Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘STORRY qali mno daah,pamoja kaka,huu ujambazi niwakisenge mno
 
Majambazi Jipe na Gabi wanawasiliana kwa simu muda mfupi kabla ya tukio.Wakati tukio la mwanzo akina Mtatiro waliacha simu Chuga wakaenda Kahama kufanya tukio!Sheria za genge lao zinabadilikabadilika au mwandishi anakosa consistency?Majambazi smart wa matukio kama hayo hawatumii masimu kwenye tukio bhana.....
Alitakiwa aedit matukio ya ukweli ili yaendane na your hollywood mindset?

FYI simu zinatumila sana kwenye uhalifu kwenye kuchonga raket lazima kuwe na muhuni mmoja anaetoa signal mkuje au mle buyu
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani.

Part 1: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 2: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 3: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 4: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 5: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 6: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 7: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 8: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 9: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 10: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 11: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 12: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 13: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 14: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 15: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 16: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 17: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 18: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 19: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 20: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 21: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 22: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 23: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 24: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Part 25: Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani
[emoji1483]
 
Duuh kama Mungu mmeachana na michongo hiyo then kikanuka.
 
Lini utatuletea ile story ya kutembea na yule mke wa mtu ambae alikuwa ni mteja wako mkubwa wa Bodaboda yako?๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kiss kingine zaidi y hiki? Unamtakia kifo wewe, lete nawewe kisa kimoja tuu hata kama cha kumwagikiwa na Chai ya moto.
๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ jamani.
Visa ninavyo halafu vya hatari. Tatizo siwezi kuhditlhia kwenye mtiririko murua kama huu. Nitaboa halafu nitachoka kuandika.
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 25.



"Wewe ni mtu muhimu sana kwangu Mtatiro na umekuwa sehemu ya furaha katika maisha yangu,ulinipokea na kunisaidia wakati mzee aliponitimua nyumbani,hukuniacha katika matatizo bali ulinishika mkono kama kijana mwenzio hivyo na mimi sitokuacha rafiki yangu" ni maneno niliyokuwa nikimwambia rafiki yangu wa damu Mtatiro ili aendelee kuwa na amani kabisa.

USHAURI

Kuishi na Virusi vya Ukimwi si mwisho wa maisha na uhai,kama kuna kitu nakichukia katika maisha yangu ni ubaguzi unaofanywa kwa hawa ndugu zangu,haya ni maisha tu na tunapaswa kupendana,unaweza ukawa muaminifu na bado mumeo/mkeo akakuletea ugonjwa,hivyo hatupaswi kuwanyooshea wengine vidole kana kwamba ni wadhambi kuliko sisi,tuache dharau za kijuaji na kebehi zisizo na msingi.

Ndugu zangu pia niwaombe mzingatie dawa kwa wakati ili ziweze kuwafubaza virusi angalau unapokutana na mwenzako usimuambikize ili muendelee kufurahia maisha,jambo la msingi ni wewe mwenyewe kuacha kujibagua,jikubali na songa mbele.Acha starehe za kijinga,panga mipango yako na timiza ndoto zako,usiwe mlevi kupita kiasi na hakuna sababu ya kuwaambukiza wengine kwa makusudi,wapende watu wote.Pia achana na imani za mitume na manabii kwamba wakupatie maji au mafuta utumie kisha uache dawa,achana kabisa na hizo imani mfu,wewe muombe Mungu atakusikia,kama akipenda anaweza kuuondoa huo ugonjwa na kama akiona inafaa wewe kuendelea nao basi Mshukuru na endelea kuishi,hata kama ukimuomba Mungu na ugonjwa usitoke lakini Mungu bado atabaki kuwa mwema hivyo usikate tamaa.

NAWAPENDA SANA



Basi baada ya afya ya rafiki yangu kipenzi Mtatiro kuimalika tuliendelea na kazi yetu ya kuuza mitumba sehemu na vijiji mbalimbali vya kanda ya ziwa.Nakumbuka siku moja Gabi alimpigia simu Mtatiro akawa amemuambia inapaswa tuonane ili tupange mikakati ya kuelekea maeneo kama kawa.Kweli,tuliondoka siku iliyofuata kuelekea kule yalipokuwa makazi ya muda ilipokuwa inasukwa mipango kabla.Tulipofika pale ndani tulimkuta Gabi kama kawaida akiwepo Jipe na jamaa yule dereva tuliyeenda nae kwenye tukio kahama.

Jipe "Wanangu mko poa"

Mtatiro "Tuko fiti kaka"

Jipe "Sasa Kesho safari ni Kagera"

Aliendelea "Si mko vizuri?"

Mtatiro "Sisi tuko tayari hata leo kaka ni nyinyi tu!"

Jipe "Sawa,Gabriel atatangulia leo halafu sisi kesho jioni tutaondoka"

Basi baada ya yale mazungumzo Jipe akatutaka tujitayarishe kwa ajili ya safari kesho yake.Mimi na Mtatiro tuliamua kurudi nyumbani huku Mtatiro akiapa na kusema safari hii wakijidai kutudhurumu basi ama zake ama zao!.

Siku iliyofuata mida ya saa 7 mchana tulikuwa tushafika eneo la tukio na ndipo tukakamata Noah na kuianza safari ya kuelekea mkoa wa Kagera,kwenye gari nilikuwa mimi na Mtatiro wakati huo jipe akiwa amekaa kwa mbele pamoja na yule jamaa dereva!.Tuliingia Kagera mida ya saa 12 asubuhi siku iliyofuata,njia tuliyotumia ni ileile ya kupitia Kahama huku tukiwa makini kupita maelekezo,Jipe alikuwa ametoa maelekezo ya kwamba,yeyote atakaye jiingiza mkenge basi ingekuwa ni halali yetu!.Baada ya kufika Kagera,Jipe aliwasiliana na Gabi ambaye alimuelekeza maeneo ambayo tungemkuta,nakumbuka tuliikamata njia na uelekeo wa Bukoba mjini,nje kidogo ya mji tukamkuta Gabi.

Gabi "wazee kwa huku itabidi tuzunguke kidogo muda uende kwasababu hatuna makazi,na ikifika mida tutaitana tufanye kilichotuleta".

Kwakuwa mimi na Mtatiro ndiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza kufika Kagera ilibidi tukae kwenye ile gari maana hatukutaka kucheza mbali tukajichanganya na ukizangatia hatukuwa na simu!.Dereva alitafuta maeneo ambayo hayakuwa na shughuli nyingi za watu akapaki gari hapo.

Ilipofika mida ya saa 10 jioni mvua ikaanza kunyesha kama masikhara lakini muda ulipozidi ndipo hali ilizidi kuwa mbaya,tangu nizaliwe sijawahi kuona radi zikipiga kama siku hiyo,ile mvua ilikuwa na radi si mchezo hadi uoga ukawa unaniingia!.Kadiri muda ulivyozidi ndivyo mvua nayo ilizidi kuongeza spidi na nilikuwa naona Jipe anaomba iendelee kunyesha vilevile isikatike.Sasa ikafika mida ya saa 12 ikapungua ikawa inanyesha kidogo sana,tulikuwa ndani ya gari wakati huo tukiendelea kuvuta muda.Ilipofika mida ya saa 3 usiku mvua ikaanza tena kunyesha kama mwanzo.

Jipe "Huu ni muda sasa"

Aliendelea "Aisee wewe utaenda kutusubiri mahali nitakapokuelekeza"

Jipe "Wengine wote tutaongozana na mtafanya kila nitakachowaambia"

Basi ile gari ikaanza kuondoka kuelekea uelekeo wa Bukoba Mjini,kuna mahali tulifika ambapo kwa umbali kama wa mita 500 kulikuwa na sheli(sitoitaja),dereva alitakiwa kuzima taa na kugeuza gari atusubiri hapo!.Kila mmoja alikuwa tayari kwa ajili ya makabiliano.Muda huo ilikuwa ni saa 4 usiku lakini kulikuwa na mvua kubwa sana,tulipofika kwenye ile sheli baada ya Jipe kuchomoa SMG kuna mlinzi alimuona akaanza kukimbia kama mwehu huku akiwa na gobole,Jipe hakutaka kumpotezea muda,alipiga risasi ya mgongoni yule mlinzi akawa amedondoka chini.

Jipe "Mtatiro kusanya hao wauza mafuta wote"

Jipe aliingia ndani kwenye vyumba vilivyokuwa kando ya ile sheli huku akiniambia niongozane nae.Pale nje Mtatiro na Gabi waliendelea kuwadhibiti wale wauza mafuta na kuchukua hela huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Jipe "Toa pesa wewe la sivyo nitakuua"

Jipe alikuwa akimwambia dada mmoja kibonge ambaye tulimkuta mle ndani wakati huo akimnyooshea mtutu wa bunduki.Yule dada alifungua boksi moja lilikuwa la mbao na kulikuwa na noti za kutosha,sasa kulibeba lile boksi mwenyewe kidogo likawa zito,Jipe akamuamuru yule demu atupatie mfuko,yule demu alitoa mfuko mmoja ambao ulikuwa kama shuka ambao ulikuwa umechakazwa na rangi ya maoili!,niliukamata ule mfuko haraka nikaanza kuchukua zile hela haraka sana,sikutaka kabisa kuhangaika na silva maana jipe alisema nitemane nazo,baada kumaliza zile hela,Jipe alimuamuru yule demu alale chini na asijaribu kuinua kichwa kwani atamuua,tuliondoka chap mle ndani kuelekea nje ambapo tuliwakuta Gabi na Mtatiro wakiwa wanatusubiri!.

Tulikimbilia gari na tulipofika dereva aliondoka kwa spidi kali sana lile eneo,wakati huo bado mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha sana.Wakati tupo njiani,Jipe alimpigia simu yule demu Kamange na kumtaka achukue ile gari Mark 2 atukute Geita.Ile Noah ilitembea vibaya mno usiku huo na tulifanikiwa kufika Geita mida ya saa 8 Usiku,Jipe akawa amemwambia Gabriel na dereva ya kwamba wao watangulie Mwanza halafu sisi tungeisubiri ile Mark 2.

Kweli,Kesho yake mida ya saa 4 asubuhi yule demu akawa amefika pale Geita kutuchukua tukawa tumeondoka,Tuliingia Mwanza mida ya saa 11 jioni.Tuliwakuta kina Gabi wao wameshafika,sasa tulipofika Mtatiro alimwambia Jipe ya kwamba pesa tulizopora ziletwe zihesabiwe ili kila mtu afe na chake,nadhani wao walidhani Mtatiro anatania lakini jamaa alikuwa serious sana,sikuwahi kufahamu kama Mtatiro akikasirika anakuwa vile aisee,mara zote mimi nimekuwa nikimuona akiwa kawaida nikawa namchukulia poa,siku hiyo ndiyo niliiona rangi halisi ya yule mkurya.

Mtatiro "Haiwezekani tupore pesa halafu nyie muwe mnagawana nyingi na sisi mnatupa kidogo,mkitaka damu leo imwagike ficheni hizo hela muone!"

Jipe "Hakuna atakayedhurumiwa hata mmoja"

Mtatiro "Mbona juzi mmetunyenga?"

Jipe "Yale yalikuwa ni maelekezo ya bosi"

Mtatiro "Basi mwambieni leo kila mtu anapata pasu,sitaki ufara!"

Baada ya jamaa kuona Mtatiro yuko serious,Jipe alimwambia Gabi walete zile pesa ili kila mmoja apewe haki yake.Kweli,mimi na Mtatiro kila mmoja alipata mioni 6,na wao pia walipata kama sisi.Tuliamua kuondoka zetu baada ya kupokea mgao wetu.

Mtatiro "Mwanangu kama ni hela ya mtaji tushapata,tuachane na hizi habari wao kama wanaendelea ngoja waendelee"

Aliendelea "Cha kufanya tukafungue duka la jumla tuachane na mitumba"

Mtatiro "Au wewe unaonaje mwanangu?"

Mimi "Kwanini tusifungue duka la vipodozi?"

Mtatiro "Eti eeeh,sawa?"

Baada ya kupata ile hela kweli tuliachana na biashara ya mitumba na tukafungua duka la vipodozi yale yale maeneo ya Usagara tukaanza kupambana,nakumbuka Mtatiro alikuwaga anafuata vipodozi Uganda kwasababu huko ndiko vilikuwa vinapatikana kwa bei ya chini,kiukweli tulipiga sana hela na maisha yetu yalianza kubadilika mdogo mdogo,ilifika sehemu tukahama pale kwa braza ake Mtatiro kila mmoja akaenda kupanga geto lake mwenyewe.

Nakumbuka siku moja Mtatiro akaja kuniambia kwamba Gabi anampigia simi twende kuna mchongo wenye hela kubwa tukapige.

Mimi "Umemwambiaje!"

Mtatiro "Mi nimemwambia kwasasa tunashughuli zetu,wao kama wanaendelea waendelee!"

Aliendelea "Jamaa baada ya kumwambia ananiambia kwamba tunataka kuwachoma,hivyo tujiangalie tutaumia"

Mimi "Sasa itakuwaje?"

Mtatiro "wale hawawezi kututisha we tulia"

Basi baada ya jamaa kuona hatuwapi tena ushirikiano wakaamua kutokutushirikisha kwenye michongo yao tena lakini walikuwa wamechukia sana baada ya sisi kuachana nao.Baada ya miezi kadhaa kupita,kuna siku Mtatiro akaja kuniambia amesikia habari mahali kuna majambazi wamedakwa wengine wameuawa huko Mbeya na mmoja wapo wa waliodakwa ni Gabi,sasa baada ya kuifatilia ile habari ni kweli kabisa ilikuwa Jipe na majambazi kadhaa wenzie waliuawa palepale eneo la tukio.

Kumbe walienda kumpora mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya India ambaye ndani ya gari alikuwa na madini pamoja na pesa alizokuwa akizitoa huko Chunya kuelekea Mbeya,sasa wao hawakujua yule mfanyabiashara alikuwa na eskoti ya askari kadhaa,yawezekana walijua hilo ila wakajifanya wabishi kwakuwa walikuwa na silaha.Walikufa majambazi wawili na mmoja akiwa Jipe huku Gabi na mwingine mmoja wakisalimu amri.

Gabi alifungwa miaka the thelathini gerezani na mwaka juzi nimetoka kumuona pale gereza la Ruanda Mbeya.Jamaa amechoka sana na aliponiona mara ya kwanza alionyesha huzuni lakini hakuwa na namna ndo hivyo ishatokea.Aliniambia yule aliyekuwa bosi wake alikimbilia huko Kenya kuanzisha maisha huko.Huwa namtembelea jamaa nikipata nafasi,na siachi kumtia moyo na kumfariji,namwambia ashukuru akufa,maadam yuko hai basi atatoka tu gerezani na ataendelea na maisha yake ingawaje atakuwa amepoteza muda.

Mimi na Mtatiro lile duka la vipodozi tuliuza na kila mmoja akaendelea na biashara zake,Mtatiro aliondoka kwenda Uganda kwa anko wake hadi leo anaishi huko.Mimi niliamua kurudi Tarime Sirari nikafungua duka nikaanza kukimbiza,kuna mtoto wa dingi mkubwa anaishi Dar es salaam alikuwa anafanya biashara ya vyombo akaniambia nije tuungane tufanye biashara kwa kua inalipa sana,hivyo nikaondoka Tarime kuja Dar,kufika nikampatia jamaa zaidi ya milioni 9 akanidhurumu hadi leo,niliamua kumuachia Mungu nikaanza kupambana upya kutafuta mtaji,nilipopata mtaji nikanunua bodaboda yangu ambayo ndiyo inaniingizia kipato kwa hapa mjini.


Nawapenda sana.


MWISHO.

Ukweli tumejifunza, kwangu mimi nimejifunza adhabu ya kufukuza mtoto haifai na sitokuja kuifanya, ingawa watoto wangu sijaona mkorofi ila hata nikisikia jirani au mtu ninayemfahamu kafukuza mtoto kisa kafanya kosa nitamwendea na kutumia funzo la UMUGHAKA kumwomba abadili adhabu.

Barikiwa sana kijana.
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 20.



Gari ilitembea tukaikamata njia ya Sirari,sasa tukawa kama tunaelekea Musoma.Yule jamaa akamwambia yule demu aliyekua akiendesha gari ya kwamba inapaswa tuweke kituo kwanza Lamadi tukapate msosi kisha ndiyo tuondoke.

Baada ya kufika lamadi na kupata Msosi tuliondoka kuelekea Bariadi,sikuwahi kufika bariadi ni hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika huko,sasa baada ya kuiacha bariadi tulianza kuingia vijijini huko ndani ndani ambako sikuvifahamu kwa haraka maana sikuwa mwenyeji huko.

Kituo chetu cha mwisho kilikuwa kwenye kijiji cha Mwanaungu ambako baada ya kushushwa hapo,yule jamaa alimwambia yule demu kwamba amsubiri kwanza atupeleke halafu waondoke!.

Mtatiro "Mwanangu kwahiyo mnatuacha?"

Jamaa "Tutarudi kuwachukua ondoa shaka!"

Tulitembea kwa umbali mrefu kidogo hatimaye tukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa umezungushiwa minyaa ya kutosha,baada ya kufika hapo tulikuta kuna vijumba vingi vya nyasi huku kukiwa na watu ambao wengine walikuwa wamelala kwenye majamvi huku wengine wakiendelea na shughuli zao!.Kuna mwanamke akaja kutupokea kwa salamu ya kisukuma huku akipiga magoti,sasa mimi kwakuwa nilikaa usukumani kwa kipindi fulani wakati baba yangu mdogo akiwa headmaster,ile salamu haikunipa taabu kabisa!,na siyo salamu tu,naweza kukizungumza kisukuma ingawaje cha kuombea maji!.

Baada ya ile salamu yule mwanamke alituletea viti ambavyo havikuwa na watu kwa wakati huo.Basi baada ya muda mfupi yule mwanamke akaja na daftari akatutaka kila mmoja wetu kutaja jina lake na kuandikwa,sasa tulipoandikwa akatuchania vikaratasi vikiwa na namba,mimi nilipewa namba 16 na Mtatiro akapewa namba 17,yule jamaa yeye akamwambia yule mwanamke kwamba anahitaji kuonana na Mwami(Ng'wana Mwami).Yule mwanamke akamtaka asubiri kwanza.

Baada ya muda yule mwanamke akaja akamuita yule jamaa akampeleka mpaka kwenye kinyumba cha nyasi kilichokuwa kikubwa kati ya vile vinyumba tulivyovikuta pale.Baada ya muda yule jamaa akatoka akaja akatuambia angerudi baada ya siku mbili,hatukujua alipoingia mle ndani alienda kuzungumza kitu gani na huyo aliyekuwa humo ndani!.Jamaa aliondoka akatuacha pale,hiyo ilikuwa mida ya mchana saa 7.

Ilipofika mida ya saa 10,kuna mwanamke alitoka kwenye kile kijumba huku akijinyoosha kana kwamba alikuwa amechoka sana!.Alianza kuwazungukiwa watu kadhaa waliokuwa pale nje huku akiongea nao kisukuma na kiswahili!.Alipofika kwetu alitusalimia kisukuma na kama kawaida nami nilimuitikia kisukuma,sasa Mtatiro halikuwa haelewi kabisa hata salamu ndipo nilimwambia yule mama ya kwamba mwenzangu haelewi kisukuma,aliamua kumsalimu kiswahili kisha akaendelea na watu wengine!.Yule mama ndiye aliyekuwa mwenyeji wetu na alikuwa mganga!.

Mtatiro "Mwanangu kisukuma kumbe unakipiga fresh"

Mimi "Nimekaa nao,dingi yangu mdogo alikuwa headmaster shule moja huko Tabora hivyo nilikinyaka kiasi fulani"

Ilipofika mida ya saa 12 jioni kuna watu takribani 7 ambao walikuwa wanaume 3 na wanawake 4 waliingia pale nyumbani huku wakiwa wamebeba majembe,mimi nilidhani ni ndugu tu wanaoishi hapo kumbe walikuwa wateja wa huyo mama.Sasa utaratibu ulikuwa ni kwamba,unapofika kwa huyo mama unapewa namba kama sisi tulivyopewa,wakati ukiendelea kusubiri ili namba yako iitwe ilipaswa kila kunapokucha ukamate jembe umfuate mwenyeji akakuelekeze shamba la kulima na ulikuwa unapewa kipande chako ili upambane nacho,na kipande chenyewe hakikuwa cha kitoto,yaani kama ukimaliza kile kipande ndipo unaambiwa sasa umekolifai kupatiwa matibabu na yule mama.Sasa wakati unasubiri matibabu ndipo mnaitwa kwa namba ambazo hata sisi tulipewa.(Yule mganga alikuwa mjanja sana,badala ya kulima mashamba yake,sisi wapumbavu ambao tulifahamika kama wateja wake ndio tuliomlimia wakati yeye akiwa ametulia nyumbani,Daaah![emoji23][emoji23],na kila mtu aliyefika hapo kwake ni lazima ilikuwa akamatishwe jembe aingie shambani![emoji23][emoji23]).

Mimi na Matatiro tulikomaa na vipande vyetu ambavyo tulivianza siku iliyofuata kwasababu siku tuliyofika tulikuwa tumechelewa,bahati nzuri ilikuwa ni palizi na hakukuwa na nyasi sana!.Siku hiyo tulipomaliza kupalilia lile shamba ilikuwa mida ya saa 9 alasiri,tuliporudi hapo nyumbani kiukweli tulikuwa tumechafuka miguu na kunuka majasho hatari,sasa nilimfuata yule mama aliyetupokea siku ile nikawa nimemwambia atupatie maji ili tuoge,alituambia inapaswa tuwasubiri wenzetu ambao nao walikuwa hawajamaliza sehemu zao ili tupate chakula kwa pamoja kisha ndio tuoge!.

Wale walipotoka huko shambani,tulitengewa ugali wa udaga kwa na furu wa kuchemsha.Sasa tulipaswa kukaa watu watatu watatu kwa ajili ya chakula,mimi nilikaa na Mtatiro kama kawaida pamoja na jamaa mmoja ambaye alikuwa mteja kama sisi!.Siku hiyo ikapita kapa bila kuitwa namba lakini kuna watu wao waliitwa wakaendelea kupewa huduma kama kawaida!.

Siku iliyofuata tukaitwa majina watu kama wanne,sasa kwakuwa mimi na Mtatiro tulikuwa na shida moja ilibidi tuambiwe tusubiri kwanza amalizane na wale wa wawili.Zamu yetu ilifika na tukaitwa ndani kwa yule mama,hatukujieleza hata kidogo bali tulipoingia ndani alitutaka tuvue shati ili kitendo cha kupigwa chale kuchukue nafasi!.

Yule mama alitupiga chale kwa kutumia kisu kilichokuwa kikali kama wembe,alituchanja kila sehemu aliyoona yeye inafaa,baada ya hapo alituchanja pia kwenye ulimi kila mtu!.Alipomaliza kutuchanja na kutupaka dawa,alichukua kitu kilichokuwa kimefungwa na kukazwa sana na kutakiwa kila mmoja akivae kiunoni,ile alituambia ni irizi na asije akatokea mtu akaivua,alisema endapo ikitokea ukaivua basi usije ukamlaumu!.

Mpaka wakati huo hatukufahamu kwa huyo mganga tulipelekwa kufanya nini,ingawa tuliambiwa tunakwenda kutengenezwa ili hatukujua utengenezwaji ulikuwa na faida gani katika ile kazi yetu mpya ambayo tungeianza siku chache zilizokuwa mbele yetu!.

Yule mama alituambia ya kwamba,ile irizi haikupaswa kabisa kutolewa kiunoni hata iweje. Basi baada ya kumaliza ile shughuli tulitoka nje tukaendelea kumsubiri jamaa aliyetuambia angekuja kutuchukua!.Ile siku jamaa hakutokea kabisa,hivyo ikatubidi tulale tena kwa yule mama.

Yale mazingira yalikuwa ya hovyo sana lakini ilibidi tukubaliane na hali kwasababu tuliitamani pesa!.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi ya siku iliyofuata yule jamaa alirudi kutuchukua na kisha tukaondoka,sasa tulipoingia kwenye ile Noah tulikuta kuna mabegi kadhaa na kulikuwa na jamaa mmoja akiwa amekaa siti za abiria,dereva alikuwa ni yuleyule demu ambaye alikuwaga azungumzi na mtu!.

Jamaa "Wanangu safari ni moja kwa moja Arusha"

Mtatiro "Kaka mngeturudisha kwanza tukachukue nguo"

Jamaa "Nguo sio sehemu ya kuwazia,utazikuta huko"

Hatukuwa na swali,tuliamua kukausha na safari kuanza.Tulitembea sana na hatimaye tukaikamata lami kuelekea Musoma,baada ya kuivuka lamadi kwa mbele,tukaikamata geti la Ndabaka linaloingia Serengeti.
๐Š๐š๐ญ๐ข๐ค๐š ๐ฌ๐ข๐ฆ๐ฎ๐ฅ๐ข๐ณ๐ข ๐ณ๐จ๐ญ๐ž ๐ฌ๐ข๐ฃ๐š๐ฐ๐š๐ก๐ข ๐ค๐ฎ๐ข๐Ÿ๐š๐ญ๐ข๐ฅ๐ข๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ฎ๐ฆ๐š๐ค๐ข๐ง๐ข ๐ณ๐š๐ข๐๐ข ๐ฒ๐š ๐ก๐ข๐ข ๐ง๐ข๐ฆ๐ž๐ข๐ฌ๐จ๐ฆ๐š ๐ญ๐จ๐ค๐š ๐ฆ๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐จ ๐ฆ๐ฉ๐š๐ค๐š ๐ก๐š๐ฉ๐š ๐ฎ๐ฅ๐ข๐ฉ๐จ๐ข๐ฌ๐ก๐ข ๐ง๐ข๐ฆ๐ž๐ข๐ฉ๐ž๐ง๐๐š ๐ข๐ค๐จ ๐ฏ๐ณ๐ซ ๐ฌ๐š๐ง๐š ๐ข๐ง๐š๐Ÿ๐š๐š ๐ฎ๐ญ๐ž๐ง๐ ๐ž๐ง๐ž๐ณ๐ž ๐ฌ๐จ๐Ÿ๐ญ ๐œ๐จ๐ฉ๐ฒ ๐ฆ๐ค๐ฎ๐ฎ ๐ง๐ข ๐ฎ๐ฌ๐ก๐š๐ฎ๐ซ๐ข ๐ญ๐ฎ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendeleea>
Baada ya kuingia serengeti,gari lilisimama parking,yule jamaa tuliyemkuta kwenye gari alishuka na kuelekea toilet.

Mtatiro aka niambia umughaka,safari hii ni ndefu sana inabidi tupate kitu ili tuweke tumbo sawa,yule dada aliyekuwa dereva akasema msijali tushajianda sawa,kuhusu maswala ya chakula.

Alitoa mfuko ukiwa na mikate,na soda zile kubwa za chupa,tulipokuwa tunaendelea kula yule jamaa aliyeshuka kwenda toilet alikuja akaungana nasi,tulikula mpaka kila mtu akaridhika.

Yule dada akatuambia sasa tupo tayari kuanza safari,dada alitekenya ufunguo,tukaondoka zetu.

Tulisafiri kwa mda mrefu sana,tulipiga story na mtatiro kuhusu mambo mengi sana,alini hadithia story ya demu wake aliyependa mapenzi kuliko chakula,mtatiro anasema demu wake huyo alikuwa anafanya mapenzi kama dozi asubuhi mchana na jioni.

Mtatiro Ali niambia brother alisanda kule alipokuwa anatafuta madini,walipiga kazi mpaka pesa zikakata ikawa hakuna chakula,wale waliokuwa wanafanya naye kazi walimkimbia,akabaki pekee yake ikabidi naye asepe,migodi ikafungwa.

Tulifika ngorongoro mida ya saa 8 mchana tukiwa tumechoka sana,tulienda toilet baada ya kurudi safari iliendelea tena.
 
Sasa ana observe kwa faida ya nani ila wabongo bhana mnapendaga kuichosha akili yenu asee
Acha wenye akili watumie. Nyie ambao ambao hamtaki ichosha ndo inaganda...na watanzania wengi wana akili mgando ni kama mazombie.
 
  • Thanks
Reactions: ARV
UMUGHAKA kapiga kimya tu atapitia sifa zake kimya kimya.
 
Sasa ana observe kwa faida ya nani ila wabongo bhana mnapendaga kuichosha akili yenu asee
YAP...MTU MAKINI LAZIMA UICHOSHE AKILI (sio mwili) VIJANA WA AINA YENU NA WENGI HAPA JAMIIFORUMS NI GABBAGE IN GABBAGE OUT.
WENGI NIMEONA HAPA WANASIFIA "Umughaka, Mtatiro, Gabi, Jipe nyie ni mwamba" YAANI TUNASIFIA MTU KUWA JAMBAZI, KUUA WATU, KUSABABISHIA WATU VILEMA NA KUPORA MALI ZA WATU WALIZOTAFUTA KWA JASHO. MTU MAKINI HAPA ANGESEMA UMUGHAKA POLE NA USIRUDIE TENA HUO UHARAMIA. GREAT THINKERS WANASIFU NA WANATAMANI ANGEENDELEA NA UPORAJI.
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 3.




Baada ya ile gari kumalizika kuoshwa tuliondoka kuipeleka nyumbani kwa yule tajiri wa ile gari aliyekuwa akikaa mitaa ya Magamaga!..Sasa baada ya kuondoka pale kwa tajiri,Mtatiro akaniambia tuingie gengeni tukapate msosi halafu anipeleke gheto nikapige mbonji na yeye aelekee kulala kwa demu wake.

Basi bana asubuhi kama kawaida akawa amekuja mida ya saa 12 akanigongea nikaamka!.

Mtatiro "Vipi mwanangu nikuache ulale au tusepe zetu?"

Mimi "Ngoja ninawe uso tuondoke mwanangu"

Sikutaka kabisa kulala kwasababu jamaa angeniona mzembe.

Baada ya kujipaka mafuta tuliondoka na Mtatiro akawa ameelekea kwa bosi wake kuchukua ile gari ili ampelekee dereva ambaye angemkuta pale stendi!.

Mtatiro "Ngoja twende kuna jamaa yangu ana kipanya kina piga ruti ya Sirari"

Aliendelea "Siunaweza kukomaa mwanangu?"

Mimi "Nitakomaa mwanangu wala usijali"

Mtatiro "Dingi yako nilikuwa namuona ni mjanja kumbe ana mambo ya kinoko hivyo!"

Sasa mtatiro yeye alichoamini ni kwamba mzee wangu ndiye mzinguaji bila kufahamu yote hayo msababishaji ni mimi.Sikutaka kabisa kumweleza mambo mengi ya nyumbani,nilichomwambia ni kwamba mzee kanitimua nyumbani niende nikajitegemee!.Baada ya kufika pale stendi akamkabidhi dereva gari kisha akamuomba simu ili ampigie yule jamaa yake mwenye kimchomoko aweze kuzungumza nae!.

Walipozungumza na huyo jamaa,jamaa alimwambia niende nitamkuta kwenye njia ya Nyamwaga Road amepaki na akawa amemuelekeza namba za gari!.Nilitembea kwa haraka ili nimuwahi jamaa.

Nilifanikiwa kumkuta jamaa na tukasalimiana!.

Jamaa "Mambo vp?"

Mimi "poa kaka"

Jamaa "Sasa tutaondoka nitakuacha pale sirari,wewe utahakikisha unakuwa unanitafutia abiria wa kuja nao Tarime halafu nitakuwa nakupa posho!"

Mimi "sawa kaka"

Jamaa "Lakini si utaweza?,maana hii kazi siyo lele mama"

Mimi "Nitaweza kaka wala usijali"

Jamaa "Ningekuweka hapa Town sema kuna wakuda fulani watakusumbua pale kijiweni"

Sikuwahi kabisa kufanya kazi za kwenye magari lakini sikuwa na namna ilibidi nipambane kama mwanaume ili nipate pesa!,nilitaka na mimi niwe kama Mtatiro aliyekuwa mchangamfu na mcheshi asiyejali kitu!.Yule jamaa alikuwa akimiliki gari aina ya Pro box(Kimchomoko) na alitaka mimi nikawe mpiga debe wa kumtafutia abiria upande wa sirari!.


Jamaa "Ingia twende zetu"

Basi tuliondoka yale maeneo niliyomkuta na kuelekea kwenye stendi za zile gari za kuelekea sirari,baada ya kufika pale nilitelemka nikakaa pembeni kuangalia wahuni walivyokuwa wakigombania abiria kuwapeleka kwenye magari waliyokuwa wakiyapigia debe!.
Baada ya zamu yetu ya kupakia kufika,kuna jamaa wakaanza kuitia abiria mpaka gari ikajaa!.Gari ilipojaa jamaa akaniambia niingie nyuma ya buti ambapo pia kulikuwa na abiria wengine wawili ili twende akaniache sirari niianze kazi yangu ya kupiga rasmi!.

Tulipofika pale sirari nikashuka na nikaanza kuchangamka maana nilitelemsha mizigo ya abiria kwenye kile kigari,nilianza kuita abiria kwa kuchangamka lakini nikaja kugundua haikuwa kazi rahisi hata kidogo!.Lile eneo kiukweli niliwakuta baadhi ya wapiga debe ambao kila mtu alikuwa na gari zake alizokuwa akiitia abiria!.

Namshukuru Mungu abiria wakajaa kwenye gari na jamaa akaondoka mimi nikabaki!Sasa kwakuwa mimi na wale jamaa kazi yetu ilikuwa moja,tulianza kupiga stori za hapa na pale!.Kuna jamaa mmoja ambaye nilikuwa nasikia wenzie wakimuita pengo na sikufahamu kama ndilo lilikuwa jina lake au ulikuwa ni utani tu!,alikuja tukawa tunazungumza!.

Pengo "Mwanangu Keraryo ni bosi wako?"

Mimi "Keraryo ndiyo nani?"

Pengo "Huyo jamaa uliyemuitia abiria!"

Mimi "Yule ni brother tu"

Pengo "Sikia mwanangu,angalia jamaa asije akakudhurumu posho yako"

Aliendelea "Jamaa wamemkataa watu kibao hapa kijiweni kwasababu hatoi posho!,unamuitia abiria akiondoka ndo imetoka!,na ndiyo maana unaona gari yake ikifika wahuni hawana habari nayo"

Mimi "Hakuna tatizo mwanangu yule ni brother"

Pengo "Sawa mwanangu kama ni brother wako haina noma"

Basi sikutaka maneno mengi sana kwakuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuifanya ile kazi!.

Sasa ilipofika jioni baada ya kujaza tena ile gari,jamaa alinikabidhi posho ya siku ambayo ilikuwa buku 3,kiukweli nilikata tamaa sana baada ya jamaa kunipatia ile hela lakini sikutaka kumwambia,niliamua kujikaza kisabuni kama mwanaume!.Kumbuka tangia asubuhi nilikuwa sijaweka kitu chochote tumboni.

Baada ya jamaa kunipatia ile posho akaniambia niingie kwenye gari turudi Tarime mjini maana sasa ilikuwa giza!,nilipofika mjini nilielekea kwa mama ntilie kupata msosi kisha niliondoka kuelekea kwenye geto la Mtatiro ambaye nilikuta amefunga,nilikaa nje kumsubiri na ilipofika mida ya usiku wa saa 4 jamaa alirudi akiwa na mwanamke!.

Mtatiro "Mwanangu umefika muda mrefu?"

Mimi "nimefika mida ya saa 1"

Mtatiro "Nilienda kwa shemeji yako"

Baada ya kuzungumza,jamaa alifungua gheto akawa ameingia yeye na demu wake,sasa kiukweli niliwaza sana ni wapi nitakwenda kulala maana jamaa alikuwa na demu wake.Sasa nadhani baada ya jamaa kuona nina mawazo aliniambia nisiwaze kwani tungelala wote mle ndani.

Basi bana,jamaa alitandika chini mifuko ambayo juu yake akaweka nguo akanitaka niegeshe ile kibishi ilimradi kupambazuke tukaendelee na mitikasi ya utafutaji!.

Ule usiku kwakweli kwa upande wangu ulikuwa usiku mbaya sana kwasababu jamaa alianza kutafuna papuchi ya yule demu wake bila huruma,hakujali kabisa na wala hakuona aibu!,kibaya zaidi yule demu wake nae akawa analia kilio kisicho cha machozi huku mwanaume mimi nikiendelea kujigeuza kila sekunde kana kwamba nimepakwa upupu!.Niliapa kabisa ya kwamba,nisingethubutu kabisa kulala kwenye geto la mshikaji kama hizo ndizo zilikuwa habari zenyewe!.

Namshukuru Mungu asubuhi kulikucha na sisi tukaondoka zetu huku demu wa jamaa akiwa bado amelala!.


Baada ya kumaliza kazi ile jioni,sikutaka kabisa kurudi Tarime mjini na nilimwambia jamaa kesho angenikuta hapo Sirari nikimsubiri!.Usiku ule niliamua kutafuta guest ya bei nafuu iliyokuwa hapo maeneo ya jirani nikawa nimelipa elfu 5 nikawa nimelala.Baada ya kufanya ile kazi ndani ya wiki moja huku nikiendelea kukaa hapo Sirari,nilipata marafiki ambao pia walinifundisha namna ya kufanya kazi zaidi,badala ya kutegemea gari ya brother Keraryo pekee,nikawa naitia abiria na gari za mabosi wengine kisha napata posho,kiukweli nilianza kuchangamka na kuizoea ile kazi,kwa siku nilikuwa sikosi elfu 15 mpaka 20 mfukoni,hiyo ilikuwa ni posho tu!.

Nilipokusanya pesa ya kutosha,ndani ya mwezi huo nilitafuta chumba cha elfu 15000 nikapanga!.

Sasa kwakuwa sikuwa na hela ya kununua godoro,nilienda kwenye duka nikanunua maboksi ya kutosha kutandika chini ili nikilala nisije nikaumia mbavu!.

Muendelezo soma >>Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani
Mama yako mkubwa, hakukutafuta kipindi chote hiko ulichosepa na Rafiki yako? Maana ulindoka ghafla, ukamwacha mtoto wa Ma mkubwa wako akichunga?
 
Back
Top Bottom