1. Nimezunguka majimbo karibu yote Tanganyika naangalia umati uliokuwa nyuma yangu. Watawapigia kura CCM? / watakwenda kupiga kura
2. Wafuasi wa madhehebu mbali mbali watawapigia kura CCM? watakwenda kupiga kura?
3. Wapenda haki watawapigia kura CCM?/ watakwenda kupiga kura?
4. Mwachieni Lisu
5. Necessary reforms lazima ziwepo ili chadema ishiriki
TAKEHOME MESSAGE
Kama hayo hayakufanyika anawataka watu kuwa MSIENDE KUPIGA KURA AMBAO WAKO NYUMA YANGU , WAKRISTO WOTE, WAPENA HAKI, WAFUASI WA LISU/CHADEMA.
FINALLY ANATUTAKA: TUSIENDE KUPIGA KURA
Mimi kwa upande wangu naamini kuwa uchaguzi huu umetugawa Watanzani si kwa itikadi za kisiasa tu bali hata dini. Najua kwa mtazamo huu watu wataamaki na wengine ambao unafiki is their cup of coffee watabisha na kukejeli, but ukweli ndio huo. Ni hivi, kuwa watanzania wanaamini rais samia anasakamwa sababu ni muislam, kwamba mbona mambo haya haya yanayotokea yalifanyika kipindi cha Jiwe na kanisa/wakristo hawakupiga kelele? Pia sasa kuna wanaosema wenzetu wako kimya sababu rais anatokea upande wao. Hii yote ina thibitisha kuwa nchini kwetu tayari dini zetu zimeanza kuwa mhimiri wa maamuzi yetu kwenye kupata viongozi.
Mimi binafsi sikubali kama kipindi cha Jiwe kanisa lilikuwa kimya maana nakumbuka serikali na Makonda walivyoangaika na kupambana na waraka wa pasaka wa kanisa katoliki, na kufikia hatua ya kumtumia Malasusa (KKKT) kuzuia waraka wa KKKT usisambazwe na kusomwa makanisani, so hapa inathibitisha kanisa halikukaa kimya.
Udini wa nchi hii uko hivi, kwa waislam rais akiwa wa upande wao hawatakia aguswe, atatetewa kila kona tena hata kwa mambo yasio thibitika, kama ile ya kusema mfumo wa elimu unabagua, ajira seriakalini n.k. Na bahati mbaya huwezi kuwasikia wakikemea mauaji, utekaji au dhulma yeyote hata akifanyiwa mwislamu mwenzao ili tu wasimtie doa rais.
Ukifuatilia hali ilivyo sasa na kinachoendela unaona kabisa mnyororo wa watu na makundi yaliyo nyuma ya utawala huu , kisiasa na kiuchumi. Nchi hii 90% ya matajiri (big businesses billionaires) ni Muslims na hawa wote wako behind samia, ofcourse matasema ,ooh hao wanaenda huko for protection, sawa, lakini je kwa Jiwe hawakuhitaji protection? Lakini pia suala la utajiri wa nchi hii kuhodhiwa na kundi moja hata Mzee Mengi enzi za rais Mwinyi aliwahi kulalamiakia.
Anyway ,hoja yangu ni hii, Wakristo mjitafakari na kujiuliza ,je uchaguzi wa mwaka huu unawahusu?