Niliweka shada za maua kwenye makaburi matano ya watu wangu wa karibu

Sehemu ya Kumi na Sita:

Nilimtwaa mtoto kwenye mikono ya Amiri nikaingia naye ndani.

Kwasababu muda ulikuwa umeenda, ni majira ya kulala sasa, nilimpeleka mtoto bafuni kumwogesha na kumfanyia maandalizi ili apate kulala, nilipomaliza shughuli hizo nikamkuta bwana Mgaya tayari ashalala zake, hakukaa kuningoja, nami sikumwamsha nikamlaza tu mtoto kisha na mimi nikajilaza nikiwa natazama dari.

Natazama feni inavyozunguka.

Natafakari yale bwana Mgaya alotoka kunieleza.

Nawazua nini kilitokea.

Nilidhani nitakaa hapo kufanya cha maana kichwani mwangu lakini sikufanyikiwa hata tembe, usingizi ulinibeba kwelikweli, msobemsobe, mpaka asubuhi nilipokurupuka nikiwa nje ya muda.

Nilitazama simu yangu nikahamaki ni saa moja ya asubuhi, sijaandaa chochote, si mtoto wala chai, na ilikuwa ni siku ya kazi!

Bwana Mgaya alikuwa tayari ashaondoka kwenda kazini, nikastaajabu sana, ina maana alipokuwa anajiandaa sikupata kusikia chochote nikaamka?

Nililala usingizi ama nililala kifo?

Nilimkwapua mtoto kumpeleka bafuni, nikakumbuka ni vema kwanza nitoe taarifa kwa simu, nitume ujumbe kule kazini kwamba nimepatwa na dharura na basi nitachelewa kufika.

Niliandika ujumbe mrefu wa wongo kisha nikautuma kwenye namba ya Mtaaluma na Mkuu wa shule, nilipomaliza ndo' nikaendelea na shughuli zangu, sasa angalau nikiwa nimeishusha presha japo kidogo.

Nilimaliza kila kitu ndani ya kama dakika ishirini hivi, nikaoga na kwenda kazini siku hiyo nikitumia usafiri wa daladala, mpaka kufika shuleni ni saa tatu, tena inayokimbilia kuitafuta saa nne.

Naingia kazini kama mkurugenzi.

Nilinyookea ofisini kwangu, kwa ratiba tayari nishapitwa na vipindi viwili, upesi nikashika kalamu kujiandaa na kipindi cha mwisho nilichobakiwa nacho, kipindi cha saa sita mchana, wakati huo jasho linanitoka na bado nahisi mwili wangu umejawa na uchovu mwingi.

Nikiwa naandaa kazi hiyo, ndo' Madam Beatha aliingia akitokea darasani alipokuwa anafundisha, akanisalimu kwa mdomo wa pembeni na kusema kwa dhihaka, "naona malkia wa shule ndo' unaingia sasa. Karibu mtukufu malkia."

Sikumsemesha jambo, niliona ni kupoteza nishati yangu bure na mtu anayetafuta jambo kwanguvu, niliendelea na kazi yangu nikipuuza kama kuna kiumbe kando yangu, kidogo mwanamke huyo alinyanyuka akaenda zake.

Bila shaka alienda kwenye ofisi ya mtaaluma maana haikupita muda alirejea akanambia naitwa huko ofisini, tena nimeambiwa niende upesi.

Sikuwa na budi bali kuitikia wito, jeuri ya kumkatalia mtaaluma wa shule mimi naitolea wapi?

Nilienda huko nikakutana na Madam mhusika, bila kuchelewa akaniuliza kuhusu kuchelewa kwangu kuwasili kazini, nini kilinikumba na kwanini sikutoa taarifa, nikajikuta nastaajabu na maswali hayo kwani nakumbuka vema nilitoa taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi kwenda kwa kila mhusika.

Nilimwambia Mtaaluma kuhusu hilo, ajabu akanambia hajapata taarifa yoyote ile kutoka kwangu, alinionyesha mpaka simu yake akiniuliza taarifa iko wapi? Ebu nionenyeshe.

Alimpigia simu mkuu wa shule akamuuliza kama ana taarifa yangu, mkuu akasema hana taarifa yoyote kutoka kwangu, hapo nikazidi kushangaa.

Nilitoa simu yangu kuonyesha kama ushahidi wa yale niloyasema, kuonyesha ujumbe wangu nilotuma, lakini ajabu nilipotazama nilikuta ujumbe ule kumbe haukwenda!

'Messages' zote zilikuwa zimeweka alama ya mshangao kumaanisha zimegoma, nikachoka kabisa, sasa nasema nini?

Nilimwonyesha mtaaluma kwamba niliutuma ujumbe lakini hakutaka hata kuelewa, alikuwa mkali kama pilipili, tena pilipili kichaa, kwa msisitizo akaandika taarifa ya kuniadhibu kwa kunikata pesa yangu ya mshahara kama ilivyo taratibu ya pale shuleni kwamba mtumishi akikosa siku ya kazi pasi na ruhusa basi siku ile uhesabiwa na kukatwa katika mshahara wake.

Nilijaribu kumweleza haikuwa siku nzima bali masaa tu lakini hakutaka maelezo, alisema masaa matatu ya kazi, tena ya majira ya asubuhi, ni sawa na siku nzima, hivyo adhabu ni ileile.

Nilipomaliza maongezi hayo sikuwa na namna ingine bali kurejea kwenye majukumu yangu, niliendelea kuandaa kile nilichokuwa naandaa na baada ya hapo nikaingia darasani.

Nilifundisha lakini kwa taabu sana, mwili ulikuwa haunitumi kabisa, najihisi nimechoka na mara kadhaa najihisi kutapika pale ninapohisi harufu za mafuta.

Mpaka namaliza kipindi salama nilishukuru. Nilirejea ofisini na sikuchukua punde nikapitiwa na usingizi palepale kwenye meza, tena usingizi mpaka mate, kuja kugutuka ni saa za watoto kuondoka, tena alokuja kunishtua ni mwanangu, mama mama let's go home.

Nilienda nyumbani na nilipofika nilijitahidi sana kupika chakula cha jioni, kumaliza niko hoi, nikaketi kwenye kochi nikitazama runinga kivivu.

Nilimwomba Amiri anisaidie kunifanyia usafi pale jikoni na alipomaliza nilimwomba pia anifanyie usafi kule chumbani mwangu, ni siku tatu sasa sikuwa nimefanya usafi huko, sasa nilikuwa naona aibu maana nimekuwa mzito kupita kiasi.

Amiri alinifanyia usafi kama nilivyomuagiza kisha akaenda zake nje na mtoto, nilishukuru sana maana nilitaka nibaki mwenyewe nipumzike vizuri, nikatuama hapo kwenye kochi mpaka pale bwana Mgaya aliporejea.

Siku hiyo nilipanga kumwambia bwana huyo kuwa nina ujauzito, nilitaka nione mwitikio wake utakuaje, lakini sikuwa na haraka naye, nilingoja muda sahihi utakapowadia basi nifanye hivyo.

Lakini isipite muda mrefu usiku wangu na bwana Mgaya ukaanza kuharibika.

Nilimletea bwana huyo chakula, chakula nilichoandaa kwa taabu za mwili wangu, akanambia ameshiba kabisa hataweza kula.

Nilimuuliza amekula wapi majira hayo, akanambia alitoka na marafiki zake kwenda pahali fulani huko wakanywa na kula mpaka kutosheka.

Kwahiyo bwana huyo, alikaa pale sebuleni akicheza na simu yake na rimoti ya televisheni mpaka alipoondoka kwenda zake chumbani.

Kwahiyo chakula nilichoandaa nikaishia kula mwenyewe.

Baadae kidogo, usiku huohuo, nilipokea simu kutoka nyumbani kijijini, mama alikuwa ananipigia, lakini nilipopokea simu hiyo ni sauti ya mdogo wangu Sarah ndiyo ilinipokea na kunisalimu.

Alinambia amemwomba mama aongee na mimi, amenikumbuka sana na pia ananikumbusha nimtumie ile pesa nilomuahidi.

Kipindi hiko na Sarah ndo' alikuwa ametoka kumaliza kidato cha nne muda si mrefu, alikuwapo tu nyumbani akingojea matokeo yake.

Siku kadhaa zilizopita nilikuwa nimezugumza naye na nilimuahidi nitamtumia kiasi fulani cha pesa kwaajili ya matumizi yake madogo madogo, lakini sasa bajeti yangu ilikuwa imepandana, nilishatuma pesa kwa mama juma lililopita ili akamilishe baadhi ya mambo kule shambani na kwa muda huo sikuwa vema.

Nikamwambia Sarah anivumilie mpaka mwisho wa mwezi, punde nitakapopata pesa basi nitamfanikishia jambo lake, kwa shingo upande akaridhia na mimi nikaikata simu.

Hayo ndo' maisha yetu sie watu wa chini, wala hakukuwa na swala jipya hapa, kwetu sisi utakapofanikiwa hata kwa hatua moja mbele basi inabidi ujiandae kuyabeba majukumu.

Kazi yangu ilikuwa ni kijungu jiko, kipato hakitoshelezi, lakini utafanyaje sasa?

Hikohiko kidogo inabidi kigawanywe kwenye mikono yote.

Nilimaliza kuongea na simu nikaenda zangu ndani kumkuta bwana Mgaya, nilimkuta bwana huyo amejilaza kitandani habari hana, taratibu anautafuta usingizi.

Sikumwongelesha, nikahangaika na mambo yangu. Nilimwogesha mtoto na mimi pia nikaoga kisha baada ya hapo nikalala usingizi mzito kandokando ya mwanangu.

Kwenye usiku mnene, sijui kilinitokea nini, sikumbuki kwakweli lakini nilijikuta usingizi wangu wote umekata ghafla na macho yapo kodo kukodolea dari.

Feni inazunguka kwa kasi, upepo wake unaniingia mpaka machoni nashindwa kutazama vizuri.

Niligeuza shingo kutazama kushoto kwangu na kisha kulia kwangu, sikumwona mtoto, mtoto alokuwa amelala kandokando yangu.

Nikatazama mlango wa bafuni pengine mtoto yumo humo ndani lakini sikuona dalili zozote kama kuna mtu humo ndani, upesi nikanyanyuka kwenda kuhakikisha.

Niliufungua mlango nikarusha macho bafu zima, mtoto hakuwepo.

Nikatoka bafuni kwenda koridoni kutazama, sikumwona mtoto. Nikaenda chumba cha wageni, mtoto hakuwepo, sasa nikawa nimebakiza chumba kimoja, chumba cha Amiri, nikawaza na kuamini mtoto atakuwa humo ndani, ametoroka chumbani akaenda kulala na Amiri.

Nilitamani kurudi chumbani mwangunkulala lakini nafsi yangu haikuridhia, nilitaka kuthibitisha kile nilichodhani kama kweli mtoto yupo mule chumbani, nikagonga mlango wa Amiri mara mbili, kimya, nikagonga mara tatu ngo-ngo-ngo, kimya, ila saa hii mlango ukafunguka kidogo, kumbe ulikuwa wazi.

Nikaita; Amiri, kisha nikauliza upo na mtoto ndani? Hamna aliyenijibu.

Kimya cha mfu.

Nikaita tena, Amiri Amiri, uko na mtoto ndani?

Kimya, hamna jibu.

Nikasukuma kidogo mlango ule ili nipate kurusha macho ndani.

Ndani kulikuwa ni kiza, kiza chepesi sababu ya dirisha lilikuwa limefunguliwa pazia likaacha mwanya wa mwanga wa mbali, mwanga kutoka nje, kupenya kwa kiasi chake mule chumbani.

Nilitazama nikamwona mtu mmja akiwa amelala kwenye godoro pale chini, ametawala godoro lote anakoroma kwa usingizi mzito, mbali na mtu huyo hamna mwingine niliyemwona hapo, chumba kilikuwa kitupu, ni begi tu la Amiri ndilo lilikuwa chini pembeni ya kabati.

Sasa mtoto yuko wapi?

Matumaini yangu yalivunjika vipandevipande, akili yangu ikacharura kwa kuchangayikiwa.

Nilitoka upesi nikaenda sebuleni pia na jikoni nikatazame kama nitamkuta mtoto huko, napo sikumwona!

Nikiwa hapo jikoni, naongea mwenyewe kutaja jina la mwanangu, nikasikia sauti ambayo mwanzoni sikutaka kuamini kama ni kweli, ilikuwa ni sauti ya geti kubwa linafunguliwa, kuchungulia dirishani namwona mtoto akiwa anamalizia kutoka akienda nje.

Nikapiga yowe kali, yowe la kumwita mtoto na kuomba msaada kisha nikafungua mlango wa jikoni mbiombio kukimbilia kule getini kumfuata mtoto.

Ajabu, pamoja na kupiga kelele kali hakuna mtu aliyetoka kunisaidia wala kupambana na mimi kumtafuta mtoto, nilikuwa peke yangu, peke yangu na ulimwengu wangu wa pekee.

Nilitoka getini nikarusha macho kumtafuta mtoto, kwa mbali, kwa mwanga mwepesi wa mbalamwezi, nikamwona mtoto akiwa anakimbia, anakimbia kuelekea maporini!

Basi nami nikaanza kurusha miguu yangu kwa kasi, kasi kubwa, nikimkimbilia mwanangu, wakati huo namuita kwa sauti yote, naita nikimwambia aningoje, naita nikimwambia asimame, asiende huko.

Taratibu nikaanza kupoteza sauti yangu, najitahidi kuongea lakini sauti haitoki, koo limekabwa kwanguvu, punde kidogo nikawa sipambani tena kutoa sauti bali napambana kuhema.

Sipati pumzi.

Simezi mate.

Nikasikia sauti ya kiume ikinambia;

"Utanambia mwanangu yuko wapi, Mage. Utanambia umempeleka wapi mtoto wangu, hayawani mkubwa wewe. Sema!"

Haukunichukua sekunde kujua sauti hiyo ni ya bwana Mgaya.

Na haikunichukua muda kubaini bwana huyo alikuwa amenikaba na mikono yake mipana juu ya kitanda, natapatapa kunusuru pumzi ya mwili wangu.

Mgaya aliendelea kusema akiwa ananiniga shingo, anamtaka mwanae, anamtaka mwanae, hapo mimi sijui chochote kilichotokea, sijui chochote kinachoendelea zaidi ya njozi ile ya maajabu.

Nipo kwenye taharuki ya kile nilichoona ingali sijui uhalisia wake, na nipo kwenye tafarani ya kujiokoa, bwana Mgaya hakuwa na masikhara hata tone, kweli kabisa alikuwa amelenga kunimalizia mule chumbani.

***
 
Numbisa Gily Antonnia Dejane Luv Depal Kalpana Angel Nylon Joannah Watu8
 
Noma Sana
 
Ngoja nimtag mtoto mzuri Antonnia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom