Niliwashauri ATC wasiende China kupitia Bangkok, hawatapata faida njia ina ushindani sana, naona hawakusikia

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Naona ATCL wameamua kwamba wataenda China kupitia Bangkok, Thailand Bangkok. Njia hii ina ushindani sana, haitakuwa na faida kwao kupitia Bangkok na kushindana na mashirika makubwa ambayo yameweka mizizi sana kwenda au kupitia Bangkok pamoja na Ethiopian Airways and Kenya Airways.

Ninawashauri kwamba wawe innovative katika kubuni njia ambapo wanaweza kuvuta abiria hata kutoka nchi jirani badala ya mentality ya Kitanzania ambapo jirani yako akifungua genge la nyanya mtaani kwenu na wewe unaenda kufungua genge la kuuza nyanya pembeni yake badala ya kuuza bidhaa ambayo wale wanaonunua nyanya kwa jirani yako wataitaka kwako!

ATCL wafikirie route kama kwenda China kupitia Hong Kong, au Mumbai, au Delhi au Bangalore badala ya kufuata mkumbo wa kila shirika linaloenda China kupitia Bangkok. Hatuhitaji kuuza nyanya kwa kuwa jirani anauza nyanya. Tuuze vitunguu na chumvi.

Wakienda China kupitia Hongkong, Bangalore, Delhi kwa mfano, unaweza kukuta wanavuta abiria kutoka nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda Zambia nk ambazo watapeleka regional flight kwa ajili ya hiyo connection, na kupata pia abiria wanaoenda huko ambao labda inabidi waende hadi South Africa au Addis Ababa kupata hiyo connection.

ATCL kwenda China kupitia Bangkok unajiweka katika wigo wa kukosa abiria pale Bangkok kwa kuwa wana options nyingi sana. Jiulize, kwa nini abiria watumie ATCL na sio Kenya Airways au Ethiopian Airways? Anzisha route kwa namna ambayo unawa-compel abiria kutumia ATCL, sio unawapa ATCL kama option nyingine kati ya nyingi zilizopo.
 
Labda kama walivyosema wahenga
"Sikio la kufa halisikii dawa "
Mkuu tatizo ni kufanya kazi kwa mazoea na kuogopa kuwa wabunifu - unafanya kile ambacho wenzako wanafanya ili tatizo likitokea ukwepe lawama na ionekane kama ni kifo cha wengi ni harusi.

Watu wengi sana katika uongozi wanaogopa kufanya kitu original kwa kuwa kikifeli wataonekana hawajui kazi! Hivyo hawako tayari kuchukua risk ya kufeli katika original thinking, hata kama decision katika routine thinking ina risk kubwa zaidi
 
Unatoa ushauri kama nani kwanza? Jitambulishe wewe ni nani kujiona una maarifa kuliko staff nzima ya ATCL
 
Tatizo la watanzania tumekuwa makambale tumeota sharubu! Hata mambo ambayo wahusika wakuu wapo mtu anachukua kisimu chake cha toch anaanza kubwabwaja!
 
Unatoa ushauri kama nani kwanza? Jitambulishe wewe ni nani kujiona una maarifa kuliko staff nzima ya ATCL
Sawa Mkuu. Nina connection na wizara inayohusika na ATCL na nina background na mambo ya transport na aviation management. Yangu yalikuwa mawazo tu, haina maana nina maarifa kuliko staff nzima ya ATCL. Lakini pia haina maana ili niwe na wazo zuri kwa ATCL lazima na mimi niwe staff wa ATCL. Hili ni shirika linanihusu kama madau Mtanzania.
 
ATCL imekuwa inashambuliwa na watu wasioitakia mema nchi wengi wao wakitaka kudidimiza juhudi za Rais za kufufua shirika letu! Nadhani ushauri wako kama ungeutoa kwa kufuata proper channel ungewafikia wahusika na kuuchukulia uzito unaostahili kuliko njia hii ambayo inachukuliwa katika mtizamo hasi!
 
Tatizo la watanzania tumekuwa makambale tumeota sharubu! Hata mambo ambayo wahusika wakuu wapo mtu anachukua kisimu chake cha toch anaanza kubwabwaja!
Hiyo ni mentality kwamba raisi kwa kuwa yeye ni raisi basi ana akili na anajua mambo kuliko Watanzania wote hawezi kukosea wala hapaswi kukosolewa. Waziri naye hivyo hivyo katika mambo ya Wizara yake.

Mkurugenzi wa ATCL hivyo hivyo, na watu tulioko nje ya ATCL hatupaswi kusema kitu kwa kuwa chochote tukachosema hakina maaan wao ndio wanajua kila kitu na ndio maana wako ATCL na sisi hatuko ATCL. Very illiterate kind of thinking.
 
Unatoa ushauri kama nani kwanza? Jitambulishe wewe ni nani kujiona una maarifa kuliko staff nzima ya ATCL

Kuna mtu amekumbushia kuwa sio mara ya kwanza natoa ushauri kwa ATCL kama mdau, kwa nia nzuri tu kwa kuwa nimesomea mambo hayo. Angalia hapa chini.

 
Unatoa ushauri kama nani kwanza? Jitambulishe wewe ni nani kujiona una maarifa kuliko staff nzima ya ATCL
Hapana mdau.
Tusijenge utamaduni wa kukataa ushauri bila kuutathimini sababu aliye toa ushauri sio wa kundi lenu.
Ushauri unapokelewa na kufanyiwa uchunguzi wa kinakujiridhisha manufaa yake au hasara zake.
 
Kuna mtu amekumbushia kuwa sio mara ya kwanza natoa ushauri kwa ATCL kama mdau, kwa nia nzuri tu kwa kuwa nimesomea mambo hayo. Angalia hapa chini.
Hao washindani wengine hawatumii hio route (via Hong Kong)? Kwanini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…