FAIDA NI NINI?
Tuanzie hapo, huenda faida ina maana tofauti kwa upande wako. Nitaeleza namna ninavyojua nin maana ya faida alafu naomba na wewe utueleze faida kwako ni nini.
Faida ni ongezeko la pesa, thamani ya bidhaa baada ya kuuza.
Mfano No. 1 :-nimenunua gari china millioni 3 nikasafirisha mpaka TZ, gharama za kununua na usafirishaji na kila kitu ikawa millioni 10. Alafu nikaliuza hilo gari kwa Millioni 15. Nitakuwa nimelata faida ya 5M
Mfano No. 2 :- nimenunua suruali elfu 10 kariakoo nikaileta hostel za magufuli nikaiuza elfu 14. Kununua, kuifata na kuieleta mahali nimeuza imenigharimu elfu 12 Hivyo basi nitakuwa nimepata faida ya elfu 2
Nimetoa mifano miwili hapo juu ili kuonesha faida ni pesa yoyote iliyokngezeka aidha iwe kubwa au ndogo. Aliyeuza gari amepata faida ya 5M na aliyeuza suruali kapata faida ya elfu 2
Zote ni faida hizo mbili ni faida. Faida ni kuuza zaidi ya ulivyonunua na gharama za uendeshaji kama business itakubidi ufanye hivyo. Haijilishi ni kubwa sana au ndogo sana.
Nataman kuandika mambo mengi zaidi ila i hope umenielewa