Ni sahihi.
1-IT wazee, unakuta hadi leo wanakomaa na PHP pamoja na jquery , aina hizi za site ni miaka ya 2008, bado wanapambana na headful frameworks.
Wakati hivi sasa kuna tech za kisasa, kuna react na framework kama nextjs ambayo ipo kasi sana, kuna vuejs, flutter , angular n.k hizo ni frameworks za kukata na shoka kwenye perfomance na muonekano, single page web app, sasa unakuta mtu bado anakomaa na PHP anatengeneza page kama 100 kwa html.
Kuna backend kama nodejs na framework yake kama expressjs ipo faster sana unaweka hosting aws huko kuna server zinaji extend specs tokana na wingi wa watumiaji, sasa hawa unakuta wameweka computer ya kawaida na windows server OS ndio server hio, ina RAM ndogo kulinganisha na watumiaji na pia port speed ni ndogo hali ya kuwa kwa kazi kama hii unahitaji port inakwenda atleast 1Gbps, cha ajabu website nyingi za gov wanatumia windows server ambayo ni nzito kwa sababu ina GUI, inapaswa watumie Linux CentOS au distributions nyingine nyingi za linux ambazo ni nyepesi na zina kasi pia ni open source na hapo kinachowashinda IT wengi kwamba Linux inatumia sana command line na hazina UI wakati windows server ina User Interface.
Google cloud, aws na azure kuna servers zinajipanua kiuwezo tokana na requests za watumiaji, hawa server zao zinazidiwa uwezo.
Kingine scripts wanazoandika error nyingi, unakuta code ambayo ingeandikwa kwa few lines of code mtu kaandika kitabu, hio ni shida kwenye perfomance hao IT wengi ni wabovu kwenye data structure and algorithms. Hovyoo kabisa.
Hio site ningeweza kuitengeneza kuanzia asubuhi hadi jua linazama namaliza kuanzia UI hadi backend, online kuna scripts nyingi tu za ku copy na customize kidogo kwa IT nondo.