shin gun wook
JF-Expert Member
- Sep 26, 2017
- 995
- 1,514
Jana jioni nikiwa nimetoka kwenye shughuli zangu,ghafla akanikimbilia msichana wa Kazi Wa jirani yangu kuomba msaada .Alikuja mbio analia mtoto katumbukia kwenye chamber ya kinyesi.Watoto wakati wanacheza sijui ikawaje mfuniko huenda waliosogeza au palikua wazi.Nilipo fika kuchungulia na kumuona mtoto na maji hayakua mengi nikaruka mpaka chini cha kufanya ilikua nimnyanyue mtoto wakati tunatafuta msaada wa kupata cha kupandia juu.kwa kua maji hayakua mengi nikafanikiwa kumnyanyua nikamuhimiza msichana wa Kazi atafute kamba haraka au mbao ndefu aishushe .wajinga wale sijui wanakulaga moto au mabomu.niliungua kwa kinyesi.nikafanikiwa na kumpa huduma ya kwanza nakumpeleka hospitali.
Sasa baba wa mtoto alikata mawasiliano na Mimi nilipomkataza asibandike mabango yake ya kampeni kwangu kipindi cha uchaguzi .akasema kuanzia siku hiyo nitakua adui yake.baada ya kumpeleka mtoto nadhani alipigiwa simu .nikakutana njiani akanipita bila salamu.
Sasa badae amekuja kujua ndio niliyomuokoa mwanae kaja mbio analia.nimeondoka bila kumsemesha kwanza .nifanye nini ili kumpa adabu?