Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Kumbe unanisomaga na kumbe mimi naonekana mwehu kwako eti eee.
Kuna wakati unajitoaga akili sana kule kwenye jukwaa la sports,sijui kwanini unakuwa mshamba wa kutambua kuwa ukikoment chechote lazima kisomwe
 
dah hatari sana Umughaka itakuwa huyo musagane kawachomesha tena
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 10.




Niliondoka mdogo mdogo nikaelekea kwenye ile bar ambayo aliniambia ningemkuta hapo.Kweli,baada ya kufika hapo nilimkuta Gabi akiwa amekaa huku akiendelea kupiga beer yake pendwa ya Safari!.

Gabi "Uko poa?"

Mimi "Niko poa kaka"

Basi na mimi nikaagiza beer nikaanza kunywa huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale.Gabi bado alionekana kabisa kutokuwa na furaha tofauti na siku nyingine nilivyokuwa nimemzoea,yaani baada ya hilo sakata la sisi kukamatwa ni kama alikuwa hana mudi kabisa!.

Gabi "Mwanangu kwanza kabisa nikuombe samahani,maana jana tulishindwa kuzungumza kabisa kwasababu sikutaka kuzungumza mambo yetu mbele ya Eric(Bosi)"

Aliendelea "Vipi lakini uko Good?"

Mimi "Mimi niko Good kaka wala usijali"

Gabi " Unajua mwanangu asubuhi nimeshindwa kukupa hela kwasababu yule mwanamke amenikwaza sana"

Aliendelea "Hivi unajua yeye ndiye chanzo cha sisi kukaa ndani kaka!"

Mimi "Acha usiniambie kaka"

Gabi "Huwezi amini umughaka!"

Aliendelea "Usimuone na mitako ile ukadhani kichwani kuna akili,kichwani kabeba kamasi tu!"

Mimi "Mimi nilishangaa tu ananipigia simu ile juzi na akataka nije home kwako,lakini nilipokupigia simu yako kujiridhisha nikaona upo kimya kaka ndiyo ikabidi nije"

Gabi "Simu yako nilikuwa naiona lakini sikuweza kupokea kutokana ile hali ambayo nadhani uliikuta,isingekuwa rahisi!"

Aliendelea "Jambo la kushukuru tupo uraiani kaka,hayo mengine sidhani kama niyakutuumiza kichwa sana!"

Gabi "Unajua hiyo juzi nilikuwa nimetoka kuna mtu nilienda kuonana nae,sasa nikiwa huko nashangaa ananipigia simu akiwa analia,nikamuuliza kuna nini?,hasemi!"

Aliendelea "Ikabidi niwashe gari kurudi nyumbani maana nikadhani uenda wakurya wamemfanya kitu mbaya!"

Gabi "Ile nimefika ndani nashangaa nawekwa chini ya ulinzi,mwanangu hakuna siku nimemchukia yule mwanamke kama juzi!"


Aliendelea "Unajua mwanangu mimi nilikuwa mwalimu huko Babati sehemu moja inaitwa Haidomu,sasa kuna mambo mengi yalijizokeza hapo katikati hivyo nikawa nimetemana na uticha!"

Gabi "Sasa yule demu mimi nilifahamiana nae kipindi hicho hapo Haidomu,nikajikuta tunafahamiana na hatimae kuwa wapenzi!"

Gabi "Tumeishi kwa muda mrefu tu mpaka mimi kuja kufahamiana na Eric na ndiye akanipa mchongo huu ambao umenipa kila ninachokitaka,na huyu mwanamke anaelewa kila kitu kaka,siyo kwamba hajui!"

Aliendelea "Tukiwa pale babati,kuna siku sikachukua hela kaenda benki eti atumiwe kwenye akaunti yake!"

Mimi wakati huo naendelea kumsikiliza Gabriel tu na wala sikuwa mchangiaji!.


Gabi " Kibaya zaidi alichukua laki 5"

Mimi "Mbona zilikuwa nyingi sana"

Gabi "Kaka ninapokwambia hana akili siyo kwamba namdharau,hapana!,ni mwanamke wangu hilo nakubali lakini tatizo lake huwa hajiongezi,kila siku namwambia lakini haelewi!"

Aliendelea "Sasa alichokifanya Babati ndicho juzi ametaka kukifanya hapa,nimemuuliza ilikuwaje ananiambia eti alichukua laki moja kwenda kumtumia mtu kwa wakala,sasa inavyoonekana yule wakala baada ya kuzitambua zile pesa alipiga simu polisi"

Gabi "Na lenyewe lisivyokuwa na akili likabaki palepale mpaka wakalidaka!"

Mimi "Sasa kaka tutafanya kazi kweli kwa mazingira hayo?"

Gabi "Kaka nina mzigo!,we acha tu!"

Aliendelea "Sema tu kwamba hii ishu inamtandao mpana hivyo hata ukikamatwa kukaa ndani ni sekunde tu unakuwa umetoka"

Gabi "Sasa kitu ambacho nataka ufanye,nimekuja na mzigo na nitakukabidhi wote,wewe pambana mdogo mdogo na utakuwa unafanya kama tulivyokubaliana mwanzo!".

Basi ilipofika mida ya saa 1 usiku,Gabi akawa amenichukua kwenye ki-Corolla chake hadi nyumbani nilipokuwa naishi!,aliamua kushuka kabisa ili aingie ndani aone ninapoishi!.Sasa wakati anashuka akafungua buti ya gari akatoa begi ambalo siku zote alikuwa akihifadhia zile hela!.

Gabi "Kaka hapa kuna usalama kweli"

Mimi "Hapa kaka kila mtu na time yake,hakuna wakuda"

Gabi "Kama ndivyo basi hakuna shaka,jambo la muhimu ni wewe kuwa makini tu"

Basi baada ya mazungumzo,yeye akawa ameondoka na nikamsindikiza kisha akaniacha pale kijiweni na yeye akawa ameondoka kuelekea Tarime.Basi baada ya kuniacha hapo niliamua kurudi zangu geto kuzitathimini zile hela na kuzipangia mpango mkakati namna ya kuziingiza mtaani,nilianza kuzihesabu usiku ule ndipo nikapata jumla yake milioni 9.Asubuhi kama kawaida kazi ya kuzingiza mtaani ikaendelea na nilikuwa nafanya kwa usiri mkubwa sana.Tangu lile jambo la kuswekwa ndani litokee sikutakaga kabisa kumwambia mshikaji wangu Mtatiro,niliamua kukaa nalo moyoni!.

Nakumbuka kila nilipokuwa nafanya kazi ikifika milioni 1,nilikuwa nampelekea jamaa chake na mimi kubaki nacha kwangu!.Kiukweli ile pesa japo ilikuwa haramu lakini ilikuwa tamu!.Kwa kipindi kile sikuona kabisa kazi nyingine ya kunipatia fedha nyingi na kwa haraka kama ile ya kubadili noti feki,japo nilijua ni kazi hatari lakini ilikuwa imenikolea mno!.

Sasa nakumbuka baada ya miezi kama miwili kupita huku nikiwa naendelea kukimbizana na zile hela hili ziishe niletewe nyingine,nikiwa pale kijiweni nikiendelea na kazi yangu ya upiga debe,kuna meseji ziliingia kwenye simu yangu kwa mfululizo!.Nilipochukua simu mfukoni na kutazama zilikuwa sms zilizokuwa zimetumwa na Gabriel!,basi ikabidi nifungue sms moja baada ya nyingine.

Sms 1 " Umughaka uko wapi?"

Sms 2 "Hizo hela unaweza kuzichoma moto muda huu?"

Sms 3 "Kama unaweza hebu ondoka kabisa hapo kwako na hizo hela"


Sasa baada ya kusoma zile sms kiukweli nilishituka sana,sasa nikakimbia kuweka vocha na kuanza kumpigia Gabriel lakini simu ikawa inaita tu haipokelewi!,baada ya kupiga sana akanitumia sms nyingine tena.

Sms "Nimekwambia kimbia kaka mambo yameharibika,tupo njiani tunakuja kwako!"


Aisee baada ya jamaa kuniambia wanakuja kwangu niliondoka nikikimbia kuelekea nyumbani kama kichaa,nilivuta picha umbali wa kutoka pale Tarime hadi Sirari nikaona kabisa kama gari ilikuwa na spidi kali,basi watakuwa wamebakiza hatua chache!.Nilipofika nyumbani nilifungua mlango kama vile mwizi,nilichukua lile begi nikavaa viatu nakutoka kisha nikaufunga mlango na kukimbia!.

Sasa kuna njia ilikuwa inakupeleka moja kwa moja mpaka mpakani(Mpaka wa Tanzania na Kenya),mimi nikaamua kuipita hiyo na sikutaka kwenda na ile njia kubwa ambayo ingetokezea kwenye lami kisha kijiweni.Nilikuwa nakimbia kama kichaa vile.

Baada ya mwendo mrefu kidogo nikajikuta nimeingia upande wa pili wa Kenya na sikutaka kabisa kuzubaa maana nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa!.Sasa baada ya kufika ng'ambo ya pili ya upande wa Kenya pale mpakani Isebania,nilijaribu kuipiga ile namba ya Gabriel ikawa haipatikani!.Nilichokifanya nilichukua elfu 50 ya Tanzania nikaibadili pale mpakani kisha nikaenda stage(stand) nikapanda shuttle zilizokuwa zinakwenda Migori.

Sikufahamu nakwenda Migori kufanya nini lakini niliona bora kukimbia kuliko kukamatwa nikaozee gerezani,nilifahamu kile kitendo cha Gabriel kuniambia nikimbie kilikuwa ni kitendo cha hatari na uenda yeye tayari alikuwa mikononi mwa ndata!.
Hii sehemu ya mwisho na mimi nilikua nakimbia kama wewe.

Bro unajua kuandika tena sana
 
Back
Top Bottom