Nilivyonasa kwenye lift jengo la Kitega uchumi kwa masaa 2 bila msaada. Ingekuwa Ulaya au Marekani ningefungua kesi ya kudai fidia

Nilivyonasa kwenye lift jengo la Kitega uchumi kwa masaa 2 bila msaada. Ingekuwa Ulaya au Marekani ningefungua kesi ya kudai fidia

Amina, namshukuru Mungu sijawahi kufanya kosa hata la traffic offense
Jela mbaya aisee
Ningekuwa badala yako kwenye lift siku hiyo ningekufa maana ina kupa woga sana na kutapatapa
Ila hata home lazima dirisha moja liwe wazi hata kama kuna barafu na ni -5 nje
Ukiwa stranded inatakiwa ujilazimishe kurelax la sivyo ukiendelea kupanic,presha inakukamata
 
2001 cd 💿? Si zilikuwa zinatumika kanda au? Nilikuwa mdogo sana kipndi hicho !

Kwa hio wewe ni msanii ? Au uliachana na sanaa
Studio zilikuwa zinatumika CD, mitaani zilikuwepo ila siyo nyingi sana kama 2003 hadi 2010.
Mitaani zilianza kuzagaa home music system (radio) za Sony 5 au 3 Disc Changer toka miaka ya 1995 huko.
 
IKawaje mkuu
Mkuu ilikuwa ni bad experience sijapata ona, ilifika kama nusu saa hivi nikawa nimekata tamaa kbs nasubiria kifo kwa ukosefu wa oxygen, nilifanya kila linalowezekana ikashindikana ikiwemo kujaribu kutumia nguvu kuachanisha mlango lkn wapi, kengele haitoki, nimepiga kelele lkn wp! nikampigia workmate mmoja ofisi ya jirani akachukulia masihara hakuzingatia...ilikuwa kama nimefungiwa kwenye kichupa. Gafla umeme ukarudi ndo pona yangu.
 
Kiutaratibu nikwamba hizi lift zinatakiwa kufanyiwa service kila baada ya wiki na wataalam.

Sasa managers wa mahotel na wamiliki wa majengo huona kama wanapoteza hela kulipia ukaguz na urekebishwaj wa hizo lift ndo mana ishu kama hiz zinajitokeza.

Binafsi nikipanda lift kabla sijabofya kitufe cha destination naangalia last service ya lift ni lini. Nikiona inamda mrefu haijapigwa service hapo natumia ngaz.
 
Ukiwa stranded inatakiwa ujilazimishe kurelax la sivyo ukiendelea kupanic,presha inakukamata
Huwa najitahidi sana kutokuwaza na ku relax ila unajikuta Una panic na unaona kabisa pumzi ya mwisho inakatika
Ni mtihani ninaoishi nao
Nikiwa safari aidha private car ambayo nina uhuru wa kufungua dirisha na kama public transport napanda train first au second na angani natumia pia ila mabasi hapana kwa huko
Ni vigumu kuzuga na kujifanya uko poa
 
Hapo paragraph ya mwisho ni vipi mkuu nyimbo ilipopigwa ilitoboa au ndio ilibuma ikawa nyota ya punda!? 😂
 
Hapo paragraph ya mwisho ni vipi mkuu nyimbo ilipopigwa ilitoboa au ndio ilibuma ikawa nyota ya punda!? 😂
 
Back
Top Bottom