Nilivyonasa kwenye lift jengo la Kitega uchumi kwa masaa 2 bila msaada. Ingekuwa Ulaya au Marekani ningefungua kesi ya kudai fidia

Hebu tupia hayo mavesi hapa tusikoe mistari na biti!, Enrico bado anarekodi muziki?...walikuwa wanawanyanyasa sana madogo na vistudio vyao mshenzi.
 
It was tough ,mwanajeshi wangu .Bado una sababu ya kuishi.Pambania kombe sasa ili iwe simu moja tu ikiita askari wako unatuambia tukutane benki.
 
Kumbe lile jengo la kitambo, juzi nilipita pale nilienda floor ya 13 ile lift yao ikifika unakoenda kuna mtikisiko fulani hivi.
Sasa 2001 unasema kitambo?nahisi ni la miaaka ya l 70s huko
Mi nimekua nimelikuta.Kuna kipindi ndio lilikuwa hengo refu kuliko yote nchini,baadae likaja PPF tower,baadae lijaja la NSSF,,BoT nk
 
Mzee mdukuzi pole sana. Umenikumbusha hiyo mitaa wakati niko chuo nilikuwa field attachment wizara ya fedha. Mimi nilikuwa na trip za nyingi za Sukari house - wizarani... pembeni ya steers kulikuwa na mama ntilie aliyekuwa anauza mno kuanzia asbh hadi mchana. Kimsingi hiyo mitaa nina kumbukumbu nayo muhimu.
 
Pole sana Mkurugenzi.... Lift hizi Huwa zinaogopesha sana.... Nikiingiaga Huwa nawaza mara mbilimbili....

Kingine Huwa nawaza, vipi ikiporomoka downward! Yaani ifyatuke kushuka chini.... Lahaulaaa....
 
Pole sana Mkurugenzi.... Lift hizi Huwa zinaogopesha sana.... Nikiingiaga Huwa nawaza mara mbilimbili....

Kingine Huwa nawaza, vipi ikiporomoka downward! Yaani ifyatuke kushuka chini.... Lahaulaaa....

Wazungu sio wajinga, unachowaza wao walishawaza siku nyingi...hata ikatike hiyo free fall haipo inagota hapo hapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…