mtu mzuri.
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Niliishi pale kwa jamaa kama Wiki mbili hivi, Story zao zote ni kuhusu Dawa tu. Aisee nilichoka. Nikasema hapa lazima nitoke. Sijajilipua kuja South kuja kuuza Dawa, Nikasema hata nyumbani wakisikia nimekamatwa kwa kesi ya dawa watanishangaa sana. Kama nimeweza kutoka Bongo mpaka South, Sasa nishindwe nini kutoka hapa kwa Washkaji kwenda sehemu nyengine.

Basi taratibu nilipanga kutafuta Marafiki wengine ambao sio wabongo. Niliona labda nikibadilisha watu nitasikia story nyengine tofauti na Madawa. Nikawa muda mwingi najichanganya na watu wengine. Ukiwa South halafu ukianza kufanya mambo tofauti na wengine lazima wabongo wenzio watachukia. Lakini nilijilipua tena kwa Mara ya pili. Liwalo na Liwe, wakichukia poa tu.

Niseme ukweli wakati natoka Bongo, Kichwani nilikuwa na Mipango miwili ya namna ya kupata Mchongo kwa urahisi. Mpango wa kwanza lilikuwa endapo nitachelewa kupata Mchongo basi niende nikajisalimishe kwenye Kanisa lolote. Ukweli nilipanga kwamba endapo nitakosa watu sahihi wa kunisaidia kufikia malengo yangu basi niwe mtu wa kwenda sana Kanisani ili kupata watu sahihi huko. Nilipanga kujisogeza kwa washua wale wa Makanisani. Nilijua washua wengi wenye Biashara zao Halali au Taasisi zao nitawapata huko.

Mpango wangu wa Pili ilikuwa kama nitachelewa kupata Mchongo basi nitafute Mrembo mwenye Kazi yake, nimpe mapenzi kama yote mpaka anipende na kunisaidia kupata Mchongo. Mjumbe hauwawi ndo yalikuwa mawazo yangu.

Nikaanza na hili la Kwanza la kutafuta Kanisa la Washua. Kumbuka Safari hii nilifanya Karibia na Sherehe za X-Mass na Mwaka Mpya, Nilifanya Karibia tarehe hizo Makusudi. Nilijua kwenye Mikesha ya Kanisani, Mkesha wa X-Mass na Mwaka Mpya lazima nitapata mtu wa kunisaidia. Basi tarehe zikasogea mpaka X-Mass ikafika. Niliwaaga wale jamaa zangu kuwa naenda kwenye Mkesha. Jamaa walinishangaa sana kwa sababu wao hawanaga mambo hayo. Tena siku niliyowaambia kuwa nakwenda kwenye Mkesha tulikuwa tumetoka wote kutembea Mitaa ya Midrand Gauteng. Midrand ipo Katikati ya Pretoria na Joberg. Ni kama dakika 20 kutoka Pretoria. Kuna Umbali kidogo sema wenzetu kwa kuwa Barabara zao nzuri ndo unatumia dakika hizi 20, Ingekuwa hapa kwetu ni umbali wa Kama kutoka Tegeta mpaka Magomeni.

Tukiwa huko Midrand ndo niliwaambia hivyo, Wakati wakuondoka wenyewe wakaondoka Mimi wakaniacha pale Midrand. Nikaanza kuzurura zangu Mitaani nauliza watu wapi nitapata Kanisa kubwa. Nilikuwa natafuta Kanisa ambalo ukiliona tu kwa nje unajua hili ni Kanisa la Washua. Sikutaka haya Makanisa Madogo Madogo.

Nilifanya yote haya ili kujiepusha na Biashara ya Dawa, ilibidi niangaike sana pale. Unajua Wabongo wengi wanajikuta wakiingia kwenye Biashara za Dawa kwa Mtindo kama huu, Yan ukifika ukakutana na Wabongo wenzio hawakupi nafasi ya kujipambania zaidi. Sasa kama wewe ni kichwa panzi basi unaishia kwenye biashara hiyo.

Mimi nilisema nitapambana mpaka dakika ya mwisho, swala la Kibali cha Kazi nitajua mbele kwa Mbele.

Basi nikafika mpaka pale Kanisani. Kuliona tu kwa nje nikajisemea hili ndo nilikuwa nalitafuta. Parking ilikuwa na Gari za Kifahari Kibao. Nikauliza Muda wa kuanza Ibada ya Mkesha wakaniambia kuwa ni saa moja usiku watu ndo wanaanza kuingia Kanisani. Washua Kibao walikuwa wamewahi pale, wamesimama kwa nje wakipiga story zao. Mimi nikasoma mazingira kisha nikatoka, nikazunguka zunguka pale Mitaani mpaka saa moja jioni ilivyofika nikarudi tena. Nikatimba zangu ndani.

Kama ilivyokawaida ya Makanisa mengi, mtu ukifika kwa Mara ya kwanza inabidi ujitambulishe. Tulisimama pale Kanisani kama wageni 50 hivi ndo ilikuwa Mara etu ya kwanza kufika pale. Baada ya kusimama na kujitambulisha kisha tulikaa. Wahudumu wa Kanisa wakawa wanapita kwenye kila Mstari kuchukua maelezo yetu. Nakumbuka kwangu alipita Msichana Mrembo hivi. Nilipomwambia kuwa Mimi ni Mtanzania na ndo nimefika south kwa Mara ya kwanza, alifurahi. Kwenye ile form yao nilijaza namba yangu ya simu. Wakuu kwa upande wa Lugha ya Kizungu siko vibaya sana. Naweza kujitetea kiasi chake.

Utaratibu mwengine wa lile Kanisa kwa mtu aliyefika Mara ya kwanza, wakati unajaza ile form yao wanakuuliza "Je kwenye hili Kanisa letu wewe utatusaidia upande upi?" Wakiwa na Maana Kama utaweza kujitolea mfano kufanya upande wa Media, Yan walikuwa wana Camera za kutosha mle ndani, Kanisa lilikuwa linaruka LIVE kwenye Mitandao ya Kijamii. Pia walikuwa wanataka kujua kama utajitolea kwenye upande wa Muziki sababu walikuwa na Kwaya yao na vyombo vyote vya Mziki. Kama wewe ulikuwa mtaalamu wa Maswala hayo ya Mziki basi utapangiwa huko.

Kwa hiyo ndani ya Kanisa Idara zilikuwa nyingi. Nikaona hapa nitumie fursa vizuri, Kwa kuwa Mimi nina taaluma Fulani ya Mambo ya Camera nikasema Mimi nitajitolea kwenye eneo hili. Yule Mrembo alifurahi kusikia hivyo. Akaniandikisha pale kisha akaondoka.

Ukweli Kanisa lilikuwa la Kishua na limechangamka sana. Kanisa lilikuwa na Gari la kwenda kuwachukua na kuwarudisha waumini wake.
Mkuu, endelea kutuwekea link za episodes pale juu kama ulivyofanya awali. Tunapata shida kutafuta muendelezo
 
Hao wanaigeria ujuaji wao unawacost kila sehemu hawakubaliki kutokana na tabia zao za kishenzi,utapeli,wizi etc
Kinachosababisha wakimbie kwao ni umasikini na kwa sasa nchi yao hali ya kisiasa sio nzuri muda wowote kitawaka
😂😂😂 Kwamba tz Ni tajiri ndo maana hamtoki kwa wingi km Nigeria, au mna mienendo poa sana🤔 ni Kama matajiri huku kitaa wanaitwa mafreemanson, ndo akili yako ilivyo na wewe,

Halafu si wanaigeria wote Ni matapeli, kubali tu wametuacha mbali katika kurisk kiutafutaji fursa za maisha
 
Yaaani na haya matatizo ya ajira ilitakiwa kila graduate akipewa cheti anapewa na gamba lake akiamua akafie mbele huko au aliweke chini ya godoro liliwe na panya

Na vijana wakizamia huko mbele wakirudishwa hapa(deported) hamna kuwafunga wala kesi wamwage mtaani waanze upya kutafuta chaka nyingine za kulowea

Sasa wao na mentality yao ya kikomunisti wanasema passport ni dokumenti ya kiusalama.....mawazo ya miaka ya 70 huko😂😂

Nakuhakikishia miaka 10 tu matokeo tungeyaona. Familia nyingi sana zingekua na msaada kwa diaspora sio kama saivi vijana wamebaki kuwa mzigo kwa familia

Bila "Conquering new frontiers" hatutoboi ng'o

Kina Livingstone, Speke,Stanley nk bila kuja kufanya upelelezi mpaka Ku(tu)gundua wala sio Mjeruman wala Muingereza angejua kuwa kuna watu bado washamba wanatakiwa kutawaliwa kuwa makoloni kwa manufaa yetu(wazungu)

Wale ni vijana walijilipua kuja sehem unknown to the world na waliua,walifanya kila aina ya unyama nqwengine walifia huku ila walileta mafanikio kwa mataifa yao.

Sio kujifungia tu huko kijijini Matombo toka umezaliwa mpaka unakufa kwa ajili ya uoga
Mkuu Nimecheka Lakini Nakufurahia Sana Comments zako... Kuna kitu unanijenga... Aisee na huu uzee Wangu Huku Kigoma Kasulu Ndani Ndani Huku Kijiji Cha Muyegera Nimetamani Sana Kujilipua. Hapa leo hi naelekea Uhamiaji kuangalia Utaratibu wa Gamba.... Asante Sana
 
Jozi, nilikuwa kwenye apartment kama siku ya pili toka nifike, natoka room kwenda kwenye vending machine iliyopo humo humo kwenye apartment kuchukua soda, nikawa niko kwenye simu naongea kiswahili, nikapishana na mdada mzuri hivi wa makamo kama 42 hivi yuko na msichana wa kazi na mtoto wa kike wana vifurushi wanaonekana wametoka shopping. Wakati narudi kwangu yule dada alikuwa bado amesimama ananisubiri nilivyotoka nilikuwa na pajama hivyo alijua kabisa siendi mbali. Akaniambia nimekusikia unaongea kiswahili wewe ni mtz au mkenya? Nikamjibu mTz, tukapiga piga stori hapo akafurahi sana, nikajua nimepata shost, Akanihoji hoji nikamwambia nimekuja tu kutembea, akaniambia yeye anaishi cape town, hapo amepita tu akitokea gaborone kwa mumewe, atakaa siku 4 then ataondoka. Nadhani alifurahi kupata mtu wa kuongea nae kiswahili siku hiyo maana appartment hiyo haikuwa na waswahili zaidi yetu, au kama ilikuwa nao sikupata kuwaona.

Basi, mi nilikaa kama miezi mitatu, nikawa namuona mara kwa mara basement kwenye parking na familia yake mi nikipanda zangu uber. Nikawa najiuliza huyu alisema atakaa siku nne sasa mbona haondoki? Nikajiongeza tu kuwa huyu anaishi hapa hapa, hakutaka tu kuniambia labda alihisi nitamzoea, au labda hakuniamini aliona sina ramani maana kiumri nilikuwa msichana mdogo bado tukawa tukionana tunasalimiana basi mpaka siku naondoka nilimuona jana yake jioni maana tulikuwa tunaishi floor moja, wing moja yeye apartment yake ilikuwa ya familia zile zina 3 bedrooms na vikorombwezi vingine, mimi yangu ilikuwa ndogo, Bedroom+sitting room, kitchen.
naomba namba yako plse
 
Back
Top Bottom