Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kuna siku nilileta uzi humu, kuhusu mchepuko mpya niliyekutana naye, na akaniomba nimuongezee mtaji ili aweze kujiajiri.
Kutokana na mtaji alio uomba ulikuwa mkubwa kiasi fulani; sikuwa mwepesi kutimiza mpaka pale baadhi ya vitu niweze kujiridhisha.
Kwanza nilimualika aje kwangu(kubadilishana joto), na tukakubaliana atafanya hivyo; lakini matokeo yake siku ya tukio hakuweza kufika, na kunijulisha amepata mwaliko kutoka kwa rafiki yake anayefanya naye kazi, na kunitaka mi niongozane nao.
Pili, alinijulisha anachangamoto ya macho na alishafanyiwa upasuaji; hivi karibuni na anatakiwa kurejea hospitali na alikuwa anahitaji nimuwezeshe fedha, kama laki 5.
Tatu, anataka nimuamishe mkoa aliopo na aende kwenye mkoa anaotaka kufanya biashara; akiwa na maana ya usafiri wa mizigo, kulipia kodi huko anakoenda n.k
Nne, natakiwa kumjali kwa kila kitu katika mahitaji yake ili asiweze/asishawishike kuchepuka.
Baada ya kutafakari kwa kina, nikaona hii ni barabara ya vumbi tena yenye makorongo mazito; nikaona hapa natafuta umasikini kwa kulazimisha.
Kwa kifupi, nimepiga chini.