wa kupuliza
JF-Expert Member
- Jun 15, 2012
- 15,216
- 37,757
Kwa hio motivational speaker unashaurije hapo?Hakuna biashara hapo,faida wastani laki moja kwa mwezi na biashara imejaa risk na changamoto lukuki
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hio motivational speaker unashaurije hapo?Hakuna biashara hapo,faida wastani laki moja kwa mwezi na biashara imejaa risk na changamoto lukuki
We nae umekuja na hivyo vingereza tu....sioni cha tofauti na alichokieleza mtoa mada, Utakuwa mhaya wewe sio bureHongera mkuu…
Mchanganuo wako unapaswa kuwa hv:-
Sales (mauzo ya Komodo)
- purchases (ununuzi wa Komodo)
- Closing (Kama kuna kondoo hukumuuza)
= Utapata: Gross profit (Faida ghafi)
Afu:- utatolea hzo gharama zengne za kuendeshea hyo biashara (Operating cost)
=baada ya apo utakachopata ni faida kamili (net profit)
Hakuna biashara hapo,mtivation speaker ni huyo mtoa uzi sio mimi laki nane miezi nane ni kupoteza mudaKwa hio motivational speaker unashaurije hapo?
Kumbuka yuko kwenye ajira, hiyo ni sehemu nyingine ya kuweza kujiongezea kipato, hata kama ingekuwa ni elfu 50 kwa mwezi lakini amethubutu kufanya, maana ya biashara ni kuuza na kupata faida hakuna hasara aliyoipata, kutengeneza laki 8 kwa miezi 8 sio kitu kidogo kuwa jobless ndio utajua vzr, tuheshimu mawazo ya watu usipoona faida kwako kuna mwingine ni faida kwake. Kuna wengine watanufaika kupitia mawazo yake aliyowasilisha kwa namna moja au nyingine.Hakuna biashara hapo,faida wastani laki moja kwa mwezi na biashara imejaa risk na changamoto lukuki
Sasa mkuu mauzo utaitaje faida…!!Wasomi uchwara mmeanza tena mambo Yenu.
Mkuu mbona kiswahili hicho apo…hv kweli faida na mauzo vinafanana!!We nae umekuja na hivyo vingereza tu....sioni cha tofauti na alichokieleza mtoa mada, Utakuwa mhaya wewe sio bure
FAIDA NI NINI?Hakuna biashara hapo,faida wastani laki moja kwa mwezi na biashara imejaa risk na changamoto lukuki
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wasomi uchwara mmeanza tena mambo Yenu.
FAIDA NI NINI?
Tuanzie hapo, huenda faida ina maana tofauti kwa upande wako. Nitaeleza namna ninavyojua nin maana ya faida alafu naomba na wewe utueleze faida kwako ni nini.
Faida ni ongezeko la pesa, thamani ya bidhaa baada ya kuuza.
Mfano No. 1 :-nimenunua gari china millioni 3 nikasafirisha mpaka TZ, gharama za kununua na usafirishaji na kila kitu ikawa millioni 10. Alafu nikaliuza hilo gari kwa Millioni 15. Nitakuwa nimelata faida ya 5M
Mfano No. 2 :- nimenunua suruali elfu 10 kariakoo nikaileta hostel za magufuli nikaiuza elfu 14. Kununua, kuifata na kuieleta mahali nimeuza imenigharimu elfu 12 Hivyo basi nitakuwa nimepata faida ya elfu 2
Nimetoa mifano miwili hapo juu ili kuonesha faida ni pesa yoyote iliyokngezeka aidha iwe kubwa au ndogo. Aliyeuza gari amepata faida ya 5M na aliyeuza suruali kapata faida ya elfu 2
Zote ni faida hizo mbili ni faida. Faida ni kuuza zaidi ya ulivyonunua na gharama za uendeshaji kama business itakubidi ufanye hivyo. Haijilishi ni kubwa sana au ndogo sana.
Nataman kuandika mambo mengi zaidi ila i hope umenielewa
Sawa ila faida ikiwa ndogo na huuku risk ziko nyingi ksma za mleta uzi kuna hatari ya kukata mtaji siku si nyingiFAIDA NI NINI?
Tuanzie hapo, huenda faida ina maana tofauti kwa upande wako. Nitaeleza namna ninavyojua nin maana ya faida alafu naomba na wewe utueleze faida kwako ni nini.
Faida ni ongezeko la pesa, thamani ya bidhaa baada ya kuuza.
Mfano No. 1 :-nimenunua gari china millioni 3 nikasafirisha mpaka TZ, gharama za kununua na usafirishaji na kila kitu ikawa millioni 10. Alafu nikaliuza hilo gari kwa Millioni 15. Nitakuwa nimelata faida ya 5M
Mfano No. 2 :- nimenunua suruali elfu 10 kariakoo nikaileta hostel za magufuli nikaiuza elfu 14. Kununua, kuifata na kuieleta mahali nimeuza imenigharimu elfu 12 Hivyo basi nitakuwa nimepata faida ya elfu 2
Nimetoa mifano miwili hapo juu ili kuonesha faida ni pesa yoyote iliyokngezeka aidha iwe kubwa au ndogo. Aliyeuza gari amepata faida ya 5M na aliyeuza suruali kapata faida ya elfu 2
Zote ni faida hizo mbili ni faida. Faida ni kuuza zaidi ya ulivyonunua na gharama za uendeshaji kama business itakubidi ufanye hivyo. Haijilishi ni kubwa sana au ndogo sana.
Nataman kuandika mambo mengi zaidi ila i hope umenielewa
Hata mimi nimewaza kama weweVipi kama ukiamua kununua na kwenda kuuza? Yaani tofauti na kusubiri miezi yote hiyo ndio uuze, namanisha nanunua leo kisha nafanya harakati za kwenda kuuza ndani ya siku mbili.
Hajapata shuruba za kuwaswaga kila sikuHata mimi nimewaza kama wewe
Maana alipata faida ya 800000 kwa miezi 9 so hapo alipata faida ya elfu 90 tu kwa kila mwezi ongeza na shuruba zote za kuwaswaga kila siku.
Hiyo pesa ingekuwa na value kama angeuza kwa muda mfupi
Haha ndio Kaka, Kupanga ni kuchagua tu.Bro yani umetumia miez 8 kutengeneza faida ya laki 8 ??
Asante sana mkuu.Mi nakusifu kwa kuwa pamoja na hiyo faida uliyoipata,
Umechangia pia kupata fedha za kigeni maana ni exporter wewe, hata kama labda ni 0. xx ni pato la taifa hilo ✌🤭
Asante sana kaka kwa maelezo yako. Nadhani umeelezea zaidi kwa kadri biashara inavyo tofautiana. Kufuga kwangu na kuuza ilikuwa kwa Mara ya kwanza.Faida ipo: 100,000 kwake ni kubwa ukizingatia ana kazi nyingine inayomuingizia kipato.Pili kajifunza jinsi ya kufanya biashara, kwahiyo hapo ana uzoefu mdogo wakati mwingine ataanza na mtaji mkubwa na kupata faida kubwa.
Tatu katoa elimu kuhusu ufugaji wa kondoo, mfano mimi sikuwa ninafahamu mbuzi ni rahisi kufuga kuliko kondoo.
Nne katoa hamasa kwa vijana wafuge au wafanye biashara ya kondoo.Hizo zote ni faida tusiangalie tu fedha zinazoingia.
Asante sana kwa uchambuzi wako mkuu.Hajapata shuruba za kuwaswaga kila siku
Labda hukumuelewa vizuri, alikuwa na mchungi aliyekuwa akimlipa. Na pia amesema unaweza ukanunua na kuuza hapo hapo hasa masoko ya nje lakini ukiwa na mtaji mkubwa ndo faida utaiona vizuri
Na akasema wapo wanaofanya hivyo na mara nyingi wanawauzia Kenya ndo soko lipo kubwa huko kuliko TZ
Salamu Wakuu wa Jukwaa.
Mimi ni moja ya wafanyakazi katika Taasisi wilaya Ya Ngorongoro Mkoani Arusha, mahala nilipo ajiriwa ni karibu sana na Kenya almost kilomita 20 kuingia nchi Jirani. Huku kabila kubwa ni Wamasai.
Mwaka jana mwezi wa 8 Nilipata wazo la kuanzisha biashara hii hasa kutokana na wilaya hii kujaliwa kuwa na mifugo wengi pamoja na eneo kubwa la malisho kwa Ng'ombe pamoja na Kondoo.
Nikatafuta mchungi mmoja ambaye alikuwa rafiki yangu kwa muda mrefu ambaye alinielekeza namna biashara inavyoenda pamoja na soko lake lilivyo katika miezi huska. Alinishauri mengi pamoja na kuniambia gharama za uchungi pamoja na dawa za kunenepesha. Alinifahamisha nikiwa tayari atachunga pamoja na Kondoo na Ng'ombe wake kwa Pamoja.
Nilipata ushauri mwingi lakini kwa kuwa nilikuwa na mtaji kidogo alinishauri nifuge Kondoo badala ya kununua ndama.
Tulienda mnadani Wote pamoja na mchungi kutokana na kufahamika maeneo yale pamoja na lugha ya eneo huska ambapo tulinunua Kondoo 23. Ilikuwa ni mwisho wa mwezi wa 8, 2021 na Kupanga kuja kuwauza Mwezi wa 4, 2022.
GHARAMA ZA UNUNUZI WA KONDOO PAMOJA NA MENGINEYO
Nilinunua Kondoo 20 kwa gharama ya 70,000/= kila mmoja.
23 x 70,000/= Jumla 1,610,000/=
Gharama za usafirishaji wa Kondoo kipindi cha ununuzi, Kondoo mmoja 2,000/=
23 x 2,000/= Jumla 46,000/=
Gharama za Uchungi kwa mwezi ni 20,000/= ambapo Jumla ni miezi 9
9 x 20,000/= Jumla 180,000/=
Gharama za dawa ya kunenepesha Kondoo kwa miezi 8 kila mwezi nilitumia 25,000/=
8 x 25,000/= Jumla 200,000/=
Gharama za kusafirisha kwenda kuuza, Kila Kondoo 3,000/= ambapo tuliwauza nje ya nchi jirani Kenya.
23 x 3,000/= Jumla 69,000/=
FEDHA niliyopata baada ya Kuuza Kondoo, Jumla kuu ni 2,905,000/=
FAIDA NILIYOPATA BAADA YA GHARAMA ZILIZOKUWEPO
(Faida 2,905,000/=) - (Gharama 1,610,000/= + 46,000/= + 69,000/= + 200,000/= + 180,000/=)
(Faida 2,905,000/=) - (Gharama 2,105,000/=)
FAIDA KUU = 800,000/=
CHANGAMOTO
1. Soko la bei ya kondoo kushuka ndani ya muda na kusababisha Faida ndogo sana.
2. Kuwepo na changamoto ya wanyama wakali kama Fisi na Chui ambao husababisha kufa kwa mifugo.
3. Mifugo/Kondoo kuugua hasa kipindi cha mvua na kusababisha hasara.
4. Mifugo/Kondoo kukosa malisho stahiki hasa kipindi cha ukame kuanzia mwez wa 8 hadi wa 11 na kupelekea kufa. Hasa Ng'ombe ndo hufa kipindi hiki kwa kukosa Majani.
5. Kubadilishiwa mifugo na mchungi hasa usipokuwa makini kwa kuto kuwatembelea mara kwa mara.
6. Malisho kutokana na kukosekana kwa maeneo ya kulishia kwa sasa hasa baada ya maeneo mengi kuchukuliwa na Serikali na kuwa PORI TENGEFU.
7. Kondoo wanahitaji matunzo mengi (gharama) sana tofauti na Mbuzi pamoja na Ng'ombe.
USHAURI
1. Biashara ya kunenepesha ina Faida kubwa sana hasa ukiwa mkazi wa eneo lenye malisho ya kutosha na ukiwa unawapatia dawa. Kondoo wengi zaidi ndo Faida kubwa zaidi.
2. Ufugaji ni kama kuwekeza benki maana ukipata shida tu unaweza kuuza Kondoo/mifugo baadhi na kutatua tatizo huska.
3. Kupitia ufugaji unaweza kupata maziwa, nyama, ngozi pamoja na mengineyo mengi.
Asanteni. Wekeza!
Hongera sana kwa huu uelewa.Faida ipo: 100,000 kwake ni kubwa ukizingatia ana kazi nyingine inayomuingizia kipato.Pili kajifunza jinsi ya kufanya biashara, kwahiyo hapo ana uzoefu mdogo wakati mwingine ataanza na mtaji mkubwa na kupata faida kubwa.
Tatu katoa elimu kuhusu ufugaji wa kondoo, mfano mimi sikuwa ninafahamu mbuzi ni rahisi kufuga kuliko kondoo.
Nne katoa hamasa kwa vijana wafuge au wafanye biashara ya kondoo.Hizo zote ni faida tusiangalie tu fedha zinazoingia.