Nilivyonasa kwenye lift jengo la Kitega uchumi kwa masaa 2 bila msaada. Ingekuwa Ulaya au Marekani ningefungua kesi ya kudai fidia

Nilivyonasa kwenye lift jengo la Kitega uchumi kwa masaa 2 bila msaada. Ingekuwa Ulaya au Marekani ningefungua kesi ya kudai fidia

Mwaka 2001 nilitoka zangu Temeke studio za Soundcrafters kwa Enrico kuchukua single yangu niipeleke Clouds.

nikapitia IFM kwa mpenzi wangu wa kipindi hicho tukapata dinner,ilikuwa mishale ya saa mbili usiku,marehenu Steve B alinipa maagizo kuwa hiyo CD niiache kwa dada flani nadhani ilikuwa floor ya 7,la haulaaaa,kufika floor ys tatu lift ikazima,niko mwenyewe tu,niliyepanda nae alishuka floor ya pili.

Nilijaribu kuiachanisha kwa mikono wapi, nikajaribu kupiga mlango wapi,simu yangu siemens 25 imeshaisha chaji sina ujanja,nikaanza kupiga kekeke wapi,nikabonyeza kengele ya dharura wapi sipati msaada,nikaamua kukaa chini kusubiri muujiza,hapo Oxygen inazidi kuisha,kijasho kinanitoka,nikavua shati nikajaribu tena kupanua mlango nikafanikiwa kwa kiasi cha kupitisha kiganja tu,nikavua kiatu changu na kukiweka jatikati ya milangi ilihewa iingie huku nikisikilizia kama kuna mtu atapita au kushuka hiyo floor,

Mungu si athumani nikasikia mlango wa lift jirani unafunguka ndio nikapiga kelele ya kuomba msaada,yule mshangazi sijui alifanyaje nikaona wanakuja technician na kufungua mlango.

Ile CD nilisahau mulemule Kwenye lift nikarudi zangu nyumbani hapo ni saa nne usiku.Niko tumbo wazi mpaka maeneo ya Steers ndio nikakumbuka kulivaa

Baadae nikafuatilia kopi ya ile single yangu studio,nikaipeleka tena Clouds safari hii kwa tahadhari zote, ule wimbo ulipigwa mara moja tu nikajua nyota njema huonekana asubuhi.

Ingekuwa nchi za watu OTIS watengenezaji wa lift wangenilipa mamilioni
Hebu tupia hayo mavesi hapa tusikoe mistari na biti!, Enrico bado anarekodi muziki?...walikuwa wanawanyanyasa sana madogo na vistudio vyao mshenzi.
 
It was tough ,mwanajeshi wangu .Bado una sababu ya kuishi.Pambania kombe sasa ili iwe simu moja tu ikiita askari wako unatuambia tukutane benki.
 
Kumbe lile jengo la kitambo, juzi nilipita pale nilienda floor ya 13 ile lift yao ikifika unakoenda kuna mtikisiko fulani hivi.
Sasa 2001 unasema kitambo?nahisi ni la miaaka ya l 70s huko
Mi nimekua nimelikuta.Kuna kipindi ndio lilikuwa hengo refu kuliko yote nchini,baadae likaja PPF tower,baadae lijaja la NSSF,,BoT nk
 
Mzee mdukuzi pole sana. Umenikumbusha hiyo mitaa wakati niko chuo nilikuwa field attachment wizara ya fedha. Mimi nilikuwa na trip za nyingi za Sukari house - wizarani... pembeni ya steers kulikuwa na mama ntilie aliyekuwa anauza mno kuanzia asbh hadi mchana. Kimsingi hiyo mitaa nina kumbukumbu nayo muhimu.
 
Pole sana Mkurugenzi.... Lift hizi Huwa zinaogopesha sana.... Nikiingiaga Huwa nawaza mara mbilimbili....

Kingine Huwa nawaza, vipi ikiporomoka downward! Yaani ifyatuke kushuka chini.... Lahaulaaa....
 
Pole sana Mkurugenzi.... Lift hizi Huwa zinaogopesha sana.... Nikiingiaga Huwa nawaza mara mbilimbili....

Kingine Huwa nawaza, vipi ikiporomoka downward! Yaani ifyatuke kushuka chini.... Lahaulaaa....

Wazungu sio wajinga, unachowaza wao walishawaza siku nyingi...hata ikatike hiyo free fall haipo inagota hapo hapo!
 
Back
Top Bottom