Nilivyopata faida ya 800k kwa Biashara ya Kondoo

We nae umekuja na hivyo vingereza tu....sioni cha tofauti na alichokieleza mtoa mada, Utakuwa mhaya wewe sio bure
 
Hakuna biashara hapo,faida wastani laki moja kwa mwezi na biashara imejaa risk na changamoto lukuki
Kumbuka yuko kwenye ajira, hiyo ni sehemu nyingine ya kuweza kujiongezea kipato, hata kama ingekuwa ni elfu 50 kwa mwezi lakini amethubutu kufanya, maana ya biashara ni kuuza na kupata faida hakuna hasara aliyoipata, kutengeneza laki 8 kwa miezi 8 sio kitu kidogo kuwa jobless ndio utajua vzr, tuheshimu mawazo ya watu usipoona faida kwako kuna mwingine ni faida kwake. Kuna wengine watanufaika kupitia mawazo yake aliyowasilisha kwa namna moja au nyingine.
 
We nae umekuja na hivyo vingereza tu....sioni cha tofauti na alichokieleza mtoa mada, Utakuwa mhaya wewe sio bure
Mkuu mbona kiswahili hicho apo…hv kweli faida na mauzo vinafanana!!
 
Hakuna biashara hapo,faida wastani laki moja kwa mwezi na biashara imejaa risk na changamoto lukuki
FAIDA NI NINI?

Tuanzie hapo, huenda faida ina maana tofauti kwa upande wako. Nitaeleza namna ninavyojua nin maana ya faida alafu naomba na wewe utueleze faida kwako ni nini.

Faida ni ongezeko la pesa, thamani ya bidhaa baada ya kuuza.

Mfano No. 1 :-nimenunua gari china millioni 3 nikasafirisha mpaka TZ, gharama za kununua na usafirishaji na kila kitu ikawa millioni 10. Alafu nikaliuza hilo gari kwa Millioni 15. Nitakuwa nimelata faida ya 5M

Mfano No. 2 :- nimenunua suruali elfu 10 kariakoo nikaileta hostel za magufuli nikaiuza elfu 14. Kununua, kuifata na kuieleta mahali nimeuza imenigharimu elfu 12 Hivyo basi nitakuwa nimepata faida ya elfu 2

Nimetoa mifano miwili hapo juu ili kuonesha faida ni pesa yoyote iliyokngezeka aidha iwe kubwa au ndogo. Aliyeuza gari amepata faida ya 5M na aliyeuza suruali kapata faida ya elfu 2

Zote ni faida hizo mbili ni faida. Faida ni kuuza zaidi ya ulivyonunua na gharama za uendeshaji kama business itakubidi ufanye hivyo. Haijilishi ni kubwa sana au ndogo sana.

Nataman kuandika mambo mengi zaidi ila i hope umenielewa
 
Hongera kwa kujaribu mleta mada..hongera pia kwa kuhamasisha vijana wawekeze.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sawa ila faida ikiwa ndogo na huuku risk ziko nyingi ksma za mleta uzi kuna hatari ya kukata mtaji siku si nyingi
 
Ufugaji una changamoto nyingi

Kama unavyosema mifugo hufa kwa kukosa majani au maji

Sasa kwa Sisi hatuko serious kwenye ufugaji wa kibiashara kwani ukiangalia duniani nchi nyingi hata jirani tu kama Zimbabwe, Uganda na hata South Africa wanalima mahindi kwa ajili ya mifugo

Wakati leo ukimuambia mfugaji wa Tanzania alime kwa ajili ya mifugo yake atakuona mwehu

Ila mifugo inapokufa kwa njaa akili hazimrudii akawaza zaidi na hata kuwa na majani makavu aliyoweka wakati wa masika

Mifugo ya Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo hatuwatunzi vizuri lakini nao wanatakiwa watunzwe kama Kuku tu kwa lishe badala ya kutegemea malisho ya majani yalioota

Hili tatizo la kusema mifugo imekufa kwa njaa naona ni kujitakia tu na kukosa maarifa
Sio naponda hapana bali ndio uhalisia wenyewe

Kuna nchi za jangwa lakini mifugo inavyonenepa utashangaa kwa matunzo ya hali ya juu

Ni gharama inatakiwa lakini pia fikiria una mifugo walioshiba haswa na Bei inakuwa juu pia
 
Vipi kama ukiamua kununua na kwenda kuuza? Yaani tofauti na kusubiri miezi yote hiyo ndio uuze, namanisha nanunua leo kisha nafanya harakati za kwenda kuuza ndani ya siku mbili.
Hata mimi nimewaza kama wewe

Maana alipata faida ya 800000 kwa miezi 9 so hapo alipata faida ya elfu 90 tu kwa kila mwezi ongeza na shuruba zote za kuwaswaga kila siku.

Hiyo pesa ingekuwa na value kama angeuza kwa muda mfupi
 
Hata mimi nimewaza kama wewe
Maana alipata faida ya 800000 kwa miezi 9 so hapo alipata faida ya elfu 90 tu kwa kila mwezi ongeza na shuruba zote za kuwaswaga kila siku.
Hiyo pesa ingekuwa na value kama angeuza kwa muda mfupi
Hajapata shuruba za kuwaswaga kila siku
Labda hukumuelewa vizuri, alikuwa na mchungi aliyekuwa akimlipa. Na pia amesema unaweza ukanunua na kuuza hapo hapo hasa masoko ya nje lakini ukiwa na mtaji mkubwa ndo faida utaiona vizuri

Na akasema wapo wanaofanya hivyo na mara nyingi wanawauzia Kenya ndo soko lipo kubwa huko kuliko TZ
 
Ulitumia Dawa gani y kunenepesha kila mwezi ulizo kua unawapatia kondoo.?
 
Asante sana kaka kwa maelezo yako. Nadhani umeelezea zaidi kwa kadri biashara inavyo tofautiana. Kufuga kwangu na kuuza ilikuwa kwa Mara ya kwanza.

Biashara ukifanya kwa Mara ya kwanza na kunielewa unaelewa mengi zaidi na nimejifunza mengi sana.
 
Asante sana kwa uchambuzi wako mkuu.
 
Vipi mkuu hujarudia hii biashara tupate uzoefu wa ziada?
 
Hongera sana kwa huu uelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…