Niliyetaka kumuoa kanidanganya kuwa mama yake amelazwa ICU nitume hela ya mchango

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
22,345
Reaction score
56,148
Kupata mke kazi ndugu zanguni.
Nilipanga kumsogeza huyu binti niishi nae sababu ji msafi,anajua kupika ,anajua mapenzi na ni mzuri sana,huwa namuachia nyumba hajawahi kuniibia wala kudokoa hata senti moja.

Juzi kajichanganya eti mama yake mgonjwa amelazwa ICU unatakiwa mchango 50,000 kila mtoto.
Hakujua kuwa mimi ujanja wa kizamani nilishaupitia,nikapambana mpaka nikafika kwao maana awali sikuwa napajua wala sina namba yandugu yake wa karibu.

Namkuta mama wa watu yuko anafagia uwanja.binti kuniona kakimbia mpaka naondoka hajarudi
 
Umesema mazuri yake mengi lakini hilo baya moja linataka kufanya umuache, au ndo zile kutenda mema 9 yasitoshe kuwa Yesu ila baya moja lifanye uitwe shetani?! Unaweza kukuta alikua na shida na wewe ni bahili (hili hata sio mjadala mana umeombwa 50K hadi umeenda kupafahamu ukweni), akakosa namna nyingine ya kufanya.
 
Maana yake ni kwamba wewe humpi huyo binti hela za matumizi. Wewe ni bahili sana ndio maana binti aliamua hata adanganye ili umpe pesa.

Usivyo na akili na ubahili wako bado ukakomaa hadi ukapajua kwao ili mradi uhakikishe ili usitoe 50k.

Kaka mpe huyo mtoto hela ya matumizi. Kama umempenda basi mhudumie, acha ubahili.

Elfu 50 tu unatafta kwao binti hadi upajue, akiomba laki 5 si itakua balaa, utatafta hadi makaburi ya babu zake.
 
na wewe unaendaje ukweni bila kuwasiliana na mhusika unaenda kwa kushitukiza kwani kwako hapo ,umeombwa hela tuma hela hujaombwa pole kama hela haipo mpe neno la faraja basi,ukihisi unataka kupigwa tukio kwepa kiaina sio lazima umwonyeshe kuwa umejua upigaji wake.
 
Maana yake ni kwamba wewe humpi huyo binti hela za matumizi. Wewe ni bahili sana ndio maana binti aliamua hata adanganye ili umpe pesa.

Usivyo na akili na ubahili wako bado ukakomaa hadi ukapajua kwao ili mradi uhakikishe ili usitoe 50k.

Kaka mpe huyo mtoto hela ya matumizi. Kama umempenda basi mhudumie, acha ubahili.

Elfu 50 tu unatafta kwao binti hadi upajue, akiomba laki 5 si itakua balaa, utatafta hadi makaburi ya babu zake.
Ni ushamba kudanganya mkuu, hata mimi hiyo tabia huwa siipendi kabisa.

Kheri unambie unaomba tu hela hata kama unaenda fanya kitu cha kijinga ila sio kudanganya kiivo .
 
Huyo binti kaamua atumie njia ya uongo ili apate pesa. Maana yake ni kwamba jamaa hampi hela, hakuna maelezo mengine zaidi ya hayo.

Inaonekana akiomba jamaa anapiga kona kona na sababu kibao. Binti akaona bora adanganye ili apate pesa, bado jamaa akaamua kukomaa hadi kupajua kwao na kwenda kumuona mama mkwe bila mualiko bila utambulisho.

Yaani mshikaji kaombwa 50k kaenda kujitambulisha mwenyewe bila washenga, angeombwa milioni sijui ingekuaje.

Halafu uongo sio tabia, ni maamuzi, wanaume hua tunadanganya sana wanawake ili tuwapate, haina maana kwamba ni tabia zetu, ni maamuzi unaamua kutumia njia ya uingo pale unapoona kuna ka kikwazo ukidanganya utafaulu, ukifauku basi na uongo unaishia hapo.
 
Uzuri wa mwanamke sio urembo ni tabia!! hapakuwa na sababu yoyote ya kukudanganya, angekuambia tu ana shida na 50K lakini sio kusema uongo...ogopa sana mwanamke mwongo!! kukiweka ndani huyo kuna siku utapigwa tukio hutaamini....
 
Mkuu mbona chai ya mapema sana......anyway, pima mazuri yake na mabaya yake unaona mzani unaelemea wapi, ila mi nakushauri muoe huyo binti hayo mengine ni mambo madogo madogo tu ya kurekebisha na atakuwa muoga hawezi kukudanganya tena
Chai ya wapi,imeniuma sana kunidanganya
 
Uzuri wa mwanamke sio urembo ni tabia!! hapakuwa na sababu yoyote ya kukudanganya, angekuambia tu ana shida na 50K lakini sio kusema uongo...ogopa sana mwanamke mwongo!! kukiweka ndani huyo kuna siku utapigwa tukio hutaamini....
Muongo na mdokozi hao ukiwekandani utalia tu siku
 
Huyo binti kaamua atumie njia ya uongo ili apate pesa. Maana yake ni kwamba jamaa hampi hela, hakuna maelezo mengine zaidi ya hayo.

Inaonekana akiomba jamaa anapiga kona kona na sababu kibao. Binti akaona bora adanganye ili apate pesa, bado jamaa akaamua kukomaa hadi kupajua kwao na kwenda kumuona mama mkwe bila mualiko bila utambulisho.

Yaani mshikaji kaombwa 50k kaenda kujitambulisha mwenyewe bila washenga, angeombwa milioni sijui ingekuaje.

Halafu uongo sio tabia, ni maamuzi, wanaume hua tunadanganya sana wanawake ili tuwapate, haina maana kwamba ni tabia zetu, ni maamuzi unaamua kutumia njia ya uingo pale unapoona kuna ka kikwazo ukidanganya utafaulu, ukifauku basi na uongo unaishia hapo.
Dah
 
Uzuri wa mwanamke sio urembo ni tabia!! hapakuwa na sababu yoyote ya kukudanganya, angekuambia tu ana shida na 50K lakini sio kusema uongo...ogopa sana mwanamke mwongo!! kukiweka ndani huyo kuna siku utapigwa tukio hutaamini....
Uongo sio tabia. Uongo ni maamuzi. Kila mtu kwenye maisha amedanganya kwa namna moja ama nyingine.

Uongo hutumika tu pale ambapo ukisema ukweli hilo jambo halitafanikiwa. Uongo hua ni last resort ya mtu, ni mbinu ya mwisho kutumika kufanikiwa jambo.

Wanasiasa ni waongo Dunia nzima daily na bado wanachaguliwa.

Binti angeomba 50k ya kwena kusuka jamaa angesema si ukanyoe tu, ukinyoa unapendeza, mimi napenda watu wa shoet hair ili mradi asitoe 50k. Ama binti angesema naomba 50k ninunue kitu nimekipenda, jamaa bado angetaka details za hicho kitu na kutoa counter response.
 
Back
Top Bottom