Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,752
- 5,609
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wewe jamaa nimecheka sana ujueRIP majambazi ya mbeya
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wewe jamaa nimecheka sana ujueRIP majambazi ya mbeya
𝐌𝐭𝐚𝐭𝐢𝐫𝐨 𝐧𝐨𝐦𝐚 𝐚𝐬𝐞𝐞𝐞!!!Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 14.
Baada ya kumsubiri Mtatiro hapo Nyasura kwa muda hatimaye nae akawa amekuja akiwa anaendesha baiskeli,kiukweli kama kawaida nilipokuwa nikionana na jamaa yangu huyo utani wa hapa na pale pia furaha kwa kiasi fulani ilichukua nafasi.
Mtatiro "Mwanangu unazidi kung'aa tu,naona Tarime imekukubali"
Mimi "Aah wapi mwanangu ni kuridhika tu!"
Mtatiro "Vipi lakini kina Monche na washikaji wengine wazima?"
Mimi "Mwanao Monche sijamcheki muda mrefu,siunajua tena mimi zangu muda mwingi huwa ni Sirari tu!"
Mimi "Nadhani atakuwepo!"
Mtatiro "Jamaa huwa nampigiaga simu hadi leo haipatikani"
Mimi "Uenda atakuwa alibadili simu"
(Monche alikuwa ni yule dereva wa ile Hiace ambayo Mtatiro alikuwa akifanyia kazi kabla hajaondoka kwenda Mwanza,hivyo walikuwa washikaji).
Wakati tunaondoka hapo Nyasura kuelekea huko walipokuwa kina Mtatiro,tuliamua kutembea ili kuendelea kupiga stori maana ilikuwa ni muda umepita sijaonana na jamaa,ile baiskeli japo ilikuwa na Carier(sehemu ya kukalia)lakini tuliona ni vema tutembee huku mastori yakiendelea.
Tukiwa njiani niliamua kumwambia ukweli Mtatiro mambo yaliyokuwa yamenitokea kwasababu ukizangatia ni yeye ndiye aliyekuwa ameniunganisha na Gabriel.
Mtatiro "Jamaa sijaongea nae muda sana"
Aliendelea "Kwahiyo mlichomokaje?"
Mimi "We acha mwanangu!"
Mimi "Kuna jamaa anaitwa Eric ndiye aliyetuchomoa"
Mtatiro "Aah Eric nammanya mwanangu"
Aliendelea "Yule jamaa ndiye mwenye ile michongo na hata Gabriel ni mpambe tu!"
Mimi "Jamaa watakuwa wamemdaka maana baada ya kutoka Migori nilimtafuta lakini hapatikani!"
Mtatiro "Zile mishe zina njuruku(pesa) lakini ni hatari sana mwanangu,kila muda unakuwa macho kodo kama popo!"
Mimi "Mwanangu ninao mzigo kwenye begi!"
Mtatiro "Acha utani wewe!"
Mimi "Kwanini nikutanie!"
Mtatiro "Hebu tuone mwanangu!"
Nilishusha kile kibegi toka mgongoni nikawa nimempatia Mtatiro akawa amefungua na kutazama zile pesa ili ahakikishe nilichokuwa nakisema kama kina ukweli!.
Mimi "Hizo nilikimbia nazo kuingia Kenya ndo zimebaki!"
Mtatiro "Mwanangu hizi mbona zitatoka,we subiri uone!"
Basi baada ya mwendo mrefu huku tukiendelea kupiga mastori,Mtatiro akanitaka nipande kwenye baiskeli ili apige pedo(aendeshe) kwasababu bado kulikuwa kuna umbali tulipokuwa tukienda!
Baada ya muda tukawa tumefika hapo Kijijini ambako aliniambia kulikuwa na mgodi umetema,kiukweli palikuwa ni kijijini ambako hakukuwa pabaya sana maana karibia huduma zile muhimu zilipatikana hapo!.
Tulifika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na nyumba mbili za nyasi, Mtatiro akawa ameingiza baiskeli ndani akanitaka niweke lile begi ndani, akafunga ule mlango na kufuli akawa ameniambia tuelekee hapo kwenye hicho kimgodi!
Baada ya kufika pale mgodini tulikuta raia wanapambana kuchimba mashimo, kuna wengine walikuwa wamechimba mashimo marefu kiasi kwamba walikuwa hawaonekani, kuna ambao bado nilikuta waking'ang'ana kuchimba huku mashimo yakiwafika magotini!
Kiukweli kulikuwa na watu wengi sana huku kina mama wakiwa wanahangaika kubeba vifusi kwenye makarai na ndoo wakirundika mchanga kila mtu kwenye eneo aliloona kwake litakuwa salama kabisa.
Mtatiro alinipeleka mpaka kwenye shimo alimokuwa kaka yake na jamaa mmoja wakiendelea kuchimba,ile kazi ya uchimbaji haikuwa ya kitoto maana kulikuwa na vikokoto mshenzi kama vyote.
Sasa kwakuwa nilikuwa hapo ili kujaribu bahati yangu kwa upande huo wa madini,baada ya kumpa Hi brother ake Mtatiro nilikamata ndoo nikawa nasogeza ule mchanga pembezoni ya lile shimo!.Ile kazi tuliifanya hadi mida ya saa 3 usiku ndipo yule brother akasema tuondoke tukapumzike halafu kesho yake tungedamka mapema kuendelea!
Kiukweli familia ya kina Mtatiro haikuwaga na mambo mengi, nilichokuja kugundua ilikuwa ni familia yenye upendo sana,sema ndiyo hivyo tu hawakujaliwa kuwa na pesa!
Ukweli ni kwamba,jamii yangu ya kikurya ni jamii ambayo huwa ina upendo na kuwajali watu wengine pia,ukiachilia tu yale madhaifu madogo madogo kama wanadamu wengine lakini wakurya ni kabila bora sana miongoni mwa makabila bora kwenye hii nchi!,yale madhaifu madogo madogo ya kupiga mwanamke, kukeketa na kuchinjana ovyo yalikuwaga ni kwasababu ya ukosefu wa elimu tu, sikuhizi hayo mambo kwa Tarime yamepungua na kama siyo kuisha kabisa baada ya watu kuelimika!
Tarime ni njema sana na atakaye na aende akajionee!.(Nilikuwa nachomekea tu ndugu zangu).
Tulipofika hapo nyumbani kwakuwa tulikuwa wanaume tupu,tulikoka moto tukaanza kupika ugali ambao tulikula na dagaa zilizokuwa zimepikwa mchana!
Namshukuru Mungu kulipokucha asubuhi Mtatiro alinipatia nguo zake ambazo zilikuwa zimechoka ili nivae twende tukapige kazi!.Kiukweli nilipofika hapo mgodini hiyo asubuhi tulikuta nyomi la watu kila mtu akiwa anapambana kwa upande wake!.Kama kawaida na sisi tukaanza kazi iliyotupeleka hapo,nikiwa nimekaa nasubiri udongo ili niupeleke maeneo husika,simu yangu ilianza kuita,ile nimeitoa mfukoni na kutazama nikakuta ni Da'Sarah alikuwa akinipigia!
Da'Sarah "Mdogo wangu uko wapi?"
Mimi "Nisamehe Dada jana sikuwa na Vocha nikashindwa kukwambia niliteremkia hapa Bunda!"
Da'Sarah "Bunda tena umeenda kufanya nini!?"
Mimi "Hivi wale watoto wa mzee Marwa bado unawakumbuka?"
Da'Sarah "Marwa yupi?,yule jirani?"
Mimi "Eeh"
Da'Sarah "Mi namkumbuka yule mwanajeshi tu Ryoba"
Mimi "Sasa yupo mdogo wao ambae ni rika langu na ni rafiki yangu anaitwa Mtatiro,nilipita kumsalimia kaka yake anaumwa,alinipigia simu jana nikiwa kwenye gari nakuja hivyo nikaona niteremke kuja kumjulia hali!"
Niliamua kumdanganya dada yangu sababu ya mimi kuteremka pale Bunda ni kwenda kumuona kaka yake Mtatiro ambaye alikuwa mgonjwa ili asiendelee kunifikiria vibaya!.
Da'Sarah "Kwahiyo unakuja lini Mwanza!"
Mimi "Najitahidi dada nitawahi"
Da'Sarah "Uwahi kuja maana niliongea na shemeji yako akaniambia kuna muhindi alikuwa anatafuta mtu wa kusimamia boti zake za uvuvi"
Aliendelea "Siyo tumpange mtu kumbe na wewe huko una mambo yako!"
Mimi "Sawa dada nakuja"
Shemeji yangu alikuwaga akifanya kazi za uvuvi na yeye pia alikuwaga na mitumbwi yake kadhaa kwa ajili ya shughuli yake hiyo.Baada ya yale mazungumzo kazi zikaendelea kama kawaida,sasa lile eneo lilikuwa maarufu sana kama Nyasana Mgodini,kiumweli ni eneo lililokuwa limechanganya sana lakini jambo la ajabu hakukuwa na madini wala nini, maana Mtatiro alikuwa ananiambia wao wapo pale ndani ya mwezi na hakuna walichoambulia zaidi ya kupoteza hela tu!.
Mtatiro "Mwanangu hapa napo ni hasara tu,kila siku mara utasikia kuna kimkanda kimepita hapa,watu wakichimba kwenye hicho kimkanda hawaambulii kitu!"
Mimi "Kwani mlianza kuchimba lini?"
Mtatiro "Mimi nimekuja mwezi uliopita,lakini kina braza hapa wana miezi miwili,ndani ya miezi yote hiyo hawajawi hata kupata punje ya dhahabu!"
Mimi "Duuu!,mbona ni hatari"
Mtatiro "Kuna jamaa wao ndiyo walidai kuna mkanda umepita chini kutokea Geita,sasa watu wote hawa unao waona wanapambana kuutafuta mkanda!"
Mimi "Hakuna watu waliopata dhahabu hata mara moja?"
Mtatiro "Watu wanadai wanapata pata kimtindo lakini ukijaribu kuuliza waonyeshe walizopata hata huonyeshwi"
Aliendelea "Nishamshauri braza tuachane na hii biashara kichaa lakini hasikii,yeye bado anaamini kuna madini"
Kama kuna sehemu watanzania huwa wanapoteza muda na kulishana matango pori ni kwenye vimigodi uchwara, yaani unakuta wanaamini eneo husika kuna madini huku wakiendelea kupambana kwa nguvu na kupoteza pesa lakini mwisho wa siku wanaambulia patupu,na ndivyo ilivyokuwa hapo Nyasana, kuna muda unawaangalia ndugu zetu watanzania wanavyohangaika hadi huruma kwakweli, lile eneo ilikuwa inasemekana dhahabu ililipuka tu na watu wakaanza kujaa kwa wingi na kuanza kuchimba, sasa sikujua kama kuna wataalamu waliwahi kupima uwingi wa dhahabu ulioko pale ama la!.(Sijui kama hadi leo huo mgodi unafanya kazi).
Kuna muda tulikuwa tunatoka na mtatiro tunaingia mtaani kule kijijini tunabadili zile hela,tulipoona chenji kijijini hapo imekuwa ngumu tulikuwa tunaelekea pale senta ya Nyasura kupambana na ubadilishaji wa kununua bidhaa halisi na kurudishiwa chenji halali!.Kiukweli ile hela ikabaki chache sana!.
Kuna siku tukiwa tumetoka na Mtatiro tukiwa maeneo ya Bunda mjini kwenye mishe mishe hizo,simu yangu ikapigwa ikiwa ni namba ngeni!.
Mimi "Halloo"
Yeye "Mambo Umughaka"
Mimi "Poa,nani!"
Yeye "Hebu acha utani,kwahiyo namba yangu ushafuta!"
Muendelezo > Sehemu ya 15
Tayari wajuaji na wachambuzi wameshatia timu[emoji28][emoji28][emoji28]Alipokumbuka kipande cha Mtatiro kuumwa na kuitwa Bugando,imenifikirisha sana nikahis ni ya kutunga maana hiki kipande kilikuwa hakina umuhimu sana
Hahaha,Mwamba Jipe hakutaka kufia kitandani we ndo shujaa wetu wa muda wote umu jf
Vipi unemuona Jipe?Nimetoka kutizama video hpa youtube 5yrs back kuna majambazi waliuliwa ple mbeya
[emoji28]Shell ya Bukoba mlipoiba ni kwa Dr Remmy
KaolewaNi sasa hivi nilikuwa nawaza hivi @lara1 yuko wapi. Huyu dada alikuwa vizuri kwenye kuhadithia.
@lara1 popote ulipo kipenzi you are missed here.
Hiv unajua pesa zilivyo tamu na maisha yalivyobana,sasa eti uache kazi yako ukamuone mtu alieko mbali ambako utatumia karibia siku 5Wewe nna wasiwasi na elimu yako, so unahisi mbeya ni kama wapi au anashindwa nini kwenda Mbeya? Au unahisi huwa anaenda na bodaboda hadi mbeya? Ifike hatua muanze ku share vyeti vyenu vya kuzaliwa tujue umri wa watu tunaojibizana nao kwanza!
Amekatazwa kutumia jf?Kaolewa
Tatzo muda atakaotumia kwenda na kurudi na wakati huo una malengo yako umeyapanga,sisi tunaofanya kazi za kujiajiri huwa tunatamani kila siku tuwe tunaingiza helaKwani sh.ngapi?
Ina maana hujui kuwa kulamba ndimu si sawa na kulamba cone?Amekatazwa kutumia jf?
Labda I we hvyo tu ila ya kwako binafsi hapnaAtunge hata ya uongo tutasoma.
Kikubwa tusikose uandishi wake murua.
Yaani ww hushituki kuwa hela zilikuwa zikirudi kwa wenyeweAisee ulikuwa umeshafika mbali sana 9 mil ni kapesa kazur sana
Yaan mtu una 9 mil bado unawaza kwenda kushirikiana na mtu kufanya biashara.
Mimi huwa siamin katika biashara moja,ni bora kuwa na biashara ndogo ndogo tofauti tofauti kuliko kuwa na libiashara limoja ambalo limeshikilia maisha yako yote,ikitokea ajari ya moto tu unakufa na presha
Mmh hayaIna maana hujui kuwa kulamba ndimu si sawa na kulamba cone?
Wala hajazuiwa bali analea kiumbe ndio maana katulia.
Tatzo sio hela ni muda atakao tumia kwenda Mbeya wakati ilitakiwa awe anaingiza hela,kwa sisi wahangaikaji wa mtaani huwa hatupendi kupoteza muda hovyo kila siku unatamani hela iingieWewe bwege acha ujuaji. Amekuambia alikwenda na pikipiki? Kwani bodaboda hawezi kuwa na nauli ya kumfikisha Mbeya? Wa hovyo kabisa wewe.
Hilo la kwenda Mbeya sio muhimu sana kwa jinsi watu tunavyokmbizana na maisha,huwez poteza siku tano za kwenda na kurudi eti kwenda kumuona mtu ambae kafungwa miaka yote hiyoUnamaanisha boda boda hawana majukumu mengine yakifamilia, ndugu, jamaa, na marafiki , wenyewe ni kushinda na kulala barabaran??