SoC02 Nilivyoweza kuongeza kipato kutoka milioni 1 hadi milioni 14 kwa mwezi

SoC02 Nilivyoweza kuongeza kipato kutoka milioni 1 hadi milioni 14 kwa mwezi

Stories of Change - 2022 Competition

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,199
Reaction score
3,307
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
 
Upvote 102
Ila wabongo mtu anajisifia kuajiriwa!! Miimi kwangu mtu ninayemkubali na kumuappreciate ni yule aliyejiajiri na kupambana na changamoto zote mpaka akawa mfanya biashara mkubwa ama mtu mwenye nguvu ya pesa lakini uyu wa kuajiriwa mimi kwangu ni big no!! ,namuona bado ni muoga wa maisha na hajui lolote kwenye maisha
 
Hpn ankali acha wivu kazi Ni tamu wee asikuambie mtu Tena ukute ya kitalamu Ni nzuri Sana
Nin jamaa angu Yuko Toyota analipwa vzr snaa tu sintasema ila analipwa vzr Sana na hao wahindi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Pole mkuu kwa baadhi ya comments za kushambulia

Mi nawafahamu watu kibao wanaolipwa 12m +,
Mmoja ni classmate yeye 25m+ Tanzania hii hii

Topic tunazopendelea ni kama "Wenzangu wenye take home ya 300k mnawezaje kutoboa mwezi?" Kwenye hiyo hakuna ambae angekoment kuwa ni uongo

Kingine ni kwamba wengi wetu tumepanic kusikia kuna mtanzania mwenzetu hapa hapa tz anaingiza hiyo hela kwa mwezi

Mi somo nililochukua hapo ni kupiga kazi mpaka watu wachanganyikiwe unapoondoka full stop

Mashambulizi potezea tu you have nothing to loose

Thank you for sharing your carrier journey experience
Asante sana mkuu.
 
Hongera kwa andiko mkuu.
Duuu nimeshangaa kuna mtu anasema hamna mtanzania anayeweza kulipwa 14 million kwa mwez kwa kigezo cha elimu, nazan atakuwa hajui vizuri company binafsi au hawajahi kufanya kazi private company, boss wangu alikuwa analipwa 12+million kwa mwezi na ni mtanzania tena level ya degree akaja kupewa offer ya 25+million bila posho na company nyingine, yy nae itikadi zake ni hzo anafika mapema sana kazini na kuondoka usiku ata saa nne yupo kazini anafanya kazi almost mda wote.
Kwa kumalizia watanzania wengi ni wavivu sana tena sana hvyo akisikia mtu analipwa hela hyo hawezi hamini, ata jamaa alituambia kuhusu offer ya 25+million tulibisha mpaka alivyotuonesha.
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Ila wabongo mtu anajisifia kuajiriwa!! Miimi kwangu mtu ninayemkubali na kumuappreciate ni yule aliyejiajiri na kupambana na changamoto zote mpaka akawa mfanya biashara mkubwa ama mtu mwenye nguvu ya pesa lakini uyu wa kuajiriwa mimi kwangu ni big no!! ,namuona bado ni muoga wa maisha na hajui lolote kwenye maisha
Asante kwa mawazo yako. Uzuri mawazo yako sio sheria. Kwa upande wangu mimi hakuna definition moja ya 'kupambana'. Mtu yoyote ambae anaamka asubuhi na kwenda kutafuta maisha aweze kulisha familia yake kwa njia za halali, ni mpambanaji bila kujali ameajiriwa au amejiajiri.
Asante kwa mawazo yako mkuu.
 
Bila Shaka ushapata uzoefu wa kutosha.

Fanya mpango ujiajiri Sasa,
uyo nayekulipa mil 14 Bila Shaka anaingiza zaidi ya Mara 10 ya anachokulipa.

Kwann usifanye mpango sasa hizo pesa ujiajiri na ujilipe mwnyw
 
Hawezi katu mm pia simshari ajiajiri apambane uko uko had astaafu kero za kujiajir Ni nyingi mno

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Bila Shaka ushapata uzoefu wa kutosha.

Fanya mpango ujiajiri Sasa,
uyo nayekulipa mil 14 Bila Shaka anaingiza zaidi ya Mara 10 ya anachokulipa.

Kwann usifanye mpango sasa hizo pesa ujiajiri na ujilipe mwnyw
Asante sana mkuu kwa ushauri mzuri sana.
Nikuhakikishie kuwa, tayari nina biashara zangu ambazo zimeanza kuingiza cash flow kuanzia May mwaka huu. Tayari nina road map yangu ambayo nime plan jinsi ya kuingia kwenye ujasiliamali kwa 100% na kutoka huku niliko. Baada ya kufanikisha hili, siku moja nitakuja pia na uzi kulielezea hilo kinagaubaga, maana mimi ni mtu ambae napenda sana kuandika na ku share uzoefu wangu.
Asante sana mkuu once again.
 
Le Akili kubwazzz... I like the big English "CASH FLOW", "ROAD MAP" mimi mdogo wako nausubiri san uo uzi utakaoleta mkuu. Mi pia ni mtu ambae napenda sana kusoma-soma na ku-pick a thing or two from them experiences and ideas
 
Siku akiingia kwenye top 10 au akawa mshindi kabisa itakuwaje?

Kwamba ataenda amevaa mask?
Until then... Hapo ndo itakuwa necessary kujireveal... Parameter zitaangaliwa kwanza na vigezo kuzingatiwa.

You never know panelist/moderators huenda wameshajiridhisha the guy is telling the truth. Truth that is advantageous to the public... Serious scrutiny imefanyika and the mr. MD passed. Or else huu uzi ungeshushwa au kuhamishwa majukwaa ya kimasihara.

HE WILL CROSS THAT BRIDGE WHEN HE GETS THERE . You just keep calm and enjoy this decent filtered coffee.

Mimi nimemuamini. 14M is peanut kwenye multinational organizations... Personality aliyoielezea ni impressive sana. During EXIT INTERVIEW they do all the trick if they truly need you to stay dough hike being one. Ukiitwa sehemu bila kuapply una advantage mkubwa shaaana ya kufanya salary negotiation... So level up, Papi!
 
Hpn ankali acha wivu kazi Ni tamu wee asikuambie mtu Tena ukute ya kitalamu Ni nzuri Sana
Nin jamaa angu Yuko Toyota analipwa vzr snaa tu sintasema ila analipwa vzr Sana na hao wahindi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wala sina wivi wowote broo sema tu nimeusema ukweli ambao umekuumiza ata wewe yaani mtu anajisifu kwa nguo ya kuazima tell wat if kesjo asubuhi kwenye meza yake akiikuta notice inayomtaka mara moja akabidhi vifaa vya ofsi kwa mkufugenzi wa kampuni unahisi atarudi apa kujisifu ama atarudi apa na kufungua uzi wa kuwalaani binadamu walivyo na toho mbaya kwa kumfanyia fitina na akafukuzwa kazi mzee fikiria nje ya box broo mimi kwangu hana nafsi for sure aje mtu anajisifu kwa kuanzisha factory kubwa from the scrach mpaka kuwa industry kubwa apa town uyo kwangu mimi ndo mwamba na ntamuunga mkono
 
Asante kwa mawazo yako mkuu. Ila tu uelewe kuwa nimefikiria hizo scenario zote unazozisema na sio kwamba nategemea 100% kuajiriwa, la hasha. Ninachokifanya ni kutumia hela ninayoipata kutoka kwenye ajira ku create multiple streams of income. Just to give you a picture, always tangu nuanze kuajiriwa, nusu ya mshahara wangu huwa unakatwa automatically kwa standing order niliyoiweka na kuwa deposited kwenye akaunti ya malengo ambapo baada ya muda fulani nakua nimepata kiasi cha fedha nilichokusudia na kuziwekeza kwenye mambo yangu.
 
Le Akili kubwazzz... I like the big English "CASH FLOW", "ROAD MAP" mimi mdogo wako nausubiri san uo uzi utakaoleta mkuu. Mi pia ni mtu ambae napenda sana kusoma-soma na ku-pick a thing or two from them experiences and ideas
Shukrani sana mkuu, tuko pamoja tuombeane uzima na afya njema!
 
Back
Top Bottom