Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 14.
Baada ya kumsubiri Mtatiro hapo Nyasura kwa muda hatimaye nae akawa amekuja akiwa anaendesha baiskeli,kiukweli kama kawaida nilipokuwa nikionana na jamaa yangu huyo utani wa hapa na pale pia furaha kwa kiasi fulani ilichukua nafasi.


Mtatiro "Mwanangu unazidi kung'aa tu,naona Tarime imekukubali"

Mimi "Aah wapi mwanangu ni kuridhika tu!"

Mtatiro "Vipi lakini kina Monche na washikaji wengine wazima?"

Mimi "Mwanao Monche sijamcheki muda mrefu,siunajua tena mimi zangu muda mwingi huwa ni Sirari tu!"

Mimi "Nadhani atakuwepo!"

Mtatiro "Jamaa huwa nampigiaga simu hadi leo haipatikani"

Mimi "Uenda atakuwa alibadili simu"

(Monche alikuwa ni yule dereva wa ile Hiace ambayo Mtatiro alikuwa akifanyia kazi kabla hajaondoka kwenda Mwanza,hivyo walikuwa washikaji).

Wakati tunaondoka hapo Nyasura kuelekea huko walipokuwa kina Mtatiro,tuliamua kutembea ili kuendelea kupiga stori maana ilikuwa ni muda umepita sijaonana na jamaa,ile baiskeli japo ilikuwa na Carier(sehemu ya kukalia)lakini tuliona ni vema tutembee huku mastori yakiendelea.

Tukiwa njiani niliamua kumwambia ukweli Mtatiro mambo yaliyokuwa yamenitokea kwasababu ukizangatia ni yeye ndiye aliyekuwa ameniunganisha na Gabriel.

Mtatiro "Jamaa sijaongea nae muda sana"

Aliendelea "Kwahiyo mlichomokaje?"

Mimi "We acha mwanangu!"

Mimi "Kuna jamaa anaitwa Eric ndiye aliyetuchomoa"

Mtatiro "Aah Eric nammanya mwanangu"

Aliendelea "Yule jamaa ndiye mwenye ile michongo na hata Gabriel ni mpambe tu!"

Mimi "Jamaa watakuwa wamemdaka maana baada ya kutoka Migori nilimtafuta lakini hapatikani!"

Mtatiro "Zile mishe zina njuruku(pesa) lakini ni hatari sana mwanangu,kila muda unakuwa macho kodo kama popo!"


Mimi "Mwanangu ninao mzigo kwenye begi!"

Mtatiro "Acha utani wewe!"

Mimi "Kwanini nikutanie!"

Mtatiro "Hebu tuone mwanangu!"

Nilishusha kile kibegi toka mgongoni nikawa nimempatia Mtatiro akawa amefungua na kutazama zile pesa ili ahakikishe nilichokuwa nakisema kama kina ukweli!.

Mimi "Hizo nilikimbia nazo kuingia Kenya ndo zimebaki!"

Mtatiro "Mwanangu hizi mbona zitatoka,we subiri uone!"

Basi baada ya mwendo mrefu huku tukiendelea kupiga mastori,Mtatiro akanitaka nipande kwenye baiskeli ili apige pedo(aendeshe) kwasababu bado kulikuwa kuna umbali tulipokuwa tukienda!

Baada ya muda tukawa tumefika hapo Kijijini ambako aliniambia kulikuwa na mgodi umetema,kiukweli palikuwa ni kijijini ambako hakukuwa pabaya sana maana karibia huduma zile muhimu zilipatikana hapo!.

Tulifika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na nyumba mbili za nyasi, Mtatiro akawa ameingiza baiskeli ndani akanitaka niweke lile begi ndani, akafunga ule mlango na kufuli akawa ameniambia tuelekee hapo kwenye hicho kimgodi!

Baada ya kufika pale mgodini tulikuta raia wanapambana kuchimba mashimo, kuna wengine walikuwa wamechimba mashimo marefu kiasi kwamba walikuwa hawaonekani, kuna ambao bado nilikuta waking'ang'ana kuchimba huku mashimo yakiwafika magotini!

Kiukweli kulikuwa na watu wengi sana huku kina mama wakiwa wanahangaika kubeba vifusi kwenye makarai na ndoo wakirundika mchanga kila mtu kwenye eneo aliloona kwake litakuwa salama kabisa.

Mtatiro alinipeleka mpaka kwenye shimo alimokuwa kaka yake na jamaa mmoja wakiendelea kuchimba,ile kazi ya uchimbaji haikuwa ya kitoto maana kulikuwa na vikokoto mshenzi kama vyote.

Sasa kwakuwa nilikuwa hapo ili kujaribu bahati yangu kwa upande huo wa madini,baada ya kumpa Hi brother ake Mtatiro nilikamata ndoo nikawa nasogeza ule mchanga pembezoni ya lile shimo!.Ile kazi tuliifanya hadi mida ya saa 3 usiku ndipo yule brother akasema tuondoke tukapumzike halafu kesho yake tungedamka mapema kuendelea!

Kiukweli familia ya kina Mtatiro haikuwaga na mambo mengi, nilichokuja kugundua ilikuwa ni familia yenye upendo sana,sema ndiyo hivyo tu hawakujaliwa kuwa na pesa!

Ukweli ni kwamba,jamii yangu ya kikurya ni jamii ambayo huwa ina upendo na kuwajali watu wengine pia,ukiachilia tu yale madhaifu madogo madogo kama wanadamu wengine lakini wakurya ni kabila bora sana miongoni mwa makabila bora kwenye hii nchi!,yale madhaifu madogo madogo ya kupiga mwanamke, kukeketa na kuchinjana ovyo yalikuwaga ni kwasababu ya ukosefu wa elimu tu, sikuhizi hayo mambo kwa Tarime yamepungua na kama siyo kuisha kabisa baada ya watu kuelimika!

Tarime ni njema sana na atakaye na aende akajionee!.(Nilikuwa nachomekea tu ndugu zangu).

Tulipofika hapo nyumbani kwakuwa tulikuwa wanaume tupu,tulikoka moto tukaanza kupika ugali ambao tulikula na dagaa zilizokuwa zimepikwa mchana!

Namshukuru Mungu kulipokucha asubuhi Mtatiro alinipatia nguo zake ambazo zilikuwa zimechoka ili nivae twende tukapige kazi!.Kiukweli nilipofika hapo mgodini hiyo asubuhi tulikuta nyomi la watu kila mtu akiwa anapambana kwa upande wake!.Kama kawaida na sisi tukaanza kazi iliyotupeleka hapo,nikiwa nimekaa nasubiri udongo ili niupeleke maeneo husika,simu yangu ilianza kuita,ile nimeitoa mfukoni na kutazama nikakuta ni Da'Sarah alikuwa akinipigia!

Da'Sarah "Mdogo wangu uko wapi?"

Mimi "Nisamehe Dada jana sikuwa na Vocha nikashindwa kukwambia niliteremkia hapa Bunda!"

Da'Sarah "Bunda tena umeenda kufanya nini!?"

Mimi "Hivi wale watoto wa mzee Marwa bado unawakumbuka?"

Da'Sarah "Marwa yupi?,yule jirani?"

Mimi "Eeh"

Da'Sarah "Mi namkumbuka yule mwanajeshi tu Ryoba"

Mimi "Sasa yupo mdogo wao ambae ni rika langu na ni rafiki yangu anaitwa Mtatiro,nilipita kumsalimia kaka yake anaumwa,alinipigia simu jana nikiwa kwenye gari nakuja hivyo nikaona niteremke kuja kumjulia hali!"


Niliamua kumdanganya dada yangu sababu ya mimi kuteremka pale Bunda ni kwenda kumuona kaka yake Mtatiro ambaye alikuwa mgonjwa ili asiendelee kunifikiria vibaya!.


Da'Sarah "Kwahiyo unakuja lini Mwanza!"

Mimi "Najitahidi dada nitawahi"

Da'Sarah "Uwahi kuja maana niliongea na shemeji yako akaniambia kuna muhindi alikuwa anatafuta mtu wa kusimamia boti zake za uvuvi"

Aliendelea "Siyo tumpange mtu kumbe na wewe huko una mambo yako!"

Mimi "Sawa dada nakuja"

Shemeji yangu alikuwaga akifanya kazi za uvuvi na yeye pia alikuwaga na mitumbwi yake kadhaa kwa ajili ya shughuli yake hiyo.Baada ya yale mazungumzo kazi zikaendelea kama kawaida,sasa lile eneo lilikuwa maarufu sana kama Nyasana Mgodini,kiumweli ni eneo lililokuwa limechanganya sana lakini jambo la ajabu hakukuwa na madini wala nini, maana Mtatiro alikuwa ananiambia wao wapo pale ndani ya mwezi na hakuna walichoambulia zaidi ya kupoteza hela tu!.


Mtatiro "Mwanangu hapa napo ni hasara tu,kila siku mara utasikia kuna kimkanda kimepita hapa,watu wakichimba kwenye hicho kimkanda hawaambulii kitu!"

Mimi "Kwani mlianza kuchimba lini?"

Mtatiro "Mimi nimekuja mwezi uliopita,lakini kina braza hapa wana miezi miwili,ndani ya miezi yote hiyo hawajawi hata kupata punje ya dhahabu!"

Mimi "Duuu!,mbona ni hatari"

Mtatiro "Kuna jamaa wao ndiyo walidai kuna mkanda umepita chini kutokea Geita,sasa watu wote hawa unao waona wanapambana kuutafuta mkanda!"

Mimi "Hakuna watu waliopata dhahabu hata mara moja?"

Mtatiro "Watu wanadai wanapata pata kimtindo lakini ukijaribu kuuliza waonyeshe walizopata hata huonyeshwi"

Aliendelea "Nishamshauri braza tuachane na hii biashara kichaa lakini hasikii,yeye bado anaamini kuna madini"


Kama kuna sehemu watanzania huwa wanapoteza muda na kulishana matango pori ni kwenye vimigodi uchwara, yaani unakuta wanaamini eneo husika kuna madini huku wakiendelea kupambana kwa nguvu na kupoteza pesa lakini mwisho wa siku wanaambulia patupu,na ndivyo ilivyokuwa hapo Nyasana, kuna muda unawaangalia ndugu zetu watanzania wanavyohangaika hadi huruma kwakweli, lile eneo ilikuwa inasemekana dhahabu ililipuka tu na watu wakaanza kujaa kwa wingi na kuanza kuchimba, sasa sikujua kama kuna wataalamu waliwahi kupima uwingi wa dhahabu ulioko pale ama la!.(Sijui kama hadi leo huo mgodi unafanya kazi).

Kuna muda tulikuwa tunatoka na mtatiro tunaingia mtaani kule kijijini tunabadili zile hela,tulipoona chenji kijijini hapo imekuwa ngumu tulikuwa tunaelekea pale senta ya Nyasura kupambana na ubadilishaji wa kununua bidhaa halisi na kurudishiwa chenji halali!.Kiukweli ile hela ikabaki chache sana!.

Kuna siku tukiwa tumetoka na Mtatiro tukiwa maeneo ya Bunda mjini kwenye mishe mishe hizo,simu yangu ikapigwa ikiwa ni namba ngeni!.

Mimi "Halloo"

Yeye "Mambo Umughaka"

Mimi "Poa,nani!"

Yeye "Hebu acha utani,kwahiyo namba yangu ushafuta!"
Yaani wewe Mzee wa Moghabiri kijiji cha ujamaa! umenikuna sana tena sana!....ndo pamenikuza huko ila rafiki zangu kina, Mwita wembe, Kasisi Mang'weina,

Wambura chacha (huyu Baba ake alikuwa Bwana shamba)......lile shamba li kijiji NKongore nimelima sana kwa ushirika lile!! Bado lipo kweli?? na trekta la kijiji mliuza siyo!!.....

Rafiki zangu wazee kina Marwa winani, na wadogo zake kina Gesase wapo!....Mwalimu Werema yaani sijui tu natamani sana nifanye ziara huko nikale Ilityambwe.......Ighichure..... .uliwahi ''kubhusugurya kweli mkuu?? au.......

Jamani Tarime raha hadi kichwa kinauma....ngoja kwanzaa..........Mzee Juhudi na Maarifa babake kina Nesi Nyaikoba wanaishi palee juu kuelekea kirighiri! daaa tarime weeee!

Ebu Kibumaye shule ya Msingi Box 172, bado ipo kweli?? daaaa!
 
Yaani wewe Mzee wa Moghabiri kijiji cha ujamaa! umenikuna sana tena sana!....ndo pamenikuza huko ila rafiki zangu kina, Mwita wembe, Kasisi Mang'weina,

Wambura chacha (huyu Baba ake alikuwa Bwana shamba)......lile shamba li kijiji NKongore nimelima sana kwa ushirika lile!! Bado lipo kweli?? na trekta la kijiji mliuza siyo!!.....

Rafiki zangu wazee kina Marwa winani, na wadogo zake kina Gesase wapo!....Mwalimu Werema yaani sijui tu natamani sana nifanye ziara huko nikale Ilityambwe.......Ighichure..... .uliwahi ''kubhusugurya kweli mkuu?? au.......

Jamani Tarime raha hadi kichwa kinauma....ngoja kwanzaa..........Mzee Juhudi na Maarifa babake kina Nesi Nyaikoba wanaishi palee juu kuelekea kirighiri! daaa tarime weeee!

Ebu Kibumaye shule ya Msingi Box 172, bado ipo kweli?? daaaa!
Haya tumekusikiaa kabla ujasoma hi Soma hyo ya uchawi ndio utadata zaid
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 15.



Mimi "Sidhani kama ningekuuliza kama ningekuwa nayo!"

Yeye "Jamani!,ila wanaume nyie hamuaminikagi kabisa!"


Aliendelea "Yaani umughaka leo nakupigia simu unaniuliza mi nani!"


Mimi "Hii line nime renew ile ya kwanza ilipotea!"

Yeye "Haya bhana,mi Leah"

Kiukweli ile sauti ya huyo mwanamke ilikuwa ni sauti mpya kabisa katika masikio yangu,mimi sikutaka mambo mengi nikawa nimeamua tu kumdanganya ya kwamba line ilipotea nika renew hivyo majina nayo yakaenda na maji,sasa aliponitajia jina la Leah ndipo akazidi kunichanganya kabisa kwasababu hakuna mwanamke niliyekuwa nikifahamiana nae akiitwa Leah.Nilikuwa nikijaribu kuvuta picha alikuwa ni Leah wa wapi lakini picha inakataa!,sasa nilifahamu uenda wakati nikiwa pale Sirari na washikaji wakati tunapiga mtungi kuna demu nimewahi kuchukua namba yake lakini kwasababu ya pombe nikashindwa kuisevu,niliamua kubaki na hiyo tafakari moja tu ya kwamba uenda tulikutana kwenye mabar huko!.

Sikutaka kumkatisha ili asijisikie vibaya,mimi nikaungana nae na kumpokea kwa kauli iliyoonyesha kumfahamu!.


Mimi "Oooh! za siku!?"

Yeye "Nzuri tu,uko wapi!"

Mimi "Nipo kijiweni"

Yeye "Mmh unanidanganya!"

Mimi "Kweli!,nipo kijiweni"

Yeye "Nimepita nikusalimie lakini sijakuona"

Mimi "Kwani we unajua mi nafanyia wapi kazi?"

Yeye " Tuachane na maswali mengi bhana,tuonane basi"

Mimi "Lini?"

Yeye "Leo kama itawezekana"

Aliendelea "Lakini leo sitaki kwenda Guest nataka kuja kwako"


Kiukweli nilijaribu kuvuta picha alikuwa ni mwanamke gani huyo lakini bado sikupata majibu yanayoeleweka!,lakini pia katika maisha yangu pale Sirari kwa wakati ule sikumbuki kama niliwahi kulala na mwanamke Guest,mimi nilikuwaga napenda kampani na washikaji tu na kunywa bia mbili tatu lakini sikuwahi kabisa kuwa addicted na masuala ya wanawake mpaka ifike steji ya kulala nao kwenye magesti,mademu wengi tuliokuwa nao wakati huo walikuwa ni mademu wa washikaji zangu na ndiyo wengi nilikuwaga na namba zao kama mashemeji zangu!.

Ile nyumba ambayo nilikuwaga nimepanga pia sikuwahi kabisa kumpeleka mwanamke wa aina yeyote,sasa ilikuwa ajabu kuongea na huyo mwanamke na kuniambia eti " Lakini leo sitaki kwenda Guest" kana kwamba hata hiyo gesti yenyewe nishalala na mwanamke!.Fedha yangu kubwa iliishia kwenye Misosi na Kupiga pamba,kiukweli hadi leo ndivyo vitu vinanilia hela na wala si wanawake!,sina hobby kabisa na mademu ingawaje ninaye demu mzuri tu wa kiwango cha kimataifa!.

Niliamua kumpigia mshikaji wangu Nyamori ili pengine anieleze uenda angekuwa anamfahamu yule demu lakini pia akasema yeye alikuwa amfahamu,pia nikampigia mwanangu Magesa nikamuuliza kuhusu jina la huyo demu nae akasema hamjui,nilijaribu kumpepeleza Magesa ili anifahamishe uenda kuna demu amewahi kuja kunitafuta pale kijiweni kwa siku za karibuni lakini jamaa akasema hakuna!.Sasa niliamua kumshirikisha Mtatiro lile suala ndipo akaniambia inapaswa niwe makini uenda mapongo walikuwa wakiandaa mtego wa panya ili wanidake kupitia mwanamke.

Mtatiro "Hebu nipe hiyo namba tuone"

Nikampatia Mtatiro ile namba akajaribu kuipiga,alipoipiga bahati nzuri ikapokelewa na mwanaume lakini mtu aliyepokea ilionekana alikuwa kwenye kelele kama za watu wengi hivyo hawakuweza kusikilizana!.

Mtatiro "Hii namba inabidi uachane nayo maana wajinga watakuwa bado wanakusaka"

Aliendelea "Tena huyo demu akipiga we usipokee mkatie kabisa"

Sikuwa na shaka na maelezo ya jamaa yangu Mtatiro maana ni mtu ambaye mara zote alikuwaga akinishauri sana!.

Nilichokifanya nilikopi majina yote muhimu kwenye ile simu na kisha nikatoa ile line ya simu nikaitupa,kesho yake nikaenda kusajili line mpya ya Airtel. Baada ya kuona hapo Nyasana mambo hayanilipi niliamua kumwambia Mtatiro ya kwamba mi inabidi nieleke Mwanza kwa sista.Mtatiro nae ni kama alikuwa keshakata tamaa ila braza ake ndiye alionekana kikwazo kwake!.

Mtatiro "Mwanangu mi namuaga kama akikataa kuondoka namuacha yeye apambane,atajua mwenyewe!".

Mtatiro alitaka arudi na yeye Mwanza akaangalie ishu nyingine maana pale kijijini ni kama alikuwa akipoteza muda,sasa aliniambia hapo Mwanza kuna nyumba ilikuwa imejengwa na kaka yao mkubwa ambaye alikuwa mwanajeshi na ndipo alipofikia,na huyo braza ake aliyekuwa hapo Nyasana mgodini pia alikuwa akiishi pale na familia yake kwakuwa hiyo nyumba haikuwa na mtu!.

Baada ya Mtatiro kumwambia huyo braza ake waondoke maana hapo ni kama alikuwa akipoteza muda lakini jamaa alikuwa haelewi kabisa,yeye alikuwa akisema lile eneo kuna madini na atabaki kukomaa,sisi kama tunaondoka basi tuondoke na yeye tumuache!.Hatukuwa na namna ilibidi sisi tuondoke kuitafuta Mwanza.Sasa mpaka wakati huo zile hela feki zilikuwa zimebaki Tsh milioni 1.8,na ambazo tulikuwa tumechenji na nyingine kutumia zikabaki halali laki 4.Hivyo zote halali na feki zilikuwa Tsh milion 2.2.

Tulipokuwa hapo Bunda tulinunua nguo na viatu pia mara kibao tulikuwa tukienda hapo mjini kupata beer na kula vizuri,hivyo kujikuta hela zinazidi kupukutika!.

Nilipofika Mwanza niliamua kutengana na Mtatiro,mimi nilielekea kwa sista aliyekuwa akiishi Meko na Mtatiro yeye akaelekea huko Usagara!.Nilimpatia jamaa yangu hela kama laki 6,feki nilimpa laki 4 na halali nikampatia laki 2 ili angalau zimsaidie atakapokuwa huko!. Baada ya kufika hapo kwa sista kiukweli sikutaka kabisa kukaa,sasa shemeji alikuwaga akitoka kuna alikuwa akimaliza hata wiki ndipo anageuka nyumbani!.Nilimwambia sista aongee na shemeji ili amwambie yule muhindi kama bado ile kazi ipo nikaifanye lakini kwa bahati mbaya jamaa akasema ishapata mtu muda mrefu tu!.

Kuna siku shemeji akawa ameniambia niende nae akanifundishe kazi ya kusimamia wavuvi wake kwenye ile mitumbwi yake ili nitakapokuwa na ujuzi wa kutosha awe ananiachia usimamizi na yeye kuendelea na shughuli nyingine,nikawa nimekubali maana sikutaka kukaa tu hapo kwa shemeji nionekane mzigo!.

Tuliondoka na shemeji tukawa kama tunaelekea Musoma,sasa tulipofika Magu tulishuka,kuna gari ilikuja kumchukua pale tukawa tumeondoka hadi kisiwani huko ndani ndani, kile kisiwa kilikuwa kinaitwa kisiwa cha Ijinga,Aisee nilipofika hapo nilikuta kuna mitumbwi kama uchafu,kuna ambayo ilikuwa imefungwa injini za Yamahama na Honda,pia ipo mitumbwi ambayo ilikuwa ya kawaida tu!.

Baada ya kufika hapo shemeji akawa amemuita jamaa mmoja wakaanza kuongea!.

Shemeji "Aisee nimewaongezea mvuvi"

Jamaa "Aaah ndo huyu bwana eeh!"

Shemeji "Eeeh bhana mfundisheni kazi ni shemeji yangu"

Jamaa "Sawa bosi wangu"

Nilibaki kuduwaa na kushangaa maana niliambiwa naenda kusimamia mitumbwi lakini baada ya kufika kibao kimebadilika na kuitwa mvuvi!.
Yan nimekua addicted na hii story kila saa nachungulia.
 
Muraaa hao mapongo wanakusetia mwanamke mweupe wakupuputishe mabawa yanayokupa kupaa na vituo, watakudakaa tu,
Hata Samson walimdaka ivo ivo
 
Nilibaki kuduwaa na kushangaa maana niliambiwa naenda kusimamia mitumbwi lakini baada ya kufika kibao kimebadilika na kuitwa mvuvi!.
 
Daaa! goroko77; mwenyewe huyooo!! hivi avatar hii ni wewe kwani??......km si wewe basi unajua kuchagua kweriii!
Kbsa Mkuu Kuna members njemba sinanifata pm wakidhani mm Ni manzi wkt huyo manz Ni mtoto wa kiongozi mmoja hapa nchini ambaye Bab ake Ni rfk ya familia yangu.

Ni rfk angu na amenipa tunda lake zuri kimasiara bas nikaamua kumuenzi ila watu wananifata pm kunitongozo mm ,mm nawachora tu wengijuwa mm Ni njemba mmoja HV wengiingia mitini tu[emoji3]
 
Back
Top Bottom