Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nadhani kati ya waandishi bora kabisa wa stori nawe utakuwa top rank.

Unaandika vizuri sana,hasa sehemu za majibizano,msomaji unasisimka mwili.

Kazi nzuri.
Ila nyie bhakita bhana mna matatizo ssna aisee
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 8.




Joto,harufu mbaya,giza na msongamano wa watuhumiwa kwenye ile Selo ilifanya nikajuta kuzaliwa.Ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukanyaga polisi!,sikuwahi kabisa kuamini ya kwamba itatokea siku moja na mimi nitajikuta mikononi mwa mapongo na kuishia lokapu!.Mazingira ya mle ndani yalikuwa mabaya sana,harufu ya mikojo,vinyesi na majasho ya wahalifu yalinichanganya sana,kibaya zaidi nilikuta kukiwa na mrundikano wa watu huku wengine wakiwa na majeraha katika sehemu tofauti ya miili yao!,wengine nadhani kutokana na kipigo cha raia huko nje walikuwa wanashindwa hata kunyanyuka na kujisogeza!.Kiukweli sitakuja kusahau hiyo siku,ingawa kwasasa nishakuwa mwanaume kamili wa kupambana na changamoto zinazonikabili za kimaisha lakini huwa naepuka sana nisijikute naangukia mikononi mwa vyombo vya dola,ndugu zangu fanyeni mfanyavyo lakini kama hujawahi kukanyaga kule ndani nakushauri tu usithubutu!,lile taizi siyo la mchezo!.

Sasa baada ya kukaa takribani kwa dakika 15 ndipo nikaona lile geti la kile chumba linafunguliwa na kuna mtu akawa ameingizwa,sasa kwakuwa wakati anaingizwa kulikuwa na mwanga wa nje hapo koridoni nilimuona alikuwa ni Gabriel,mle ndani kulikuwa na giza lisilokuwa la kawaida ingawa ilikuwa mchana mida ya saa 9.Nilimuita Gabriel akawa amesogea eneo nililokuwa nimekaa kwa taabu kwa kukunja na kubana miguu,kuna jamaa alikuwa kando yangu nikamuomba abane kimtindo ili nikae na mshikaji!.

Mimi "Kaka kwani kimetokea nini?"

Gabi "We acha tu,yaani sijui hata nisemeje!"

Gabi aliendelea kusikitika sana akawa anashindwa hata kuongea,mimi ndiyo alizidi kunichanganya kabisa kwasababu nilitegemea kitu kutoka kwake lakini nae akawa kama haelewi ni nini kilotokea!.

Mimi "Sijui tutaachiwa lini kaka!"

Gabi "Nimejaribu kuongea na yule afande kiutu uzima lakini naona kama haelewi"

Mimi "Sasa itakuwaje kaka au ndiyo tunapelekwa gerezani?"

Gabi "Ngoja tuone itakavyokuwa,nimefanya mawasiliano na bosi wangu ameniambia anashughulikia"

Sasa wakati tunazungumza,kuna jamaa mmoja aliyekuwa kando yetu alikuwa kama kachanganyikiwa hivi,kuna muda alikuwa akiongea mwenyewe kama chizi!.Aliposikia Gabi anazungumzia ishu ya kutoka ndani akawa amedakia!.

Jamaa "Humu ndani ukiwa na hela unadhani unakaa?,labda uwe umeua lakini kama hujaua mbona unateleza tu kama nyoka"

Basi sisi hatukutaka kumjibu kitu chochote tulibaki kumsikiliza akiwa anaongea.Kadiri muda ulivyokuwa unayoyoma ndivyo nilizidi kuchanganyikiwa na nilidhani ingekuwa jambo jepesi mimi kutoka kumbe haikuwa kama nilivyofikiria!.

Mimi "Shem wamemweka wapi?"

Gabi "Amepelekwa kwenye selo ya wanawake"

Kiukweli hatukuwa na maneno mengi ya stori mule ndani zaidi ya kila mtu kichwani mwake kuwaza alichokiwaza!.Sasa ilipofika mida ya saa 10 kama na nusu jioni,nilisikia kuna afande anaita kwa sauti!.

Afande "Humu ndani kuna mtu anaitwa mzee wa kuzugia?"

Aliendelea "Narudia,humu ndani kuna mtu anaitwa mzee wa kuzugia?"

Mimi "Nipo afande"

Niliitikia kwa sauti kubwa ili aweze kunisikia,nilinyanyuka nikawa nimesogea mpaka pale kwenye lile geti!.

Afande "Jina lako halisi unaitwa nani?

Mimi "Naitwa Umughaka"

Afande "Aisee hebu taja majina yako uliyoandika kwenye kitabu usinipotezee muda"

Nilipomtajia jina langu kamili nadhani alikuwa akiangalia kwenye orodha ya majina ya wahalifu waliokuwa wamefika siku hiyo.Sasa kumbe kuna washikaji zangu wale ambao nilikuwa nafanya nao kazi pale kijiweni wakawa wamefika hapo polisi kuniulizia,kutokana na kwamba hawakujua jina langu halisi nililokuwa nimepewa na wazazi wangu,wao wakawa wamemwambia yule afande aliyekuwa zamu ya kwamba natambulika kwa jina moja la "Mzee wa kuzugia".Basi bana yule afande baada ya kuniuliza maswali kadhaa pale na kujiridhisha akawa amenifungulia ule mlango,kiukweli nilipotoka mle ndani nikakutana na hewa safi ya nje ya kile chumba,nilitamani kabisa nisirudi mle ndani lakini sikuwa na namna!.

Nilipofika pale mapokezi,niliamriwa nikae chini,sasa yule jamaa yangu Nyamori akawa amekuja na wadau wangu wengine wawili huku wakiwa wamebeba mkate na soda ya fanta orange!.Haikutakiwa kabisa nisimame,kama ni kuongea walipaswa kuongea kwa nguvu na mimi niwajibu nikiwa pale chini!.

Nyamori "Mwanangu vipi?"

Mimi "Mwanangu wee acha tu"

Mimi " Hebu wanangu kama mnaweza hakikisheni mnafanya mpango nitoke halafu hayo mengine tutaongea huko nje!"

Nyamori "Usijali kaka haya mambo huwa ni kawaida kwa wanaume,chukua mkate na soda upunguze njaa"

Basi kabla sijapewa ule mkate,yule afande akaamuru ufunguliwe kutoka kwenye mfuko na ukaanza kuchambuliwa kipande baada ya kipande,alipojiridhisha akawaambia kila mmoja aliyekuwa amekuja kuniona achukue kipande kimoja kimoja ale na ile soda kila mmoja apige pafu!,baada ya dakika tano kupita akawa amenikabidhi mkate na ile soda na kutakiwa kula pale pale!.

Nilipomaliza kula tukawa tumeagana na wanangu nikachukuliwa nikarudishwa ndani ambako nilikuwa napaona kama jehanamu!.Japo Nyamori na washikaji zangu waliniletea soda na mkate wa kupunguza njaa lakini kiukweli nilikuwa sihisi njaa na wala sikuwa na hamu ya kula chochote kutokana na yale matatizo!.

Gabi "Alikuwa nani amekuja kukucheki?"

Mimi "Walikuwa washikaji zangu wa kijiweni!"

Gabi "Kwani walifahamu umedakwa?"

Mimi "Kuna muda nilimpigia simu mshikaji wangu kumjulisha"

Gabi "Ooh sawa!".


Ilipofika usiku kiukweli sikuweza hata kupata usingizi wa mang'amu ng'amu kutokana na joto kali lililokuwa likinasibishwa na harufu kali iliyo mbaya pamoja na mbu waliodhani mle ndani kuna sherehe!.Kiukweli nilipata tabu sana na ni moja ya siku ambazo sitokuja kuzisahau kabisa katika maisha yangu!.

Sasa asubuhi mida ya 2 kuna watu walikuja kutolewa mle ndani angalau kukawa na unafuu wa hewa!.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi niliskia jina la Gabi likiitwa na akawa ameitika kisha akafunguliwa mlango akatoka.Nilifahamu kabisa Gabriel uenda akawa amechomoka na mimi kuniacha mle ndani,kiukweli nilijisikia vibaya sana hadi machozi yakaanza kunitiririka!.Kibaya zaidi muda ulizidi kwenda huku nikijifariji labda nitaitwa lakini haikuwa hivyo!.

Sasa baada ya saa 1 kupita nikasikia naitwa jina langu!.

Ipo vzr mzee baba
 
Back
Top Bottom