Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Kumbe Ndiomana ulisema ngono si kipaumbele Chako kabisa...ulipata somo toka kwa rafiki zaidi ya Ndugu.
Pole yake sana mtatiro natumae bado yu hai kama alizingatia ushauri wa daktare!
Alipotuambia kuwa ngono sio kipaumbele kwake, bado alikuwa hajajua status ya Mtatiro.........mambo hayo sio ya kujifunza kutoka kwa mtu, bali ni tabia na hulka ya mhusika. Unaweza kumwona mtu aliyeathirika na mambo haya, ukajiapiza kuwa hutokuja kufanya upuuzi huo, lakini akili ya binadamu imeumbwa kusahau. Utajikuta baada ya muda kupita unarudia kufanya jambo ulilolikataa hapo awali.
 
Alipotuambia kuwa ngono sio kipaumbele kwake, bado alikuwa hajajua status ya Mtatiro.........mambo hayo sio ya kujifunza kutoka kwa mtu, bali ni tabia na hulka ya mhusika. Unaweza kumwona mtu aliyeathirika na mambo haya, ukajiapiza kuwa hutokuja kufanya upuuzi huo, lakini akili ya binadamu imeumbwa kusahau. Utajikuta baada ya muda kupita unarudia kufanya jambo ulilolikataa hapo awali.
Ni kweli mkuu sema hapa tunachangamsha genge tu vingine usivitilie maanani kiivo 🙃! Ajali kazini but kuna cha kuendelea kujifunza pia!!
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 24.



Kamange ndiye aliyekuwa dereva kwenye ile Noah na mara zote alikuwaga hana kabisa stori na mtu!.Tulifanikiwa kufika Geita salama kabisa mida ya saa 6 usiku tukipitia njia ya Kahama,kwa mujibu wa malekezo ya Jipe ni kwamba,endapo tungepitia Kigongo/Busisi yawezekana kabisa tungeweza kugundulika kwenye ukaguzi,hivyo kwakuwa hatukuwa na haraka,jamaa akasema tupitie Kahama.

Baada ya kufika Geita usiku huo,aliyekuwa akituelekeza mahali pa kwenda alikuwa ni Jipe ambaye yawezekana aliifahamu vizuri ile mitaa ya Geita na viunga vyake,binafsi ukiacha siku tuliyoenda na Mtatiro kwenye mnada wa kuuza mitumba huko kwenye kijiji cha Nzera,sikuwahi tena kufika Geita hadi siku hiyo.Sasa Jipe alikuwa akimpatia yule demu dereva maelekezo namna ya kuifata njia yenye uelekeo sahihi wa kutufikisha tunakokwenda!.Haukupita muda tukawa tumefika kwenye nyumba ambayo haikuwa na fensi wala geti,sasa ile nyumba ilikuwa mbali kidogo kutokea pale mjini!.

Mimi,Mtatiro na Jipe tuliteremka wakati huo huo Gabi na Yule demu waliondoka na gari wakaahidi wangerudi kesho asubuhi!.Jipe alianza kugonga mlango wa ile nyumba hatimae mwenyeji akawa amefungua mlango.

Jipe "wachamawe sengi"

Yule mama "Wachatata"

Jipe "Mwasibhao"

Yule "Chasibhao lata,jendeyo"

Jipe "Ni jakisi sengi"


Jipe alinyanyua lile begi ambalo lilikuwa na silaha kwa chini na juu likiwa na nguo baadhi tukawa tumeingia ndani.

Jipe "Aisee huyu ni Shangazi yangu anaishi hapa Geita ni mwalimu,hivyo jisikieni huru"

Aliendelea "Shangazi,hawa ndiyo wale marafiki zangu ambao nilikwambia tunapita kulala hapa halafu kesho tunaelekea Nyarugusu"

Yule mama "Sawa baba,hapa ni kwenu,usijali"

Aliendelea "Mtalala kwenye hicho chumba wanangu"

Yule mama baada ya maongezi ya dakika kadhaa alituacha pale sebuleni akawa ameingia chumbani kwake kulala.

Jipe "Twendeni tukapige mbonji wazee"


Basi tuliingia chumbani tukawa kulala hadi asubuhi,ilipofika asubuhi Jipe aliamka akawa ameondoka pale kwa shangazi yake na akatutaka tusitoke hadi ile gari itakapokuja kutuchukua.Wakati tukiwa hapo kwa huyo mama,Mtatiro alianza kuniambia anajisikia vibaya sana na hali yake si nzuri!.

Mimi "Shida ni nini kwani?"

Mtatiro "Yaani nahisi tu baridi na najisikia kizinguzungu!"

Aliendelea "Ila niko poa wala usijali"

Mimi "Au nikakuchukulie panadol"

Mtatiro "Ngoja jamaa arudi umwambie"

Baada ya muda Jipe alirudi akatutaka tukapande gari tuondoke zetu,nilijaribu kumshirikisha hali ya mshikaji wangu Mtatiro akaniambia watamnunulia dawa tukifika tulikopaswa kwenda!.Tulipotoka nje,yule mama hatukumkuta bali tuliwakuta mabinti wawili wakubwa wakiwa wanaendelea na shughuli zao.

Jipe "Mi naondoka,mtamwambia Shangazi nitarudi"

Binti "Sawa kaka"


Tuliondoka na kushika njia kama tunarudi Mwanza,kuna mahali tulifika tukaikamata barabara ya vumbi iliyokuwa inatutoa nje ya ule mji wa Geita,baada ya kutembea kwa umbali mrefu kidogo hatimaye tukafika kwenye nyumba moja iliyokuwa na tofauli za kuchoma,ambapo Jipe alishuka akaenda kufungua ile nyumba kisha akatutaka tuteremke na kuingia ndani!.Baada ya kufika ndani Jipe akaanza kutoa maelekezo kwa kila mmoja!.

Jipe "Jamani hapa ndipo tutakaa mpaka usiku wa leo,na tukimaliza kufanya kilichotuleta tunaondoka leoleo!"

Aliendelea "Gabi nadhani nenda nilikokwambia"

Jipe "Kamange hakikisha hiyo gari ni nzima,kama kuna tatizo ipeleke gereji muda huu!"

Kamange "Gari inawasubiri nyinyi tu!"

Jipe "Ok,sawa"

Jipe alitoa hela kidogo akawa amempa yule demu aende pharmacy akamnunulie Mtatiro Panadol ili kuondoa ile hali ya sintofahamu aliyokuwa nayo.Sasa kwakuwa ile nyumba ilikuwa na vyombo vya kupikia,Jipe alishauri zikanunuliwe dagaa na unga tuje tukorofishe ili tuweze kupata chakula,na hivyo ndivyo tulivyofanya.Ilipofika mida ya Saa 1 usiku hali Mtatiro ilizidi kuwa mbaya hata baada ya kumeza vidonge,yeye kwa maelezo yake alikuwa akidai anaihisi baridi na kujisikia vibaya mwili mzima.

Jipe "Kwahiyo sa itakuwaje mwanangu"

Aliendelea "Chuma utaweza kushika?"

Mtatiro "Kwani tunaondoka sa hivi?"

Jipe "Mida inakaribia"

Mtatiro "Ngoja tuone"

Sasa ilipofika mida ya saa 4 usiku kuelekea saa 5,Jipe baada ya kuona hali ya Mtatiro haikuwa ya kuridhisha Jipe alinipatia maelekezo!.

Jipe "Umughaka utashika chuma ya Mtatiro"

Mimi "Sawa"

Jipe "Usifanye tofauti na nitakachokwambia"

Mimi "Sawa"

Baada ya nusu saa tukiwa tupo tayari kuondoka,simu ya Jipe ilikuwa ikiita,jamaa aliipokea akaanza kuzungumza. Aliyekuwa amepiga ile simu alikuwa Gabi ambaye yaelekea alikuwa akimpatia maelekezo Jipe.

Jipe "Kamange yuko wapi?"

Mimi "Nadhani atakuwa kwenye gari!"

Jipe "Twendeni"

Aliendelea "Tukitoka huko ni kuondoka tu kurudi Mwanza,hatuna muda wa kupoteza!"

Baada ya kutoka nje ya ile nyumba,Jipe alifunga kofuli kisha ufunguo akauweka juu ya mlango kwenye venti.Tuliondoka lile eneo kuelekea ambako walikuwa wakipafahamu Jipe na Gabi,sisi wengine ilikuwa ni wafuata maelekezo tu.Haukupita muda tukawa tumefika kwenye nyumba zilizokuwa mtaa wa kifahari kweli kweli.

Jipe "Umughaka ile nyumba yenye geti jeusi unaiona?"

Mimi "Ile ya mbele?"

Jipe "Ukiacha hiyo yenye paa refu,ile yenye geti jeusi siunaiona?"

Mimi "Ndiyo"

Jipe "Ok,hakikisha ukifika wewe gonga na wakiuliza nani waambie mimi respis geti,wakifungua tu hiyo kazi nyingine niachie mimi!"

Aliendelea "Kamange nyuma ya hii nyumba kuna njia isiyo rasmi,nenda kapaki hapo tunakukuta"

Kamange "Gabi yuko wapi?"

Jipe "Tutamkuta mbele"

Kamange "Mjulishe kabisa akae standby,sitaki lawama"


Mimi na jipe tulitelemka kwenye ile Noah huku tukiwaacha Kamange na Mtatiro ambaye hali yake haikuwa nzuri.Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuikamata silaha na kiukweli ilikuwa nzito kwa kiasi chake.

Nilichukua kitambaa cha kiujifunika nikakiweka mfukoni huku ile silaha nikiwa nimeiweka kwenye ndani ya koti.Nilipofika kwenye lile geti nilianza kugonga kwa nguvu mara kadhaa!.Wakati nilipokuwa nikigonga lile geti Jipe alikuwa pembeni huku akiwa makini sana.

Sauti ya mwanaume "Naniii !?"

Mimi "Mimi Respis"

Sauti "Nakuja"

Haukupita sekunde 20 lile geti lilifunguliwa kisehemu kidogo kile ch a watu kupita.Geti lilipofunguliwa tu Jipe alisukuma kwa nguvu huku akitoa silaha na kumuonyeshea yule jamaa.Jamaa alitaka kupiga kelele lakini Jipe alimdhibiti akamwambia akipiga kelele atamuua!.

Jipe "Ingia ndani fasta na ufunge hilo geti!"


Jipe alimchukua yule jamaa akiiingia nae ndani huku na mimi nikiwa nyuma nimeshika ile silaha iliyokuwa imenipatia kiburi kisichokua cha kawaida.

Jipe "Kaka yako yuko wapi?"

Yule jamaa "Braza amesafiri"

Jipe "Upo na nani humu ndani?"

Jamaa "Nipo na shemeji yangu pamoja na mdogo wake"

Jipe "Umughaka kaa tayari kwa lolote,ukiona hatari ruksa kuua"

Mimi "Sawa"

Jipe alimchukua yule jamaa ambaye alikuwa akitetemeka kama kashikwa na degedege kisa kuona ile SMG,baada ya muda Jipe alirudi na watu watatu pale sebuleni huku yule mwanamke akiwa ndani ya chupi tu.Alikuwa mwanamke,yule jamaa aliyetufungulia geti pamoja na dogo mmoja wa kiume ambaye kimuonekano alikuwa na miaka 12.

Jipe " Laleni chini mfunike sura zenu"

Aliendelea "wewe mume wako yuko wapi"

Mwanamke "Amesafiri"

Jipe "Kwenda wapi?"

Mwanamke "Ameenda Dar"

Jipe "Nataka pesa,ziko wapi?"

Mwanamke "pesa huwa tunapeleka benki,tafadhali msinifanye chochote twendeni benki nikawapatie"

Jipe "Wewe nitakupasua ubongo,nahitaji pesa wewe unaleta ujinga!"

Mwanamke "Hapa kipo kiasi kidogo,tafadhali usiniue"

Yule mwanamke alikuwa anaongea huku machozi yakimtoka kama mvua,wakati fulani huruma ilikuwa ikiniingia lakini sikuwa na namna!.

Jipe "Zipo shilingi ngapi wewe acha kutupotezea muda!"

Kabla mwanamke hajajibu swali,Jipe alimnyanyua akawa amerudi nae huko chumbani,wakati huo mimi pale sebuleni niliendelea kuwachunga wale madogo huku silaha ikiwa tayari kwa lolote.Baada ya muda Jipe alirudi pale sebuleni akiwa na kanga iliyokuwa imejaa pesa,ile kanga namna ilivyokuwa imefungwa ni kama furushi la nguo chafu.

Jipe aliwaambia wale madogo wasimame wote na tulielekea chumbani ambako aliwaambia waingie chini ya uvungu kisha akafunga mlango kwa nje na funguo.

Baada ya hapo tuliingia kwenye kile chumba cha yule mwanamke na kupekua kika mahali lakini hatukupata pesa nyingine.

Jipe "Ingia chini ya uvungu,ole wako upige kelele ndipo utajua mimi ni nan!"

Yule mwanamke aliingia chini ya uvungu kama kafukuzwa,ndipo jipe alichukua funguo akafunga mlango kwa nje akaniambia tusepe.Tulitoka ndani haraka kuifata ile Noah iliyokuwa imepaki nyuma ya ile nyumba,tuliingia ndani na kuondoka haraka sana lile eneo.

Baada ya mwendo mrefu kidogo huku tukiiacha Geita,kuna mahali tulifika Jipe akamwambia yule demu asimamishe gari.Jipe alitoa simu akaanza kupiga.

Jipe "Uko maeneo gani wewe?"

Aliendelea "Subiri hapo njiani tumekaribia"

Sasa kumbe alikuwa amempigia Gabi akitaka kujua yupo maeneo gani.Baada ya mwendo ambao haukuzidi dakika 3 tulimuona Gabi akiwa barabarani ndipo gari ikasimama akapanda tukaondoka zetu.

Jipe "Umefanikisha"

Gabi "Kama kawa"

Sikuelewa ni kitu gani ambacho Gabi alikuwa akikifanya muda huo huko alipokuwa,hiyo ilibaki ni siri yake yeye na Jipe.

Tulifanikiwa kufika Mwanza saa 11 alfajiri ambako moja kwa moja tulipitiliza hadi kwenye ile nyumba ambayo ndipo yalikuwa makazi yetu ya mipango mikakati. Ilipofika mida ya saa 2 asubuhi,Jipe alitupatia kila mmoja wetu mimi na Mtatiro laki 5,sikufahamu wale wengine walipewa kiasi gani maana sisi tuliondoka zetu.

Kiukweli ile pesa iliyokuwa imefungwa kwenye ile kanga sikufahamu ilikuwa kiasi gani maana kule Geita hatukuwa na muda wa kuhesabu,na hata tulivyofika hapo kwenye hiyo nyumba,Jipe na Gabi waliingia chumbani na lile furushi!.


Mtatiro "Hawa wasenge ngoja uje uone"

Mimi "Kwanini?"

Mtatiro "Wewe unaona makubaliano yetu yanatekelezwa?"

Aliendelea "Hawanijui vizuri,siwezi kuweka roho yangu rehani halafu unilipe laki 5"


Ile hela Mtatiro aliniambia tuiweke kwenye mtaji wa mitumba ili tuzidi kuizungusha .Sasa nakumbuka siku moja tukiwa pale Hungumahlwa kwenye harakati za kupambana na mitumba,ghafla hali ya mshikaji wangu mtatiro ilibadilika na akaniambia yeye inabidi arudi nyumbani akatafute dawa ameze ili hali itengemae,tulikubaliana tungeonana nyumbani!.

Ilipofika mida ya saa 8 mchana nilipigiwa simu,nilipotoa ile simu mfukoni nikakuta ilikuwa namba ya Mtatiro akinipigia,lakini baada ya kupokea nikakuta si yeye akiongea!.

Sauti "Hallo!"

Mimi "Hallo"

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga nikaenda kuupakia kwenye fuso ambalo mara zote tulikuwaga tukipakia mizigo yetu kisha nikampatia dereva maagizo mahali pa kwenda kuushusha.Niliondoka hapo Hungumalwa na nikafanikiwa kufika Bugando mida ya saa 11 jioni.Sasa nilipofika niliipiga ile namba ya Mtatiro na hatimae ikapokelewa na yule yule mtu aliyekuwa amenipigia,alinielekeza mahali alipokuwa ndipo nikamfuata.Kumbe yule mtu alikuwa ni daktari na alitaka kunipatia taarifa ya Mtatiro.
Kiukweli nilianza kuingiwa na hofu sana kwasababu Mshikaji wangu Mtatiro aliondoka akiwa anajiweza kutembea sasa sikujia ni kitu gani kilikuwa kimempata.

Niliingia hadi kwenye chumba alichokuwa ameniambia niingie,nilipoingia nilimkuta Mtatiro pia yupo akiwa amekaa kwenye kiti,baada ya kumuona Mtatiro pale kwenye kiti angalau moyo wangu ulitulia.

Jamaa(Daktari) "Mambo vipi kaka"

Mimi "Safi kabisa kaka"

Jamaa "Karibu kiti kiti"

Aliendelea "Bila shaka huyu unamfahamu"

Mimi "Ndiyo"

Jamaa "Ni nani yako?"

Mimi "Ni rafiki zaidi ya ndugu"

Jamaa "Kwahiyo mnaaminiana?"

Mimi "Ndiyo"

Jamaa "Sasa mimi nimekuita hapa kwa ridhaa ya huyu ndugu yako,maana nilimwambia aniitie ndugu yake wa karibu ndipo akasema nikutafute wewe,bila shaka hali yake unaiona"

Aliendelea "Amewahi kukwambia kinachomsibu?"

Mimi "Hapana kwakweli"

Jamaa "Sawa,Bwana Mtatiro,ni vema rafiki yako akafahamu kinachokusibu atakuwa msaada kwako kama hutojali!"

Mtatiro "Haina tatizo dokta wewe mwambie huyu ni rafiki yangu tunapendana na kuheshimiana!"

Jamaa "Sawa,sasa bwana mimi nimekuita hapa kwa ajili ya huyu ndugu yako,ndugu yako ni muathirika wa virusi vya Ukimwi na kama ulivyoutaratibu mgonjwa anapopimwa na kugundulika na hilo tatizo huwa tunamuanzishia utaratibu wa kuanza matibabu"

Aliendelea "Ndugu yako huyu alianza dozi kama kawaida lakini kuna muda huwa anategea sana kuja kuchukua dawa mara zile tulizompa zinapokwisha,hivyo inamuondolea ufanisi wa afya yake,pia kwakuwa wewe upo hapa naomba uwe unamshauri asiwe mtu wa kunywa sana pombe,si nzuri kwa afya yake!"

Niliendelea kumsikiliza yule daktari kwa makini wakati huo moyo wangu ulikuwa unauma sana,sikutaka kuonyesha hadharani pengine ningemfanya mshikaji wangu aliyekuwa akiniamini Mtatiro ajisikie vibaya,nilikuwa makini sana ili nisije kuleta sintofahamu!.

Jamaa "Sasa naomba hizi dawa nazompatia hapa,hakikisha kila siku anameza kwa masaa yale yale atakayojipangia yeye ili kuweza kumjengea kinga imara dhibi ya mashambulizi nyemelezi"

Aliendelea "Naomba umsimamie awe anameza dawa kila siku na kama nimivyokwambia umshauri aache pombe,pia azingatie lishe bora!"


Baada ya mazungumzo tulitoka nje na Kuondoka zetu nyumbani,nilikuwa namlaumu sana rafiki yangu Mtatiro kwanini aliacha kuzingatia dawa wakati alilifahamu tatizo lililokuwa likimkabili,kiukweli sikumuonyesha chuki bali nilimpenda sana rafiki yangu na nilitaka afanye vema zaidi ili afya yake iendelee kuimarika.Sikumbagua bali niliendelea kumshauri na kumfanya awe na furaha muda wote kama rafiki yangu.


Itaendelea.............
UKO KWENYE GENGE LA UJAMBAZI, UMETOKA KUFANYA UJAMBAZI. UNAPIGIWA SIMU NA MTU HUMJUI (ingawa alitumia simu ya mtu wako) ANAKUAMBIA UJE SEHEMU FULANI, UNAFUNGA HARAKA BIASHARA NA KUJIPELEKA..[emoji38][emoji38].

INAWEZEKANA HUYO MTATIRO KAKAMATWA NA AMEBANWA ATAJE WASHIRIKA WAKE WA UJAMBAZI, UMUGHAKA UNAJIPELEKA!!!!! JAMBAZI HAWEZI KUWA NA AKILI YA HOVYO HIVI.

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga
 
UKO KWENYE GENGE LA UJAMBAZI, UMETOKA KUFANYA UJAMBAZI. UNAPIGIWA SIMU NA MTU HUMJUI (ingawa alitumia simu ya mtu wako) ANAKUAMBIA UJE SEHEMU FULANI, UNAFUNGA HARAKA BIASHARA NA KUJIPELEKA..[emoji38][emoji38].

INAWEZEKANA HUYO MTATIRO KAKAMATWA NA AMEBANWA ATAJE WASHIRIKA WAKE WA UJAMBAZI, UMUGHAKA UNAJIPELEKA!!!!! JAMBAZI HAWEZI KUWA NA AKILI YA HOVYO HIVI.

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga
Sasa huyu si Ni jambazi mwanafunzi?? Atapata huo ujanja kadri anavyokutana na mabalaa Kama kukamatwa kwa mtego Kama huo!!!
 
UKO KWENYE GENGE LA UJAMBAZI, UMETOKA KUFANYA UJAMBAZI. UNAPIGIWA SIMU NA MTU HUMJUI (ingawa alitumia simu ya mtu wako) ANAKUAMBIA UJE SEHEMU FULANI, UNAFUNGA HARAKA BIASHARA NA KUJIPELEKA..[emoji38][emoji38].

INAWEZEKANA HUYO MTATIRO KAKAMATWA NA AMEBANWA ATAJE WASHIRIKA WAKE WA UJAMBAZI, UMUGHAKA UNAJIPELEKA!!!!! JAMBAZI HAWEZI KUWA NA AKILI YA HOVYO HIVI.

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga
askari gani smart,atumie simu ya rafiki yako kukupigia kwa sauti yake?lazima angemwambia mtatiro ndo apige,kama kwa yule dada wa pesa za bandia,kule musoma alipiga yeye kumwita umughaka,na akaenda.
 
UKO KWENYE GENGE LA UJAMBAZI, UMETOKA KUFANYA UJAMBAZI. UNAPIGIWA SIMU NA MTU HUMJUI (ingawa alitumia simu ya mtu wako) ANAKUAMBIA UJE SEHEMU FULANI, UNAFUNGA HARAKA BIASHARA NA KUJIPELEKA..[emoji38][emoji38].

INAWEZEKANA HUYO MTATIRO KAKAMATWA NA AMEBANWA ATAJE WASHIRIKA WAKE WA UJAMBAZI, UMUGHAKA UNAJIPELEKA!!!!! JAMBAZI HAWEZI KUWA NA AKILI YA HOVYO HIVI.

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga
Sasa mtu ameachana na rafiki yake akiwa anaumwa na simu imepigwa kutokea Bugando Hospital, logically alishajua jamaa yake Mtatiro amezidiwa.
 
Back
Top Bottom