SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

Stories of Change - 2022 Competition

Theorist Mosses

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
345
Reaction score
253
Habari, ndugu jamaa na marafiki kwa jina naitwa Moris, nilizaliwa mkoa wa mara nilisoma na kumaliza masomo ya sekondari na kufaulu vizuri mkoani mara.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari nili jiusisha na kazi ya ufundi umeme wa majumbani, ambapo kazi hii hapo awali alikuwa akifanya baba yangu.

Ndoto yangu ilikuwa nikuja kuwa rubani wa ndege na nilipenda sana maswala ya utafiti na uchunguzi. lakini pia nilipenda kushirikiana na watu wadogo kwa wakubwa, pamoja na kujifunza "kinaganaga" vitu vingi sana.

Kama vile usomaji wa vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu vya dini na bidii katika kazi ya ufundi umeme ilinisaidia sana. lakini pia nilifanya bidii katika ibada, ambapo nilikuwa nikifanya bidii ili nije kutimiza ndoto yangu ambayo ni kuja kufanya kazi ya urubani wa ndege.

Katika chunguzi na tafiti zangu Kwa mara ya kwanza nilifanikiwa kutengeneza mashine ya kuzarisha umeme, ambayo ilifanya kazi vizuri lakini nakumbuka mashine hii ilinipa "wigo" msukumo mzuri wa kuiboresha mashine iwe bora zaidi. sikuishia hapo lakini nilijiendeleza kwa kujifunza kupitia vitabu vya kisayansi, ambapo baadae nilipata "shauku" iliyo nipelekea kufanikiwa kwa wazo la kutengeneza helikopta.

Nadhani nilitengeneza kitu bora na cha tofauti kuliko ninavyokielezea hapa. lakini kwa sababu sikuwa na vibali maalum kutoka vitengo husika vya kiserikali pamoja na mamlaka ya anga ilinipelekea kufungiwa kwa sababu ya kukosa vigezo sababu nyengine sikuwa na reseni.

Pengine wapo vijana wenzangu wengi sana mitaani, ambao hawaja fahamika "kinagaubaga" Kutokana na kazi zao. Ingawa pamoja na mapinduzi makubwa ya teknolojia walio yafanya ndani na nje ya Tanzania, wenye ndoto sawa na zangu lakini wame fukiwa kwenye shimo "kindakindaki" hata wasiweze kupewa nafasi ya kuonesha maarifa walio nayo na vipaji vyao.

Matokeo yake wanatokea watu wenye jicho la "husuda" ambao wasiokuwa na maslahi bora kwa vijana pamoja na taifa kwa ujumla. ambao wanafanya kazi ya kuzima vipaji kupitia madaraka na siyo kwamba nchi yetu hatuwezi kuendelea kwenye maswala ya kisayansi na kiteknolojia "la hasha" kumbe tunajiangamiza wenyewe na kujiteketeza "kimasomaso" bila kujua.

Kupitia kwa vijana wanao zaniwa kuwa wao siyo kitu na kufungiwa kazi zao kwasababu zisizo za msingi, matokeo yake wanaendeleza watu wasio na ujuzi wowote kwenye hizo fani ambapo inapelekea taifa kuzidi kushuka kimaendeleo na kiuchumi.

Nina imani kwamba kitaka kila kizazi kipya ndani ya kila miaka mitano, lazima kuna vijana wenzangu wanao chipuka kwenye fani mbalimbali kwenye nyanja zote ambao naweza kusema ni vijana hodari sana ambao hawaja somea kwenye hizo fani walizopo.

Taifa zuri hujengwa na vijana, watu wengi wamekuwa wakishuhudia vijana ambao tunaishi nao tu mitaani. wengine ni ndugu zetu tumeona vipaji vyao walivyo vionesha kwa njia mbalimbali lakini kwa sababu ya kutoendelezwa imewapelekea kualibikiwa kisaikolojia matokeo yake kuanguka kwenye "ngada" na madawa ya kulevya.

Najua wapo vijana wenzangu miongoni mwetu walio fanikiwa kutengeneza vitu vingi vikubwa zaidi yangu, lakini wameshindwa kujiendeleza katika nyanja zote ikiwemo katika sayansi na teknolojia. pamoja na kwamba vitu walivyo vitengeneza vimeonekana lakini kwa sababu ya kuto kizi vigezo vya kiserikali wamefungiwa.

Hivyo naungana pamoja na vijana wenzangu kutoa "lai" kwa serikali, iangalie kwa ukaribu namna bora ya kutuendeleza sisi vijana kwenye nyanja zote. kwamba vijana wapewe kipaumbele itapelekea vijana wengi kupata "hulka" ya ajira na kujiamini pamoja na kuimarika kisaikolojia.

Hakika"penye nia pana njia"Itasaidia sana pia kuwavuta vijana wengine wa mitaani kupata fursa kuacha tabia ambazo ni mbovu mara moja. kama vile "panya road" tabia ambazo zinaweza kuyumbisha au kuangusha kabisa uchumi wa taifa, jambo ili nalitazama kwa mapana zaidi kwa sababu vijana ni "mbegu" ambazo zina paswa kuangaliwa ili ziweze kustawi vizuri zitazamwe Kama kitovu cha taifa la kesho.

Serikali ihakikishe vijana wanapata haki zao za msingi, iwapo kama ikitokea kuna kijana amegundua kitu flani ndani ya sayansi na kwamba kipaji chake kimeonekana na kuthibitishwa tayari.

Serikali isimfungie kwa sababu kwa kufanya hivyo itamuharibu kijana kisaikolojia, kama ikatokea ajakizi vigezo asifungiwe lakini iangaliwe namna bora ambapo kijana aweze kupata kibali pamoja na elimu zaidi. kwasababu kwakufanya hivyo taifa litakuwa linapanda "mbegu" iliyo bora na imara zaidi kwa ajiri ya maendeleo bora na kupata vijana wenye ujuzi.

Kama ikitokea kijana hana elimu ya kutosha kwamba ameshindwa kupata kibali kwa sababu ya elimu ndogo aliyo kuwa nayo. Lakini tukirudi kwenye uwezo wake na ujuzi kwamba kipaji chake tayari kime onekana pamoja na kuthibitishwa na wataalam mbalimbali wa serikali basi kijana asomeshwe.

Serikali na vyombo husika vichukulie kwa mitazamo mipana sana na kwaajiri ya sayansi na teknolojia ya taifa la kesho. ili kijana anapo maliza masomo afanye kazi ya ndoto zake kwasababu kipaji ni "kimwasu" naamini kwa namna moja ama nyengine kwa njia hii nchi yetu itaendelea kiuchumi katika nyanja zote ikiwemo kwenye ajira, sanaa, elimu, michezo, sayansi na teknolojia.

Lakini pia wazazi na walezi muhakikishe mnakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wanapata malezi na ushauri mzuri ulio bora wenye tija ndani yake. ambayo ni njia itakayo wafanya vijana kujisikia kuwa wao ni watu wa muhimu sana wanaohitajika na wenye mchango mkubwa ndani ya jamii inayo wazunguka. Ili waimarike vizuri kisaikolojia pamoja na kuwakumbusha vijana kwenda na kuhudhulia kwenye nyumba za ibada ili kukomesha tabia chafu za vijana Kama vile. kushinda kijiweni mda wote, kujiunga na makundi ya kijambazi, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.
 
Upvote 53
Tukisema kuwa kabla ya kuwepo chochote hata hilo giza halikuwepo.

Giza limeanza kuwepo baada ya kugawanya sifuri fulani kuwa pande mbili za giza na mwanga.

Mwanzoni ilikuwa ni hamna/nothingness/utupu yaani ziiiip
Sifuri inagawanyaje Giza na mwanga hebu nitumie hiyo formula tugawanye hapa ?

Unajua nini maana ya mwanga?
 
Tafathali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshale "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Sifuri inagawanyaje Giza na mwanga hebu nitumie hiyo formula tugawanye hapa ?
Sifuri ni hamna, wewe tafuta utafutavyo ukiipata hamna katika ulimwengu huu ilete hapa tuigawanye tupate vitu vipya. Kimsingi lakini hiyo huwa ni kazi ya Mwana wa Mungu na Roho wa Mungu - Ndio wanaofahamu maisha katika sifuri na mahali pa kuipata sio sisi. Sisi tumeibukia tu sifuri ilishagawanyagwa zamaaaaaaaaaani huko
Unajua nini maana ya mwanga?
Mwanga kwa tafsiri sipo deep lakini najua kinyume chake ni giza.
 
Tafathali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshale "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Tafathali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshale "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Ya kuambiwa changanya na zako ingekuwa hevyo watu huko russia na ulaya ambako ndiko zinanyweka sana
 
Punguza hizi sasa. Utaharibu andiko lako kwa kuonekana uko desperate...

Unaweza ukawa unakumbusha mara moja moja tu inatosha.

Na kupigiwa kura nyingi haina maana kuwa ndiyo utashinda.

Mwaka jana aliyepata kura nyingi hata hakuwemo miongoni mwa washindi labda mwaka huu wawe wamerekebisha.

Kama ni andiko lenye kugusa jamii na lenye manufaa watu watakupa tu kura usiwe na wasiwasi. Hata wasipokupa utakuwa tu miongoni mwa washindi hivyo usijipe presha sana mpaka kugeuka ombaomba...
 
Tafathali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshale "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
Tafathali [emoji777]️[emoji777]️[emoji777]️
Tafadhali [emoji736]️[emoji736]️[emoji736]️
 
Una picha yo yote ya hiyo helicopter uliyowahi kutengeneza? Unaweza kuiweka hapa?

Iliweza kuruka?

Umbali gani?

Uliishia kuiuza au ilikuwaje?

(Sijasoma andiko lako lote...labda baadaye kidogo)
 
Tafathali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshale "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Back
Top Bottom