mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Kule New York kuna makaburi fulani yanaitwa Green Wood Cemeteries, pale hazikwi mtu yoyote, ni mastaa na matajiri, unalipia hela nyingi.nilikuwa naona kama uchuro fulani kununua sehemu utakayozikwa ila baadae nilijua umuhimu wake.
Hata hapa nchini utaratibu huo upo wa kununua plot mapema ya sehemu utakapozikwa siku ukifa(nadhani tunafahamu makaburi ya xxxxxx sio kila mtu anazikwa pale, yako reserved)
Miaka kadhaa iliyopita niliona si vibaya na mimi nilipie 'plot yangu'
Unajua sie tuliozaliwa mjini ukizubaa ukikata moto utazikwa Mbagala bila kupenda na miaka yote ukiwa hai uliponda kuishi Mbagala
Nilijenga utamaduni wa kutembelea ile 'plot' yangu na kuwasalimia walinzi wa pale
Kuna siku nikapigiwa simu na mlinzi akidhani nimekufa maana kuna watu wanachimba kwenye 'plot' yangu nikamwambia mi ni mzima nakuja fasta.
Kufika pale nakuta maandalizi ya kumzika yule mfanyabiashara kwenye the so called kaburi langu nikiwa na full documents za malipo.
Kimbembe niligoma kabisa asizikwe pale maana nilikuwa na rafiki yangu ni askari niliambatana nae akiwa kwenye gwanda.
Kilichofuata ile plot ilibidi watupe hela ndefu nadhani ni balance ya michango ya msiba. Ile hela nisingeweza kuiacha, niliichukua na kutatulia matatizo yangu.
Nikifa nizikeni popote tu