SoC02 Nilivyoweza kuongeza kipato kutoka milioni 1 hadi milioni 14 kwa mwezi

Stories of Change - 2022 Competition

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,199
Reaction score
3,307
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
 
Upvote 102
Until then... Hapo ndo itakuwa necessary kujireveal... Parameter zitaangaliwa kwanza na vigezo kuzingatiwa.

You never know panelist/moderators huenda wameshajiridhisha the guy is telling the truth. Truth that is advantageous to the public... Serious scrutiny imefanyika and the mr. MD passed. Or else huu uzi ungeshushwa au kuhamishwa majukwaa ya kimasihara.

HE WILL CROSS THAT BRIDGE WHEN HE GETS THERE . You just keep calm and enjoy this decent filtered coffee.

Mimi nimemuamini. 14M is peanut kwenye multinational organizations... Personality aliyoielezea ni impressive sana. During EXIT INTERVIEW they do all the trick if they truly need you to stay dough hike being one. Ukiitwa sehemu bila kuapply una advantage mkubwa shaaana ya kufanya salary negotiation... So level up, Papi!
Umeelezea vizuri sana mkuu, thanks for your understanding.
 
Bado una akili za kitumwa

Pole sn
Asante sana. Uzuri, "akili za kitumwa" ni subjective. Akili za kitumwa zimeniwezesha kuwa na multiple sources za income hadi sasa ambazo ni mchanganyiko wa za kuajiriwa na za biashara zangu binafsi, lakini source ya hizo capital ni kuajiriwa.
Kama kuchuma kutoka kwenye kuajiriwa inanifanya niwe na akili za kitumwa kwa mawazo yako, acha iwe hivyo.
 
Hongera sana,ila nimesoma mistari ya mwanzo nikaona umeandika Kwa walio ajiriwa sekta binafsi ,paaap nikawa mpole..nikasema ngoja tu nisome nitajifunza kitu,nimejifunza kuwa na bidii na muaminifu katika kaz na mi hapo Niko vizuri.
Mkuu m nipo apa Bado Nashangaa mji natufuta kaz nimehitimu chuo mwaka huu IAA degree arusha ila Nina pia diploma in IT,sio mbaya kama nitapata ata pa kujishikiza maisha yasonge mbele,au kaz yoyote nipo tayari.
 
Karibu sana mkuu
 
Until then... Hapo ndo itakuwa necessary kujireveal... Parameter zitaangaliwa kwanza na vigezo kuzingatiwa.

You never know panelist/moderators huenda wameshajiridhisha the guy is telling the truth. Truth that is advantageous to the public... Serious scrutiny imefanyika and the mr. MD passed. Or else huu uzi ungeshushwa au kuhamishwa majukwaa ya kimasihara.

HE WILL CROSS THAT BRIDGE WHEN HE GETS THERE . You just keep calm and enjoy this decent filtered coffee.

Mimi nimemuamini. 14M is peanut kwenye multinational organizations... Personality aliyoielezea ni impressive sana. During EXIT INTERVIEW they do all the trick if they truly need you to stay dough hike being one. Ukiitwa sehemu bila kuapply una advantage mkubwa shaaana ya kufanya salary negotiation... So level up, Papi!
You have said it all. Unajua kuna vitu watu hawaelewi, halafu badala ya kuuliza wanabisha. Nimeshangaa mno mtu kuja kabisa jukwaa la heshima kama JF na kusema kuwa hakuna muajiriwa Mtanzania anaelipwa 14m kwa kazi ya kuajiriwa. Angejua kuna watu wana double hiyo amount na wapo tu Bongo hii hii. Ama kweli, "information is power"
 
Hongera kwa andiko mkuu.
Duuu nimeshangaa kuna mtu anasema hamna mtanzania anayeweza kulipwa 14 million kwa mwez kwa kigezo cha elimu, nazan atakuwa hajui vizuri company binafsi au hawajahi kufanya kazi private company, boss wangu alikuwa analipwa 12+million kwa mwezi na ni mtanzania tena level ya degree akaja kupewa offer ya 25+million bila posho na company nyingine, yy nae itikadi zake ni hzo anafika mapema sana kazini na kuondoka usiku ata saa nne yupo kazini anafanya kazi almost mda wote.
Kwa kumalizia watanzania wengi ni wavivu sana tena sana hvyo akisikia mtu analipwa hela hyo hawezi hamini, ata jamaa alituambia kuhusu offer ya 25+million tulibisha mpaka alivyotuonesha.
Aisee 25mil !! Balaa hili sii mbususu unagegeda mpaka basi.

Bwana asikwambie mtu kuajiriwa rha sana hasa kama unachapa mzigo. Unalipwa kapu la mshahara yani wee ni full kupiga nondo tuu. Alafu bwana upate kampuni inajielewa...tarehe 25 kitu kinasoma kwenye account acha kabisa....bonge la motivation. Mbona kukesha unaona kitu cha kawaida kabisa.

Wee kampuni inakuuliza mkeo analipwa ngapi tumlipe mshara upige kazi yetu....yaani wanamlipa mkeo kwa ajili ya kugegedwa na wewe mume🤣🤣🤣🤣 alafu anatokea fala mmoja eti ukajiajiri. Utani huu. Tuchape kazi wanaume.
 
😂 😂 😂 Ila we jamaa una utani mwingi sana. Unawaza mbususu tuu😂😂
 
Sio utani bro...i kid u not! These companies fully understand that for u to be productive u need to fully focus on the task at hand. Sio tena mara mke sijui anaumwa mara sijui tatizo gani. Wee leta mke wako kaa hapo na tutamlipa msharaha wa kugegedwa.

Nitakupa mfano kwenye industry ya football venye wenzetu wanafanya ulaya. After procuring player, kuna mtu maalum kwenye club ambaye kazi yake ni kumsaidia mke wako wewe mchezaji kusettle in. Sijui mambk ya kutafuta wapi muishi, shule za watoto etc...yote hiyo ni kuhamikisha mchezaji akili yote ipo focused kwenye kucheza ball.

Top level management is like a formula one car, every thing has to be precise, attention to detail is paramount.

Personally nilishaona close family members wakilipwa excess of 30mil ila sio wakifanya kazi bongo. So suala la kuajiriwa kwangu mie naona poa sana. Yaani mtu unapewa fully furnished house, a brand new car, 80% ya school fees inalipwa na muajiri, mke analipwa. Niache hivyo eti nisikilize tantalila za kujiajiri za wanasiasa. No ways.
 
Halafu nimegundua wewe jamaa una madini sana na exposure ya kutosha sana. Ulichoandika ni sense kwa 100%, ila inahitaji mtu mwenye exposure kufahamu haya. Ngumu sana mtu ambae ni ni mpasha joto tu siti ya anakofanyia kuelewa. Absolutely on point.
Nimeielewa sana hii statement yako, "
"Top level management is like a formula one car, every thing has to be precise, attention to detail is paramount"
 
I am intrigued by management issues bro. Piga kazi mzeya utengeneze mihela hiyo and bliv me when i say sie wabongo ni wavivu na wapenda ngono tuu, mie mwenyewe nikiwa mfano hai🤣🤣🤣🤣🤣🤣 so look no further!
Your next aspiration should be beyond making moolah but rather in pursuit of managerial excellency. If i can play a part in that...then ningekushauri tafuta hiki kitabu.
16618457843507657489487979180022.jpg
 
I am intrigued by management issues bro. Piga kazi mzeya utengeneze mihela hiyo and bliv me when i say sie wabongo ni wavivu na wapenda ngono tuu, mie mwenyewe nikiwa mfano hai🤣🤣🤣🤣🤣🤣 so look no further!
Your next aspiration should be beyond making moolah but rather in pursuit of managerial excellency. If i can play a part in that...then ningekushauri tafuta hiki kitabu.View attachment 2339725
Safi sana mkuu, nitakitafuta hiki kitabu aisee.
 
I am intrigued by management issues bro. Piga kazi mzeya utengeneze mihela hiyo and bliv me when i say sie wabongo ni wavivu na wapenda ngono tuu, mie mwenyewe nikiwa mfano hai🤣🤣🤣🤣🤣🤣 so look no further!
Your next aspiration should be beyond making moolah but rather in pursuit of managerial excellency. If i can play a part in that...then ningekushauri tafuta hiki kitabu.View attachment 2339725
This book .. nakipata wapi mkuu i need it. Can you please kindly pass it on?

Watu hawana exposure kabisa eti 14M ni mingiii shaaana na ubishi wao umebase hapo dah maajabu.

Mleta thread katembea vizuri sana i believe ni ukweli... Hata kama ipo MANUFACTURED bado kitu kama iki kipo....

What i see based on the story he has a bright future ahead akiendelea na spirit hii... cause he already seem to be in the right place but still striving. Hivi mtu kama yule MAVERE TUKAI si alikua ana over 38M kabisa.

Tanzania inahitaji watu kama mleta thread. Licha ya kuwa loaded with em banknotes ila bado wanakua humble na kushare his story unfortunately watu wapo so negative badala wajifunze kitu.

I say kama hakuna watu wa ku-claim hizi prize za shindano then it belongs to decent soul kama mleta thread no matter if he is loaded. So watu wasione hii ni another ground ya kubisha kwamba hana io 14M but ana njaa ndio maana. After all bringing that story here seem effortless and automatic. So this author might be entitled ha ha ha u know😄
 
Cheki amazon....mie nilikinunua huko
 
Ndugu yangu wa kAribu kabisa (damu) alikua anafanya kazi kampuni ya ABB ambayo ilikua hapa kwetu Tanzania (nadhani imehamishwa/kufungwa kwa hapa Tz), yeye ni electrical engineer, alikua analipwa take home 15M na marupupu kibao, safari za kuzurura Afrika na Ughaibuni ni kama mimi navyokwendaga Chamwino, mara msalato kula nyama au hombolo kula zabibu😅 na kila ifikapo sikukuu za krismasi, pasaka na mwaka mpya alikua anapewa vocha ya miliioni tano kwenda kufanya shopping THE Game, ko alikua anatubeba tunaenda kuenjoi hiyo vocha yake pale mcty na sikumbuki kama tuliwahi kumaliza hizo vocha, haya yote nimeyashuhudia kwa macho yangu, kwahyo anachokisema mleta mada sikitu kipya cha kustaajabisha hata kiniletee mashaka kuamini.
Hongera sana kwa mapambano Mkuu na Hamasa kwetu Vijana, Sijui wanavopiga kura ningekupia Mkuu!
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
 
Hard copy au soft tu? Naomba maelekezo kidogo mkuu
Mie ni mpenzi wa hardcopy mzeya. So nilikuwa na jamaa yangu yupo majuu alikinunua amazon alivyuka anakuja bongo akaniletea. But am sure aiku hizi ukiwa na p.o box unapata tuu. Uliza wataalam wa manunuzi ya online
 
Ndugu yangu wa kAribu kabisa (damu) alikua anafanya kazi kampuni ya ABB ambayo ilikua hapa kwetu Tanzania (nadhani imehamishwa/kufungwa kwa hapa Tz), yeye ni electrical engineer, alikua analipwa take home 15M na marupupu kibao, safari za kuzurura Afrika na Ughaibuni ni kama mimi navyokwendaga Chamwino, mara msalato kula nyama au hombolo kula zabibu😅 na kila ifikapo sikukuu za krismasi, pasaka na mwaka mpya alikua anapewa vocha ya miliioni tano kwenda kufanya shopping THE Game, ko alikua anatubeba tunaenda kuenjoi hiyo vocha yake pale mcty na sikumbuki kama tuliwahi kumaliza hizo vocha, haya yote nimeyashuhudia kwa macho yangu, kwahyo anachokisema mleta mada sikitu kipya cha kustaajabisha hata kiniletee mashaka kuamini.
Hongera sana kwa mapambano Mkuu na Hamasa kwetu Vijana, Sijui wanavopiga kura ningekupia Mkuu!
Asante sana mkuu kwa ushuhuda konki.
 
Mie ni mpenzi wa hardcopy mzeya. So nilikuwa na jamaa yangu yupo majuu alikinunua amazon alivyuka anakuja bongo akaniletea. But am sure aiku hizi ukiwa na p.o box unapata tuu. Uliza wataalam wa manunuzi ya online
Unapata tu ukiagiza kwa Amazon
 
Back
Top Bottom