Niliyetaka kumuoa kanidanganya kuwa mama yake amelazwa ICU nitume hela ya mchango

Kupata mke kazi ndugu zanguni.
Nilipanga kumsogeza huyu binti niishi nae sababu ji msafi,anajua kupika ,anajua mapenzi na ni mzuri sana,huwa namuachia nyumba hajawahi kuniibia wala kudokoa hata senti moja.

Juzi kajichanganya eti mama yake mgonjwa amelazwa ICU unatakiwa mchango 50,000 kila mtoto.
Hakujua kuwa mimi ujanja wa kizamani nilishaupitia,nikapambana mpaka nikafika kwao maana awali sikuwa napajua wala sina namba yandugu yake wa karibu.

Namkuta mama wa watu yuko anafagia uwanja.binti kuniona kakimbia mpaka naondoka hajarudi
Sasa kama anafanya hayo yote mazuri. 50K ndiyo uone tatizo. Are you seriously kweli wewe. Acha ujinga kama nguo za ndani zimeisha au alitaka kununua pedi akatumia lugga hiyo. Try to be genteman
 
Sasa vijana mmeanza kuelewa somo. Ukimpa binti hela mpe kwa sababu umependa kumpa, sio kwa sababu amekuzidi akili, amekudanganya au amekutapeli. Safi kijana wetu wa JF
 
Maana yake ni kwamba wewe humpi huyo binti hela za matumizi. Wewe ni bahili sana ndio maana binti aliamua hata adanganye ili umpe pesa.

Usivyo na akili na ubahili wako bado ukakomaa hadi ukapajua kwao ili mradi uhakikishe ili usitoe 50k.

Kaka mpe huyo mtoto hela ya matumizi. Kama umempenda basi mhudumie, acha ubahili.

Elfu 50 tu unatafta kwao binti hadi upajue, akiomba laki 5 si itakua balaa, utatafta hadi makaburi ya babu zake.
Nyie ndio mnatuharibia wake humu ndani. Mnawaaminisha kuwa kupewa pesa ni haki yao. Mwenye haki ya kuhudumiwa ni mke tu, girlfriend mpe unapowiwa ila sio lazima. Kwa kuwadanganya kwenu, ona sasa huyu binti ndoa inaweza yeyuka kwa tamaa za vitu vidogo. Angeingia kwenye ndoa angekua na haki ya kupewa zaidi ya hivyo.
 
Sasa kama anafanya hayo yote mazuri. 50K ndiyo uone tatizo. Are you seriously kweli wewe. Acha ujinga kama nguo za ndani zimeisha au alitaka kununua pedi akatumia lugga hiyo. Try to be genteman
Brother ,uongo ni kitu kibaya,angesema tu shida yake sio kumsingizia mama wa watu ugonjwa,kesho atadanganya kitu kikubwa
 
Nyie ndio mnatuharibia wake humu ndani. Mnawaaminisha kuwa kupewa pesa ni haki yao. Mwenye haki ya kuhudumiwa ni mke tu, girlfriend mpe unapowiwa ila sio lazima. Kwa kuwadanganya kwenu, ona sasa huyu binti ndoa inaweza yeyuka kwa tamaa za vitu vidogo. Angeingia kwenye ndoa angekua na haki ya kupewa zaidi ya hivyo.
Kwa ufupi imeshayeyuka
 
😁😁😁
Tatizo sio binti mkuu, tatizo ni wewe.
Kwa sifa ulizompamba mpaka kufikia kukudanganya kweli alikamatwa na shida, kama uliweza mpaka kufukunyua kwao, basi njia nyingine za kupata pesa kutoka kwako aliona zitakwama.
 
Kwa ufupi imeshayeyuka
Unaweza kumpa second chance mkuu, au uka kaa nae mzungumze kwanini alifanya vile. Shida yao mkikaa chini kuzungumza, atatumia silaha yao ya machozi kujilizaliza akidai alikua na shida, ila ukiwa vizuri kichwani fake na real utavijua. Kwenye hizi mambo kuna muda Sir God huwa anatuonesha rangi halisi za watu tunaotaka kuingia nao kwenye ndoa, ili uamue mwenye unabeba hivyohivyo au unapiga chini. Wazoefu huwa wanadai, kilichoonekana wakati wa uchumba usijipe moyo kuwa kitaondoka wakati wa ndoa. Uchumba ndio wakati wa kumu impress mwenzio kwa tabia nzurinzuri ambazo pengine hata hauna. Ila inapotokea mauzauza kwenye uchumba, huwa sio dalili nzuri kwa ndoa.
 
😁😁😁
Tatizo sio binti mkuu, tatizo ni wewe.
Kwa sifa ulizompamba mpaka kufikia kukudanganya kweli alikamatwa na shida, kama uliweza mpaka kufukunyua kwao, basi njia nyingine za kupata pesa kutoka kwako aliona zitakwama.
Nimeumia roho sana,nilishamzoea na tuliendana sana ila uwongo huwa siupendi
 
Unaweza kumpa second chance mkuu, au uka kaa nae mzungumze kwanini alifanya vile. Shida yao mkikaa chini kuzungumza, atatumia silaha yao ya machozi kujilizaliza akidai alikua na shida, ila ukiwa vizuri kichwani fake na real utavijua. Kwenye hizi mambo kuna muda Sir God huwa anatuonesha rangi halisi za watu tunaotaka kuingia nao kwenye ndoa, ili uamue mwenye unabeba hivyohivyo au unapiga chini. Wazoefu huwa wanadai, kilichoonekana wakati wa uchumba usijipe moyo kuwa kitaondoka wakati wa ndoa. Uchumba ndio wakati wa kumu impress mwenzio kwa tabia nzurinzuri ambazo pengine hata hauna. Ila inapotokea mauzauza kwenye uchumba, huwa sio dalili nzuri kwa ndoa.
Yaani niko njia panda,nikikumbuka wiki mbiki nyuma alifanya overall cleanliness nyumba nzima siku nzima ,hakudokoa hata mia
Akanipikia ugali dagaa safi na usiku nikapewa show hatari,asubuhi nikampa helayanatumizi kama kawaida
Kumuacha ngumu,kuendelea nae pia ngumu
 
Kama sifa zingine ziko fresh, mpe onyo kali sana la kiume. Amini kwamba hata kwenye ndoa kutakua na mambo mambo ambayo hayatakufanya umuache ila yatakutaka uoneshe rangi yako halisi kama mwanaume. Ape action ambayo akilaa na shoga zake atawaambia kuwa huwa hupendi ujinga, kisha sogeza jiko
 
Nimeumia roho sana,nilishamzoea na tuliendana sana ila uwongo huwa siupendi
Msamehe, endelea na mpango wako juu yake. Hatokudanganya tena.

Nawe pia usimtengenezee mazingira magumu mpaka kufikia hatua ya kukudanganya.
 
Uzuri wa mwanamke sio urembo ni tabia!! hapakuwa na sababu yoyote ya kukudanganya, angekuambia tu ana shida na 50K lakini sio kusema uongo...ogopa sana mwanamke mwongo!! kukiweka ndani huyo kuna siku utapigwa tukio hutaamini....
Mwanamke muongo sio tu atakusaliti bali na unaweka rehani mambo yako mengi kwa kumuamini.
 
Back
Top Bottom