Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 21.

Gari ilitembea tukaikamata njia ya Sirari,sasa tukawa kama tunaelekea Musoma.Yule jamaa akamwambia yule demu aliyekua akiendesha gari ya kwamba inapaswa tuweke kituo kwanza Lamadi tukapate msosi kisha ndiyo tuondoke.

Baada ya kufika lamadi na kupata Msosi tuliondoka kuelekea Bariadi,sikuwahi kufika bariadi ni hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika huko,sasa baada ya kuiacha bariadi tulianza kuingia vijijini huko ndani ndani ambako sikuvifahamu kwa haraka maana sikuwa mwenyeji huko.

Kituo chetu cha mwisho kilikuwa kwenye kijiji cha Mwanaungu ambako baada ya kushushwa hapo,yule jamaa alimwambia yule demu kwamba amsubiri kwanza atupeleke halafu waondoke!.

Mtatiro "Mwanangu kwahiyo mnatuacha?"

Jamaa "Tutarudi kuwachukua ondoa shaka!"

Tulitembea kwa umbali mrefu kidogo hatimaye tukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa umezungushiwa minyaa ya kutosha,baada ya kufika hapo tulikuta kuna vijumba vingi vya nyasi huku kukiwa na watu ambao wengine walikuwa wamelala kwenye majamvi huku wengine wakiendelea na shughuli zao!.Kuna mwanamke akaja kutupokea kwa salamu ya kisukuma huku akipiga magoti,sasa mimi kwakuwa nilikaa usukumani kwa kipindi fulani wakati baba yangu mdogo akiwa headmaster,ile salamu haikunipa taabu kabisa!,na siyo salamu tu,naweza kukizungumza kisukuma ingawaje cha kuombea maji!.

Baada ya ile salamu yule mwanamke alituletea viti ambavyo havikuwa na watu kwa wakati huo.Basi baada ya muda mfupi yule mwanamke akaja na daftari akatutaka kila mmoja wetu kutaja jina lake na kuandikwa,sasa tulipoandikwa akatuchania vikaratasi vikiwa na namba,mimi nilipewa namba 16 na Mtatiro akapewa namba 17,yule jamaa yeye akamwambia yule mwanamke kwamba anahitaji kuonana na Mwami(Ng'wana Mwami).Yule mwanamke akamtaka asubiri kwanza.

Baada ya muda yule mwanamke akaja akamuita yule jamaa akampeleka mpaka kwenye kinyumba cha nyasi kilichokuwa kikubwa kati ya vile vinyumba tulivyovikuta pale.Baada ya muda yule jamaa akatoka akaja akatuambia angerudi baada ya siku mbili,hatukujua alipoingia mle ndani alienda kuzungumza kitu gani na huyo aliyekuwa humo ndani!.Jamaa aliondoka akatuacha pale,hiyo ilikuwa mida ya mchana saa 7.

Ilipofika mida ya saa 10,kuna mwanamke alitoka kwenye kile kijumba huku akijinyoosha kana kwamba alikuwa amechoka sana!.Alianza kuwazungukiwa watu kadhaa waliokuwa pale nje huku akiongea nao kisukuma na kiswahili!.Alipofika kwetu alitusalimia kisukuma na kama kawaida nami nilimuitikia kisukuma,sasa Mtatiro halikuwa haelewi kabisa hata salamu ndipo nilimwambia yule mama ya kwamba mwenzangu haelewi kisukuma,aliamua kumsalimu kiswahili kisha akaendelea na watu wengine!.Yule mama ndiye aliyekuwa mwenyeji wetu na alikuwa mganga!.

Mtatiro "Mwanangu kisukuma kumbe unakipiga fresh"

Mimi "Nimekaa nao,dingi yangu mdogo alikuwa headmaster shule moja huko Tabora hivyo nilikinyaka kiasi fulani"

Ilipofika mida ya saa 12 jioni kuna watu takribani 7 ambao walikuwa wanaume 3 na wanawake 4 waliingia pale nyumbani huku wakiwa wamebeba majembe,mimi nilidhani ni ndugu tu wanaoishi hapo kumbe walikuwa wateja wa huyo mama.Sasa utaratibu ulikuwa ni kwamba,unapofika kwa huyo mama unapewa namba kama sisi tulivyopewa,wakati ukiendelea kusubiri ili namba yako iitwe ilipaswa kila kunapokucha ukamate jembe umfuate mwenyeji akakuelekeze shamba la kulima na ulikuwa unapewa kipande chako ili upambane nacho,na kipande chenyewe hakikuwa cha kitoto,yaani kama ukimaliza kile kipande ndipo unaambiwa sasa umekolifai kupatiwa matibabu na yule mama.Sasa wakati unasubiri matibabu ndipo mnaitwa kwa namba ambazo hata sisi tulipewa.(Yule mganga alikuwa mjanja sana,badala ya kulima mashamba yake,sisi wapumbavu ambao tulifahamika kama wateja wake ndio tuliomlimia wakati yeye akiwa ametulia nyumbani,Daaah![emoji23][emoji23],na kila mtu aliyefika hapo kwake ni lazima ilikuwa akamatishwe jembe aingie shambani![emoji23][emoji23]).

Mimi na Matatiro tulikomaa na vipande vyetu ambavyo tulivianza siku iliyofuata kwasababu siku tuliyofika tulikuwa tumechelewa,bahati nzuri ilikuwa ni palizi na hakukuwa na nyasi sana!.Siku hiyo tulipomaliza kupalilia lile shamba ilikuwa mida ya saa 9 alasiri,tuliporudi hapo nyumbani kiukweli tulikuwa tumechafuka miguu na kunuka majasho hatari,sasa nilimfuata yule mama aliyetupokea siku ile nikawa nimemwambia atupatie maji ili tuoge,alituambia inapaswa tuwasubiri wenzetu ambao nao walikuwa hawajamaliza sehemu zao ili tupate chakula kwa pamoja kisha ndio tuoge!.

Wale walipotoka huko shambani,tulitengewa ugali wa udaga kwa na furu wa kuchemsha.Sasa tulipaswa kukaa watu watatu watatu kwa ajili ya chakula,mimi nilikaa na Mtatiro kama kawaida pamoja na jamaa mmoja ambaye alikuwa mteja kama sisi!.Siku hiyo ikapita kapa bila kuitwa namba lakini kuna watu wao waliitwa wakaendelea kupewa huduma kama kawaida!.

Siku iliyofuata tukaitwa majina watu kama wanne,sasa kwakuwa mimi na Mtatiro tulikuwa na shida moja ilibidi tuambiwe tusubiri kwanza amalizane na wale wa wawili.Zamu yetu ilifika na tukaitwa ndani kwa yule mama,hatukujieleza hata kidogo bali tulipoingia ndani alitutaka tuvue shati ili kitendo cha kupigwa chale kuchukue nafasi!.

Yule mama alitupiga chale kwa kutumia kisu kilichokuwa kikali kama wembe,alituchanja kila sehemu aliyoona yeye inafaa,baada ya hapo alituchanja pia kwenye ulimi kila mtu!.Alipomaliza kutuchanja na kutupaka dawa,alichukua kitu kilichokuwa kimefungwa na kukazwa sana na kutakiwa kila mmoja akivae kiunoni,ile alituambia ni irizi na asije akatokea mtu akaivua,alisema endapo ikitokea ukaivua basi usije ukamlaumu!.

Mpaka wakati huo hatukufahamu kwa huyo mganga tulipelekwa kufanya nini,ingawa tuliambiwa tunakwenda kutengenezwa ili hatukujua utengenezwaji ulikuwa na faida gani katika ile kazi yetu mpya ambayo tungeianza siku chache zilizokuwa mbele yetu!.

Yule mama alituambia ya kwamba,ile irizi haikupaswa kabisa kutolewa kiunoni hata iweje. Basi baada ya kumaliza ile shughuli tulitoka nje tukaendelea kumsubiri jamaa aliyetuambia angekuja kutuchukua!.Ile siku jamaa hakutokea kabisa,hivyo ikatubidi tulale tena kwa yule mama.

Yale mazingira yalikuwa ya hovyo sana lakini ilibidi tukubaliane na hali kwasababu tuliitamani pesa!.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi ya siku iliyofuata yule jamaa alirudi kutuchukua na kisha tukaondoka,sasa tulipoingia kwenye ile Noah tulikuta kuna mabegi kadhaa na kulikuwa na jamaa mmoja akiwa amekaa siti za abiria,dereva alikuwa ni yuleyule demu ambaye alikuwaga azungumzi na mtu!.

Jamaa "Wanangu safari ni moja kwa moja Arusha"

Mtatiro "Kaka mngeturudisha kwanza tukachukue nguo"

Jamaa "Nguo sio sehemu ya kuwazia,utazikuta huko"

Hatukuwa na swali,tuliamua kukausha na safari kuanza.Tulitembea sana na hatimaye tukaikamata lami kuelekea Musoma,baada ya kuivuka lamadi kwa mbele,tukaikamata geti la Ndabaka linaloingia Serengeti.
We jamaa hujipendi kabisa 😎
 
Jamaa inaonesha ndo wale watu ambao maisha yao yapo straight yani mtu kasomeshwa shule ya msingi nzuri ,secondary nzuri kafaulu vizuri alilishwa vizuri na wazee ametafutiwa kazi nzuri ila kuna watu wanaraha sana haya maisha kila kitu wamefanyiwa kmmk [emoji16].

Sasa ndo unawakuta wanabisha tu kila kitu wakiambiwa hawaijui dunia wao ni school - chuo - kazini asubuh hadi jioni

Mimi nishapewa Mil1.5 kuna dili ilitakiwa tukamilishe yani ile ilikua kama kishawish tu yani chambo unavutwa moyo uingie mzima mzima kwenye game na hayakuwa malipo yani iyo fanya maandalizi yako ujitengeneze kimazingira ya kazi baada ya wiki nikapewa tena kama laki 4
Nilichokifanya nilikimbia na ile pesa moyo wangu haukuwa tayari kufanya ule mchongo kwaiyo kupewa pesa kabla ya kazi kwa ishu haramu ni kawaida

Ila ndugu zangu aya maisha bora usakwe na polisi unaweza pona ukaishia nyuma ya nondo sio wahuni
Now nipo free nilisha clear tofauti zangu na wahuni[emoji16]
One day utupe mkasa
 
Story kama hii Kwa kutunga inatakiwa uwe bonge la genius na ikuchukue mda mrefu sana kuiweka Sawa, bado katika suruba yote hyo uje uianike hapa JF bure , si Bora ukamuuzie shigongo , possibly ni masimulizi ya halisia , just only time to write
hii ni ya kweli,huwezi tunga story ki rafu hivi,
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 21.



Haikuwa safari ya kitoto hata kidogo,tuliingia pale Arusha saa 3 usiku.Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kufika Arusha,japo nimefika mara kadhaa lakini sikuwahi kuwa mwenyeji,mara zote wakati naenda shule Tanga nilikuwa nikipita Arusha.Baada ya kufika Arusha mjini yule jamaa akawa ametuambia inapaswa tupate chakula mahali fulani ili tukimaliza tuondoke kwakuwa tulipokuwa tukienda hakukuwa na chakula wala mtu wa kukipika!.

Tulipomaliza kula tuliondoka zetu kuelekea ambako mimi na Mtatiro tulikuwa hatupajui.Baada ya muda ile gari ikaanza kupiga honi baada ya kufika mbele ya nyumba ambayo ilikuwa na geti;geti lile lilifunguliwa kisha gari ikaingia ndani.Tuliteremka huku tukiendelea kushangaa shangaa ndipo yule jamaa akaja akatuambia tumfuate,tulielekea ndani ambako tulionyeshwa chumba cha kulala ambacho kilikuwa na vitanda 2.

Wakati ule kiukweli hakuna mtu tuliyemkuta pale kwenye ile nyumba zaidi ya yule mtu aliyetufungulia lile geti,sasa kumbe baada ya ile Noah kutuacha pale wao waliondoka na hakuelewa walienda kulala wapi.Asubuhi mida ya saa 2 yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza alikuja kutuchukua na kutuambia inapaswa tuondoke!.Tuliondoka kuelekea Tengeru hatimaye tukafika kwenye nyumba moja ambayo tulimkuta yule bosi wake na Gabi akiwa na jamaa wawili,miongoni mwa wale jamaa tulikuwa nae Mwanza ila yule mmoja sikumfahamu,sasa ilifanya idadi yetu kuwa watu wanne ukimuondoa yule Bosi.Yule bosi alimuita yule jamaa tuliyekuja nae wakaanza kuzungumza kitu ambacho hatukukilewa,sasa baada ya yale mazungumzo jamaa alitoka akawa ameondoka,baada ya muda kuna jamaa mmoja miongoni mwa wale tuliowakuta alikuja akawa ametuuliza mimi na Mtatiro tunavaa viatu namba ngapi kila mmoja.

Baada ya kumueleza size ya namba ya viatu tulizokuwa tunavaa,jamaa aliondoka.Haukupita muda akawa amerudi na viatu aina ya safari boot ambazo kila mtu alipaswa kuchukua size yake!.Sasa ilipofika mida ya jioni yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza alirudi akiwa kwenye gari aina ya Mark 2 nyeupe iliyokuwa na tinted,ile gari iliingia mpaka pale ndani kisha jamaa akawa ametelemka na begi jeusi ambalo lilionekana lilikuwa zito.

Jamaa "Aisee hebu njoeni ndani mara moja"

Baada ya kufika ndani,jamaa hakutaka kupoteza muda,alifungua lile begi ambalo lilikuwa na nguo kadhaa akawa amezitoa na kututaka kila mmoja ajaribu itakayo mtosha.Mimi zilizonitosha ilikiwa ni jeans mbili pamoja na cadet moja iliyokuwa nzito,Mtatiro yeye kwakuwa alikuwa na mwili mkubwa kidogo,alipata nguo ambazo ziliendana na mwili wake vizuri.

Sasa baada ya hapo jamaa alituambia tukae chini kisha akawa ametoa bunduki iliyokuwa kwenye lile begi!.Sikufahamu ile bunduki ilikuwa ni aina gani kwasababu sikuwa mtaalamu wa bunduki kwa wakati huo,ile bunduki ilikuwa ni fupi kisha ikawa imekazwa kwa mapira katikati.Sasa baada ya kuitoa ile bunduki yule jamaa alituambia tumsubiri yule aliyekuwa bosi wa Gabi anakuja.

Yule bosi baada ya kurudi na yeye hiyo mida ya saa 2 usiku pia alikuwa na bunduki ambayo niliifahamu ilikuwa SMG.

Bosi "Msiogope bhana haya ni mambo ya kawaida"

Aliendelea "Jamaa yenu mtamkuta Kahama anawasubiri,pale kuna mtu ana hela zangu itapaswa mkazichukue"

Aliendelea "Hii Mashine ningekupatia wewe(Mtatiro)lakini nahitaji kwanza muda"

Aliendelea "Jipe atawapa hiyo nyingine mtaondoka nayo kwenda Kahama halafu hii kuna mtu mtaongozana nae ndiyo atakuwa nayo"

Aliendelea "Sasa naomba simu zenu mziache hapa maana huko hampaswi kwenda na simu"

Basi tulichukua zile simu tukawa tumemkabidhi yule aliyeitwa Bosi.Kumbe muda huo ambao sisi tulikuwa hapo Arusha,Gabi yeye alikuwa Kahama mkoani Shinyanga ambako hatukufahamu alikwenda kufanya shughuli gani!.

Bosi "Nyie mtaondoka kesho kutwa,kaeni hapa mpumzike kwanza"

Baada ya yale mazungumzo,yule Bosi aliondoka na yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza wakawa wametuacha pale kwenye ile nyumba tukiwa pamoja na wale jamaa wawili tuliowakuta.

Kweli!,baada ya siku mbili tuliondoka asubuhi na mapema,ilikuwa mida ya saa 10 usiku ndipo tuliianza safari kuelekea Kahama mkoani Shinyanga,mimi kiukweli sikuelewa kilichokuwa kimetupeleka Arusha ilikuwa ni kitu gani maana hata bunduki zenyewe hatukupewa kwa muda huo bali tuliishia tu kuonyeshwa na kupewa maelekezo,sikuweza kuhoji sana niliamua tu kutulia maana nilikubali mwenyewe kujiingiza kwenye genge la ujambazi!.
Tuliondoka na ile Toyota Mark 2 ambayo tulikuwa mimi na Mtatrio pamoja na yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza ambaye alifahamika kwa jina la Jipe,sikujua kama ndilo jina lake halisi lakini hata sisi baada ya kuzoeana tulikuwa tukimuita hivyo!.Dereva aliyekuwa akiendesha ile gari kiukweli alikuwa jamaa fulani wa kawaida sana na mwembamba lakini alikuwa dereva mzuri sana,nakumbuka ile gari ilikuwa ikitembea mpaka unahisi inapaa!.

Baada ya safari ndefu hatimaye tukafika Kahama,sasa tulipofika maeneo ya mgodi wa buzwagi,tuliingia kushoto tukaikamata barabara ya vumbi kuelekea Mwendakulima kwa ndani ndani huko.

Haukupita muda tukawa tumefika kwenye nyumba moja ambayo haikuwa na geti lakini ilikuwa imejitenga mbali na nyumba nyingine,sasa tulipofika hapo ndipo tukakutana na Gabriel ambaye baada ya sisi kuteremka kwenye ile gari alimchukua pembeni yule jamaa wakaanza kuzumngumza!.

Baada ya yale mazungumzo Gabi alituambia tuingie ndani huku yule jamaa akibeba lile begi lililokuwa na silaha kuingia nalo ndani!.Tulipiga stori na Gabi huku yeye akiendelea kutupa moyo kwamba yale mambo yalikuwa ni kawaida tu na hatukupaswa kuwa na hofu!.

Siku iliyofuata ilipofika saa 6 usiku,yule jamaa alituambia mimi na Mtatiro tutaongozana nae kuelekea mahali fulani,sasa alimpatia Mtatiro ile bunduki iliyokuwa imefungwa na mapira kwa nguvu sana na yeye akachukua ile SMG.

Jipe "Mtakuwa manafuata maelekezo yangu kila nitakachokuwa nawaambia!"

Mtatiro "Sawa"
Jipe "Hiyo silaha tayari risasi iko chemba,hivyo kuwa makini!"

Aliendelea "Gabriel atabaki hapa kuweka mambo sawa,sisi tutaondoka na tutawahi kurudi,kule tukifika hakuna kusubiri,tunaenda kufata kilichotupeleka!"

Jipe "Wewe jamaa(mimi)utakuwa kando yetu na utafanya nitakachokuwa nakwambia"

Mimi "Sawa"

Mtatiro alivyokuwa ameishika ile silaha ungemuangalia kwa haraka haraka ungezani uenda alikuwa askari mwenye uzoefu wa miaka mingi,jamaa alikuwaga jasiri sana alikuwa mtu ambaye ulikuwa ukimpatia maelekezo mara ya kwanza basi hurudii tena maana alikuwa na kichwa chepesi!.Mpaka muda huo ukweli ni kwamba,Mtatiro ndiye aliyenishawishi hadi na mimi kujikuta naingia mkenge!,sikuwa na namna ilipaswa nitafute pesa!.
Umughaka kama umughaka
 
Back
Top Bottom