Nilivyozaa mtoto wa 2 nje ya ndoa

Nilivyozaa mtoto wa 2 nje ya ndoa

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
2,977
Reaction score
3,798
1.JALADA LA KWANZA

Hii ni true story. Japo nina ndoa mbili lakini nimezaa watoto kadhaa nje ya ndoa.Hadithii hii ambayo ni ya kweli ni jinsi nilivyozaa mtoto wangu wa pili wa nje ya ndoa. Ni miaka 15 iliyopita nilikuwa mkuu wa taasisi moja isiyo ya kiserikali,ambayo makao yake yalikuwa nje ya Dar,basi kuna kibali tulikuwa tunakiomba kutoka wizara fulani,basi tulizungushwa sana,mwisho nikaona bora niende mwenyewe wizarani kuulizia.

Nikaenda mimi na dereva wangu mpaka Dar,tukalala hoteli na asubuhi yake tukaenda wizarani. Nikamkuta dada mmoja hivi nikamuuliza akanijibu kwa dharau sana kuwa maombi yako yamepotea.Kwa hasira nikamuuliza kwahiyo kama yamepotea,akanijibu kaombe upya.

Aisee nilichukia na kufoka vibaya,yule dada akanipandishia na akautukana weupe wangu kwa maana mie ni chotara,basi tulitukanana sana mpaka bosi mkuu akaja kutuamua.Ilimchukua boss saa 2 kutuweka sawa na akatupatanisha .Itaendelea baadae leo
 
Wewe unahitaji kuja tuisheni kwangu. Nikufunze jinsi ya kuwa hivyo unavyodhani upo. Bado sana wewe. Ongeza bidii.
 
2.SEHEMU YA PILI
Tulikaa watu 3 mimi,yule dada niliyegombana nae na boss wa hapo tukakubaliana kuwa nirudi hapo kesho ili kumpa nafasi huyo dada kutafuta hilo jalada na tukapeana namba za simu.Jioni kama saa 11 nilimpigia akaniambia yupo hospitali amana baba yake ni mgonjwa,nikamwambia naweza kwenda alipo,akasema sawa,nikaenda kwa teksi na nkampata.Nikawa nae mpaka baba yake alipo maliza kutibiwa,tukawa tunatoka chumba cha dawa kuelekea nje,basi nikawa nataka kutafuta usafiri,akanijibu tulia,kumbe mdada yupo na gari yake,basi tukapanda gari hadi nyumbani kwa baba,sipakumbuki vizuri ilikuwa mbali sana,wakati wa kurudi kaniuliza umefikia wapi,nikamjibu maeneo ya sinza,tukaenda nikamkaribisha kula na kunywa,ila akaniambia huwa hanywi pombe.Basi tulienjoy hapo kwa saa 3 hivi na hatimae akaniaga akaondoka na urafiki ulianzia hapo.
Kesho yake mida ya saa 6 mchana akaniita,nikaenda,nikapewa fomu fulani nikajaza na akaniambia nirudi baada ya wiki 2 kila kitu,kitakuwa tayari.Nikamwambia sawa nikamuba jioni tukutane pub moja oysterbay,akakubali ila akasema nimsubiri hotelini anipitie twende huko oysterbay pamoja, nikasema ok na alikuja kunipitia na alivaa vizuri sana,basi siku hiyo tuliongea mengi sana kuhusu kazi,maisha,nikaanza kumtamani sana na pole pole nikawa narusha ndoano,naye akaniuliza vitu vingi,nilimjibu kila kitu,na sikumficha kuwa nina ndoa 2 naye akaniambia yupo dingo na hana mtoto japo ana rafiki ingawa ni wa kupitishia muda tu.By saa 6 usiku tukaondoka kurudi hotelini kwangu naye arudi kwake maeneo ya magomeni.Nilimkaribisha room kwangu apaone,alikubali lakini alikaa kwa nusu saa akaniambia anaondoka ila kesho atanikaribisha kwake nikapaone.Itaendelea kesho ha ha ha najua watazuka jamaa kutoa lawama msururu.Kaeni mkijua siandiki hadithi ya kutunga hiki ni kisa cha kweli na naandika jinsi kilivyotokea na kutakuwa na dosari kadhaa ambazo sio rahisi kuzizuia.Alamsiki
 
Oyaaa
 
Back
Top Bottom