Niliyetaka kumuoa kanidanganya kuwa mama yake amelazwa ICU nitume hela ya mchango

Niliyetaka kumuoa kanidanganya kuwa mama yake amelazwa ICU nitume hela ya mchango

Hata kama jamaa ni bahili, kuna namna mwanamke wako akikulilia shida utamsaidia tu, tatizo ni huyo mwanamke kusema uongo!! aisee mimi nachukia sana kudanganywa
Acheni ubahili! Kama uongo hata wewe ni muongo sana tu!
 
Trust me hayo unayosema mazuri ni ya kulazimisha ila hilo moja la kukudanganya ndio uhalisia wake hiko ni kimeo,mtu anakupenda hawezi kumzushia mama yake ugonjwa ili apate pesa be careful
 
Je, kama na yeye alikuwa anaupima mzani wa mapenzi yako kwake?
"Mtu hawezi kuwa na imani na wewe ikiwa na wewe huna imani naye.".
 
Kupata mke kazi ndugu zanguni.
Nilipanga kumsogeza huyu binti niishi nae sababu ji msafi,anajua kupika ,anajua mapenzi na ni mzuri sana,huwa namuachia nyumba hajawahi kuniibia wala kudokoa hata senti moja.

Juzi kajichanganya eti mama yake mgonjwa amelazwa ICU unatakiwa mchango 50,000 kila mtoto.
Hakujua kuwa mimi ujanja wa kizamani nilishaupitia,nikapambana mpaka nikafika kwao maana awali sikuwa napajua wala sina namba yandugu yake wa karibu.

Namkuta mama wa watu yuko anafagia uwanja.binti kuniona kakimbia mpaka naondoka hajarudi
Huko kukimbia kimwili chukulia kakukimbia moyoni, mchezo umeisha.
 
Maana yake ni kwamba wewe humpi huyo binti hela za matumizi. Wewe ni bahili sana ndio maana binti aliamua hata adanganye ili umpe pesa.

Usivyo na akili na ubahili wako bado ukakomaa hadi ukapajua kwao ili mradi uhakikishe ili usitoe 50k.

Kaka mpe huyo mtoto hela ya matumizi. Kama umempenda basi mhudumie, acha ubahili.

Elfu 50 tu unatafta kwao binti hadi upajue, akiomba laki 5 si itakua balaa, utatafta hadi makaburi ya babu zake.
😁😁😁🙌mkuu una hoja usikilizwe
 
Itakuwa wewe ni bahili na huyo Binti hawezi kuombaomba.
Mara ya mwisho kumpa pesa ya matumizi yake zaidi ya laki ni lini?
Nyie ndio masipms tunaiwazungumzia kila siku utoe laki umpe mwanamke ambae hata ujamuoa, mwanmake ambae anaweza kukuacha muda wowote vp maisha yako wewe yapoje jijenge kwanz acha kuwekeza kwa mwanamke. Uzee unakuja msiseme atujawaambia
 
Back
Top Bottom