Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Nakubaliana na wewe 100% lakini tatizo linakuja pale ambapo Jamii hii hii hatushikamani linapokuja suala la Uvunjifu wa sheria na kuwafanya raia wema kukosa amani.e.g. Hao panya rodi walipovuma sana kwa uhalifu huo watu hatukusimama wote dhidi yao ila lawama na kejeli nyingi sana zilielekezwa kwa Serikali na hususan polisi.
Huwezi amini kuwa vijana(Panya rodi) wanafanya msako hata kuweka vizuizi katika mtaa wenye watu wengi(na pengine watu katika mtaa huo wanazo silaha e.g. zile wanazoenda nazo baa kutishia walevi wenzao Lakini hakuna anayetoka au uongozi wa mtaa kufanya mobilisation ya kuwadhibiti hao panya rodi. Kwa hiyo polisi wachache waliopo eti wao ndo watoke wakapambane na hao panya rodi. Kumbuka hoja ya mahakamani ni nzuri sana lakini inachukua muda na pengine itawaweka baadhi ya watu hatarini kwani mtu apatikane na hatia ni lazima kuwepo na kithibiti, mtuhumia huwa na haki ya dhamana na yote hayo huchukua muda mrefu. Mara nyingi, na uzoefu unaonesha watuhumiwa wa wizi, kama hakuna kithibiti hushinda kesi na kuachiwa huru. Je, itakuwaje usalama wa wale walioshiriki kutoa ushahidi mahakamani? Tukumbuke Polisi nao ni watu kama mm na ww. Wanachoka na hawapendi kwenda kudhalilika mahakamani pale kesi inapotupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi. LAKINI ukweli unajulikana kabisa kwamba fulani ni Jambazi,ni panya rodi etc.Mbona tunaishi nao humuhumu mitaani? Sasa polisi wanasaidia kutupunguzia hao wahalifu tunaowalinda/tunaowahifadhi/ tunaowaonea haya/tunaowaogopa na kukaa kimya. Vijana tuwazae halafu wageuke kuwa Nunda kwetu? Ndio maana nikasema Kimya kiendelee wakati ambapo ni zamu ya serikali kuwashughulikia panya rodi the same kama tulivyokaa kimya wakati panya rodi wanafunga mitaa na kuwajeruhi watu, kupora mali, kubaka n.k. Si tunawasetiri ni ndugu zetu?? Basi kwa Polisi hao sio ndugu hata kidogo. Zingatia hili: Kwa Mwanajeshi yeyote huwa unatekeleza amri kwanza maswali ni baadaye. Panya rodi nao walikuja na kanuni/maswali yanayofanania kama hivyo eti unaulizwa (tena ujibu haraka) unataka bokoboko au pilau? Ukichelewa kujibu wanakutolea jibu chap wao wenyewe. We acha tu, panyarodi sitaki hata kuwasikia aisee.
 
mbona wanajulikana sana tu. kuna watu wanajuliakana kwa majina ni madalali wa vitu vya wizi kama simu, tv nk endapo tukio limefanyika mali ikaibiwa baada ya muda ikaonekana mahali. atakamatwa mtumiaji au mnunuzi akiulizwa atamwonyesha dalali aliyemuuzia nae atakamatwa. kwahiyo haya majina yapo huko vituoni. nashangaa sana mtu anapokuja kudai eti polisi wanaaua raia wa kawaida sio wahalifu.
 
Ndio maana inatakiwa mshukiwa apelekwe mahakamani ukweli wa kosa udhibitike, na adhabu stahiki itolewe. Sio sahihi kuruhusu polisi wasio na weledi kuua watu wanaowatuhumu.
Panya Road ni ngumu sana kupata ushahidi ingawa huko mitaani wanafahamika! Kama unaishi mtaani na kujihusisha na mambo ya kijamii utafahamu viongozi wa serikali za mitaa wanajua kila nyumba na uhalifu wake ingawa ushahidi ni mgumu sababu lazima umkamate mtu na kidhibiti.

Siungi mkono mtu kuuawa bila ushahidi wa kutosha lakini wakati mwingine "nawaelewa" polisi. Siku ukipigwa tukio na hao vijana nakuapia utawaelewa polisi! Siku wakuvamie na familia yako ndio utajua walivyo wanyama kama utabakia hai.

Kuna eneo nimeishi, mnaishi jirani na mtu ni bingwa wa kuchora ramani na kutuma vijana kutoka mbali kuja kuvamia! Tulipata shida kubwa kupata ushahidi ingawa wakazi wote tulishajua kinachoendelea! Mara kadhaa kila ulipotokea wizi tulihakikisha amekamatwa kwa mahojiano lakini ushahidi haukupatikana na polisi walisema hawawezi kutumia nguvu sababu ya wamezuiwa "kubinya" watuhumiwa.

Huyo mtu ilitulazimu wakazi tumfungie "kazi" wenyewe na baada ya hapo aliondoka na mkewe eneo letu tukarudisha amani mtaani. Kudeal na wahalifu kwenye hizi nchi zetu za kimaskini ni mtihani mkubwa sababu ya mapungufu ya kisheria, uwezo wa kiuchunguzi, tamaduni n.k
 
Niliowataja hawana kinga yoyote, benchmark ya kesi itasimama kwa kurejea kesi ya Lengai Ole Sabaya ambaye anasulubiwa leo kwa kutumwa na viongozi wakubwa wenye kinga ya kushitakiwa. Kwa hiyo usijipe moyo eti kwa ajili ya kulinda usalama, mnatengeza magaidi bila kujitambua.
 
Jeshi la wananchi wanafundishwa kulenga kichwani tu ndio, lakini polisi wanafundishwa kulenga miguuni ili wamkamate mtuhumiwa na kumpeleka kwenye chombo cha kutoa haki sio kuua.

Tambua Jeshi la wananchi na Polisi ni vitu viwili tofauti. Kama kuna tatizo Jeshi la wananchi hawana majadiliano lakini wana nafasi hiyo kufanikisha upatikanaji wa kiini cha tatizo baada ya kupeleleza.

Polisi walioua, aliyewatuma na kuagiza operesheni hiyo atashitakiwa tu, Kesi rejea ni Lengao Ole Sabaya hii itakuja kuwasumbua sana mpaka kuna baadhi watakimbia nchi
 
Uko sahihi sana, kama kweli wanachokifanya polisi cha kuua wezi ni sahihi, kuna mtu alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta hapo nyumbani kwake. Mbona mtu huyu hatujasikia kapigwa risasi maana yeye kaiba kikubwa kuliko panya road?

Shida ya panya road ni body attack wanazofanya kumpiga mtu mapanga kumchoma na bisibisi pia marungu ndo maana tunaona ni sahihi ata wao kuuliwa ivo, kama wangekua wanatapeli tuu kijanja janja bila kukaba basi wangeuliwa ata mimi ningekataa ila nimeshidua mtu alie dhurika na hao na ghalama familia yake ilizotumia kumtibisha asee hata kwa risasi naona kama wanawadekesha ilitakiwa wakatwekatwe vipande wazima alafu wawe wanaeushia ngurue na fisi.
 
Mkorinto , Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi
sheria na mahakama ni kielelezo cha ustaarabu lakini sio omega ya kutoa haki. mfano kwa sasa adhabu ya kunyongwa haitekelezwi!!unadhani mhukumiwa anakuwa katendewa haki na mahakama kwa kosa atakaloshitakiwa nalo???kumbe haki ya hapa mahakamani ni mtambuka.
, ndio maana kuna Mahakama ,ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,
makosa mengi yametafsiriwa kisheria na adhabu zake,lakini upande wa uhalifu na ugaidi sheria zinaonekana kupitwa na wakati hasa ukizngatia uhalifu ni mpya kila leo.
changamoto inabaki kwa mtendaji wa mwisho(polisi)anayetarajiwa atoe huduma ya usalama lakini pia atende haki kwa wote mhanga na mtuhumiwa.mahakama wanasoma kipi kimeandikwa wapi tukioanisha na kilichopo mbele yetu.
kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa.
nguvu ingeongezwa hapo,lakini ni upuuzi kusema polisi waache kudeal vyema na watu amabo wanasababishia wengine madhara vifo na hasara.
sheria inasema mtu mpaka akutwe na hatia inayeoweza kumweka matatani ni pale itakapothibitika bila shaka kwamba yeye kwa kushiriki au kusaidia kutenda kosa fulani kwa vielelezo,embu nieleze kwa aina ya uhali panyaroad wanavyofanya ni lini utakuja kumkuta na hatia???
Kama tunaona hakuna haja ya kuchunguza na kushtaki Polisi washinikize sheria zibadilishwe ili iwe rahisi wao kufanya wanachokifanya , hakuna mtu anatetea wanalifu
sheria ndizo zitabadilika,lakini wahalifu na uhalifu na polisi watabaki vile vile,point yako na maandishi tu kitabuni yafuatwe!!!unahisi wanaonewa sababu sheria tu haisemi hivyo!!!
,ninachotaka utaratibu ufuatwe ktk kupambana na uhalifu na kama sheria zetu ni Butu basi tuzibadili na sio Polisi kuchukua hatua ya kuuwa Watuhumiwa bila kuwapeleka mahakamani.
mahakamani hapelekwi mtu kama anakwenda kuchukua mgao wa shati kaka,ni zoezi refu.sheria wacha zibaki hivyo maana hata uwezo wa kuhudumia wafungwa hatuna.
 
Kama sheria imeshindwa kumaliza panya road acha njia zilizo nje ya sheria zijaribiwe.Siwapendi polisi lakini ninawachukia zaidi hao watoto wasela mavi.Wao wanaumiza,wanaiba na wanaua kirahisi tuu..kisela mavi tuu.Hapana,wauawe tuu.Tena operation iendelee hata miezi sita,vibaka wote polisi wamalizane nao kihunihuni hivyohivyo....Muhimu ni kuwa wahakikishe ni watu sahihi,na nina uhakika polisi wanawajua na hadi kupewa kibali cha kuwamaliza ni lazima wanajiridhisha kwa kiasi kikubwa..Hatuwezi kuishi kwa kuhofia masela mavi tuu eti...wapigwe risasi wote.Pumbavu sana
 

Duuu, mkuu Kwahiyo vita ya Burundi ilisababishwa na panya road wa huko? Mkuu hao watu wanaobaka, kuvuta bangi nk ni wa taasisi gani ya kimamlaka ili tuseme hawafanyi sawa?
 
Mbuta , ninachokifanya Nina tetea sheria zetu ,katiba na kanuni .

Niliyoyasema yote ni matakwa ya Sheria zetu ,kama sheria zetu hazifai basi tuzibadili.
Amini bro. Hizo sheria unazotetea zilishafeli kitambo. Na wakiachwa matukio yakaendelea utakuja tens kuwalaumu polisi wameshindwa kazi.. Kuna mdau kakushauri upite kuhoji wananchi wanaowafahamu vizuri hao marehemu tabia na shughuli zao zilikuwa vp. Huenda hata baada ya kujua maisha yao usingekuja post huu Uzi. Kutumia ushahidi wa risiti na duka alilonunua TV haitoshi. Uliza pesa ya kununua TV aliipataje. Utachoka. Acha wauwawe tu kwasababu nao waliua
 
Ndio maana inatakiwa mshukiwa apelekwe mahakamani ukweli wa kosa udhibitike, na adhabu stahiki itolewe. Sio sahihi kuruhusu polisi wasio na weledi kuua watu wanaowatuhumu.
Mpaka kufikia kuuwawa inamaana ukweli wa makosa yao tayari umeshathibitika. Mbona hawajakuuwa wewe, mimi au huyo Nondo?
Wewe unafikiri polisi hawana informs za kutosha juu ya hao wauaji? Unafikiri polisi walipita nyumba ngapi mpaka kufikia nyumba za hao waliowauwa?
Kama ingekuwa ni kuuwa tu basi si wangeanza na nyumba zingine kabla ya kufikia hizo za hao vijana waliofatwa kwao na kwenda kuuwawa?

Tatizo lenu wengi wenu mmekuwa mkiingiza siasa uchwara katika mambo ya msingi. Nina imani kama yule binti alieuwawa bila hatia kule kawe angekuwa ni dada yako wala usingekuja kuandika haya uliyoandika.
Kama Nondo na nyie mnaomuunga mkono mnategemea kupata kura kupitia sakata hili la mauaji ya panya road, basi mjue mmeshindwa mapema kabla hata ya kuanza.

Hakuna mwanasiasa uchwara atakaepigiwa kura kwa sababu ya kuwatetea panya road dhidi ya polisi.

Hawa panya road kabla ya kuanza kuuwawa walikuwa washakamtwa si zaidi ya mara 1 na kuhukumiwa, lkn kila wanapotoka baada ya hukumu huendelea na matendo yao ya kinyama dhidi ya raia wema wasiokuwa na hatia yeyote na matokeo yake wanasababisha mauaji, ulemavu, hasara nk.
 

Unachofanya hapa ni kuhalalisha utetezi wako dhidi ya mauaji ya polisi dhidi ya watuhumiwa. Hilo neno siasa ww na wengine mnalitumia ili kuondoa uhalali wa tunaotaka sheria ifuatwe. Polisi wetu wangekuwa na weledi nisingepata shaka juu ya mauaji ya hao washukiwa wa uhalifu. Kwa maneno marahisi siku hizi mtu akitaka sheria ifuatwe ili kutekeleza jambo fulani, basi hiyo ni siasa?
 
Sisapoti kwa hicho kilichotokea lakini vijana tujaribu kuishi maisha mbali ya kufanya au kujishughulisha na mambo ya kihalifu, mie mwaka jana mwezi wa 8 nilifatwa na polis nyumbani kwangu kwa kutumia simu ya wizi na walikuja na difenda na silaha juu,

Lakini sikufungwa pingu na wala sikupanda difenda yao bali niliwasha gari yangu na tukaongozana mpaka kituoni ambako ndani ya nusu saa tu alikuja,mjumbe,mwenyekiti,na diwani wa ilala kuthibitisha kuwa siyo mhalifu na the way nilivyokamatwa tu sikuguswa hata shati na askari wenyewe wakawa wanakataa kuwa siwez kuwa mhalifu.

Niliandika maelezo na aliyeibiwa mwwnyewe alishangaa na kukataa kata kata kuwa siyo mimi niliyemuibia simu hyo iliyokuwa na thamani ya 1m+,

hapo ukifatilia kwa makini huenda wakawa ni kweli ni panya road au siyo au wanajihusisha na uhalifu na mda mwengine unaweza kuwa syo mfanya uhalifu lakini unavyojiweka katika jamii watu wanakuchukulia kama mhuni,hasa kimavazi,maneno yako,na hata matendo yako unaweza kuwa si mhalifu lakini ni mvutaji bange au muuza bange mkubwa mtaani.

Na usilofahamu ni kwamba hao oye waliouliwa wana record za uhalifu polisi na mpka kuja hapo kukamatwa jua kuwa kuna wajumbe,mwenyekiti au askari jamii wamewapoint hao watu
 
Nondo you're more than this bro.

Please respect yourself!

Suala la Demokrasia mnalitumia vibaya ndugu zangu!

Hata hizo nchi mnazoziita za kidemokrasia kuna muda ukifika unakuwa muuaji WA raia unauawa Tu!

Ghaddafi aliuawa na Marekani mnaesema ni Baba WA Demokrasia.

Sadam Hussein alikuwa raisi Halali WA Iraq akauawa na USA.

Ninaelewa mapungufu ya Jeshi la police Ila Kwa hili kwakweli Acha panya road wauawe!


Ni Sawa na kule kigoma Kuna majambazi wanaua halafu eti wakamatwe wapelekwe mahakamani. Hapana. Ni Shaba Kwa shaba

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kinacho nisikitisha ni kuona nyie mnaojiita watetezi wa Haki za Binadamu ni kuwa tayari kuna upande wenu mmeuchagua wa kutetea na mara nyingi mmekuwa mpo upande wa wahalifu.
Imefikia hatua tumeona kuwa watetezi wa Haki za Binadamu ni watetezi wa haki za wahalifu.
Wakati hao vijana wanaojiita Panya road wakifanya uhalifu wao taarifa mlizisikia lakini hamkuonekana kutoka hadharani kukemea dhuluma dhidi ya Haki za Binadamu zinazofanywa na kundi hilo kwa Raia wasio na hatia kwa kuwapora mali zao, kuwajeruhi na hata kuwaua raia wema bila kosa lolote lile.
Ila kwasasa Serikali imeanza kuchukua hatua kikamilifu dhidi ya hao wahalifu ndiyo mnajitokeza sasa kulaani hatua zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya kukomesha vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani katika jamii..
1. Je, watu mnaojiita watetezi wa Haki za Binadamu mlitaka Taifa lisichukue hatua dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo?
2. Mnafurahia vitendo vya uvunjifu wa amani na kuzua taharuki kwenye jamii?
3. Dhumuni lenu mnataka nchi isitawalike kutokana na kukithiri vitendo vya uvunjifu wa Amani?
4. Mna ajenda gani ya siri na makundi haya ya wahalifu?
5. Kuna watu wanafadhili na kuwachagulia ni kundi lipi ndiyo mtetee haki zao?


Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Acha kumshirikisha Mungu katika matendo yenu machafu. Wakati mnapowatuma panya road wakavunje nyumba zao watu usiku waibe, wajeruhi na wengine wauwe mbona haujagi humu kuwakemea kwa wanayoyafanya? Leo hii na wao kufanyiwa yale wanayofanyia wenzao ndo umekuja haraka haraka kujifanya unaguswa na vifo vyao!

Aisee nyie mnaowatumia panya road na panya road wenu mnachekesha sana. Kifupi mkae mkijua kwamba sasa muda wenu wa kufanya machafu katika nchi yetu umekwisha.
 
Tafuta kazi ya halali ufanye kijana, ukikaa nyumban kwa kutegemea kuvamia nyumba za watu usiku uibe, ujeruhi na kuuwa basi na wewe utauwawa tu haijalishi mauaji yako yamefata sheria ua la.
 
Watetezi wa panya rodi wanataka kutufikisha huku๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
 

Attachments

wazungu wanasema"you nailed it all"kwa lugha yetu ya kibantu inamaanisha umemaliza kila kitu!sina cha kuongeza!vijana wanatakiwa wafanye kazi kwa bidii hii njia ya shot cut haisaidii!hata vitabu vyote vinasema mshahara wa dhambi ni mauti
Kweli mkuu, wakati mwingine ni lazima tuelezane ukweli ili kudhibiti tatizo mapema.
Waswahili washasema mficha maradhi kifo humuumbua. Hawa kina Nondo na genge lake tukiwaacha waendelee kuandika upuuzi wao hapa jukwaani, basi tutakuwa tunaendelea kulifuga tatizo la panya road sisi wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ