Nilivyowahi kutapeliwa na aliyejitambulisha ni polisi nikiwa jiji la Arusha

Nilivyowahi kutapeliwa na aliyejitambulisha ni polisi nikiwa jiji la Arusha

Utapeli hauna mjanja, yeyote akifikiwa lazima aliwe.

Nimekuwa msomaji sana wa visa na mikasa inayowatokea watu na nimeweza kupata experience, mafunzo, kujua kujitahadhari, n.k. Leo nimeoamua na mimi niweze kuwaletea mkasa uliowahi kunitokea mwaka 2014 jiji la Arusha nikiwa mwanachuo wa chuo cha uhasibu, IAA.

Likizo ilipoisha nikiwa Mbeya, nikageuza kurudi Arusha, safari ilikuwa ndefu na hatimae nikafika saa nane usiku, kipindi hicho barabara zilikuwa mbovu mkiwahi ilikuwa saa sita usiku, kawaida ilikuwa sa saba hadi saa tisa.

Basi lilikuwa ni la Sumry / Arusha Express likafikia kituo cha mwisho stendi ofisi za Dar Express, guest mbili za karibu niliyozoea kulala kwa elf 10 & 15 zimejaa, Kuna teksi ilipaki kidogo hapo stendi, kuulizia bei ya kwenda njiro ni elf 25, bei ya mwisho kakazia 20, mi niliona nachoma pesa nikomae tu hapo masaa kadhaa panakucha nipande daladala, bodaboda sikufikira nilihofia wanaweza kucheza michezo ya kunigeuka njiani (Arusha miaka hio ilikuwa yamoto)

Nikaamua nikomoae nishinde pale pale stendi ya Dar Express pamoja na walinzi, nisubiri masaa matatu ama manne, pakipambazuka nianze kwenda Njiro chuo kilipo na ninapoishi. Kiukweli usingizi ulikuwa mzito ila nilijikaza hadi alfajiri.

Kwenye saa 11 na dakika kadhaa nikaanza kushuka kwenda stendi ya Crdb lile tawi kuu karibu na maduka ya Benson, nimefika stendi nikapanda kifodi (daladala), kulikuwa na waru wanahesabika, bado konda anaendelea kutafta abiria,

Ghafla kuna mtu akaja ambae kwa haraka haraka kimavazi ni polisi yupo yupo na mwenzake ambae kavalia nguo za raia kwa unadhifu, wakaniambia nishuke pale na begi, niliwaambia kuna nini ila wao wakakaza nipo chini ya ulinzi nishuke, kiukweli niliingia na woga hasa ukizingatia ni polisi kabisa, hata dereva na konda hawakuthubutu kuzungumza chochote.

Nikashuka na begi langu, tukaelekea kwenye gari ni kama taxi hivi, nilikaa siti ya nyuma pamoja na yule polisi, alikuwa ni mbaba flani hivi mrefu kimtindo, mweupe japo kwa mbali yule mwegine ambae kavalia nguo za uraia akakaa siti ya mbele kwenye usukani.

Huko siti ya nyuma yule askari akaanza kuniambia "tumekufatilia ukiwa unavuta begi hili (lenye matairi) tumpeta intelejensia humu kuna bangi" , dah nilipaniki. tukaanza kuzozana pale mimi sijabeba kitu wakitaka wafungue begi, nikataka kufungua mlango niondoke maana huo ni uhuni, yule mwenzake akafunga mlango, nikataka nipige kelele kuomba msaada! hata sijamaliza nikapigwa kofi wakaniambia nikirudia watanimaliza, nikifikiria Arusha watu kutembea na visu kawaida nikatulia !

Gari ikaanza kutembea ila hatuendi kule kaloleni kituo cha polisi, askari wa siti ya nyuma akaanza kupiga search begi langu, hapo najua tayari hawa ni wahuni tu na si ajabu wakaniwekea bangi ya kubambikiwa, nachowaza hapo ni kwamba nipo mtu kati, wahuni wamenibananisha na nikawa nawaza mbali zaidi kama watanidhuru maana kipindi hicho matukio ya kuchomana visu kwa Arusha ilikuwa ni kawaida na navyosema visu ni hizi sime kama za wamasai zimenolewa haswa, mwaka uliopita kwa pale chuoni kunamwenzetu alivamiwa na wahuni wakamuua kwa kumpiga visu, Tulijaribu kuandamana ila Ffu wakaja kama kawaida yao kipigo kwanza maelezo baadae, binafsi nashukuru sikukamatwa wala kupigwa.

Kwenye begi kulikuwa na nguo, vyeti vya sekondari na kuzaliwa, laptop na shilingi laki 2 na nusu ipo kwenye kabahasha, yule afande alichukua hela yote, vingine aliacha. mfukoni nilikuwa na elf 6 tu na simu.

Gari ikafika kituo cha Kijenge pale uwanjani kwenye mabasi yanayoenda njiro, nikaambiwa nishuke na begi langu, wanavyoondoka tu kitu cha kwanza nilinakili plate number, nazikumbuka hadi leo T2—ACB (kwenye dash hapo sikumbuki kwa uhakika ila picha inanijia ni T212 ama T232) ila sikuweza kuhitimisha kwa uhakika kama zilikuwa ni plate number za ukweli au za kufanyia utapeli wao wasigundulike kirahisi.

Basi mimi cha muhimu nikashukuru nipo salama na wameniachia begi lenye vitu muhimu kwajili ya chuoni.

Nilienda hostel nikaweka begi langu, nikaanza safari ya kwenda Kaloleni kituo cha polisi, nilikata RB nimeibiwa na Polisi lakini hata pale counter walishangaa sana. navyoondoka hapo kituoni kuna afande alikuwa analinda nje pale, aliniomba namba ya gari nikampa, nikaondoka.

Zaidi ya hapo niliwapigia wazazi simu kuwajulisha hali iliyonipata, ila wakaniasa nisifatilie niachane nao maana wanaweza kuwa watu hatari, Nashukuru pia waliweza kunitumia kiasi cha fedha kufidia fidia kilichopotea.

Kuanzia hapo nilijifunza kufanya booking ys vhumba cha gesti mapema hata siku 2 kabla sijafika Arusha, pia nilipata namba ya dereva Taxi mwaminifu.

Funzo nililopata ni kufanya kila jitihada kudeal na mambo haya hadharani sehemu yenye watu bila aibu, hawa jamaa moja ya mbinu yao kuu ni kuhakikisha wanakupeleka mazingira ambayo yana usiri wawe peke yao na wewe.
Arusha usela mavi mwingi ni kawaida kubadi baadhi ya maneno na kuongea mengine ya ajabu ajabu
 
Muonekano ndgu, ulionekana boya. Au labda ulikumbatia begi lako na uoga kama wote wakawa wanakuchora tu.

Hata mm nilitapeiliwa kiboya zaidi yako ni muonekano tu, mtu anakuchora the way unarespond anajua hili kolo.
Utapeli hauna formula, nikujuze tu ya kwamba hata mawaziri, maprofesa, wafanya biashara wakubwa, wasanii, wanatapeliwa.

factors za kutapeliwa ni nyingi sana,
 
usimcheke mtu kisa alitapeliwa au kuporwa
Hii tabia ya kuchekana kwa hapa kwetu ndio inarahisisha zaidi utapeli.

Mtu akitapeliwa anaona soo kuwaambia wengine anaogopa atadharaulika na kuchekwa, ajabu ni kwamba hata hao wataomcheka washapigwa na vitu vizito walipotezea kimya kimya.

Kuna mtu huu uzi kakomenti kwa kebehi ila nimefatilia post zake za nyuma alikuwa analalamika mganga kamtapeli dawa ya biashara

Nchi za wenzetu kuna magroup kabisa ya kuhaarishana mambo haya ili kuelimisha watu wajue kujitahadhari,
 
A
Hii tabia ya kuchekana kwa hapa kwetu ndio inarahisisha zaidi utapeli.

Mtu akitapeliwa anaona soo kuwaambia wengine anaogopa atadharaulika na kuchekwa, ajabu ni kwamba hata hao wataomcheka washapigwa na vitu vizito walipotezea kimya kimya.

Kuna mtu huu uzi kakomenti kwa kebehi ila nimefatilia post zake za nyuma alikuwa analalamika mganga kamtapeli dawa ya biashara

Nchi za wenzetu kuna magroup kabisa ya kuhaarishana mambo haya ili kuelimisha watu wajue kujitahadhari,
Anajisahau kama vile yeye siyo binaadamu aliyeumbwa akiwa na mapungufu
 
Ulokuwa muoga Sana ila pole hapo iaa ulisoma coz gani
 
Muonekano ndgu, ulionekana boya. Au labda ulikumbatia begi lako na uoga kama wote wakawa wanakuchora tu.

Hata mm nilitapeiliwa kiboya zaidi yako ni muonekano tu, mtu anakuchora the way unarespond anajua hili kolo.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom