Niliwashauri ATC wasiende China kupitia Bangkok, hawatapata faida njia ina ushindani sana, naona hawakusikia

Niliwashauri ATC wasiende China kupitia Bangkok, hawatapata faida njia ina ushindani sana, naona hawakusikia

Hao washindani wengine hawatumii hio route (via Hong Kong)? Kwanini?
Swali nzuri sana. NI kwamba kwa sasa eneo letu lote hili lina option ya kwenda Bangkok kutumia Kenya Airways na Ethiopian Airways. Sasa Ethiopian airways inaunganishwa pia na Rwandair. Sasa haya mashirika mawili yote yanaenda China, kwa hiyo yameshajizatiti kwenda China kupitia Bangkok na sio rahisi ATCL kuteka abiria kutoka hii region kwenda Bangkok na China. ATCL itabidi wategemee abiria toka Tanzania peke yake.

Sasa ukitaka kupitia Hong Kong. Katika ukanda huu ni South African Airways na Ethiopian Airways. Nikiwa Zambia, labda nitaenda kwanza Johannesburg. Nikiwa Burundi itabidi niende Ethiopia. Nikiwa Kenya labda pia itabidi niende Ethiopia. Sasa unapoingiza ATCL route ya Hong Kong tayari unakuwa unawapa abiria option inayoonekana kuwa rahisi na convenient zaidi kuliko kupitia Ethiopia au South Africa. Lakini pia inabidi uwe na flights za Dar kwenda hizi nchi ambazo abiria watafanya ili kuja Dar kupata connection ya China kupitia Hong Kong.

Licha ya hivyo, kuna uhusiano wa karibu (in fact ni nchi moja) kati ya Hong Kong na China, na Hong Kong ina fursa zaidi za kibisahara na utalii kuliko Bangkok. Watalii wa Hong Kong kuja Tanzania utapata wengi kuliko Bangkok kuja Tanzania.
 
Hao washindani wengine hawatumii hio route (via Hong Kong)? Kwanini?
Hong Kong wanaenda SAA na Ethiopian Airways kutoka hili eneo. Ethiopia ni mbali. Kwa hiyo unaweza kutawala abiria wa karibu nchi zote zinazotuzunguka isipokuwa zile zilizo karibu sana na Johannesburg. Unaweza hata ukapata abiria wa Rwanda japo Rwandair ina connect na Ethiopian Airways kwenda Hong Kong. Abiria wa Rwanda ataona ni rahisi kuja Dar na kwenda Hong Kong direct kuliko kupitia Adis Ababa. Kwanza uwanja wa Adis kila mtu anataka kuukwepa.

Sababu nyingine angalia hapo juu.
 
Back
Top Bottom