Oh sorry sana.Mimi ni ke bwana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Oh sorry sana.Mimi ni ke bwana
Tunazipata hapa hapa mjini.Watu wengine mnapata wap Hela jamani million 150 za kujenga aiseee
Dah aisee kweli mji una wenyeweTunazipata hapa hapa mjini.
Msingi wa nyumba ndio kila kitu au ukipaua ndio ujenzi unaanza ?Binafsi naamini sana kuwa na sehemu yako ya kuishi bila bugudha ya kodi wala maudhi ya wapangaji wengine,
Mambo machacho kuhusu mimi
1. Niko under 30
2. Kipato changu ni kati ya 500k - 550 k kwa mwezi
Baada ya kununua kiwanja، nilianza kununua maatofali kidogo kidogo.
Mambo niliojifunza
1. Anza kujenga na ulicho nacho, kwenye fungu ndio kwenye nyongeza, ukishaweka tofali kama kweli unania ya kugenga kichwa kitapata moto, Mungu atakufungulia
2. Msingi wa nyumba ndio kila kitu, nilipoanza kujenga nilikua na bajeti ndogo, ujenzi ulikuaa wa kimasikini kweli, matokeo yake, sasa nyumba imeisha ila msingi uko chini na kuna vitu ningetamani vingekuepo ila ndo nyumba ishamalizika, hili silijutii kwani ni funzo, hata hapa nilipofika sikutegemea kufika.
3. Hata kama fundi unamuamin, ni muhimu sana kuwepo wakati wa ujenzi, kuna makosa mengi ambayo yanaweza kutokea, kusimamia ujenzi sio kwa kuzuia uizi tu bali hapa usahihi wa nyumba unavyotaka iwe. Nyakati muhimu za kuwepo ni wakati wa kuset msingi wa nyumba, wakati wa kufunga mkanda wa nyumba, ukataji wa madirisha na milango, na kufunga lenta makosa mengi yanatokea hapa
4. Ujenzi hauna gharama kamili, kama ulipiga bajeti ya milioni 30, hakikiaha una milioni tano ya extra. Mengi yanatokea, ikiwemo vitu kupanda bei
5. Kuna muda utakua unajua kua fundi amekula hela ila hakuna jinsi, ikiwa hujui vifaa vya plumbing au umeme, chukua bei ya fundi, nenda madukani kaulizie, ukipata tofauti isio kubwa na ukiwa na uhakika wa kuletewa kitu original ambacho wewe unahofu ya kuuziwa fake , basi mpe tu fundi hela ( kwa wasio na uzoefu)
6. Siku unayomaliza kupaua ndio ujenzi unaanza, kati ya vitu ambayo ni kuhimu katika nyumba na vina gharama kubwa ni kama mfumo wa maji, umeme, milango ya mbao na grill, hivi vitu usivichukulie kirahisi kwenye budget, gharama zake hua ni M M tu.
7. Unapotaka jugenga aim for high, nilikua nimeingia mtego wa kutaka kujenga chumba kimoja na sebure, ila nilipoamua kujenga nyumba ya vyumba vitatu niliona kabisa kama ni kitu ambaacho hakiwezekani ila hatimae imewezekana, lesson-- panga kwa kuangalia wewe unakua au unataka kua nani nani na si sasa hivi una hali gani .
Plan besed on who you want to be not who you are, by this utaepuka regret za kujenga kitu ambacho baadaae hukifurahii sana
Gharama kubwa inaanzia kupaua. Yangu ilinikula 15m kupaua tu. Aluminium 6 m, milango ya mbao complete 840k kila mmoja, milango ya kisasa ya chuma 2,200,000 wa mbele na nyuma. Tiles 20m za India, hizi ni pamoja na za skirting nje. Umeme, maji etc ni shida. Bado grills za madirisha, fundi tiles, fensi etc. Nyumba ya kisasa ni gharama sana. Ila Mungu ni mwema niko kwangu
Ndio,inatagemea unanunua za wapi na aina ganiTiles expensive kuliko kupaua/kuezeka?
Natamani ningefanya hivyo ila nilishajibu hapo nyuma, kuna watu wakiiona nyumba watagundua ID yangu, kifupi ni nyumba ya vyumba vitatu, kimoja masta, sitting room imeunganika na dinning room, public toilet na jiko, nyumba ina urefu wa mita 9 na upana wa mita 11
Chemba 25k kila moja na mifuniko yakeChemba walijenga kila moja 40,000, zilikua 8, nimepigwa ?
Huyu mbona kama mimi🤣🤣Grill Mlango wa mbele na nyuma,kwa wakati husika Mlango utakua maPazia
kuna boya mmoja napga nalo story kila siku lishamaliza kupaua,lishatia grill madrisha yote
ila linalalamika kila siku halina hela linatafuta hela ndio lihamie kwake, mi imefika wakati namwambia
mwanangu usiniletee mastory yako ya huna hela,shida unazitaka mwenyewe,lipo tunaendelea nalo umia
kwenye ma kodi yale unampa mwenye nyumba hela huku roho inakuuma,una nena kwa lugha zote kimoyo moyo,ila halikomi wala halijifunzi.
1. Msingi ndio kila kitu katika kutengeneza shape ya nyumba, kuanzia muonekano wa nje na structure ya ndani, urefu wa msingi na style ya kutenganisha msingi na boma.Msingi wa nyumba ndio kila kitu au ukipaua ndio ujenzi unaanza ?
Chagua moja.
Kwa hiyo msingi, kuta na paa ujenzi unakuwa haujaanza.1. Msingi ndio kila kitu katika kutengeneza shape ya nyumba, kuanzia muonekano wa nje na structure ya ndani, urefu wa msingi na style ya kutenganisha msingi na boma.
2. Ukimaliza kupaua ndo ujenzi umeanza nikimasnisha vitu vingi vingi in term ya gharama like grill, blundering, plasta, frame na top za milango, rough floor na tiles, wiring, plumbing, alminium window kama unahitaji na gypsum. Hapo ukipiga hesabu ya hivyo vitu utaelewa
nilichosema
so kauli hizo mbili zinajitegemea na huhitaji kuchagua kati ya moja
Mm mwenyewe nimeanza kujenga mwenz uliopita mdogo mdogo ntafika nakipato changu nikidogo tu. Ila dar chamoto nakionaBinafsi naamini sana kuwa na sehemu yako ya kuishi bila bugudha ya kodi wala maudhi ya wapangaji wengine.
Mambo machacho kuhusu mimi
1. Niko under 30
2. Kipato changu ni kati ya 500k - 550 k kwa mwezi
Baada ya kununua kiwanja، nilianza kununua maatofali kidogo kidogo.
Mambo niliojifunza
1. Anza kujenga na ulicho nacho, kwenye fungu ndio kwenye nyongeza, ukishaweka tofali kama kweli unania ya kugenga kichwa kitapata moto, Mungu atakufungulia
2. Msingi wa nyumba ndio kila kitu, nilipoanza kujenga nilikua na bajeti ndogo, ujenzi ulikuaa wa kimasikini kweli, matokeo yake, sasa nyumba imeisha ila msingi uko chini na kuna vitu ningetamani vingekuepo ila ndo nyumba ishamalizika, hili silijutii kwani ni funzo, hata hapa nilipofika sikutegemea kufika.
3. Hata kama fundi unamuamin, ni muhimu sana kuwepo wakati wa ujenzi, kuna makosa mengi ambayo yanaweza kutokea, kusimamia ujenzi sio kwa kuzuia uizi tu bali hapa usahihi wa nyumba unavyotaka iwe. Nyakati muhimu za kuwepo ni wakati wa kuset msingi wa nyumba, wakati wa kufunga mkanda wa nyumba, ukataji wa madirisha na milango, na kufunga lenta makosa mengi yanatokea hapa
4. Ujenzi hauna gharama kamili, kama ulipiga bajeti ya milioni 30, hakikiaha una milioni tano ya extra. Mengi yanatokea, ikiwemo vitu kupanda bei
5. Kuna muda utakua unajua kua fundi amekula hela ila hakuna jinsi, ikiwa hujui vifaa vya plumbing au umeme, chukua bei ya fundi, nenda madukani kaulizie, ukipata tofauti isio kubwa na ukiwa na uhakika wa kuletewa kitu original ambacho wewe unahofu ya kuuziwa fake , basi mpe tu fundi hela ( kwa wasio na uzoefu)
6. Siku unayomaliza kupaua ndio ujenzi unaanza, kati ya vitu ambayo ni kuhimu katika nyumba na vina gharama kubwa ni kama mfumo wa maji, umeme, milango ya mbao na grill, hivi vitu usivichukulie kirahisi kwenye budget, gharama zake hua ni M M tu.
7. Unapotaka jugenga aim for high, nilikua nimeingia mtego wa kutaka kujenga chumba kimoja na sebure, ila nilipoamua kujenga nyumba ya vyumba vitatu niliona kabisa kama ni kitu ambaacho hakiwezekani ila hatimae imewezekana, lesson- panga kwa kuangalia wewe unakua au unataka kua nani nani na si sasa hivi una hali gani.
Plan besed on who you want to be not who you are, by this utaepuka regret za kujenga kitu ambacho baadaae hukifurahii sana.
Ulinunua wapi hiyo milango ya laki Tatu tunaomba namba pleaseDuh milango ya chuma mbele na nyuma tu M ngapi? Duh tunaomba utupe picha ya hio milango wakati mi hio milango wa mbele na nyuma ya chuma nilitumia laki 3 yote kweli ujenzi tunatofautiana kutoa ela si mchezo.
tufundishe basi na sie namna ya kuzipata jamani mbona mnakuwa wachoyoTunazipata hapa hapa mjini.
Hee , ni kwenye hizihizi ajira za mjini .tufundishe basi na sie namna ya kuzipata jamani mbona mnakuwa wachoyo