Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

ANGALIZO


Episode kadhaa zinazofuata zinaukakasi,uenda zikakuudhi na zikakukera!.

Naomba mniwie radhi maana hapa nasema kile nilichokipitia na huko nilishaacha muda mrefu,mimi kwasasa ni raia mwema kama mlivyo nyie,hivyo msinihukumu kwa yaliyopita!.

Nia na madhumuni ni kujifunza na kuwatahadharisha vijana wenzangu kuachana na maisha ya starehe ya muda mfupi.

Nawapenda sana.
Kuna vitu kwako vizuri nimevichukua sitavisema.
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 5.




Nilibaki kushangaa zile hela namna zilivyokuwa zimejaa kwenye lile begi!,kiukweli mate ya tamaa yalianza kunitoka ndani ya moyo!.Nilikuwa nipo tayari kusikia maelekezo atakayonipa ndugu Gabi ili niweze kuyafuata ilimradi tu niweze kujipatia zile hela!.Mawazo yangu kiukweli yalihama na kunichukua kuanza kufikiria vitu vya kijinga,nilitaka baada ya kuzipata hizo hela nikanunue mkoko(Gari) ili niende nikamdolishie dingi ajute kunikataa na kuniona sifai!.Kiukweli niliwaza ujinga sana.


Gabi "Sa sikia jamaa yangu"

Aliendelea "Hii ni pesa ya Tanzania lakini si halali"

Mimi "Si halali!,kivipi tena isiwe halali?"

Gabi "Yes!,swali zuri,ndiyo maana nimekutafuta wewe nikiamini unataka hela"

Mimi "Hakuna mtu asiyetaka hela kaka,we niambie nini nifanye"

Gabi "sawa,sasa humu ndani tupo watu watatu,yaani mimi,wewe pamoja na wife".

Aliendelea "Tulipoingia ndani nilimwambia wife afunge mlango ili isije ikatokea mtu akaingia ghafla kama anaingia chooni"

Gabi "Sidhani kama wewe ni mtoto baada ya hapa ukaanza kupayuka payuka kama mwendawazimu"

Aliendelea "Hizi ni hela bandia na ndiyo maana nimesema si halali"

Gabi "Mimi kukuleta hapa ni kwasababu nina muamini sana Mtatiro na tumeshapiga sana hizi mishe,sasa naomba mwanangu tukubaliane kwanza"

Baada ya jamaa kuniambia zile hela niza bandia,kiukweli nilibaki kushangaa kwasababu ulikuwa ukiziangalia zilikuwa zinaonekana kabisa ni pesa halali kwa matumizi na ilikuwa ni vigumu sana kuzitambua labda mpaka uwe mtaalamu wa hali ya juu.

Gabi "Sababu ya mimi kukwambia ni pesa bandia ni kukulinda wewe na sisi pia"

Aliendelea "Ningeweza kukwambia tu shika mzigo nenda kafanye moja mbili tatu halafu kila mtu akafa na chake,lakini nimeona wewe bado mgeni wa haya mambo na pengine ungedakwa ungewaleta hapa mapongo"

Mimi "Kaka siwezi kabisa kufanya huo upuuzi"

Gabi "Sa sikia Umughaka,kwenye kila elfu 10,wewe yako tano na sisi yetu ni tano"

Aliendelea "Sasa ni juu yako kuhakikisha kila mzigo nitakao kuwa nakupatia unamaliza ili uchukue chako na chetu tukipate!"

Mimi "Sawa kaka,kwahiyo niambie sasa nafanyaje"

Gabi "Mimi kila siku nitakuwa nakupatia shilingi laki moja,wewe ndiyo utahakikisha hiyo laki unaichenji unabaki na yako fyu(50) na sisi ya kwetu fyu".

Basi baada ya jamaa kuniambia vile ikabidi sasa akili ianze kukimbia fasta!,Jamaa alitaka kwenye ile laki moja atakayonipatia kila siku,nihakikishe naingia mtaani kuwashikisha wadau ili pesa yao iwe ni elfu hamsini na yangu pia iwe elfu hamsini,kwakifupi tuwe tunakula pasu kwa pasu!.Baada ya yale mazungumzo jamaa akanitia laki moja nikatia mfukoni akanipatia na nauli ya kunirudisha mpaka Sirari!.

Gabi "Ukiwa unamaliza mzigo utakuwa unanicheki kwenye simu,kama sipo nitakuwa nakujulisha ili ukija utamkuta shemeji yako utamuachia cha kwetu atakupatia mzigo mwingine"

Mimi "Haina noma kaka"

Basi nikaondoka zangu kurudi Sirari!,nikiwa njiani nikamtafuta Mtatiro kwenye simu kutaka kumfahamisha lile dili!.

Mtatiro "Mwanangu hilo dili lina hela kama ukituliza akili,cha muhimu ni kuwa na siri sana na pia jiamini usije kujishitukia shutikia"

Aliendelea "Mwanangu mi mbona nimefanya sana hiyo kazi na mshikaji,vitu vyangu vyote vya ndani ulivyoviona nimenunua kwa pesa ya mshikaji,ni dili tamu sana sema mshikaji kuna muda nae anapoteaga sana ndo maana nikaamua niingie kwenye hiace angalau niwe napata hela ya kula"

Aliendelea "Mimi nikirudi kama jamaa bado akiwepo tutaungana kaka"

Mimi "Kwahiyo Mtati wewe ulikuwa unafanyaje fanyaje mwanangu,nipe mbinu za kuzibadilisha"

Mtatiro "Jamaa amekwambia atakuwa anakugei kiasi gani?"

Mimi "Ameniambia kwenye kila elfu kumi,yangu tano na yake tano"

Mtatiro "Ni vile vile tu kama kwangu ilivyokuwa,sasa sikiliza wewe uwe unaingia madukani unanunua vocha ya buku,hiyo ni rahisi mno na kwa pale Sirari bado kuna wajinga wengi"

Mimi "Mbona kama buku ni nyingi sana kaka,au niwe nanunua tu ya jero!?"

Mtatiro "Vocha ya jero ni ngumu sana kupewa chenji na nirahisi kushituka ila ukinunua Vocha ya buku kwenye kila teni wewe utakuwa unachukua yako buku nne na jamaa unampelekea buku tano yake"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa,ngoja niingie kitaa"

Mtatiro "Kwani uko wapi sasa hivi?"

Mimi "Ndiyo natoka kwa mshikaji"

Mtatiro "Sawa mwanangu kapambane,uwe unanikumbuka angalau ka vocha"

Mimi "Haina noma"


Basi niliucahapa mwendo kuelekea barabarani ambapo nilikamata Hiace za kunipeleka mpaka mjini ili nikadandie vimchomoko vya washikaji nirudi Sirari!.Kwa wakati huo baada ya kupata umaarufu na kuwa mwenyeji pale Sirari,nilikuwaga silipi nauli kama nikitaka kwenda Tarime au kurudi Sirari,nilikuwa nadandia tu gari yoyote iliyokuwa ikielekea sehemu husika kwasababu nilikuwa nafahamika!.

Baada ya kufika pale Sirari siku hiyo niliamua kuendelea na kazi yangu ya upiga debe huku nikiendelea kusoma mazingira na namna ya kuifanya hiyo kazi yangu mpya.
Sasa siku iliyofuata nilichukua noti ya elfu kumi kati ya zile hela bandia na kuitazama vizuri,kwakweli ilikuwa ni ngumu sana kuijua kwasababu ilikuwa na kila kitu ambacho kilipatikana kwenye noti halali,utofauti ambao nao ulikuwa kwa mbali labda ilikuwa harufu tu!,zile hela ulikuwa ukizinusa kwa ukaribu sana zilikuwa na harufu fulani ya karatasi nyeupe(rim paper).

Nilichukua noti 3 ambazo zilikuwa elfu 30 nikaingia zangu pale stendi kupiga debe kama kawa!,sikutaka kabisa kuchenji zile hela kwa wadau wangu wa vimchomoko kwasababu niliona ningewaumiza wadau!.Sasa ilipofika mida ya saa 4 asubuhi nilielekea kwenye duka moja kubwa lililokuwa hapo jirani na mara nyingi tulikuwa tukinunua hapo bidhaa mbalimbali ikiwemo soda,nilipofika nilichomoa noti ya elfu 10 nikamwambia yule maza anipatie Coca baridi,bila tatizo yule Maza aliikamata ile hela akaitia kwenye droo kisha akafungua friji akanipatia soda niliyoiomba!.

Maza "Umughaka utafata chenji bhana sina chenji asubuhi hii"

Mimi "Haina tatizo"

Baada ya kuichukua ile hela nilifurahi kimoyo moyo huku nikijisemea siku zote jamaa alikuwa wapi!.Basi nilihakikisha siku ile zile noti mbili zilizokuwa mfukoni ninahakikisha nazimaliza na ndivyo ilivyokuwa!. Ile kazi kiukweli niliifanya bila mtu yeyote kushitukia kabisa,sasa kuna muda nilikuwa namkamata mwana yeyote pale kijiweni nampiga liteni namwambia akanunue soda,moja yangu na moja yake,bila kujua unakuta muhuni anafurahi anaenda kununua huku akikimbia!.Uzuri wa pale kijiweni tulikuwa tukiishi kama ndugu,hivyo ukimpatia muhuni hela akanunue eidha soda au fegi anaona unamjali kinoma.

Kiukweli ndani ya mwezi mmoja baada ya kuifanya ile kazi maisha yangu nayo yalianza kubadilika,niliamua kuhama kwenye kile chumba nilichokuwa nina kaa mara ya kwanza ambacho nilikuwa nalipia elfu 15 kwa mwezi,nikaamua kwenda kupanga chumba na sebule,ambavyo nilikuwa nalipia elfu 50 kwa vyote viwili!.

Kazi ile ilikuwa tamu sana na nzuri na ule ukonda kiukweli nilikuwa nazugia tu!.

Ndani kwangu kulianza kubadilika baada ya kununua makochi ya kawaida,nilinunua kapeti nikatandika chini,baadae pia nikanunua subwoofer na TV,nilihakikisha najijenga na kujipanga kama kijana.

Baada ya pesa kunizidi nilianza kujichanganya na wanangu tukawa watu wa viwanja vya starehe pale Sirari,ule mji japo ulikuwa ni mdogo lakini ulikuwa na vistarehe uchwara vilivyokonga nyoyo!.Kipindi hicho ndipo sasa na mimi nikajifunza kunywa pombe huku bia yangu pendwa ikiwa ndovu lager!.Baada kupiga kazi ile ya magumashi kwa miezi 3,jamaa aliniambia mzigo umeisha na ataondoka kwenda Arusha na haitochukua mwezi atakuwa amerudi ili tuendeleze libeneke.
Hatari lakini salama.

#MaendeleoHayanaChama
 
Vitu viwili vya kufikirisha;
1. Siku zote nimekaa pale Sorari sikuwa na demu wala sikuwahi kwenda kulala na demu guest na pale nilopopanga sikuwahi kuleta demu. Inawezekanaje mwanaume kukaa muda wote huo bila kupiga demu?

2. Mwanangu Nyamori aliniambia nishuke hapo Bunda kuna kijiji kuna mgodi unatema sana madini, baada ya kufika huyo huyo Nyamori anamuambia hapa hakuna kitu tunapoteza tu muda.
Inawezekana mkuu,mi nilishakaa geto Moshi miaka 3 sikuwahi kuleta demu na wala sikuwa na demu moshi,kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 nikiwa na umri zaidi ya miaka 21 ,inawezekana sana,mara nyingi mi nilikua naweza kukaa hata miezi 8 sijakutana na demu
 
Back
Top Bottom