Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 15.
Mimi "Sidhani kama ningekuuliza kama ningekuwa nayo!"
Yeye "Jamani!,ila wanaume nyie hamuaminikagi kabisa!"
Aliendelea "Yaani umughaka leo nakupigia simu unaniuliza mi nani!"
Mimi "Hii line nime renew ile ya kwanza ilipotea!"
Yeye "Haya bhana,mi Leah"
Kiukweli ile sauti ya huyo mwanamke ilikuwa ni sauti mpya kabisa katika masikio yangu,mimi sikutaka mambo mengi nikawa nimeamua tu kumdanganya ya kwamba line ilipotea nika renew hivyo majina nayo yakaenda na maji,sasa aliponitajia jina la Leah ndipo akazidi kunichanganya kabisa kwasababu hakuna mwanamke niliyekuwa nikifahamiana nae akiitwa Leah.Nilikuwa nikijaribu kuvuta picha alikuwa ni Leah wa wapi lakini picha inakataa!,sasa nilifahamu uenda wakati nikiwa pale Sirari na washikaji wakati tunapiga mtungi kuna demu nimewahi kuchukua namba yake lakini kwasababu ya pombe nikashindwa kuisevu,niliamua kubaki na hiyo tafakari moja tu ya kwamba uenda tulikutana kwenye mabar huko!.
Sikutaka kumkatisha ili asijisikie vibaya,mimi nikaungana nae na kumpokea kwa kauli iliyoonyesha kumfahamu!.
Mimi "Oooh! za siku!?"
Yeye "Nzuri tu,uko wapi!"
Mimi "Nipo kijiweni"
Yeye "Mmh unanidanganya!"
Mimi "Kweli!,nipo kijiweni"
Yeye "Nimepita nikusalimie lakini sijakuona"
Mimi "Kwani we unajua mi nafanyia wapi kazi?"
Yeye " Tuachane na maswali mengi bhana,tuonane basi"
Mimi "Lini?"
Yeye "Leo kama itawezekana"
Aliendelea "Lakini leo sitaki kwenda Guest nataka kuja kwako"
Kiukweli nilijaribu kuvuta picha alikuwa ni mwanamke gani huyo lakini bado sikupata majibu yanayoeleweka!,lakini pia katika maisha yangu pale Sirari kwa wakati ule sikumbuki kama niliwahi kulala na mwanamke Guest,mimi nilikuwaga napenda kampani na washikaji tu na kunywa bia mbili tatu lakini sikuwahi kabisa kuwa addicted na masuala ya wanawake mpaka ifike steji ya kulala nao kwenye magesti,mademu wengi tuliokuwa nao wakati huo walikuwa ni mademu wa washikaji zangu na ndiyo wengi nilikuwaga na namba zao kama mashemeji zangu!.
Ile nyumba ambayo nilikuwaga nimepanga pia sikuwahi kabisa kumpeleka mwanamke wa aina yeyote,sasa ilikuwa ajabu kuongea na huyo mwanamke na kuniambia eti " Lakini leo sitaki kwenda Guest" kana kwamba hata hiyo gesti yenyewe nishalala na mwanamke!.Fedha yangu kubwa iliishia kwenye Misosi na Kupiga pamba,kiukweli hadi leo ndivyo vitu vinanilia hela na wala si wanawake!,sina hobby kabisa na mademu ingawaje ninaye demu mzuri tu wa kiwango cha kimataifa!.
Niliamua kumpigia mshikaji wangu Nyamori ili pengine anieleze uenda angekuwa anamfahamu yule demu lakini pia akasema yeye alikuwa amfahamu,pia nikampigia mwanangu Magesa nikamuuliza kuhusu jina la huyo demu nae akasema hamjui,nilijaribu kumpepeleza Magesa ili anifahamishe uenda kuna demu amewahi kuja kunitafuta pale kijiweni kwa siku za karibuni lakini jamaa akasema hakuna!.Sasa niliamua kumshirikisha Mtatiro lile suala ndipo akaniambia inapaswa niwe makini uenda mapongo walikuwa wakiandaa mtego wa panya ili wanidake kupitia mwanamke.
Mtatiro "Hebu nipe hiyo namba tuone"
Nikampatia Mtatiro ile namba akajaribu kuipiga,alipoipiga bahati nzuri ikapokelewa na mwanaume lakini mtu aliyepokea ilionekana alikuwa kwenye kelele kama za watu wengi hivyo hawakuweza kusikilizana!.
Mtatiro "Hii namba inabidi uachane nayo maana wajinga watakuwa bado wanakusaka"
Aliendelea "Tena huyo demu akipiga we usipokee mkatie kabisa"
Sikuwa na shaka na maelezo ya jamaa yangu Mtatiro maana ni mtu ambaye mara zote alikuwaga akinishauri sana!.
Nilichokifanya nilikopi majina yote muhimu kwenye ile simu na kisha nikatoa ile line ya simu nikaitupa,kesho yake nikaenda kusajili line mpya ya Airtel. Baada ya kuona hapo Nyasana mambo hayanilipi niliamua kumwambia Mtatiro ya kwamba mi inabidi nieleke Mwanza kwa sista.Mtatiro nae ni kama alikuwa keshakata tamaa ila braza ake ndiye alionekana kikwazo kwake!.
Mtatiro "Mwanangu mi namuaga kama akikataa kuondoka namuacha yeye apambane,atajua mwenyewe!".
Mtatiro alitaka arudi na yeye Mwanza akaangalie ishu nyingine maana pale kijijini ni kama alikuwa akipoteza muda,sasa aliniambia hapo Mwanza kuna nyumba ilikuwa imejengwa na kaka yao mkubwa ambaye alikuwa mwanajeshi na ndipo alipofikia,na huyo braza ake aliyekuwa hapo Nyasana mgodini pia alikuwa akiishi pale na familia yake kwakuwa hiyo nyumba haikuwa na mtu!.
Baada ya Mtatiro kumwambia huyo braza ake waondoke maana hapo ni kama alikuwa akipoteza muda lakini jamaa alikuwa haelewi kabisa,yeye alikuwa akisema lile eneo kuna madini na atabaki kukomaa,sisi kama tunaondoka basi tuondoke na yeye tumuache!.Hatukuwa na namna ilibidi sisi tuondoke kuitafuta Mwanza.Sasa mpaka wakati huo zile hela feki zilikuwa zimebaki Tsh milioni 1.8,na ambazo tulikuwa tumechenji na nyingine kutumia zikabaki halali laki 4.Hivyo zote halali na feki zilikuwa Tsh milion 2.2.
Tulipokuwa hapo Bunda tulinunua nguo na viatu pia mara kibao tulikuwa tukienda hapo mjini kupata beer na kula vizuri,hivyo kujikuta hela zinazidi kupukutika!.
Nilipofika Mwanza niliamua kutengana na Mtatiro,mimi nilielekea kwa sista aliyekuwa akiishi Meko na Mtatiro yeye akaelekea huko Usagara!.Nilimpatia jamaa yangu hela kama laki 6,feki nilimpa laki 4 na halali nikampatia laki 2 ili angalau zimsaidie atakapokuwa huko!. Baada ya kufika hapo kwa sista kiukweli sikutaka kabisa kukaa,sasa shemeji alikuwaga akitoka kuna alikuwa akimaliza hata wiki ndipo anageuka nyumbani!.Nilimwambia sista aongee na shemeji ili amwambie yule muhindi kama bado ile kazi ipo nikaifanye lakini kwa bahati mbaya jamaa akasema ishapata mtu muda mrefu tu!.
Kuna siku shemeji akawa ameniambia niende nae akanifundishe kazi ya kusimamia wavuvi wake kwenye ile mitumbwi yake ili nitakapokuwa na ujuzi wa kutosha awe ananiachia usimamizi na yeye kuendelea na shughuli nyingine,nikawa nimekubali maana sikutaka kukaa tu hapo kwa shemeji nionekane mzigo!.
Tuliondoka na shemeji tukawa kama tunaelekea Musoma,sasa tulipofika Magu tulishuka,kuna gari ilikuja kumchukua pale tukawa tumeondoka hadi kisiwani huko ndani ndani, kile kisiwa kilikuwa kinaitwa kisiwa cha Ijinga,Aisee nilipofika hapo nilikuta kuna mitumbwi kama uchafu,kuna ambayo ilikuwa imefungwa injini za Yamahama na Honda,pia ipo mitumbwi ambayo ilikuwa ya kawaida tu!.
Baada ya kufika hapo shemeji akawa amemuita jamaa mmoja wakaanza kuongea!.
Shemeji "Aisee nimewaongezea mvuvi"
Jamaa "Aaah ndo huyu bwana eeh!"
Shemeji "Eeeh bhana mfundisheni kazi ni shemeji yangu"
Jamaa "Sawa bosi wangu"
Nilibaki kuduwaa na kushangaa maana niliambiwa naenda kusimamia mitumbwi lakini baada ya kufika kibao kimebadilika na kuitwa mvuvi!
Muendelezo>
Sehemu ya 16