Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 3.
Baada ya ile gari kumalizika kuoshwa tuliondoka kuipeleka nyumbani kwa yule tajiri wa ile gari aliyekuwa akikaa mitaa ya Magamaga!..Sasa baada ya kuondoka pale kwa tajiri,Mtatiro akaniambia tuingie gengeni tukapate msosi halafu anipeleke gheto nikapige mbonji na yeye aelekee kulala kwa demu wake.
Basi bana asubuhi kama kawaida akawa amekuja mida ya saa 12 akanigongea nikaamka!.
Mtatiro "Vipi mwanangu nikuache ulale au tusepe zetu?"
Mimi "Ngoja ninawe uso tuondoke mwanangu"
Sikutaka kabisa kulala kwasababu jamaa angeniona mzembe.
Baada ya kujipaka mafuta tuliondoka na Mtatiro akawa ameelekea kwa bosi wake kuchukua ile gari ili ampelekee dereva ambaye angemkuta pale stendi!.
Mtatiro "Ngoja twende kuna jamaa yangu ana kipanya kina piga ruti ya Sirari"
Aliendelea "Siunaweza kukomaa mwanangu?"
Mimi "Nitakomaa mwanangu wala usijali"
Mtatiro "Dingi yako nilikuwa namuona ni mjanja kumbe ana mambo ya kinoko hivyo!"
Sasa mtatiro yeye alichoamini ni kwamba mzee wangu ndiye mzinguaji bila kufahamu yote hayo msababishaji ni mimi.Sikutaka kabisa kumweleza mambo mengi ya nyumbani,nilichomwambia ni kwamba mzee kanitimua nyumbani niende nikajitegemee!.Baada ya kufika pale stendi akamkabidhi dereva gari kisha akamuomba simu ili ampigie yule jamaa yake mwenye kimchomoko aweze kuzungumza nae!.
Walipozungumza na huyo jamaa,jamaa alimwambia niende nitamkuta kwenye njia ya Nyamwaga Road amepaki na akawa amemuelekeza namba za gari!.Nilitembea kwa haraka ili nimuwahi jamaa.
Nilifanikiwa kumkuta jamaa na tukasalimiana!.
Jamaa "Mambo vp?"
Mimi "poa kaka"
Jamaa "Sasa tutaondoka nitakuacha pale sirari,wewe utahakikisha unakuwa unanitafutia abiria wa kuja nao Tarime halafu nitakuwa nakupa posho!"
Mimi "sawa kaka"
Jamaa "Lakini si utaweza?,maana hii kazi siyo lele mama"
Mimi "Nitaweza kaka wala usijali"
Jamaa "Ningekuweka hapa Town sema kuna wakuda fulani watakusumbua pale kijiweni"
Sikuwahi kabisa kufanya kazi za kwenye magari lakini sikuwa na namna ilibidi nipambane kama mwanaume ili nipate pesa!,nilitaka na mimi niwe kama Mtatiro aliyekuwa mchangamfu na mcheshi asiyejali kitu!.Yule jamaa alikuwa akimiliki gari aina ya Pro box(Kimchomoko) na alitaka mimi nikawe mpiga debe wa kumtafutia abiria upande wa sirari!.
Jamaa "Ingia twende zetu"
Basi tuliondoka yale maeneo niliyomkuta na kuelekea kwenye stendi za zile gari za kuelekea sirari,baada ya kufika pale nilitelemka nikakaa pembeni kuangalia wahuni walivyokuwa wakigombania abiria kuwapeleka kwenye magari waliyokuwa wakiyapigia debe!.
Baada ya zamu yetu ya kupakia kufika,kuna jamaa wakaanza kuitia abiria mpaka gari ikajaa!.Gari ilipojaa jamaa akaniambia niingie nyuma ya buti ambapo pia kulikuwa na abiria wengine wawili ili twende akaniache sirari niianze kazi yangu ya kupiga rasmi!.
Tulipofika pale sirari nikashuka na nikaanza kuchangamka maana nilitelemsha mizigo ya abiria kwenye kile kigari,nilianza kuita abiria kwa kuchangamka lakini nikaja kugundua haikuwa kazi rahisi hata kidogo!.Lile eneo kiukweli niliwakuta baadhi ya wapiga debe ambao kila mtu alikuwa na gari zake alizokuwa akiitia abiria!.
Namshukuru Mungu abiria wakajaa kwenye gari na jamaa akaondoka mimi nikabaki!Sasa kwakuwa mimi na wale jamaa kazi yetu ilikuwa moja,tulianza kupiga stori za hapa na pale!.Kuna jamaa mmoja ambaye nilikuwa nasikia wenzie wakimuita pengo na sikufahamu kama ndilo lilikuwa jina lake au ulikuwa ni utani tu!,alikuja tukawa tunazungumza!.
Pengo "Mwanangu Keraryo ni bosi wako?"
Mimi "Keraryo ndiyo nani?"
Pengo "Huyo jamaa uliyemuitia abiria!"
Mimi "Yule ni brother tu"
Pengo "Sikia mwanangu,angalia jamaa asije akakudhurumu posho yako"
Aliendelea "Jamaa wamemkataa watu kibao hapa kijiweni kwasababu hatoi posho!,unamuitia abiria akiondoka ndo imetoka!,na ndiyo maana unaona gari yake ikifika wahuni hawana habari nayo"
Mimi "Hakuna tatizo mwanangu yule ni brother"
Pengo "Sawa mwanangu kama ni brother wako haina noma"
Basi sikutaka maneno mengi sana kwakuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuifanya ile kazi!.
Sasa ilipofika jioni baada ya kujaza tena ile gari,jamaa alinikabidhi posho ya siku ambayo ilikuwa buku 3,kiukweli nilikata tamaa sana baada ya jamaa kunipatia ile hela lakini sikutaka kumwambia,niliamua kujikaza kisabuni kama mwanaume!.Kumbuka tangia asubuhi nilikuwa sijaweka kitu chochote tumboni.
Baada ya jamaa kunipatia ile posho akaniambia niingie kwenye gari turudi Tarime mjini maana sasa ilikuwa giza!,nilipofika mjini nilielekea kwa mama ntilie kupata msosi kisha niliondoka kuelekea kwenye geto la Mtatiro ambaye nilikuta amefunga,nilikaa nje kumsubiri na ilipofika mida ya usiku wa saa 4 jamaa alirudi akiwa na mwanamke!.
Mtatiro "Mwanangu umefika muda mrefu?"
Mimi "nimefika mida ya saa 1"
Mtatiro "Nilienda kwa shemeji yako"
Baada ya kuzungumza,jamaa alifungua gheto akawa ameingia yeye na demu wake,sasa kiukweli niliwaza sana ni wapi nitakwenda kulala maana jamaa alikuwa na demu wake.Sasa nadhani baada ya jamaa kuona nina mawazo aliniambia nisiwaze kwani tungelala wote mle ndani.
Basi bana,jamaa alitandika chini mifuko ambayo juu yake akaweka nguo akanitaka niegeshe ile kibishi ilimradi kupambazuke tukaendelee na mitikasi ya utafutaji!.
Ule usiku kwakweli kwa upande wangu ulikuwa usiku mbaya sana kwasababu jamaa alianza kutafuna papuchi ya yule demu wake bila huruma,hakujali kabisa na wala hakuona aibu!,kibaya zaidi yule demu wake nae akawa analia kilio kisicho cha machozi huku mwanaume mimi nikiendelea kujigeuza kila sekunde kana kwamba nimepakwa upupu!.Niliapa kabisa ya kwamba,nisingethubutu kabisa kulala kwenye geto la mshikaji kama hizo ndizo zilikuwa habari zenyewe!.
Namshukuru Mungu asubuhi kulikucha na sisi tukaondoka zetu huku demu wa jamaa akiwa bado amelala!.
Baada ya kumaliza kazi ile jioni,sikutaka kabisa kurudi Tarime mjini na nilimwambia jamaa kesho angenikuta hapo Sirari nikimsubiri!.Usiku ule niliamua kutafuta guest ya bei nafuu iliyokuwa hapo maeneo ya jirani nikawa nimelipa elfu 5 nikawa nimelala.Baada ya kufanya ile kazi ndani ya wiki moja huku nikiendelea kukaa hapo Sirari,nilipata marafiki ambao pia walinifundisha namna ya kufanya kazi zaidi,badala ya kutegemea gari ya brother Keraryo pekee,nikawa naitia abiria na gari za mabosi wengine kisha napata posho,kiukweli nilianza kuchangamka na kuizoea ile kazi,kwa siku nilikuwa sikosi elfu 15 mpaka 20 mfukoni,hiyo ilikuwa ni posho tu!.
Nilipokusanya pesa ya kutosha,ndani ya mwezi huo nilitafuta chumba cha elfu 15000 nikapanga!.
Sasa kwakuwa sikuwa na hela ya kununua godoro,nilienda kwenye duka nikanunua maboksi ya kutosha kutandika chini ili nikilala nisije nikaumia mbavu!.