Niliweka shada za maua kwenye makaburi matano ya watu wangu wa karibu

Sehemu ya Sita:

Lakini ilikuaje?

Siku hiyo mama mkwe alokuja, sikupata kuzungumza jambo na wala sikutaka, hata pale bwana Mgaya aliponisogelea kwaajili ya swala hilo nilimkwepa kwa kumwambia sipo katika hali ya maongezi, aniache kwa muda.

Siku hiyo nilikaa kwa kujitenga, mara nyingi huwa nafanya hivyo nikiwa na msongo wa mawazo, najitenga ili nipate kuyatafakari yanayonisibu pasipo usumbufu hivyo badala ya kukaa ndani mimi nilienda kuketi huko nje baada ya mtoto kulala, lakini huko badala ya kutafakari, ajabu, nikawa najikuta nabubujikwa na machozi, nilijutia sana maamuzi yangu ya kipumbavu, maamuzi ya kuolewa na yule bwana.

Yalikuwa ni maamuzi ya kukurupuka ambayo sasa yananigharimu.

Ingali nikiwa hapo, nawaza na kumwagilia ardhi kwa machozi yangu, nyakati ni kama saa nne hivi ya usiku, mara nikasikia sauti ya kishindo cha mtu, mtu anayetembea, kuangaza nikamwona Amiri akiwa anatokea kule bandani.

Kijana huyo alikuwa amevalia suruali aloikunja mpaka magotini, miguu yake imejawa na matope, chini yu pekupeku.

Alinifuata moja kwa moja pale nilipokuwapo akanisalimu, nikamjibu pasipo kumtazama, sikutaka ajue nasumbuliwa na uchungu ndani yangu, lakini ajabu kijana yule alinipa pole kwa yanayonisibu, hapo nikalazimika kumwangalia usoni.

"Pole ya kitu gani?"

Akaniambia aliniona nikiwa nalia tangu akiwa umbali ule wa bandani, ameniona nikifanya hivyo kwa dakika kadhaa na ndo' maana amesogea hapo kunipa pole. Baada ya kunieleza hayo, aliniuliza kama anaweza akafanya chochote kunisaidia, mimi nikamwambia hapana, ni mambo binafsi tu, nitayamaliza kwa mikono yangu mwenyewe.

Akaniuliza, "kwa mikono yako mwenyewe?"

Sikuelewa anamaanisha nini na swali hilo ila mimi nikamjibu ndivyo, nitayamaliza kwa mikono yangu mwenyewe, basi akaniaga na kwenda zake, alirudi kule mabandani alipotokea. Sikujua alikuwa anafanya nini huko lakini sikujali, alimradi nilibaki peke yangu basi ilinitosha.

Niliangaza kule mabandani, kwa umbali ule nilokaa sikuweza kuona jambo lolote zaidi ya giza, Amiri alinionaje kama nalia? Nilijiuliza, au upande ule alokuwapo aliweza kuona upande wangu sababu ya mwanga? Yawezekana.

Nilihitimisha hivyo na sikukaa tena hapo nikaondoka kwenda zangu ndani, sebuleni nikamkuta mama yule ameketi anatazama runinga, sikusumbuka naye mimi nikanyoosha zangu niende chumbani, hatua nne akaniita.

Aliniuliza kama chakula chake nimeshamwandalia, nikamjibu ndivyo, kila kitu kipo tayari. Hii ilikuwa ni mara ya pili ananiuliza, mara ya kwanza alifanya hivyo nikiwa natoka kwenda kule nje, nikamwambia kila kitu kipo tayari na pia nikamuuliza kama angependa nimhudumie? Akakataa.

Sasa nilirudia tena kumuuliza, nikuhudumie mama? Napo akakataa, hakusema kitu bali alitikisa tu kichwa chake, basi mimi nikaenda zangu chumbani, huko nikamkuta bwana yule ameegamia kingo ya kitanda, yuko 'busy' na simu yake. Sikutaka kuhangaika naye, nikafanya taratibu ya kwenda bafuni kuoga ili nilale zangu mapema maana kesho kuna kwenda kazini.

Nilipoingia bafuni, sijakolea na kuoga, nikasikia sauti ya mama mkwe ikimuita Mgaya kule sebuleni. Mgaya alifungua zake mlango akaenda huko, baada ya hapo sikusikia kitu tena mpaka nilipokuja kutoka bafuni.

Kule sebuleni kulikuwa na maongezi yanaendelea baina ya mama na mwana, nami sikuyajali sana nikaendelea na mambo yangu, wakati huo najifutafuta maji mwilini, kidogo mlango wa chumbani ukafunguliwa bwana Mgaya akaingia ndani, bwana huyo alikuwa amefura sura yake, alipoingia aliufunga mlango akasimama hapo akiwa ananitazama.

"Bwana vipi?" Nilimuuliza, hapo nikawa nimefungulia rasmi koki ya maneno, bwana huyo akaanza kunimwagia maneno yaso na kifani. Alinisema simjali mama yake, simpatii chakula na wala simuagui. Hakunipa hata muda wa kuongea, aliyasema maneno yote mwenyewe nisibakiziwe hata moja la kutamka.

Nilimsihi basi apunguze sauti ili tusimwamshe mtoto lakini hakujali, hasira ilikuwa imemkaba koo, hakuweza kujimudu, ninachoshukuru mtoto hakuamka hata na yote yale.

Lakini,

Ubaya wangu mimi ulikuwa ni nini? Mbona niliamka mapema kufanya maandalizi yote na hata kumpikia mama yule chakula kinachoendana na hali yake ya ugonjwa? Mbona nilimfuatia na kumtimizia kila alichoniagiza? Sikuelewa.

Wakati mume wangu anaongea hayo, nikasikia sauti ya yule mama, sauti ambayo ilinifanya niwaze hivi kweli mama yule alikuwa anaumwa au lah? Mwanamke yule alipaza sauti akisema ni heri arudi nyumbani akauguzwe na Momo, Momo ni yule mwanamke aliyeolewa na Mgaya kule kwao, kweli kauli hiyo ikanipenya kama mkuki wa moto kifuani mwangu, mdomo wangu haukusema jambo lakini macho yangu yalieleza, ilifikia kipindi nikawa sioni kwa mboni zangu kumezwa na machozi.

Nilijilaza kitandani nisiseme na mtu, baada ya muda mchache nilimezwa na usingizi nisijue hata ni saa ngapi ulinikwapua. Nilizama humo kwenye kiza cha usingizi angalau nipate ahueni ya maisha yangu halisi, ahueni ya yale niliyokuwa nayapitia, lakini napo ilishindikana! Sikupata unafuu wowote ule.

Katikati ya usiku huo,

Niliamka nikamtazama mume wangu, alikuwa anakoroma kama gari moshi, nikamtazama mwanangu pia, naye anamwaga mate kwa utamu wa usingizi, basi taratibu nikaamka kuufuata mlango kwa kunyata, niliufungua mlango huo pasipo kutoa sauti yoyote ile, taratibu sana kama mwizi, niliposhika korido nikajongea kuufuata mlango wa chumba alichokuwamo mama mkwe wangu, hapo pia nikaufungua mlango huo kwa umakini sana, taratibu mno pasipo kutoa sauti kisha nikazamia humo.

Nilitupia macho kitandani, nikamwona mama yule amelala kifudifudi, kwenye dari feni linapepea kwa kasi sana, sauti ya feni hiyo ndo' imemeza chumba kile kizima.

Basi nikajongea na kukwea kitandani kisha nikamkalia mama yule na kumfunika uso wake kwa nyama za mto.

Kufa! Kufa! Kufa!

Alipapatuka kutafuta hewa lakini sikumpatia hiyo nafasi kabisa. Nilitumia nguvu zangu zote nilizonazo kuhakikisha ninammudu na kweli hakunishinda. Mto ulifyonza pumzi yake yote aliyoitoa mapafuni lakini asipate pumzi nyingine ya kuingiza, muda si mwingi mama huyo akakubali kuongozana na kifo, kuongozana nacho kwenda huko kusikojulikana, miguu na mikono yake ilitulia tuli, nikajiaminisha tayari nishamaliza kazi.

Basi nikamtazama uso wake, uso ulomezwa na umauti, moyo wangu ukafurahi, sasa mnongwa huyo alikuwa amekwenda, aende sasa huko aendako akaharibu ndoa za malaika kama zipo, dunia imemshinda ustaarabu.

Nikiwa hapo, natabasamu na huku feni yanipuliza, mara nikakurupuka baada ya kusikia mtu anaufungua mlango, kutazama namwona mume wangu akiwa anaingia bafuni, kiunoni amefunga taulo, kumbe muda wote huo nilikuwa kitandani nikiyaota yalotokea.

Nilikuwa naota? ...

Hapana, hapana!

Nilisema mwenyewe nikijipapasa mwili kama mwehu. Kama kweli ilikuwa ni ndoto mbona mikono yangu, humu mabegani, pananiuma? Sikuelewa. Nilinyanyuka nikaenda kutazama mlango ule wa chumbani, nikauona una upenyo mdogo wa uwazi, mlango haukuwa umefungwa, nikafungua kutazama koridoni, hapana mtu, nikatazama mlango wa chumba alicholala mama mkwe, nao mlango wake nikauona u wazi, tena si kama huu wa kwangu, la hasha, wenyewe ulikuwa umeachama kama behewa.

Upesi nikafunga mlango wangu kisha nikarudi kitandani, sikupata tena usingizi mpaka majira ya saa kumi na moja, majira ambayo ndo' huwa naamka kumwandaa mtoto na mimi pia kwaajili ya kwenda kazini.

Nilimwamsha mtoto nikamwandaa vema kisha nami nikaanza kujishughulikia, muda wote huo bwana Mgaya akiwa amelala hana hili wala lile. Nilipokuwa bafuni naoga akili yangu ikawa inarejelea mambo ya ndoto ile, ndoto niliyoota usiku wa manane.

Niliitafakari hatua kwa hatua nikiyakanda mabega yangu yalokuwa na maumivu kwa mbali, maumivu kana kwamba nilibeba kiroba cha mawe, nikisema na nafsi yangu; maumivu haya nimeyatolea wapi?

Niliitazama mikono yangu, vidoleni kupanda mpaka kwenye viwiko, hakukuwa na kitu, nikaibinua mikono kutazama nyuma ya vidole na mgongo wa viganja vyangu, kwenye mkono wa kushoto, nikaukuta mkwaruzo mdogo.

Niliugusa mkwaruzo huo nikahisi maumivu kwa mbali, ulikuwa ni mkwaruzo mbichi, sikukumbuka niliupatia wapi na nilikuwa nikifanya nini, nikamalizia zangu kuoga kisha nikatoka kwenda kuvaa.

Niliweka kila kitu sawa hapo nyumbani, ikiwemo kuacha chakula cha mgonjwa na pia cha Amiri na bwana Mgaya, bwana huyo alishanambia ana mapumziko ya siku kadhaa hapo nyumbani hivyo kwangu haikuniwia ugumu kuondoka kuendelea na majukumu yangu.

Muda si mrefu, basi la shule lilifika kutuchukua mimi na mwanangu, tukakwea humo na safari ya kwenda shuleni ikaanza. Nikiwa nimeketi kwenye kiti nilitoa simu yangu nikawa naitazama kupotezea muda na kufupisha safari.

Nilitumia muda huo kutazama 'messages' za bwana Mgaya, messages ambazo zilikuwa zimejaa pomoni lakini sikuhangaika kuzisoma wala kuzijibu, nilizipitia moja baada ya nyingine.

Ujumbe wa kuniomba msamaha kwa yale yalotokea kule Iringa, niliouona, ujumbe wa kuniambia ameachana na yule mwanamke tuijenge familia, niliuona, ujumbe wa kwamba anakuja na mama yake kumuuguzia Dar, niliuona, ujumbe wa kunitaka tuongee na kuyamaliza, niliuona, yani kila kitu nilikiona.

Lakini ilikuwa 'too late', Mgaya.

Tulishachelewa.

Sasa tuko nje ya muda.

... Wakati tunaingia kwenye uzio wa shule, simu yangu iliita na nilipotazama nikaona jina la Mgaya. Nilipokea simu hiyo, kabla sijasema kitu Mgaya akaniambia kwa pupa mama amezidiwa sana sana, yuko njiani pamoja na Amiri wakielekea hospitali.

Alinitajia jina la hospitali hiyo.

Nami pasipo kupoteza muda, punde tu baada ya kumwacha mtoto darasani, nilikimbilia kwenda huko hospitali huko kutazama. Kufika, Mgaya ananiambia mama amekwishafariki. Sababu ya kifo chake ni sukari na presha iliyopanda kwa mkupuo!

***
Ahsante sana brother SteveMollel vitu kama hivi usiache kuniita.
 
Ahsante sana Huuruly'iin ajaye baby zu

Ila hawa wawili nao ni km walikuwa wanatafutana hivi, yaani mama mkwe na mkwe wake.

Sitoshangaa hata huyu mke wa mgaya nae kuja kuwa mkwe katili.

Nawaza anavyoota ndoto mpaka za kuua.

Jamani wazazi watengezeni watoto wenu wawe waume na wake bora huko waendako kwenye maisha yao. Ukimuandaa mtu vizuri bila shaka nawe utakuwa vizuri na kinyume chake...

Sijamuona dada yetu Bantu Lady
 
Lovelovie leadermoe Unforgettable kitalembwa moneytalk Doctor G Santos06 Advicer one mistakes mmash Mafian cartel Restless Hustler
Antonio de Guzman episode 6 tayariii
 
Ahsante sana Huuruly'iin ajaye baby zu

Ila hawa wawili nao ni km walikuwa wanatafutana hivi, yaani mama mkwe na mkwe wake.

Sitoshangaa hata huyu mke wa mgaya nae kuja kuwa mkwe katili.

Nawaza anavyoota ndoto mpaka za kuua.

Jamani wazazi watengezeni watoto wenu wawe waume na wake bora huko waendako kwenye maisha yao. Ukimuandaa mtu vizuri bila shaka nawe utakuwa vizuri na kinyume chake...

Sijamuona dada yetu Bantu Lady
hio sio 'ndoto' ila ni amiri alitumia mwili wake kumuua huyo mama,.....

si umesoma hapo alimuuliza 'kwa mikono yako?’ alipojibu ndio ndipo amiri akaondoka,
sema huyo amiri inaonekana ni mwanga si wa nchi hii, [emoji23]
 
Back
Top Bottom