SoC02 Nilivyoweza kuongeza kipato kutoka milioni 1 hadi milioni 14 kwa mwezi

Stories of Change - 2022 Competition

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,199
Reaction score
3,307
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
 
Upvote 102
Mkuu nadhani ni swala la exposure tu.
Kuna mtu mmoja namjua aliyepanda kama jamaa, sema jamaa kapanda ndani ya kampuni 1 mara 2 akaondoka, akarudi kwa nafasi ya juu, nayo akapanda tena.

Jamaa ana bachelor tu, sema kasoma kwa wazungu.

Aliingia wa kawaida, akapanda kuwa HOD, akataka raise wakashindwana pesa, akaenda kampuni nyingine, walioshindwana mshahara wakamuita kwa nafasi ya juu zaidi, tena nchi nyingine kaenda kawa expatriate, then kapanda kwa mara nyingine.

Jamaa ana allowance zaidi ya dollar 3000 kwa mwezi na anapewa ticket ya ndege kwenda destination yoyote duniani yeye na familia yake kila mwaka.

Ila jamaa ni mpiga kazi balaa halafu bishoo, na yuko peace sana.
Inawezekana kabisa mkuu
 
Voted.

It does not matter whether its true or brewed,

It contains logic. Its very possible.

I get that you cant disclose companies you have been with or in now...

ONE THING... ni degree gani hiyo ya science. You dont have to name the college/university you attented... JUST NAME THE COURSE😎
 
Mkuu, information is power. Especially in this era, kila taarifa sahihi unayokua nayo inakupa an edge fulani ya advantage kwenye mambo fulani. Kwa mfano huu uzi nilioleta hapa, una taarifa ambayo pengine baadhi ya waajiri wa sekta binafsi wasingependa kabisa ziwafikie waajiriwa, kwa sababu zinawapa power fulani waajiriwa wa kuweza kujua kuwa kumbe inawezekana kuwa highly paid katika mazingira fulani, provided kwamba you are worthy it. The less people believe this,the more advantage kwa upande wa waajiri.
The more people believe that haiwezekani kwa kijana kulipwa that range of amounts, the better kwa waajiri.
Nimetoa information, what you do with it is up to the person reading the information, sina cha kupoteza ukiondoa labda muda wangu, ambao na wenyewe kwa vile nimeutenga kwa ajili ya kutoa taarifa za kurudisha kwa jamii kama hivi, sio mbaya sana. Uzuri nimeitoa hii information bure kabisa, kwa hiyo sidaiwi na mtu.
Kuhusu kozi niliyosomea, nimesomea MD mkuu.
Shukrani sana na ubarikiwe.
 
14M is not jaw dropping at all esp for one in corporate circle or knows that circle. Hongera sana na kama ni MD basi umeandika ukweli sana. Keep my vote mkuu.

Its all true. Keep the energy, who know one day you could be Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus... Keep my vote wadau more votes to this gentlemen please. You are worth it.

Such an inspiration yet wanatokea low life kudisi
 
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
Crocodile crocodile crocodile crocodile madona
 
Nafurahi zaidi watu mnavyotoa uzoefu wenu juu ya hili, itasaidia vijana wengi zaidi waamini kuwa inawezekana kabisa na kwao pia. Ambao hawataamini basi pia, watakua wamechagua kuendelea na 'business as usual', sio mbaya sana wapasha joto viti maofisini lazima wawepo ili majembe machache yapae. That is life.

Hongera mkuu kwa kipaji hicho cha kupiga kazi kama mashine. Mimi wangu ni ushauri mdogo tuu...

Watu wengi sana ninaowafahamu ambao ni "workaholics" kama wewe, hua wanasahau kabisa kwamba kuna KUISHI..!!

Life is not only about making milions, ni kujua ku balance kati ya kazi, maisha, relationships, afya, starehe nk. Kwa mtu ambae unafanya kazi sunrise to sunset 7 days a week mara nyingi ni ngumu sana ku balance hivyo vitu. Mwisho wa siku utajikuta sawa, u have the milions lakini mambo mengine yote kwenye maisha yako yanaenda mrama. Wapo wanaolipwa pesa nyingi kuliko wewe lakini ukiwaona maisha yao ni miserable.
 
Mkuu, information is power. Especially in this era, kila taarifa sahihi unayokua nayo inakupa an edge fulani ya advantage kwenye mambo fulani. Kwa mfano huu uzi nilioleta hapa, una taarifa ambayo pengine baadhi ya waajiri wa sekta binafsi wasingependa kabisa ziwafikie waajiriwa, kwa sababu zinawapa power fulani waajiriwa wa kuweza kujua kuwa kumbe inawezekana kuwa highly paid katika mazingira fulani, provided kwamba you are worthy it. The less people believe this,the more advantage kwa upande wa waajiri.
The more people believe that haiwezekani kwa kijana kulipwa that range of amounts, the better kwa waajiri.
Nimetoa information, what you do with it is up to the person reading the information, sina cha kupoteza ukiondoa labda muda wangu, ambao na wenyewe kwa vile nimeutenga kwa ajili ya kutoa taarifa za kurudisha kwa jamii kama hivi, sio mbaya sana. Uzuri nimeitoa hii information bure kabisa, kwa hiyo sidaiwi na mtu.
Kuhusu kozi niliyosomea, nimesomea MD mkuu.
Shukrani sana na ubarikiwe.
Nakingereza chako cha mchongo wewe ni jobless usituongopee ungekuwa na kazi ya kukuingizia million 14 usinge kuwa hapa. Nakuona unajikuta Swahili English nakuchora tu, na hivi story zako za vijiweni wakati wewe ni jobless na story umehadisiwa kijiweni ungekuwa na kazi ya ma a na usingekuja kugombania laki laki hapa.

Unajua hili nishindano na Kama unania ya kusaidia vijana unatikiwa utolee ufafanuzi Wa machapisho yako nimekuiliza umefanya kazi kampuni gani ?
 
Relax kijana, hakuna haja ya kuwa na hasira hivyo. Kama mimi ni jobless sasa wewe hasira za nini? Hebu relax.
Kampuni siwezi kukutajia maana kwa mtu atakaeunganisha dots anaweza kunihisi aki triangulate information.
Kama hii post imekusababishia mlipuko hasi wa hisia pole sana kwako, na bahati mbaya sina control na hilo.
Uwe na siku njema.
 
Kwani lengo la post siume sema Una taka kusaidia vijana au una concept tofauti ?
 
Hongera mkuu kwa kipaji hicho cha kupiga kazi kama mashine. Mimi wangu ni ushauri mdogo tuu...

Watu wengi sana ninaowafahamu ambao ni "workaholics" kama wewe, hua wanasahau kabisa kwamba kuna KUISHI..!!

Life is not only about making milions, ni kujua ku balance kati ya kazi, maisha, relationships, afya, starehe nk. Kwa mtu ambae unafanya kazi sunrise to sunset 7 days a week mara nyingi ni ngumu sana ku balance hivyo vitu. Mwisho wa siku utajikuta sawa, u have the milions lakini mambo mengine yote kwenye maisha yako yanaenda mrama. Wapo wanaolipwa pesa nyingi kuliko wewe lakini ukiwaona maisha yao ni miserable.
Asante sana mkuu, hili nimelichukua kama lilivyo.
Barikiwa sana.
 
14M is not jaw dropping at all esp for one in corporate circle or knows that circle. Hongera sana na kama ni MD basi umeandika ukweli sana. Keep my vote mkuu.

Its all true. Keep the energy, who know one day you could be Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus... Keep my vote wadau more votes to this gentlemen please. You are worth it.

Such an inspiration yet wanatokea low life kudisi
Shukrani mkuu.
 
Relax kijana, hakuna haja ya kuwa na hasira hivyo. Kama mimi ni jobless sasa wewe hasira za nini? Hebu relax.
Kampuni siwezi kukutajia maana kwa mtu atakaeunganisha dots anaweza kunihisi aki triangulate information.
Kama hii post imekusababishia mlipuko hasi wa hisia pole sana kwako, na bahati mbaya sina control na hilo.
Uwe na siku njema.
Mimi chapisho lako sielewi kwamba unatulingishia kazi uliyo nayo au unataka kusaidia vijana, na Mimi ngoja nikuache nisije nikawa na bishana na Dogo wa darasa la Saba B bure.
 
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
Huu ni uongo wa kawaida wa mitaani ambao vijana wa kizazi hiki huutengeneza na kuja kujitambia.

Narudia tena, mleta mada hii kitu umetunga na haipo kabisa hapa Tanzania. Nitaweka sababu za msingi kukukosoa ili ufahamu.

1. Mchapakazi wa style hiyo hawezi kuwa ana hama hama kutoka taasisi moja kwenda taasisi nyingine ili kufuata mshahara. Wachapakazi wa hivyo huwa wanasukumwa na passion&legacy na sio mshahara.

2. Kwa hapa Tanzania hakuna mtu aliyeajiriwa na kulipwa mshahara wa 14milion kwa mwezi kwa kigezo cha elimu yake au uchapa kazi wake. Hakuna. Huo ni mshahara wa mtu anayejilipa mwenyewe, intertainer (wasanii na wanamichezo), Managing director wa big companies.

3. Mchapakazi wa kweli au mtu mwenye mshahara mkubwa hivyo hawezi kuja hapa JF kueleza hayo, hana huo muda wala hizo swaga, watu wengine ndio watakuja hapa na kueleza mambo yake.
 
Duuuhh..!! Mkuu, ni vyema ungechukua muda wako kujifunza zaidi:
1.Kuna personalities za aina nyingi sana kwenye corporate world- Wapo wahamaji wazinguaji na wapo wahamaji ambao wanapiga kazi vizuri tu. Kwanza kitendo cha kuhama tu lazima uwe vizuri, usifikiri kuhama ni rahisi tu,kwamba unaamua tu na it happens, lazima uwe vizuri maana kuhama kuna involve competition kubwa kwenye interview process, so mtu anaehama sana most times anakua vizuri tu, fanya uchunguzi wako utaelewa.
2.Sasa nakwambia nalipwa that amount, ans I am not even among the top paid people kwenye corporate world. Kuna watu wanalipwa more than that amount, again, do your research utaelewa. You are very mis-informed on this mkuu.
3.Huo ni mtazamo wako, na siwezi kupinga perception ya mtu, ni haki yako ya kimsingi.
 
Pole mkuu kwa baadhi ya comments za kushambulia

Mi nawafahamu watu kibao wanaolipwa 12m +,
Mmoja ni classmate yeye 25m+ Tanzania hii hii

Topic tunazopendelea ni kama "Wenzangu wenye take home ya 300k mnawezaje kutoboa mwezi?" Kwenye hiyo hakuna ambae angekoment kuwa ni uongo

Kingine ni kwamba wengi wetu tumepanic kusikia kuna mtanzania mwenzetu hapa hapa tz anaingiza hiyo hela kwa mwezi

Mi somo nililochukua hapo ni kupiga kazi mpaka watu wachanganyikiwe unapoondoka full stop

Mashambulizi potezea tu you have nothing to loose

Thank you for sharing your carrier journey experience
 
Hongera kwa andiko mkuu.
Duuu nimeshangaa kuna mtu anasema hamna mtanzania anayeweza kulipwa 14 million kwa mwez kwa kigezo cha elimu, nazan atakuwa hajui vizuri company binafsi au hawajahi kufanya kazi private company, boss wangu alikuwa analipwa 12+million kwa mwezi na ni mtanzania tena level ya degree akaja kupewa offer ya 25+million bila posho na company nyingine, yy nae itikadi zake ni hzo anafika mapema sana kazini na kuondoka usiku ata saa nne yupo kazini anafanya kazi almost mda wote.
Kwa kumalizia watanzania wengi ni wavivu sana tena sana hvyo akisikia mtu analipwa hela hyo hawezi hamini, ata jamaa alituambia kuhusu offer ya 25+million tulibisha mpaka alivyotuonesha.
 
Back
Top Bottom