Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Majambazi Jipe na Gabi wanawasiliana kwa simu muda mfupi kabla ya tukio.Wakati tukio la mwanzo akina Mtatiro waliacha simu Chuga wakaenda Kahama kufanya tukio!Sheria za genge lao zinabadilikabadilika au mwandishi anakosa consistency?Majambazi smart wa matukio kama hayo hawatumii masimu kwenye tukio bhana.....
 
Umughaka, unakipaji kikubwa sana, hadithi imekidhi vigezo kwa kugusa nyanja mbalimbali za maisha yetu.

Nimeburudika, nimejifunza na kuelimika. Barikiwa sana sana!
Binafs kuna wakat natulia kmya nikizisoma episode na comment za mateja wenzangu licha ya kua nlitakiwa niwe natimiza baadhi ya majukum ya uingizaji wa kpato cha familia lkn ata sijali UMUGHAKA anatosha kwa sasa
 
UKO KWENYE GENGE LA UJAMBAZI, UMETOKA KUFANYA UJAMBAZI. UNAPIGIWA SIMU NA MTU HUMJUI (ingawa alitumia simu ya mtu wako) ANAKUAMBIA UJE SEHEMU FULANI, UNAFUNGA HARAKA BIASHARA NA KUJIPELEKA..[emoji38][emoji38].

INAWEZEKANA HUYO MTATIRO KAKAMATWA NA AMEBANWA ATAJE WASHIRIKA WAKE WA UJAMBAZI, UMUGHAKA UNAJIPELEKA!!!!! JAMBAZI HAWEZI KUWA NA AKILI YA HOVYO HIVI.

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga

Majambazi Jipe na Gabi wanawasiliana kwa simu muda mfupi kabla ya tukio.Wakati tukio la mwanzo akina Mtatiro waliacha simu Chuga wakaenda Kahama kufanya tukio!Sheria za genge lao zinabadilikabadilika au mwandishi anakosa consistency?Majambazi smart wa matukio kama hayo hawatumii masimu kwenye tukio bhana.....
Huu ndio ujuaji wa kijinga kila mda tunauzungumzia. Mbona mnajikuta ma-director sana kwenye kibwebwe kisicho wahusu. Mkiona ana puyanga si mkae muandike za kwenu kisha mziweke vile mnavyotaka ziwe?

Kwenye mtiririko wa story ake kuna mahala aliposema ye ni Jambazi konki? Kuna chuo amekwambia au amesimulia kua alienda kusomea ujambazi hivo keshakua Pro so hakupaswa kufanya mistake alizofanya?

Na namna mnavyoziona hizo mistake za kihalifu so mnataka kutushawishi tuone kua nyie ndio mijambazi mlio kubuhu so mnazijua mbinu zote au vp?

Waswahili tuna shida gani lakini? Mnachowashwa kitu gani kwani? Kama story mnaona ina chai nyingi si mpite tu kule kimya kimya 🤣...

Em acheni ujuha wa kipumbafu, kaandikeni zenu basi zilizo 100% perfect. Mnaboa sana! Huo ujuaji wenu em uwekeni kwenye maisha yenu ya kila siku yawe perfect ili msikae jukwaani mnasubiri story za uongo!

Mijitu mizima ya hovyo kabisa, wakati wengine wanasoma kujiburudisha yenyewe yanasoma kutafuta makosa utafikiri yanafanya udahili wa waandishi. Hivi na huko mtaani kwenu mnaishije na jamii zenu watu wa aina yenu mmh?
 
Ndugu Asante. Mbona sometimes mtu anaweza kuwa great thinker bila kutoa neno.
 
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane!

Kwenye haya maisha kuna wakati huwa ninakaa chini na kusema "Kama sikufa kipindi kile,basi siwezi kufa mpaka Mungu atakaporuhusu"

Nadhani wengi mtakumbuka ni siku chache tu zimepita nimeandika kisa cha maisha ambayo nilikutana nayo wakati nikiwa nimekwenda kumsalimia baba yangu mdogo akiwa ni Headmaster, maisha yale yalikuwa ya kawaida ila washirikina walifanya tukakosa amani.

Sasa baada ya hapo nilifaulu vizuri tu kuelekea shule ya upili(advance)na nikapangiwa huko Tanga kwa mchepuo wa Sayansi wenye combination PCB.

Hali yangu ya maisha ya shule kiukweli ilikuwa mbaya sana mpaka nikajuta kwanini nilichukua hiyo combination, siyo kwamba sikuwa na akili, la hasha!, akili ilikuwepo ya kutosha kwasababu nilifaulu kwenda advance kwa divisheni 2, ni combination iliyohitaji kupiga msuli kana kwamba umetumwa na kijiji, haikutaka mchezo wala kujisahau hata kidogo,sasa mimi nilipofika huko nikajikuta naungana na makundi na kujanjaruka kuwashinda hata niliyowakuta!.

Mkurya mimi kutoka wilayani Tarime kijiji cha Mogabiri nikajikuta nazamia kwenye dimbwi la mapenzi ya mtoto wa kitanga ambaye alifanya hata kusoma nikaacha nikawa namuwaza yeye na utamu wa papuchi yake!.

(Shamima popote ulipo ulaaniwe mbwa wewe kwa kuniharibia maisha[emoji23][emoji23]). All in all ni kwamba napambana na maisha yanasonga japo ni kibishi!. Sasa haya ya kwanini nilifeli nadhani kwa leo si mahala pake,nitawaeleza tu kilichofuata baada ya mimi kufeli shule!.

Kiasili mimi ni mkurya kutokea wilaya ya Tarime huko kijijini Mogabiri,ingawa hatukuishi sana hapo kijijini lakini ndipo chimbuko letu lilipo hapo, kwa pale Tarime mjini nyumbani kwetu ni Rebu.Pia tunao ndugu wengi tu waliotapakaa karibu kila kona ya hii nchi!, hapa Dar es salaam wamejaa ila wanajifanya kama hawanioni vile! (Maisha ya sikuhizi yamekuwa yakipumbavu sana).Kwakuwa wanajifanya kukausha na mimi pia napiga mikausho ya hatari!,sitaki kumgasi mtu!.

Basi bana, nakumbuka ile nimemaliza skonga nikawa nashangaa shangaa pale nyumbani kusubiri tokeo la kuelekea chuo, sasa nilifahamu kabisa siwezi kufaulu kwa kile nilichokifanya kule skonga, Mzee yeye aliamini toto lake limemaliza shule na anajivunia kwasababu nilikuwa nina akili,hakuelewa kabisa kwamba baada ya kufika shule nilijanjaruka kuwazidi hata niliowakuta!. Baada ya matokeo kutoka na ikaonekana nimepata divesheni zero, mimi kwa upande wangu sikushituka ila Mzee alihamaki sana na kushangaa nilipatwa na nini hadi nifeli!.

Tangu nimeanza darasa la kwanza hadi darasa la saba, sikuwahi kuvuka namba 5,ingawaje sikuwahi kuwa namba 1 lakini nilikuwa nacheza kwenye namba 2-4. Nilipofika form 1 hadi form 4 wembe ukawa uleule! nashika namba 3 -5,sasa hadi nafaulu kuingia advance Mzee wangu hakushangaa maana alifahamu kabisa toto lake nilikuwa nina akili!

Mzee wangu kiukweli alikuwa mkali mno na ilikuwa ikitokea nimefanya kosa akanikamata, kiukweli nilikuwaga naimba Haleluya!.Yeye alikuwaga achapi kwa fimbo za miti ya kawaida,bali alikuwa anachapa kwa nyaya ya umeme! Aisee usiombe kukutwa!

Kuna muda nilikuwa nikifahamu nimefanya kosa siku hiyo najiwahisha kuoga na kuingia kulala na kujifanya naumwa! Sasa akija akikushika shingoni kama anakupima joto akakuta huna joto,aisee utaomba ardhi ipasuke ikumeze ili ikuepushe na kipigo kisichokuua ila chenye kukufanya ukajuta kwanini ulizaliwa!.

Kutokana na kutokuridhika kwa mzee na yale matokeo, kuna siku kadhaa sikumuona pale nyumbani nikajua uenda atakuwa kwenye mambo yake, sasa kumbe mzee amesafiri hadi Tanga kwenda kuonana na Headmaster kufahamu mwanae ni kwanini nimefeli kiasi kile na wenzangu kufaulu!

Alichoamini mzee ni kwamba sikustahili kufeli na nilipaswa nifaulu!. Ule mpango wa yeye kwenda Tanga kumbe hadi Maza nae alikuwa akifahamu ila aliamua kula buyu ili ukweli ufahamike! Mama yangu alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na yeye peke yake ndiye shida zangu zote nilikuwaga nikimwambia!.Ila safari hii na yeye aliukaza uso wake na hakutaka kabisa kucheka na kima!

Mwanaume niliendelea kujinafasi na kujimwayamwaya kwa kipindi kile kifupi ambacho mzee hakuwepo nikiamini atakuwa ameenda kwenye shughuli zake, akili yangu iliamini kwasababu mzee wangu alikuwa akinimini basi angenipatia mtaji ili nianze biashara!.

Baada ya kama siku 5 mzee alirejea, sasa tukiwa tunapata chakula usiku alikuwa akiniangalia kwa jazba sana, sikuwa na tatizo nae kwasababu niliamini yeye kuwaga na hasira za karibu ndiyo ilikuwa kawaida yake!. Sasa ile naendelea kula sijui ili wala lile,nilishitukia amenipiga kofi ambalo lilifanya kuanza kuona maluweluwe!.

Mama "Tatigha omwana araghere!"(Muache mtoto ale)

Mzee "Amos hebu niletee waya hapo chumbani"

Sasa mdogo wangu aitwaye Amos akaagizwa waya akachukue waya ili viboko vichukue nafasi!.

Mzee "Leo nakuua mbwa wewe"

Kiukweli siku hiyo nilijua kabisa nakufa maana mzee wangu alikuwaga hana masikhara kabisa na maneno yake! Basi mama alikuwa akijaribu kumtuliza mzee lakini bado ikashindikana, kwa wakati huo sikuelewa kabisa ni kitu gani kilimsibu mzee wangu ambaye alikuwa amerejea kutoka huko alikokuwa ameenda!

Mzee alinyanyuka akatoka akaenda ndani ambako sikufahamu alikwenda kufanya nini,wakati huo kiukweli hata chakula sikuwa na hamu nacho tena kwasababu mabanzi na makwenzi niliyokuwa nimechezea yaliniharibia mudi kabisa!.Baada ya mzee kutoka chumbani alikuja na kamba ya katani akanisogelea akanifunga na kunibana miguu kana kwamba anataka kuchinja kuku.

Sasa akauchukua ule waya uliyoletwa na dogo nikaanza kuchezea stiki! kiukweli nilipigika sana!. Baada ya kuona ameniadhibu vya kutosha alinilaza kifudi fudi wakati huo kanifunga mikono kwa nyuma kama vile jambazi au mwizi amepigwa pingu.

Mzee "Leo nakuua, sali sala yako ya mwisho!"

Aliendelea "Siwezi kuharibu pesa yangu halafu wewe uende shule kuwa mtoro!"

Baada ya kusikia ile kauli basi nikajiongeza kiakili na nikafahamu kabisa atakuwa alikwenda shuleni kuutafuta ukweli wa mimi kufeli!.Kiukweli nilikiona kifo kiko karibu yangu!.

Mzee "Yaani nakulipia karo wewe unaenda kuvuta bangi shule?"

Aliendelea "Hizo bangi ulianza kuvuta lini?"

Sasa nikaanza kushangaa ni nani alimwambia nilikuwa navuta bangi? Kiukweli kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwenye maisha yangu ni huo uvutaji wa bangi alionieleza!.

Mimi "Hapana baba sivuti bangi!"

Mzee "Leo utanitambua mshenzi wewe"

Kiukweli kujitetea ilikuwa ngumu sana maana kila nilipojaribu kujitetea nilionekana muongo na kuishia kukandamizwa viboko visivyokuwa na idadi!

Sasa kumbe alipokwenda kule shuleni, walimu walimwambia ya kwamba mimi nilijiingiza kwenye kundi la waliokuwa wameshindikana na kuanza kujihusisha na uvutaji wa bangi!walimu pia hawakufahamu hicho hakikuwa chanzo cha mimi kufeli bali ilibidi wamwambie mzee kwasababu ya kuniona mimi kukaa na watu ambao pale shuleni walikuwa wameshindikana!

Na kwa kipindi kile walimu walikuwaga hawaangaiki na mtoto wa mtu,wao walikuwa wakituambia mwisho wa mambo yote ni pepa(mtihani)ndiyo utakaochuja nafaka halisi na magugu!.

Basi bana, baada ya kupigika sana na mzee kunishikia panga, ilibidi maza aingilie kati kwa kujifunga kibwebwe na kumkoromea mzee!.

Mama "Hivi baba Sarah unataka kumuua mtoto kisa kufeli shule!"

Aliendelea "Kama humtaki mtoto muache akatange tange huko!"

Basi baada ya mama kuingilia kati, mzee aliniacha na akanitaka nipotee pale nyumbani na nisije kumtambua kama baba yangu. Mama alinisogelea na kunifungua zile kamba mkononi na miguuni!. Kiukweli nilipigika sana.

Nilitoweka pale sebuleni nikaelekea chumbani kulala huku nikiendelea kulia kwa kwikwi, mwili wangu wakati huo ulikuwa umejaa alama ya nyaya za umeme zilizosababishwa na kile kipigo!

Usiku huo kiukweli sikupata usingizi kabisa kutokana na maumivu ya viboko!

Soma zaidi:
DhuD
 
Sasa mtu ameachana na rafiki yake akiwa anaumwa na simu imepigwa kutokea Bugando Hospital, logically alishajua jamaa yake Mtatiro amezidiwa.
Mi nachoka watu wanavyojifanya wachambuzi😂
kuna watu wanasoma uzi ili watafute mapungufu tu yaani ndio walivyo huwezi kuwabadilisha, ni kuishi nao hivyo hivyo tu mkuu
 
UKO KWENYE GENGE LA UJAMBAZI, UMETOKA KUFANYA UJAMBAZI. UNAPIGIWA SIMU NA MTU HUMJUI (ingawa alitumia simu ya mtu wako) ANAKUAMBIA UJE SEHEMU FULANI, UNAFUNGA HARAKA BIASHARA NA KUJIPELEKA..[emoji38][emoji38].

INAWEZEKANA HUYO MTATIRO KAKAMATWA NA AMEBANWA ATAJE WASHIRIKA WAKE WA UJAMBAZI, UMUGHAKA UNAJIPELEKA!!!!! JAMBAZI HAWEZI KUWA NA AKILI YA HOVYO HIVI.

Sauti "Wewe bila shaka ni Umughaka"

Mimi "Ndiyo"

Sauti "Hebu kama unaweza njoo hapa Bugando"

Mimi "Niko mbali kidogo"

Sauti "Uko nje ya Mwanza?"

Mimi "Nipo Hungumalwa"

Sauti "Jitahidi ufike haraka"

Sikutaka kupoteza muda pale mnadani,nilichukua mzigo wangu nikaufunga
Upo sahihi kabisa nakuunga mkono, but no one is perfect!

Kumbuka Umughaka sio professional criminal amedandia tu under influence ya Mtatiro. (He was just desperate and naive)

Tangu kwenye dili haramu ya fedha bandia Umughaka tumeona ana weeknes hii yakutokua na sixth sense.(machale)

Unadhani Mtatiro, Gabi au Jipe wangepigiwa simu kwa simu ya Umughaka halafu anaongea mtu mwingine wangekuja?
 
Sasa mtu ameachana na rafiki yake akiwa anaumwa na simu imepigwa kutokea Bugando Hospital, logically alishajua jamaa yake Mtatiro amezidiwa.
Mi nachoka watu wanavyojifanya wachambuzi[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu ndio ujuaji wa kijinga kila mda tunauzungumzia. Mbona mnajikuta ma-director sana kwenye kibwebwe kisicho wahusu. Mkiona ana puyanga si mkae muandike za kwenu kisha mziweke vile mnavyotaka ziwe?

Kwenye mtiririko wa story ake kuna mahala aliposema ye ni Jambazi konki? Kuna chuo amekwambia au amesimulia kua alienda kusomea ujambazi hivo keshakua Pro so hakupaswa kufanya mistake alizofanya?

Na namna mnavyoziona hizo mistake za kihalifu so mnataka kutushawishi tuone kua nyie ndio mijambazi mlio kubuhu so mnazijua mbinu zote au vp?

Waswahili tuna shida gani lakini? Mnachowashwa kitu gani kwani? Kama story mnaona ina chai nyingi si mpite tu kule kimya kimya [emoji1787]...

Em acheni ujuha wa kipumbafu, kaandikeni zenu basi zilizo 100% perfect. Mnaboa sana! Huo ujuaji wenu em uwekeni kwenye maisha yenu ya kila siku yawe perfect ili msikae jukwaani mnasubiri story za uongo!

Mijitu mizima ya hovyo kabisa, wakati wengine wanasoma kujiburudisha yenyewe yanasoma kutafuta makosa utafikiri yanafanya udahili wa waandishi. Hivi na huko mtaani kwenu mnaishije na jamii zenu watu wa aina yenu mmh?
Hakika umenibariki sana kwa huu ujumbe natamani sana kuona watu wajinga kama huyo jamaa wanausoma huu ujumbe in a positive way wabadirike waache upumbavu uliokithiri mijitu muda wote inaingia humu kwa ajili ya kukosoa wenzao inakera sana
 
Back
Top Bottom