Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Mnajuaje kama ni bosi wanakikundi kamojawapo la panyaroad🥱
 
Usije jiteka Tena ili kutafuta Kiki
 
Uko sahihi sana, kama kweli wanachokifanya polisi cha kuua wezi ni sahihi, kuna mtu alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta hapo nyumbani kwake. Mbona mtu huyu hatujasikia kapigwa risasi maana yeye kaiba kikubwa kuliko panya road?

kama alitumia panga kukata bomba haina shida,hao watoto na shemeji zenu wanaotumia mapanga kukata mikono ya watu,watapelekewa hewa ya moto tu mpaka waishe.
 
Acha kuchukulia kila kitu ni siasa wewe jamaa madhila ya kukutana na hao vibaka usiombe yakakukuta , mimi 2015 maeneo ya mbagala nilisomeshwa namba na vijana wakiwa kama nane hivi walininyanganya kila kitu mpaka viatu nilivyo vaa na nilikuwa safarini naenda mtwara sitasahau hiyo kitu.
Halafu ww mwanasiasa unakuja kuleta porojo zako hapa sjui kinyume na katiba shika adabu yako wewe kijana Abdul nondo.
 
Jirani jukwaa la siasa? Huku uwa siji 😅😅
 
You and your party are hopeless. Mnaunga mkono serikali ya mauaji. So long ni wa dinibyenu hamuoni haja ya kupaA sauti kwa nguvu, unaongea kirejareja
 
Ndio maana inatakiwa mshukiwa apelekwe mahakamani ukweli wa kosa udhibitike, na adhabu stahiki itolewe. Sio sahihi kuruhusu polisi wasio na weledi kuua watu wanaowatuhumu.

kenge hasikii mpaka atoke damu masikioni,

wakiwa wanatoa matamko huwa mnahisi wanatania, utekelezaji ukianza mara weledi, mara form for feilure, mara ccm b. wakati huo mnazika panya wenu.
 
Kwa warekebishe sheria wapi ?
Samahani, Una umri gani.
Zamani ilikuwa ngumu mhalifu au gaidi au mhamiaji haramu kuwepo nchini, lazima ajulikane mapema sana.

Zamani ilikuwa mtu yeyote anaweza kuukemea uhalifu mahali popote na ukasita,..
Raia na vvyombo vya usalama vilishiriki pamoja kama jamii tofauti na sasa kila kimoja vikwake.

Sasa hivi polisi pana kizuizi ukitaka kuingia unajua nini kimetokea.Polisi wanaogopa? au.

Kuna mahali tumeyumba ki maadili kama raia na kimaadili kama askari.
 
PANYA ROAD HAWATOKI SHIMONI, HAWATOKI NCHI JIRANI.
Ni jamii tuliyonayo iliyokosa malezi, maadili, elimu na kujitambua, huwezi kurekebisha aina flani ya watu kwa kuwaua.
Panya road ni kama mbu, kuwamaliza mbu ni kuanza na mazalia ya mbu na sio kujipiga makofi mbu amapokuuma !!
 
Sawa tumeshajua wewe ndiye sponsoro wao kumbe basi tulia zamu yako itafika..Kwa cv yako ya huko nyuma kuhusika kufanya matukio ya vuruguvurugu kipindi unasoma no wonder siku tukiambiwa na wewe ni moja ya wahusika wa Panya road binafsi mimi sitashangaa..

Umeongea mengi na yenye facts ndani yake na umeweka marejeo ya vifungu vya sheria lakini its too late mdogo wangu maana njia sahihi ya kudili na mtu mshenzi ni kuwa mshenzi zaidi yake hata nchi zenye sheria kali za dini huwa zinachukua maamuzi magumu kwa ajili ya watu wapuuzi yaani ukiua kwa upanga na wewe unakufa kwa upanga..

Hao vijana unaowatetea hapa wengi wao wamekaa jela sana lakini wametoka wakaendeleza yaleyale yaliyowapeleka jela so unadhani ipi ni njia sahihi ya kudeal nao!? Chuma tu hakuna mbadala hatuwezi kubembeleza watu washenzi kwa kuwawekea soseji na karimati na kuwaomba waache uhalifu kama ndugu yangu Extrovert alivyosema...

Mkono wa chuma ni njia sahihi kwao maana si wameshindwa kwenda vijijini kulima!!??..Halafu labda hujaishi uswahilini wewe tuulize sisi tuliozaliwa na kukulia Mwananyamala,Tandale Mabibo tukwambie hali halisi ya kuwa hakuna familia itakayokubali kwamba ndugu yao alikuwa ni mhalifu thus why panya Road wanaendelea kusurvive mitaani polisi hawawezi kukusingizia mtu bila kuwa na taarifa nae kwa kesi ndogondgo kama hizo mbona hawajaja nyumbani kwetu kukamata ndugu zetu!?,au mbona hawajaenda kwa kina Mshana Jr au kwa kina reymage ???

Tuache ujuaji wa kiboya katika ishu sensitive hasa zinazohusu usalama wa nchi,serikali ilimpiga chuma komando wake Tamimu miaka ile ya 80 pale Kinondoni Mkwajuni bila kujali kwamba alikuwa mtu muhimu sana jeshini wakati ule hii yote ni sababu ya kulinda amani nchini..acha polisi wafanye kazi yao
 
Binafsi nina uhakika hao vijana ni wahalifu.

Polisi sio wajinga waruke nyumba zote waje kugonga nyumba zao tu.

Ukisoma majina yao tu unajua ni wahuni.. mtu anaacha jina lake alilopewa na wazazi wake anajiita TOSHA na anakuwa maarufu kwa jina la kihuni maana yake nini?

Polisi wanatumia teknolojia ku trace wezi.. hao mawasiliano yao yamesikilizwa kwanza.. na pia movement zao zimefatiliwa kwa kutumia simu zao na teknolojia zingine za polisi. Unakuta kila kwenye tukio la uhalifu mtu simu yake inasoma alikuwepo. Why polisi wamuache ?
 
Allah Akbar!! Kwa kweli inasikitisha kusoma habari kama hii katika nchi ambayo ina uhuru kwa mika sitini!Sialaumu sana kwani najua huu ndio uwezo wako.Saudi Arabia inakat watu vichwa kila Ijumaa,je uhalifu umekwisha Saudi Arabia?Uhalifu na kukengeuka katika jamii (social deviance) ni jambo la kawaida na hata ungechukua hatua kali kiasi gani bado wapo watu ambao wataangukia hapo na ndipo ambapo magereza yanahitajika ili angalau watu wajifunze na warekebishwe tabia.La pili ni jamii ya sasa ya Watanzania,ni wa kuonea huruma,leo bodaboda kawa swahiba wa polisi mpka anaandamana kumpongeza Polisi kuua!!!
Someni barua ya kujiuzulu Mwinyi angalau mueleimike.
Abdul Nondo,umetimiza wajibu wako na najua umehatarisha usalam wako.
 
Panya road wangekua nao wanabusara kwamba wanakuibia tu halafu wanakutema nasi tungefikiria kutumia sheria.

Kumbe ni wanakuibia na kukupa kilema cha maisha au kukuua kabisa kwa mali yako. Kibaya zaidi anakuibia mtu hohehahe kabisa maisha yako ya kuunga unga na bado wanakupa kilema cha maisha 😡😡😡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…