Niliweka shada za maua kwenye makaburi matano ya watu wangu wa karibu

"Tivu mollel" katika ubora wake[emoji16][emoji16] mzee wa BIG wa kule goba [emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Sehemu ya Kumi na Nne:

Nilienda nje ya uzio, moja kwa moja mpaka shambani, palepale ambapo mimi na Amiri tulimfukia mwili wa mtu, nikaangaza hapo na macho yangu bora, kidogo nikaona mahali penye alama ya kuchimbikachimbika, hapo sasa nikasema na nafsi yangu, alah! Unaona?

Kile nilichokiota kilikuwa halisi halisia!

Hapa ndo' tuliuzika mwili wa Zai, ndio ni hapa, nina uhakika kabisa.

Lakini mbona nimemwona Zai kule ndani, jikoni? Tena nimemwona akiwa mzima wa afya tele, anasimama kwa miguu yake na anaongea kwa mdomo wake?

Sasa hapa tulizika nini?

Mgaya alishafika hapo, hapo nilipokuwa nimesimama naangaza, akaniuliza ni nini nafanya hapo? Nini kimenikumba?

Natamani kumwambia lakini naanzia wapi? Nikimweleza ya ndoto ile si ataniona mimi muuaji? Ikabidi nimdanganye ...

Nilimweleza yale yote yalikuwa ni ndoto mbaya niliyoota usiku ule. Niliota mnyama mkubwa wa kutisha ambaye alivunja akaingia ndani, akaharibu na kutekeza kisha akatoka kukimbilia kule nje.

Nilijaribu kuyatengeneza hayo maneno yaonekane uhalisia ili aamini uongo ninaosema, kweli nikafanikiwa, bwana Mgaya alinipa pole kisha akanitaka turejee ndani, bila hiyana nikaongozana naye lakini kichwa changu nilikiacha pale shambani.

Niliwaza lakini nilishindwa kuwazua, pale pamefukiwa nini?

Niliona ni vema nikatulia kwanza bwana Mgaya ajiandae na kwenda zake kazini ili nibaki huru kufanya uchunguzi wangu.

Kweli, kama lisaa mbele, bwana Mgaya akawa tayari ameshajiandaa na yupo kwenye gari tayari kwaajili ya safari.

Kama kawaida yangu nilienda kumuaga bwana huyo kabla hajajiendea, nilikuwa na desturi ya kumuaga kwa kumpatia busu na kumtakia kheri ya kazi, hii ni endapo tukiwa kwenye kula 'mema ya nchi' lakini akinitibua maji huwa namwacha aende zake kama mtoto yatima.

Nilimuaga akaniuliza jambo...aliuliza kwa sura ya utani lakini swali lile liliacha alama katika fikra zangu.

Alisema, "hivi unakumbuka yale ulokuwa unayaongea wakati unaota?"

Akatabasamu, tabasamu ambalo halikuendana na macho yake, kisha akaondoka zake akiniacha na fumbo.

Atakuwa ameyasikia mangapi? Alinisikia kwa muda gani nikiwa naongea?

Niligunia kifuani mwangu.

Nilitumai sikuharibu kiasi kikubwa, nikameza mate na kuendelea na mengine, mengine ambayo yalikuwa yanangoja bwana huyo anipe nafasi.

Nilimwendea Amiri kule bandani nikamuuliza kama anahisi chochote kuhusu usiku wa jana, ajabu Amiri alinitazama kwa macho ya mshangao, akaniuliza kitu gani haswa?

Nikamweleza hakuota kitu chochote siku hiyo? Akaniambia kweli ameota ila aliota akiwa anapambana na ng'ombe tu, zaidi ya hilo alikurupuka asubuhi akiwa amekawia kidogo kwaajili ya kukamua maziwa.

Nikamtaka aongozane na mimi mpaka kule shambani, huko nikamwambia afukue pale nilipokuwa napatilia shaka, pasipo ubishi Amiri akafukua kwa jitihada zake zote, alipakua chepe baada ya chepe mpaka chini ambapo tulikuta mzoga wa paka.

Paka mweusi.

Paka huyo alikuwa anatoa harufu kali kweli, tukaziba pua.

"Amiri!" Niliita nikauliza, "ni wewe ulimfukia huyu paka hapa?"

Amiri akanambia ndiye, alimdaka paka huyo akiwa anazengea kule mabandani, ndiye paka anayeua mifugo na kula pia mayai, hivyo alivyomkamata hakufanya ajizi bali kummaliza kabisa.

Alinambia alifanya zoezi hilo usiku wa jana yake akiwa peke yake, anastaajabu mimi nimefahamu vipi habari hiyo maana hakuna aliyemweleza.

Aliniuliza, "uliniona wakati nakuja kumfukia?"

Sikumjibu, nilirudi zangu ndani nikiwa nayatafakari yale niloyasikia na kuyaona, kweli mambo yalikuwa tafarani kichwani mwangu nisielewe 'a' wala 'be'.

Nilimkuta Zai ameketi pale sebuleni, anapata kifungua kinywa.

Aliponiona alinisalimu tena kisha akaniuliza nini kimenisibu? Mbona naonekana sipo sawa mapema yote ile asubuhi?

Niliketi nikamwambia ni ndoto mbaya niliota, hamna jingine zaidi ya hilo, baada ya hapo nikamuuliza kuhusu usiku wake, nilitaka kujua kama kuna kitu chochote alihisi usiku ule lakini ajabu akanambia hamna jambo, alilala kama mtoto mdogo mpaka asubuhi ile ya mapema.

Alisema, "baada ya kuchoma ubani na kufanya dawa yangu sidhani kama nilijigeuza mwili mpaka asubuhi naamka."

Aiposema hayo, akaniuliza mimi, kwani wewe umeota nini?

Sikutaka kumpa maneno mengi na sikutaka kusababisha taharuki pale, nikamdanganya kama nilivyomdanganya bwana Mgaya, muda ukasonga.

Baadae majira ya mchana, kama alivyokuwa amepanga, Zai aliniaga anaenda zake, alinambia anashukuru sana kwa kumpokea na kumkarimu pale nyumbani kwangu, sasa yampasa aende zake akaendelee na shughuli zingine.

Nami ningefanya nini? Ningemkataza mtu asiende nyumbani mwake?

Japo sikutaka, mpango wangu haukwenda vile nilivyodhamiria, ila sasa sikuwa na budi.

Nisingeweza kumzuia Zai na tayari ameshanambia amepata fursa adhimu kwa wazungu, malipo yake pomoni, si ningeonekana mshirikina?

Nilimsindikiza mpaka kituoni, akakwea usafiri na kwenda zake.

Akaondoka akiniacha na mawazo kichwani, nini kinachofuatia? Nini mwanamke huyo alichopanga? Nini hatma yangu kwake?

Nilijikuta nakosa raha kila nilipofikiria yale ya Anwari.

Nilirudi nyumbani kinyonge, kichwa kizito kama jabali, miguu kama mibuyu, nilipofika nikajilaza kwenye kochi nikijaribu kuwazua.

Hata hamu ya chai sikuwa nayo kabisa, sihisi njaa kana kwamba nimekula chakula cha maana.

Haikupita muda mrefu nikakutana na kijana Amiri katika pilika zake za hapa na pale.

Kijana huyo aliniuliza mambo ya rafiki yangu Zai, nikamweleza kila kitu, akaniambia si unaona? Yale nilokueleza ni kweli, sasa kuwa makini na mwanamke yule, si rafiki wa kweli.

Hashindwi kunitokomeza muda wowote ule.

Aliposema hayo nilishikwa na hasira sana, ni kama vile kidonda kilitoneshwa upya, nikakumbuka namna nilivyojitoa kwa Zai, namna nilivyompambania mwanamke yule kwa mambo yake yote, nikajiuliza tena na tena ubaya wangu kwake ulikuwa wapi?

Ulikuwa upi?

Sikuuona.

Hamna kingine nilichotamani sasa kwa Zai, isipokuwa jambo moja tu.

Kifo chake.

Niliamini yeye, kwa muda huo, ndo' alikuwa kikwazo pekee kilichobakia mbele ya familia na ndoa yangu yenye furaha.

Laiti asingalikuwapo, nilisema mwenyewe ndani yangu, basi ningaliweza kumudu chochote kile kumhusu mtoto yule ambaye kiukweli hakuwa wa bwana Mgaya.

Siku hiyo ilienda na taabu zake vivyo hivyo, kesho yake asubuhi na mapema nikadamka kushika kazi za nyumbani, kazi kama ilivyo ada kila nipatapo nafasi ya kushinda nyumbani.

Wakati natimiza agizo hilo la mwenyezi Mungu, asiyefanya kazi na asile, ndipo simu yangu ikaita mwanangu akanikimbizia kuniletea.

Kutazama kwenye kioo, namba ni ngeni.

Nikasita kupokea, niliitazama simu hiyo ikiita mpaka kukata kwake kisha nikaendelea na shughuli zangu, kidogo tena namba ile ikanibishia hodi, inaomba hima hima nipokee, nikaitazama nikijiuliza na kujidai sababu ya kupokea simu hiyo.

Mwishowe, nikaona na akili yangu, ni vema nikapokea na kus'kiza, acha niamini kwenye wito, ujumbe nitaukubali ama lah.

Vipi kama namba hiyo ni ya msamaria anayetaka kunipasha habari ya Zai? Au ni mtu wa nyumbani aliyebeba ujumbe maalum?

Kupokea nikasikia sauti ngeni, sauti ya mwanamama aliyenisalimu kisha akauliza kama anaongea na mama fulani.

Nilipomjibu ndio, mama huyo alijitambulisha kwangu kama mama yake na Anwari kisha akaeleza haja ya simu yake.

Haja yenyewe ni kuonana na mimi.

Alisema, "tafadhali naomba tuonane, kuna jambo muhimu naomba tujadili."

Siwezi kuelezea ukanielewa ni namna gani simu na sauti ile ilin'tibua ubongo wangu.

Kwa muda mchache nilijikuta katika bumbuwazi la karne, akili inawaza mambo alfu kumi na kenda kwa wakati mmoja alafu yote yanatakiwa majibu kwa upesi.

Mama huyu anataka nini kwangu? Kapata wapi namba yangu? Anataka kunieleza nini? Huyo alompa namba yangu ameishia hapo? Ama amempatia mpaka anwani ya makazi yangu? Anafahamu huyu mtoto ni wa Anwari? Nani kamwambia?

Nilijisahau kama naongea na simu kisa butwaa, butwaa la mawazo.

Mwanamke yule sijui aliniita mara ngapi, mimi nilikuja kuambulia 'hello' ya mwisho aloisema kwanguvu, ndo' kuamka na kumshushia maswali lukuki, maswali ambayo hakunijibu hata moja zaidi ya kunisisitiza na kunisisitiza tuonane na hayo yote yalonikalia kooni nitapata majibu yake.

Sasa ikawa rasmi simu ile imetibua siku yangu nzima, tena tokea asubuhi ya mapema.

Waswahili husema nyota njema huonekana asubuhi, lakini siku ile hapana, haikuwa hivyo, nyota ile ya asubuhi haikuwa na wema wowote kwangu zaidi ya kuniangazia balaa.

Simu ilipokata niliacha kila nilichokuwa ninafanya nikatulia kwanza kwenye kochi, hata nguvu ya kunyanyua kijiko sikuwa nayo, macho yenyewe kuna muda yaligoma kuona yakanitupia kizani, kiza cha dunia ya mawazo, dunia ya msongo.

Lakini mwisho wa yote hayo haukuwa mwingine bali malangoni mwa Zai.

Hakukuwa na njia nyingine isipokuwa yeye, njia yangu ya mateso.

Niliamini ni yeye ndiye alimpa mama Anwari namba yangu, lakini bila shaka atakuwa pia kampa na maneno, hayo maneno ndo' yakawa yananiumiza kichwa zaidi, atakuwa kamfungukia mangapi?

Nilipiga simu ya Zai haikupokelewa. Simu iliita kama mara tatu hivi pasipo majibu.

Nilijaribu tena na tena lakini matokeo yalikuwa yaleyale, nikaona nitume ujumbe, ujumbe wa kumtaka anipigie punde tu atakapopata nafasi.

Lakini ajabu nilimgoja na kamwe mwanamke huyo hakukaa akapiga kama nilivyotegemea, sasa nikahisi anafanya makusudi, makusudi baada ya kujua alichokifanya kwangu, hataki kupokea maana anaona haya.

Nikaachana naye.

Keshokutwa yake, nikiwa naendelea na majukumu yangu ya kila siku shuleni, simu yenye namba ngeni iliniita kwenye kioo.

Nilipoona namba hiyo haipo katika kumbukumbu zangu, nilisita kupokea, nilidhani ni mama yule ananitafuta lakini nilipokuja kutazama vema nikaona namba hizo ni tofauti, hata mitandao yake haikuwa sawa, nikakata shauri kupokea.

Kumbe alikuwa ndugu yake na Zai, mwanamke huyo baada ya salamu fupi aliniuliza kama ninampata Zai hewani, yeye anampigia mara kadhaa lakini hampati, nikamweleza nami ni hivyohivyo, sijabahatika kumpata hewani pasi na kujali nimemtafuta mara ngapi.

Ndugu yake na Zai akanieleza ati ni jana tu alitoka kuwasiliana na mwanamke huyo, tena wakapanga mambo kadhaa, akakata simu akinisisitiza basi nitakapompata mwanamke huyo nimwambie ndugu yake anamtafuta.

Baada ya hapo sikuwasiliana tena na mwanamke huyo na nisiwe muongo sikumtafuta hata Zai vilevile, kwenye majira ya jioni baada ya kurejea nyumbani ndipo mama yake na Anwari naye akanitafuta.

Niliona namba yake kwenye kioo, pasipo kujiuliza mara mbili nikamtambua na nikaweka nadhiri sitaipokea simu hiyo.

Simu ilipoita na kukata, ujumbe uliingia, ujumbe toka kwa mwanamke huyohuyo alokuwa anapiga, nilipuzia ujumbe huo nikaendelea na shughuli zangu, ni baadae baada ya kupigiwa simu na ndugu yake Zai ndipo nikaukumbuka ujumbe huo na kuusoma.

Ujumbe ulisema: 'habari yako? Naomba unipatie namba ya Zainabu inayopatikana.'

Ujumbe huo na na ile simu ya ndugu yake Zai vikanifanya sasa nizingatie jambo la Zai kwa mapana yake.

Nilijaribu kumtafuta tena lakini sikumpata hewani kama ilivyo kwa wenzangu, nikapanga basi kesho nitasumbuka na jambo hilo lakini siku hiyo isiishe, nikaja kupokea simu hapo baadae kama majira ya saa nne hivi, simu kutoka kwa ndugu yake na Zai.

Mwanamke huyo alinambia habari ambayo kwakweli ilinishangaza.

Alinambia alienda nyumbani kwa Zai kumjulia hali kutokana na maagano walokuwa wameyaweka, maagano ya pesa ambayo hakutaka kunieleza kwa undani.

Alinambia alikuta mwili wa Zai umetolewa ndani na kupelekwa hospitali baada ya majirani kuvunja mlango wake kwasababu ya kuhisi harufu kali kutoka humo ndani.

Majirani hao waligonga na kuita, walipoona kimya wakavunja komeo kushuhudia, humo ndo' wakamkuta mwanamke huyo kando ya kitanda chake akiwa anatoa harufu kali wasielewe nini kilimuua.

Majirani walisema shaka lao lilikuwa kubwa zaidi maana hawakumwona mwanamke huyo kwa muda kidogo, nami nilielewa shauri hilo kwa maana Zai alikaa kwangu kwa siku mbili na hapo kabla alikuwa anakaa kwa yule ndugu yake kabla ya kukosana.

Lakini kwa mahesabu yangu, tangu Zai alipotoka nyumbani kwangu na pia tangu alipoonana na ndugu yake, haikumalizika hata siku mbili kama sio siku moja, sasa mbona Zai kuoza kiasi cha kutoa harufu kali ya kukera pua za majirani?

Nilinyanyuka upesi nikaelekea huko, huko nyumbani kwa Zai, kufika nikakutana na ndugu yake ambaye alinieleza kila anachojua kuhusu tukio hilo, mengi yakiwa yale aloambiwa na majirani ambao walishuhudia yalosibu.

Ajabu maelezo yale alonipa ndugu yake na Zai niliyaona kama sio mapya katika mafikirio yangu, ni kama vile nilikuwa nasikia upya kitu ambacho nishawahi kukiona ama kusimuliwa pahala fulani.

Mwili wa Zai ulikuwa unanuka kama mzoga wa paka ... Mwili wa Zai ulikutwa pembeni kwenye kingo ya kitanda ... Kichwa cha Zai kilikutwa na jeraha kubwa kisogoni ... Chumba cha Zai kilikutwa na mabaki ya udi dirishani ... Yote haya kwangu hayakuwa mageni, yote haya nilishayaona pahala, na pahala penyewe si kwingine bali kule nyumbani kwangu.

Sasa niliona naelekea kuchanganyikiwa, nahitaji msaada wa haraka, hii sio hali ya kawaida.

Nilitamani nipate mtu wa kumweleza yote hayo lakini nani ataniskiliza akanielewa bila kunihukumu na kunishtumu?

Kuna mwingine zaidi ya Amiri?

Kweli sikuona.

Pasi na kujua kumbe ndo' nazama kwenye mdomo wa mamba, mdomo ambao hautaniacha na nyama yoyote ile mwilini bali mifupa tu.

Amiri, sijui huko uliko utakuwa upande gani wa jehanamu?

Kukaa pamoja na wezi wa kuku, waongo na vibaka kweli itakuwa ni dhulma, si haki, Amiri unastahili zaidi ya uji huu wa moto tunaoambiwa kwenye vitabu vya dini.

Na bila shaka, mimi nitakuwapo pembeni yako.

...
 
Pmj mwamba
 
Back
Top Bottom