Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Uko sahihi sana, kama kweli wanachokifanya polisi cha kuua wezi ni sahihi, kuna mtu alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta hapo nyumbani kwake. Mbona mtu huyu hatujasikia kapigwa risasi maana yeye kaiba kikubwa kuliko panya road?
Mkuu , hata hao panya road wangekuwa wanaiba bila kudhuru mwili wa mtu kelele zisingekuwa nyingi.

Shida wao wanajeruhi na kuua na mali wanachukua pia. Hivyo haifanani na huyu aliyejiunganishia bomba bila kuingilia usalama WA watu wengine.
 
Ni sawa, lakini polisi hawaaminiki wanapomtuhumu mtu, ndio maana tunataka hao wauaji wakadhitishwe mahakamani.
 
Sasa wewe katika kufanya uchunguzi wako huo ulitegemea familia za hao panyaroad wakwambie walikuwa ni wezi? Acha kwanza polisi wafanye kazi yao la sivyo hao vibaka mtawapa nguvu ya kurudi upya maana wanatetewa, huu sio muda muafaka wa kuongea haya.
 
THREAD YA KUPUUZA HII.
POLISI NAO WANACHOKA JAMANI ACHA WAWAFYEKE,KUMBUKENI POLISI WETU KABLA YA KUFANYA LOLOTE HUWA WANAKUWA WAMESHACHUNGUZA KWA KINA,KABLA YA UTEKELEZAJI.
Rubbish! Polis wetu ni dhaifu sana kuchunguza ndo maana hutumia short cut kwani mahakamani watashindwa.
 
Maandamano ya POLISI kujikaimisha mamlaka ya Mahakama kuhukumu wananchi adhabu ya kifo bila kufikishwa MAHAKAMANI.

Kwani hii ni POLICE STATE???🙃🙃🙃
Yaani polis wetu wanatoa judgement za capital punishment? Khaa!!! Under what law?
 
Uatajisikiea nitajisikia sawa kwani nimemta mm akafanye uhalifu policy siyo wajinga wamchukuwe bila sababu ....taitizo unakah na mtot Hana kazi anasimu macho matatu anakunywa kila saa nne supu alfu ukute hajasoma kila saa Yuko kijiweni na kiduku asieeee mimina risasi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hujaelewa nilichokisema. Mwanao hajafanya uhalifu lakini anapigwa rusasi. Mahakama za nini Sasa?
Mnasahau ya akina Zombie?
 
Operesheni ya Polisi-Dar es salaam dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road ichunguzwe.

Kukithiri kwa vitendo vya Panya Road Mkoa wa Dar es salaam ,kumezua hofu miongoni mwa jamii kwa makundi hayo kuvamia,kupora na hata kuuwa ,mfano.Kifo cha mwanafunzi wa SJMC(UDSM) Maria Basso kilichotokea tar.14 Sept.2022 saa 2:30 usiku kwao Kawe- Mzimuni.Mungu amlaze mahali Pema.

Matendo haya ya kihalifu ni kinyume na katiba ya JMT- 1977 ibara ya 14,ni kinyume na kanuni ya adhabu sura 16,kifungu cha 287 na 288 (kudhuru kwa lengo la kuiba ) na kifungu cha
196 ,197 kinachohusu kuuwa kwa kukusudia na adhabu yake ni kifo kwa mujibu wa sheria na adhabu hutolewa na mahakama kwa mujibu wa katiba ya JMT- 1977 ibara ya 107 A(1) kwamba mahakama ndicho chombo chenye maamuzi ya mwisho katika utoaji haki.

Jamii na kila mtu tulifarijika tulipoanza kusikia viongozi wa serikali na Polisi wakiahidi kupambana ili kukomesha kadhia na uhalifu huu wa Panya Road kwa mujibu wa sheria.

Kwa kuamini ya kuwa nchi yetu ni nchi inayoamini katika misingi ya utawala wa sheria (Rule of Law),ni wazi kila mwananchi aliamini ya kwamba njia zitakazotumiwa na Polisi kukabiliana na uhalafu huu hazitakuwa kinyume na katiba ,sheria na taratibu bali kwa kutumia maarifa ,elimu na taaluma yao katika upelelezi,uchunguzi na Intejensia na kushughulikia kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20, kifungu cha 4(1,2) na sheria zingine zinazohusu wajibu wa Polisi kuchunguza makosa yote ya jinai na kuyashugulikia kwa mujibu wa sheria".

Jambo la kushangaza sana, ni kauli aliyoitoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,Mh.Amos Makalla tar.15 /Sept./2022 alipokutana na wananchi kata ya Zingiziwa ,Chanika Wilaya ya Ilala akisema " Wazazi wenye watoto Panya Road kuanzia leo tar 15/ Sept.2022 ,asipomuona nyumbani mtoto wake ,asihangaike akamtafute Polisi kituoni au Hospital (Monchwari)

Kauli ya Mkuu wa Mkoa Mh.Amosi Makala ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa, ilichochea Polisi kujipa mamlaka ya kutuhumu ,kukamata na kuhukumu kwa kutoa adhabu ya kifo. Na hiki ndicho kilichotokea kuanzia tar.16 ,17,18 na 19 Sept. 2022 vijana kadhaa waliotuhumiwa kuwa Panya Road katika maeneo tofauti tofauti waliuliwa na Polisi kwa Risasi na miili yao kupelekwa Muhimbili (Monchwari ) na njia waliyokuwa wakitumia ni kuwatafuta vijana watukutu mtaani waliowahi kuwa na rikodi ya kukamatwa na Polisi huko nyuma aidha kwa tuhuma za Bangi au wizi na kuwakamata kuwapeleka kutuo cha Polisi, na kuwapiga ili wataje na wengine hivyo vijana wengine walikuwa wanakamatwa sababu wametajwa na hatimaye kupigwa Risasi na miili yao kupeleka muhimbili.

Achana na tukio alilotangaza Kamanda Jumanne Muliro la watu 6 waliotuhumiwa Panya Road kuuwawa Makongo Juu tar 18/Sept/2022 .Hilo walitoa sababu zao Polisi kwamba walikuwa wanajihami siwezi zungumzia sababu sijui ukweli wake.

Mimi nitazungumzia matukio ambayo hayajazungumziwa na Polisi ya vijana watatu waliotuhumiwa kuwa ni Panya Road kutoka katika Familia tatu ,huko Tandika waliokamatwa na polisi kutokea nyumbani kwao na kupelekwa kituo cha Polisi Maturubali (Mbagala) wakauliwa kwa kupigwa Risasi na maiti zikapelekwa muhimbili (Monchwari) ,kinyume kabisa na katiba ya JMT- 1977 ibara ya 14 na ibara ya 107 A(1) kinyume,pia ni kinyume kabisa na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 196 na 197, kinyume kabisa na kanuni za Jumla za Jeshi la Police (Police General Order-PGO) kifungu cha 4, kifungu cha 15,kifungu cha 16 (kifungu hiki kinaelezea kuhusu Police kutumia nguvu inapohitajika kifungu hiki pia hakikuzingatiwa ,sababu watu walipigwa Risasi za shingo /Unlawful killings), kifungu cha 19,kifungu cha 20, kifungu cha 27, kifungu cha 28, kifungu cha 33 na kifungu cha 34 lakini pia ni kinyume kabisa na Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kifungu cha 4(1,2),ni pia na sheria ya inquest act sura ya 24 , kifungu cha 14(1)(c).

Kama mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT Wazalendo Taifa na Waziri Kivuli wa vijana ACT Wazalendo ,Jana tar.28 /Sept/2022 niliamua kufuatilia familia baadhi ambazo zimepoteza vijana wao waliotuhumiwa kuwa Panya Road ili nipate kujua zaidi kuhusu yaliyojificha katika Operesheni hii ya Polisi .

Nilipata fursa kufika katika Familia 3 ,zote zipo Tandika,mtaa wa Nyambwela.

Familia ya kwanza.

Hii ni Familia ya Bi.Amina Allawi Alli ,ambaye mtoto wake aliyeuwawa alikuwa anaitwa Amiry Athuman Hassan , umri miaka 25 alikuwa akiishi na wazazi wake Tandika mtaa wa Nyambwela.

Kwamba tarehe 17/09/2022 ,saa 10 usiku-Alfajiri Polisi walivamia nyumbani kwao wakigonga mlango kwa nguvu,kusukuma na kufanikiwa kuingia ndani ,wakavunja milango ya vyumba vitatu wakimtafuta huyo kijana Amiry waliomtuhumu kuwa ni Panya Road na mwizi,wakamkuta ndani amelala wakamuamsha kwa vibao na kumwambia yeye ni mwizi hata TV waliyoikuta ndani kwamba ni ya wizi wakamchukua yeye na TV wakaichukua.

Mtuhumiwa alijiaribu kujitetea kwamba hana hatia na hata TV hiyo alinunua Dukani Tandika ,Duka la Gaza Electronics tar 29/05/2022 na Risiti anayo ,Polisi hawakusikia wakaondoka nae.

Palipo kucha wazazi walifuatilia katika vituo vyote vya Polisi Makangarawe, Chang'ombe,Maturubali,Stakishari ,Tazara hadi Central bila mafanikio siku ikaisha bila mafanikio, tar 18 ,Sep.2022 wakamkia tena Kituo cha Maturubali-Mbagala sababu jana yake walimuona Polisi mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliomkamata kijana wao hapo Maturuba,wakiwa Kituo cha Polisi Maturubali walijibiwa waendelee kutafuta vituo vingine au waende Muhimbili Monchwari, walienda muhimbili na kweli walikuta maiti ikiwa na alama mbili za Risasi shingoni.

Walinyimwa kupewa Maiti hadi waende na Polisi ,ikabidi wakarejea Kituo Cha Polisi Maturubali -Mbagala kuomba waende na Polisi ili wapate Maiti ya mtoto wao ,Polisi alihitaji fedha ya nauli elf 20 ndio wakaenda nae kutoa Maiti ya kijana wao,na Muhimbili waliombwa pia kulipa fedha ili kutoa Maiti.

Nilichukua hatua ya kufuatilia hilo Duka ambalo marehemu alinunua hiyo TV ambayo Polisi waliichukua kwa kusema ni ya wizi ,nilipata Duka hilo lipo Tandika ,linaitwa Gaza Electronics karibu na Stendi ya Gari za Mbezi ,niliuliza wakakiri kwamba ni kweli ni Risiti ya Duka lao na huyo kijana ni kweli walimuuzia TV hiyo aina ya Solar Max inch.32 .

Na niliamua kumtafuta Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyambwela anaitwa Ndug.Bushiri Ali Napwiri kumuuliza kuhusu tukio hili akasema yeye alienda Polisi Kituo cha Maturubali-Mbagala akiwaambia huyo kijana Amiry hana tabia hizo kwa sasa,wamuache ni Kijana mwema.

Polisi walimjibu Mwenyekiti Bushiri akubali wamuache huyo kijana Amiry ili wamkamate yeye (Mwenyekiti) kumuweka lock up, Mwenyekiti ikabidi aondoke na hata Kijana Amiry alipouwawa Mwenyekiti alipewa taarifa na Polisi kwamba kijana tayari ameuwawa, Mwenyekiti anasema aliogopa kuipa familia taarifa sababu hakujua aanzaje.

Familia nyingine.

Familia nyingine ni ya Bi.Asha Ally na kaka yake Ndug.Swedy Ally Shoo ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi (CCM) huko Kiwalani anapoishi sasa.Bi Asha Ally alikuwa na watoto wawili tuu mmoja wa kike na mwingine wa kiume aliyeuwawa, alikuwa anaitwa Khatibu Said Kabwele au Tosha.

Kwamba tar 17/Sept/2022 saa 12 Asubuhi,Polisi walifika wakigonga mlango ,wakiomba kuongea na huyo kijana Khatibu au Tosha waliulizwa wao ni nani, wakasema ni Polisi wanaongea nae tuu wanamuacha akaamshwa na Mama yake ,na Polisi wakaondoka nae wakisema yupo mikono salama atarudi ikapita tar 17,18, tar 19,Sept.2022 baada ya kuzunguka vituoni katika Kituo hicho hicho cha Maturubali-Mbagala walijibiwa waende Muhimbili Monchwari, Polisi alikataa kwenda nao Muhimbili akiomba fedha elf 40 ya nauli wakampa na walipofika Muhimbili Familia ilitoa tena fedha ya kulipia maiti kuhifadhiwa Monchwari na kukuta Maiti ya kijana wao ikiwa na alama za Risasi Begani na katika koromeo.

Tukio lingine.

Kijana aliyefahamika kwa jina la Khalfan Jongo,mkazi wa Sandali-Tandika alifuatwa nyumbani kwa kutajwa na wenzake,akachukuliwa tar 16 ,Familia inasema walikuja kujua baada ya siku kadhaa kupita,wakaenda Muhimbili wakakuta Maiti ya kijana wao ikiwa na alama za Risasi shingoni.

Tukio lingine.

Ni kijana aitwaye Mbwana Kambi,Mkazi wa kata ya Tandika mtaa wa Nyambwela,alikamatwa na sungusungu tar 23 ,Sept.2022 akapelekwa kituo cha Polisi Makangarawe,akaambiwa atoe laki mbili asipotoa anapewa kesi ya Panya Road,hakutoa fedha hiyo hivyo tar 24 /Sept/2022 wakampeleka kituo cha Police Chang'ombe na kesi ya Panya Road,amekaa chang'ombe akipigwa na nyaya hadi tar 27 ,Sept/2022 Ndugu zake walivyofuatilia ndio akaachiwa hajui kama ndugu walitoa fedha au aliachiwa tuu.

Kwa matukio haya,ndio maana nimehitimisha kwa kusema kwamba Operesheni ya Polisi Dar es salaam dhidi ya Panya Road ichunguzwe,kuna viashiria vingi kwamba Polisi hawafanyi uchunguzi, bali wana tuhumu, wanakamata na kuadhibu jambo ambalo ni kinyume na katiba na Sheria nilizozitaja hapo juu, haya mambo yakiachwa yanaweza kupelekea wasio na hatia kukumbwa, lakini pia Polisi kujichukulia Sheria mkononi na kudharau utawala wa Sheria inaweza tengeneza Precedents kwamba hakuna haja ya kuchunguza wala kupeleka Mahakamani ,matokeo yake Haki (Justice) itatoweka, utawala wa sheria utatoweka nchini ,ni kinyume na Kanuni za Jumla za Jeshi la Polisi (PGO) kifungu cha 20, kinachohitaji Polisi kuzingatia dhana ya Presumption of innocence kwamba katika hatua ya kukamata na kupeleleza lazima Polisi ione aliyekamatwa hana hatia hadi itakapothibitishwa na mahakama.

Kama Polisi wanaona uchunguzi na kushtaki mahakamani sio njia sahihi ya kupambana na uhalifu basi wabadili sheria ,Polisi hao hao ndio wajipe mamlaka ya kutuhumu,kukamata , kuhukumu au kuadhibu kwa kifo kama wanavyofanya sasa katika Operesheni hii katika baadhi ya maeneo niliyoyataja.

Hao Polisi waliofanya matendo hayo wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria iwe waliagizwa au walifanya kwa utashi wao ili wawajibike ,lakini pia Tume huru iundwe ili kuchunguza haya matukio ya namna hii katika Operesheni hizi za Polisi,tulinde utawala wa sheria ndio nguzo ya Haki na usawa kwa wananchi na katika Taifa.

Tunaunga Mkono jitihada za Polisi za kupambana Panya Road na uhalifu mwingine wowote ikiwa tuu jitihada hizo za kupambana na uhalifu zitafanyika kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu, kanuni na miongozo tuliyo nayo tofauti na hapo hayo ni mauaji (Extrajudicial Killings).

Mfano,Police wanaweza kujitetea kwamba walitumia nguvu ilipohitajika kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Polisi sura ya 322 na Kanuni za Jumla za Jeshi la Polisi( PGO) kifungu cha 16 , ndio maana hao wakapigwa Risasi ,lakini tujiulize swali je ni kweli kutumia nguvu inapohitajika (Reasonable force) inahalalishwa kwa kumpiga mtu Risasi ya shingo? au kifua?

Hiyo kweli ni Reasonable force? .Kwanini mtu asipigwe ya mguu kama kweli kulikuwa na haja ya kutumia nguvu ili kukabiliana, Je, mtu aliyemchukuliwa kutoka nyumbani kwao na akakubali kutoka kweli kulikuwa na haja ya kutumia hiyo nguvu?

Mashiriki ya Haki za Binadamu ,Chama Cha mawakili -TLS, vyama vya siasa, wanaharakati na kila Mtanzania kwa pamoja tulaani mienendo hii ya Polisi na matendo yao katika kupambana na uhalifu nchini.

Na hatua zichukuliwe ili matendo haya yakome na yasizidi kuota mizizi katika nchi yetu ambayo utawala wa sheria ndio nguzo yetu.

Na Jambo la msingi sana,sasa tuone umuhimu na haja kubwa ya kubadili sheria na mifumo ya Jeshi letu la Police tuwe na Jeshi la Polisi la kisasa (Modern Police Service)/Democratic Police.

Lakini pia ni muda sasa tuwe na chombo kitakacho simamia matendo ,mienendo ya Jeshi la Polisi na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kutokana na makosa au matendo ya Polisi dhidi ya wananchi ,chombo hicho kiitwe Independent Policing Oversight Authority -IPOA.

Ahsante,

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT Wazalendo Taifa.

Waziri Kivuli wa vijana, kazi na Ajira -ACT Wazalendo.

29/Sept./2022.View attachment 2371373View attachment 2371374View attachment 2371376View attachment 2371375View attachment 2371377View attachment 2371379View attachment 2371380View attachment 2371378View attachment 2371381
Police puuzeni kelele hizi za wachache endeleeni na zoezi la kuua hawa viroboto na mapanya, tena msirudi nyuma wala msipoe mmezoeleka mno hadi raia hawana uwoga teketeza hao vibwengo panya buku wote
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam na kamanda wa kanda maalum ya Dar Es Salaa kuna siku lazima washitakiwe kwa makusudi kuvunja katiba ya nchi na kuvunja haki za binadamu. Kuna tofauti gani kati ya wananchi wenye hasira kali na polisi wenye wajibu wa kulinda raia na mali zake? Panga na mshale inaweza ikajibiwa kwa risasi ya moto?

1. Mkuu wa mkoa Dar
Kamanda kanda maalum ya Dar
3. Kamanda wa upelelezi kanda maalu ya Dar
4. Waziri wa mambo ya ndani

Hao watajwa hapo juu hata ikichukua miaka kumi mbele watakuja kushitakiwa kujibu ni nani aliwapa mamlaka ya kuua raia aisye na silaha inayozidi bunduki. Hata huko Serengeti haiwezekani raia akamiliki silaha ya G3, hiyo ipo jeshi ya ulinzi na JKT pekee. Kila silaha huwa ina namba tambuzi je, silaha hiyo ni ya Tanzania au imepatikana kwa wakimbizi na ilifikaje Mara, Serengeti wakati haina mgogoro wa kivita na mipaka ya Kenya?

Yanayosemwa na wananchi yapuuzeni tu majuto ni mjukuu.
 
Uko sahihi sana, kama kweli wanachokifanya polisi cha kuua wezi ni sahihi, kuna mtu alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta hapo nyumbani kwake. Mbona mtu huyu hatujasikia kapigwa risasi maana yeye kaiba kikubwa kuliko panya road?
Huyu hajamtoboa mtu na bisibisi mkuu
 
Abduli Nondo a.k.a Mwalimu na wakili wa Panya Road na wewe ni lofa .
Unacheza na amani ya nchi.
Halafu uko kwenye Chama Cha kijamaa. Unawezaje kujenga ujamaa na Wahalifu.

Polisi Kwa raia wema ni wastarabu sana. Tena siku hizi wanakupigia simu au kukupelekea barua kupitia mtendaji. Unaenda Kistarabu mwenyewe kituoni.

Kwa hiyo ukiona Polisi wametoka kituoni na kukufuata ujue wanataarifa zote za uhalifu. Kwa hiyo wanakuja Kwa tahadhari zote ulijaribu kuzingua wanakuzingua.

Lakini pia wewe ni mtanzania asiyefaa kabisa yaani ni Msaliti. Na dawa ya Msaliti ni Moja TU. Wanaokua kwenye vita dhidi ya panya road wanajua dawa ya Msaliti hivyo Huyo Nondo sijui Nunda anapaswa kupewa dawa yake.
Hawa akina Nondo wakiachwa ndio watakaoleta uhalifu na mauaji ya wafanyakazi wa mabenki , Wasafiri kama kule kwao Burundi wanavyopora wasafiri kwenye mabasi. Huyu Nunda na ndugu zake Kule Burundi waliwaua sana watanzania miaka ya 2000 mpaka 2010 Kwa kuvamia mabasi kule Kagera na Kigoma . Kwao huyo mpuuzi uporaji ni kazi halali hivyo hatuna haja ya kumsikiza.

Wewe na wanaharakati washenzi kama wewe kama wanaweza kufanya uchunguzi Kwa Polisi basi ni wahuni mana wanashindwa kuchunguza Wahalifu halafu wanaweza kuchunguza Polisi. Wachunguzeni Wahalifu ili muwabaini Kisha Polisi watawakamata na kuwapeleka mahakamani . Lakini wewe na wahuni wengine mnashindwa kutumia ujuzi wako wa uchunguzi kuwabaini Wahalifu halafu inakuja kulia lia hapa.

Panya road wasipoacha uhalifu wataendelea kuliwa kichwa TU na mwishowe wakili wao Nondo naye naye atakula chuma TU mana hakuna namna nyengine
 
Rubbish! Polis wetu ni dhaifu sana kuchunguza ndo maana hutumia short cut kwani mahakamani watashindwa.
Upelelezi ni pamoja na Jina LA muhalifu kuwa na kesi au mashauri mengi ya kihalifu katika vituo mbalimbali na kufungwa jela zaidi ya Mara 3-4,bila mtuhumiwa kukoma KUFANYA uhalifu.,ndio maana nikasema probably wengi hao huwa ni wahalifu sugu,wasiotaka kubadilika hata baada ya kufunzwa na serekali.
KUYAFUGA MAJITU SUGU NI HATARI KUBWA NA USUMBUFU MKUBWA KWA SIKU ZA USONI.
N.b,-Acha kutukana bila hawa ndugu zetu hata usingizi wako pengine ungekuwa mashakani.
 
Nina mashaka humu kuna majambazi.
Au kuna watu hawajawahi kukutwa na dhahma za vitendo vya kihalifu wakawaona jinsi madogo wakishavuta mabangi na ugoro jinsi wasivyo na huruma,huku tabata kuna mama mjamzito aliwahi kufyekwa mimba kwa upanga,dada wa watu akajifia bila sababu.
 
Umeandika yote Ila sijaona sehemu umesema kuwa umewahoji Majirani na wanasemaje kuhusu Hao waliouawa!

Lete interview ya Majirani tuone wanasemaje!

Unadhani mzazi anaweza kukiri mwanae ni panya road ?

Halafu mbona majuzi kuna Panya road kauawa na raia Manzese hujaifuata familia yake kuwahoji na uanze kukemea raia kuchukua hatua za kisheria mkononi.

Tunajua police Wana mapungufu Yao, tuwakemee. Ila Kwa hili la Panya road hapana kabisa Acha hawa vijana walambwe Shaba!
 
Mkuu , hata hao panya road wangekuwa wanaiba bila kudhuru mwili wa mtu kelele zisingekuwa nyingi.

Shida wao wanajeruhi na kuua na mali wanachukua pia. Hivyo haifanani na huyu aliyejiunganishia bomba bila kuingilia usalama WA watu wengine.
Issue kubwa hapa ni kwamba polis wana uhakika gani waliomuuwa ndiye alifanya uhalifu huo wa kuiba, kujeruhi na hata kuua.
Yaani polis nao wanauwa tu kitu ambacho hawaruhusiwi kwani wanalazimika kisheria kuwapeleka mahakamani.

Inavyoonekana wengi humu moja kwa moja akamatwaye na polis tayari ana makosa.

Mbona watuhumiwa wengine huwapeleka mahakamani? Siwangekuwa wanawahukumu wao tu na kuwapeleka jela kama wanao uwezo huo kisheria?

Watz hebu tujaribu kufikiri masuala haya kwa kufuata misingi ya Sheria.
 
Ndiyo maama watu walilalmikia teuzi za Wambura na Kingai kuwa IGP na DCI. Historia zao toka wakati wa JPM si nzuri.

Mikono ya SSH imeshachafuka kwa damu za watu wasio na hatia.

Hii damu itamlilia, sidhani kama damu hii itamuacha salama!.Mikono yake imeshaloa damu!
 
Haidhuru basi polis wanapowauwa washukiwa wa panya road wangekuwa wanataja vifungu vya Sheria vinavyowapa uwezo kufanya hivyo.
Najua Kuna watu watakuja hapa na hoja ya kijinga kama: 'Kwani wao panya road wanatumia vifungu gani vya Sheria kuua'.
Hoja za kijinga sana hizi kwani wahalifu huwa hawafuati Sheria yoyote lakini polis analazimika kufuata Sheria.
 
Back
Top Bottom