Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Haijarishi Panya Road wamefanya uhalibifu mkubwa kiasi gani, Polisi bado haruhusiwi kuua mtuhumiwa.

Yote kwa yote, jeshi letu la Polisi ni taasisi inayoongoza kwa kutuhumiwa kufanya uhalifu zaidi.
 
Samahani, Una umri gani.
Zamani ilikuwa ngumu mhalifu au gaidi au mhamiaji haramu kuwepo nchini, lazima ajulikane mapema sana.,
Zamani ilikuwa mtu yeyote anaweza kuukemea uhalifu mahali popote na ukasita,..
Raia na vvyombo vya usalama vilishiriki pamoja kama jamii tofauti na sasa kila kimoja vikwake.
Sasa hivi polisi pana kizuizi ukitaka kuingia unajua nini kimetokea.Polisi wanaogopa? au...
Kuna mahali tumeyumba ki maadili kama raia na kimaadili kama askari..
Nina 72+🚶
 
wazungu wanasema"you nailed it all"kwa lugha yetu ya kibantu inamaanisha umemaliza kila kitu!sina cha kuongeza!vijana wanatakiwa wafanye kazi kwa bidii hii njia ya shot cut haisaidii!hata vitabu vyote vinasema mshahara wa dhambi ni mauti
Naunga mkono hoja. Halafu inashangaza sana wakati hao panya rodi wanapofanya yao; wazazi,ndugu, marafiki na jamaa zao hukaa kimyaa i.e. haiwahusu. Hapo Wanaachwa waathirika peke yao na maumivu yao. Sasa panya rodi anashughulikiwa unashangaa wanaibuka watu from no where na mikelele yao oh, hapana sheria na katiba, oh kimeenda kimerudi. Nawashauri hao wapiga tararira kimya kile kitakatifu walichokuwa nacho kiendelee. Waiache Serikali ilinde raia na mali zao ....Au kuna watu wao wameguswa na operesheni hii??? Kama sio ndugu yako unapiga kelele za nini? Watu waliokatwa mapanga na panya rodi sio ndugu zako??
 
Haijarishi Panya Road wamefanya uhalibifu mkubwa kiasi gani, Polisi bado haruhusiwi kuua mtuhumiwa.

Yote kwa yote, jeshi letu la Polisi ni taasisi inayoongoza kwa kutuhumiwa kufanya uhalifu zaidi.
Thibitisha.
 
Ndio maana inatakiwa mshukiwa apelekwe mahakamani ukweli wa kosa udhibitike, na adhabu stahiki itolewe. Sio sahihi kuruhusu polisi wasio na weledi kuua watu wanaowatuhumu.
Washapelekwa sana wanarudi.
Mtu kaua kumfunga hakupunguzi hasara ya aliyekufa, anatakiwa ma yeye afe ili iwe even
 
Komeni kabisa.
IMG-20220928-WA0036.jpg
 
Huyo Nondo sio nini hawa hajui lolote tena ni vyema akanyamaza tu. Ukiona Polisi wanasema hadharani neno kuua maana yake njia za mwanzo zimefeli. Hao panya road wako juu kisheria kwamba wanaweza kuua, kujeruhi, kuiba mbaya zaidi kwa raia mwema tu ambaye anavuja jasho lake kutafuta. Namwambia Nondo hao vijana wanajulikana na vinara wa uhalifu ni wenye rekodi tayari ya matukio ya kihalifu ushahidi upo wazi tu. Kibaka anaiba, anajeruhi anapelekw mahakamani anahukumiwa miezi au miaka akitoka anarudia alipoishia. Ushahidi upo kama unataka nitafute. Tuache siasa kwenye mambo muhimu.
nitatoa mfano, kuna mshkaji flan alikuwa anakunywa bia zake jioni mida ya saa 1 hivi maeneo fulani baada ya kutoka kazini. ghafla vijana wenye mapanga, nondo, sime, shoka, mundu, nyundo, visu, bisibisi, waya za umeme zile nzito nk wanavamia wakamwambia toa simu wallet hela kila kitu jamaa katika ile hali ya kuhamaki asijue ya kufanya akawa kama anadelay hivi (si kwamba aligoma ila ule mshtuko), kijana mmoja akasema oya anazingua akapigwa panga lilikuwa linaelekea kichwani jamaa akaweka mkono kuzuia. panga likapiga ktk kiganja damu zikachuruzika wakamchukulia vyake wakasepa. yule mshkaji akaenda hosp akatibiwa tu kawaida ile huduma ya kwanza na akawekwa bandage akapewa tablets na sindano ya tetenus. akarudi home kujiuguza. baada ya kama wiki akahisi kile kiganja kiko tofauti maumivu yanaongezeka. akaenda hosp kwa vipimo zaidi CT scan ikaonyesha panga lilitaka mishipa ya fahamu kiganjani. ikabidi afanyie oparation kama tatu atlast ikashauriwa waukate tu huo mshipa. hapa tunapoongea jamaa baadh ya kidole cha kiganja cha mkono hauna connections na ubongo. nerve zake zimakatwa. imagine kijana wa miaka 25-30 tu. inasikitisha sana.

NB na kitu ambacho wengi hawajui hata hao watoto/vijana wanajua kuna loophole ktk sheria anajua fika atafanya anachokitaka then akapelekwa mahakamani atakula mvua 2 anarejea na kumbuka huko jela wanazidi kujazana uzoefu wa wizi na wengineo humo ndani akirudi uraiani ni kama kaongeza ujuzi.
Nondo acha siasa kama ulivyofanya huo itafiti sijui nn tembelea na waathirika wa hizi mambo ujue watu wanaumia kiasi gani, wanarudishwa nyuma kiasi gani.
Inatosha tu kumwambia kwamba: "Panya rodi walianza bila sheria na wataisha bila sheria".
 
Allah Akbar!! Kwa kweli inasikitisha kusoma habari kama hii katika nchi ambayo ina uhuru kwa mika sitini!Sialaumu sana kwani najua huu ndio uwezo wako.Saudi Arabia inakat watu vichwa kila Ijumaa,je uhalifu umekwisha Saudi Arabia?Uhalifu na kukengeuka katika jamii (social deviance) ni jambo la kawaida na hata ungechukua hatua kali kiasi gani bado wapo watu ambao wataangukia hapo na ndipo ambapo magereza yanahitajika ili angalau watu wajifunze na warekebishwe tabia.La pili ni jamii ya sasa ya Watanzania,ni wa kuonea huruma,leo bodaboda kawa swahiba wa polisi mpka anaandamana kumpongeza Polisi kuua!!!
Someni barua ya kujiuzulu Mwinyi angalau mueleimike.
Abdul Nondo,umetimiza wajibu wako na najua umehatarisha usalam wako.
Uhalifu hauwezi kuisha ndio, ila ni lazima upigwe vita. Nenda kaangalie takwimu kuhusu kiwango cha uhalifu nchini Saudi Arabia uone ilivyo na kiwango kidogo cha uhalifu.
 
hawa vijana ninavyojua polisi hawawezi kutoka tu huko na kuwafuata nyumbani, lazima kunanamna walivyokuwa wanashirikiana na hao wahalifu. Naomba operesheni hii ifanyike kwa miezi mitatu na maeneo mengine ya Jiji
Mkuu umesema ...lazima kunanamna walivyokuwa wanashirikiana na hao wahalifu.....
Sikukuelewa. Ila ni kweli Polisi hawawezi kukurupuka tu na kukufuata nyumbani kwako. Lazima kuna "ramani"
 
Maneno mengi yaliojaa pumba tupu kwa hili la panyarodi polisi wanazotaarifa zote kuhusu hao majambazi hivyo tuwaache askari wetu waendelee kuwamaliza hawa wachafuzi wa amani.Nondo acha siasa panyarodi ni wakatili kama unawapenda wewe na chama chako waambieni waache kufanya uharifu kwani hauna faida au muwaajiri kwa chama chenu ili mkiwavuruga wawapige roba hadi mkate gogo huku mkikorotoa macho kama mijusi iliyobanwa na mlango.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Uhalifu hauwezi kuisha ndio, ila ni lazima upigwe vita. Nenda kaangalie takwimu kuhusu kiwango cha uhalifu nchini Saudi Arabia uone ilivyo na kiwango kidogo cha uhalifu.
Zipo sababu zinazopelekea watu kujiingiza kwenye uhalifu mathalani majanga ya Asili e.g. janga la njaa kali/ukame, mtu anaiba ili anusuru maisha yake au ya familia yake. Lakini leo waulizwe hao panya rodi ni nini kinachowasukuma hadi wafanye kama wanavyo fanya??
Najua hawatasema hata kidogo ila ukweli ni kwamba wanatamaa ya maisha ambayo haiwezekani kuyapata, wanavuta bangi,madawa ya kulevya na wanakosa fedha ya kununulia starehe hizo n.k. yaani ni vitu vya kijinga-kijinga. Hawakulelewa vizuri au walikengeuka mawaidha na mafunzo yale waliyofundishwa au maelekezo wanayopata kwa wazazi na kutoka kwa Jamii. Wanadhani ubabe ndio maisha yanaenda.
Wameshupaza shingo. Wao kama wao(Nafsi) binadamu hakuna shida kabisa. Shida iko katika matendo yao. Yaani kile wanachofanya/tenda ndicho hatukubaliani nacho na ndicho kinapigwa vita. Waache au wajiepushe na tabia hii uone kama kuna mtu atawafuata.
 
Huyo Nondo sio nini hawa hajui lolote tena ni vyema akanyamaza tu. Ukiona Polisi wanasema hadharani neno kuua maana yake njia za mwanzo zimefeli. Hao panya road wako juu kisheria kwamba wanaweza kuua, kujeruhi, kuiba mbaya zaidi kwa raia mwema tu ambaye anavuja jasho lake kutafuta. Namwambia Nondo hao vijana wanajulikana na vinara wa uhalifu ni wenye rekodi tayari ya matukio ya kihalifu ushahidi upo wazi tu. Kibaka anaiba, anajeruhi anapelekw mahakamani anahukumiwa miezi au miaka akitoka anarudia alipoishia. Ushahidi upo kama unataka nitafute. Tuache siasa kwenye mambo muhimu.
nitatoa mfano, kuna mshkaji flan alikuwa anakunywa bia zake jioni mida ya saa 1 hivi maeneo fulani baada ya kutoka kazini. ghafla vijana wenye mapanga, nondo, sime, shoka, mundu, nyundo, visu, bisibisi, waya za umeme zile nzito nk wanavamia wakamwambia toa simu wallet hela kila kitu jamaa katika ile hali ya kuhamaki asijue ya kufanya akawa kama anadelay hivi (si kwamba aligoma ila ule mshtuko), kijana mmoja akasema oya anazingua akapigwa panga lilikuwa linaelekea kichwani jamaa akaweka mkono kuzuia. panga likapiga ktk kiganja damu zikachuruzika wakamchukulia vyake wakasepa. yule mshkaji akaenda hosp akatibiwa tu kawaida ile huduma ya kwanza na akawekwa bandage akapewa tablets na sindano ya tetenus. akarudi home kujiuguza. baada ya kama wiki akahisi kile kiganja kiko tofauti maumivu yanaongezeka. akaenda hosp kwa vipimo zaidi CT scan ikaonyesha panga lilitaka mishipa ya fahamu kiganjani. ikabidi afanyie oparation kama tatu atlast ikashauriwa waukate tu huo mshipa. hapa tunapoongea jamaa baadh ya kidole cha kiganja cha mkono hauna connections na ubongo. nerve zake zimakatwa. imagine kijana wa miaka 25-30 tu. inasikitisha sana.

NB na kitu ambacho wengi hawajui hata hao watoto/vijana wanajua kuna loophole ktk sheria anajua fika atafanya anachokitaka then akapelekwa mahakamani atakula mvua 2 anarejea na kumbuka huko jela wanazidi kujazana uzoefu wa wizi na wengineo humo ndani akirudi uraiani ni kama kaongeza ujuzi.
Nondo acha siasa kama ulivyofanya huo itafiti sijui nn tembelea na waathirika wa hizi mambo ujue watu wanaumia kiasi gani, wanarudishwa nyuma kiasi gani.
Watanzania wengi siyo watu wakutafakari. Na inaonyesha wewe ni mmoja wao. Ni hivi: hakuna mtu anayekataa kuwa panya road ni tatizo kubwa na ni hatari sana. Kuna wengi tumeshaathirika na hawa vibaka. Tunataka sana hatua zichukuliwe na watokomezwe wote. Tunachokataa ni hili jambo la polisi kuua baada ya kuwakamata. Historia dunia kote inaonyesha kuhukumu wahalifu namna hii i.e. kwa kuwaua bila kwenda mahakamani na ukweli ukajulikana siku zote husababisha baadhi ya watu wema kuuawa. Polisi siyo malaika, hivyo kuna watakaotumia huu mwanya kutimiza malengo yao maovu. Je, kama kwa mfano ulikuwa umewachomea polisi kula rushwa na wakafukuzwa, wale marafiki zao waliopona hawataweza kutumia mwanya kama huu kukumaliza? Kiufupi ni kuwa polisi mwovu anaweza kukufanya lolote kwani atasingizia kuwa ulikuwa panya road. Pia kuna wengine watatumia huu mwanya kudai rushwa hata kama huna kosa. Hivi ukikamtwa na ukaambiwa kuwa usipotoa kiasi fulani cha fedha utafanywa kama panya road utakataa? Na pia kuna wengine watakaouawa kwa makosa. Hujawahi kuona mtu anashukiwa kuwa ni mchawi wakati hana uchawi wowote? Hivi mtaani kama kuna majirani wenye chuki na wewe wakikuchongea kuwa ni panya road huoni kuwa utakufa bila kufanya kosa lolote? Hebu acheni kuwa na akili fupi kama za ndezi!
 
Mkuu Nondo ebu usizunguke mbuyu kwa kuandika pumba nyingi ambazo hata kuku ukiwamwagia hawawezi kuzimaliza.
Unachotakiwa kufanya ni kuwashauri vijana waache kujihusisha na uhalifu maana utawa cost.
Sheria zetu za sasa ni butu juu ya adhabu za uhalifu. Unakuta mtu amefanya kitendo cha kinyama, lkn sheria kupitia hakim inamuhukumu kwenda jela miezi 3, sita au mwaka.
Huko jela anakula bure, analala bure kupitia kodi zetu watanzania wote wakiwemo na walioathirika na uhalifu huo.
Mwisho wa siku panya road akitoka jela anatoka yuko vizuri na baada ya muda anafanya uhalifu mungine ili arudishwe akale na kulala bure.
Sasa watanzania tumeshachoka ndio maana tunaona ni sawa tu polisi kuchukua njia walioichagua kuwaangamiza hao kunguni ili kurudisha amani na usalama ndani ya nchi yetu.

Leo hii katika ardhi ya Rwanda hauwezi kuona panya road kutokana na hatua kali inayochukuliwa na vyombo vyao vya usalama.
Nchi yoyote ikikosa usalama ni vigumu sana hata kupata wawekezaji na watalii. Muda wa kuwalea lea wahalifu umeshapitwa na wakati, sasa ni kipindi cha "iba uuwawe".

Nakuhakikishia hili zoezi likiendelea kwa miezi 6 bongo itakuwa sehem salama kuliko nchi nyingi za Afrika Mashariki.

Kuiba, kujeruhi na kuuwa ni dhambi, na siku zote mshahara wa DHAMBI ni MAUTI.
Ni mtu mpumbavu sana tu ndiye anayeweza kuandika upumbavu kama huu. Hujui watu tunataka sheria zifuatwe ili kuondoa kosa la watu kuuawa bila makosa? Hujakutana na watu wenye makosa ya kubambikiwa wewe? Hujasikia mpaka rais anayekiri kuwa kuna watuhumiwa wengi wenye makosa ya kubambikiwa? Kwa nini mtu anapokamatwa wasitumie muda kujiridhisha kuwa ni mhalifu na badala yake waue hapo kwa hapo? Kuna kuna mijitu mingine kama wewe ni hatari kuliko hata hao panya road. Mijitu kama wewe mpaka ndugu yako auawe kimakosa ndiyo utasikia inahaha. Idiot!
 
Duh mbona una hasira sana we panyaroad.
 
Back
Top Bottom