Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Mkuu Nondo ebu usizunguke mbuyu kwa kuandika pumba nyingi ambazo hata kuku ukiwamwagia hawawezi kuzimaliza.
Unachotakiwa kufanya ni kuwashauri vijana waache kujihusisha na uhalifu maana utawa cost.
Sheria zetu za sasa ni butu juu ya adhabu za uhalifu. Unakuta mtu amefanya kitendo cha kinyama, lkn sheria kupitia hakim inamuhukumu kwenda jela miezi 3, sita au mwaka.
Huko jela anakula bure, analala bure kupitia kodi zetu watanzania wote wakiwemo na walioathirika na uhalifu huo.
Mwisho wa siku panya road akitoka jela anatoka yuko vizuri na baada ya muda anafanya uhalifu mungine ili arudishwe akale na kulala bure.
Sasa watanzania tumeshachoka ndio maana tunaona ni sawa tu polisi kuchukua njia walioichagua kuwaangamiza hao kunguni ili kurudisha amani na usalama ndani ya nchi yetu.

Leo hii katika ardhi ya Rwanda hauwezi kuona panya road kutokana na hatua kali inayochukuliwa na vyombo vyao vya usalama.
Nchi yoyote ikikosa usalama ni vigumu sana hata kupata wawekezaji na watalii maana watahofia usalama wao na maisha yao.
Muda wa kuwalea lea wahalifu umeshapitwa na wakati, sasa ni kipindi cha "iba uuwawe".

Nakuhakikishia hili zoezi likiendelea kwa miezi 6 bongo itakuwa sehem salama kuliko nchi nyingi za Afrika Mashariki.

Kuiba, kujeruhi na kuuwa ni dhambi, na siku zote mshahara wa DHAMBI ni MAUTI.
🤝🏻🤝🏻🤝🏻 nipo upande wako. Au nayeye panya road.?
 
Uko sahihi sana, kama kweli wanachokifanya polisi cha kuua wezi ni sahihi, kuna mtu alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta hapo nyumbani kwake. Mbona mtu huyu hatujasikia kapigwa risasi maana yeye kaiba kikubwa kuliko panya road?
Panya road anaua watu kabisa

huyo kajiunganishia tu bomba.

kwa akili zako unaua BORA PANYA ROAD?

unahitaji kutinduliwa kimawazo ukae sawa
 
Uko sahihi sana, kama kweli wanachokifanya polisi cha kuua wezi ni sahihi, kuna mtu alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta hapo nyumbani kwake. Mbona mtu huyu hatujasikia kapigwa risasi maana yeye kaiba kikubwa kuliko panya road?
Kweli hata huyo aliyejiunganishia Bomba kaiba, ila tatizo hapa ni kubeba silaha na kujeruhi, kuua na kupora.
Wote wezi ila njia wametumia kuiba tofauti. Kwahiyo na adhabu zitumike njia tofauti.
Muuaji risasi, mwizi wa akili mahakamani.
 
Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi , kuna Mahakama ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa. Hata hao Panya Road wanaofanya uhalifu sheria zipo wakikutwa na hatia wanaadhibiwa sawa na sheria inavyosema kuna kifungo adhabu ya kifo , kifungu cha maisha ,miaka 30 na adhabu zingine . Kwanini wasishtakiwe kwa mujibu wa sheria wajibu wa Polisi ni kufanya upelelezi na uchunguzi kuisaidia Mahakama sio kuuwa watuhumiwa.
Nondo ndugu yangu wewe na chama chako tulikuwa tunawaamini mno kutokana na yale yenye mantiki mliokuwa mnatueleza.Kuhusu panyarodi kupelekwa mahakamani unaweza kutuambia ni mahakama zipi na za nchi gani?kama unakumbuka hata akina Zombe walipelekwa mahakamani jee Zombe yuko jela au yuko nje free?majizi ya nchi hii waliwengi wapo jela au wako free?huku mtaani tunawakamata hao vibaka lakini wakipelekwa mahakamani huachiwa huru kwa kukosa ushahidi madhubuti wakati mtuhumiwa ni kweli mharifu.Lakini ni Mara ngapi waharifu wanafanya mauaji lakini mahakama hutoa hukumu rahisi za kifungo chini ya miaka mitano na wengine huachiwa huru au kutolewa kwa msamaha?.Nondo unasema umefuatilia familia tatu za panyarodi vipi familia nyingi za wahanga hujazitembelea?lakini pia Nondo wakati panyarodi wanaua na kujeruhi kwa nini hukuzitembelea familia za panyarodi ukawashauri waache uharifu na pale wasipofanya hivyo ukalisaidia jeshi la polisi?Polisi wanayomapungufu yao ila kwenye suala la kudhibiti uharifu wako vizuri na hawamuonei MTU.Tuliache jeshi la polisi limalizane nao kiume hao wahalifu tena hata hao waliofikishwa mahakamani sisi wananchi tunawaomba polisi wamalizane nao kiume tumechoka sisi.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
"Tufamu hili neno " OPERESHENI MAALUMU KWANZA"tutenganishe na taratibu za kawaida za kiutendaji,nadhani mnakumbuka operesheni majangili miaka hiyo!
Niambie Wewe sheria inayotambua hiyo Operation maalumu kama exception ya Polisi kuuwa bila kupeleleza na kupeleka Mahakamani.Sababu katika hiyo hiyo Operation maalumu Unaweza poteza maisha ya wasio na hatia ,ndio maana Mahakama ipo .
 
Narudia Tena acha siasa kwenye Mambo muhimu,wanakamatwa mara ngapi wanarudi uraiani?wanaua watu bila kosa,wanabaka wanajeruhi na hakuna kinachoendelea ngoja washughulikiwe kwanza,hizo sheria zenu za kwenye vitabu bakini nazo
Kama sheria zetu hazisaidii Polisi kupambana na uhalifu, zibadilishwe! Kwanini Bado tunazikimbatia na kuzivunja ? Sheria zibadilishwe.
 
Ok , wamepeleke mahakamani sio kuuwa , Polisi hawana hayo mamlaka
Hila panyalodi wana mandate ya kuua? Polisi inawaua hao mbwa hili kuwatisha wapuuzi Wengine wasijaribu kuja kuingia kwenye hayo makundi ya kihalifu waogope.
Hata M/mungu aliyetuumba alikuwa anaua watu washenzi kwa upepo,au radi,au kwa dhoruba yoyote
 
Ukiacha polisi wauweuwe watuhumiwa ipo siku wataanza kupiga vyuma hata wapinzani wa serikali kama alivyofanyiwa Lissu kisha watasingizia kuwa mwanasiasa huyo kwa mujibu wa intelijensia yetu ndiye mmiliki wa panyaroad nchini!
 
Niambie Wewe sheria inayotambua hiyo Operation maalumu kama exception ya Polisi kuuwa bila kupeleleza na kupeleka Mahakamani.Sababu katika hiyo hiyo Operation maalumu Unaweza poteza maisha ya wasio na hatia ,ndio maana Mahakama ipo .
Panyarodi ni kikundi Cha waasi ndani ya nchi, dawa yake ni kuwaua tu
 
hawa vijana ninavyojua polisi hawawezi kutoka tu huko na kuwafuata nyumbani, lazima kunanamna walivyokuwa wanashirikiana na hao wahalifu. Naomba operesheni hii ifanyike kwa miezi mitatu na maeneo mengine ya Jiji
Yap...... well said.
 
Hao panya road mbona kipindi cha Magufuli hawakuwepo,wameona Mama ni mfuata sheria ndio wakaanza.
Wapigwe shaba wote tu
 
Panya road anaua watu kabisa

huyo kajiunganishia tu bomba.

kwa akili zako unaua BORA PANYA ROAD?

unahitaji kutinduliwa kimawazo ukae sawa

Mahakama ndio yenye wajibu wa kutoa hukumu. Polisi hawana weledi, hivyo hawawezi kutuhumu na kutoa hukumu.
 
Kweli hata huyo aliyejiunganishia Bomba kaiba, ila tatizo hapa ni kubeba silaha na kujeruhi, kuua na kupora.
Wote wezi ila njia wametumia kuiba tofauti. Kwahiyo na adhabu zitumike njia tofauti.
Muuaji risasi, mwizi wa akili mahakamani.

Ok, huyo mwizi wa mafuta ukiacha yeye kuuwawa, ulisikia hata hao polisi kumfikisha mahakamani?
 
Nangu ,hoja uwe ni kweli ni Panya Road au sio Panya road bila kujali namna walivyo kamatwa kwa kufuatwa nyumbani,hoja yangu Mimi hayo mamlaka ya Polisi kuuwa watuhumiwa wameyapata wapi ?

Nondo, jamii yetu kwa zaidi ya 90% ni uncivilized, nani kakwambia sheria zinafanya kazi kwa watu uncivilized.

Tunahitaji kwanza kuwa civilized ndio tuanze kutumia sheria kwenye maisha ya kila siku, Europe na America zilipitia hii stage tuliyopo ya uprimitive na brutality ndio iliamua mpaka watu walioingia kwenye civilization.

Nimeishi Tandika, Tandale, Temeke, Vingunguti, Manzese, na maeneo mengi ya uswazi Dar es salaam nayajua vizuri kuanzia Kawe ukwamani, Msasani, keko nk.
Kifupi naijua Dar es salaam vizuri saana na binafsi naujua uhuni mwingi wa vijana wa uswazi na nina exposure ya kutosha unayoweza kuiita PHD ya kitaa.

Kupitia exposure yangu ya huko uswahilini ninachoweza kukwambia, tatizo kubwa la society yetu ni umasikini unaotengeneza uncivilized society, umasikini unaletwa na mambo mengi kuanzia utawala mbovu, uvivu wa watu nk.
tupambane wote kwa pamoja taifa litoke kwenye umasikini na jamii kuwa civilized ili haya mambo yaishe.
Polisi masikini na uncivilized unataka akadhibiti uhalifu unaofanywa na masikini uncivilized unategemea nini?
 
Blacks Mirror ,lazima sheria ifuatwe sababu karibu Makosa yote ya jinai ya adhabu yake kupitia (Penal code) ,hivyo ni wajibu wa Mahakama sio Polisi kuuwa.
Panyarodi ni kikundi kidogo Cha waasi wa sheria za Nchi,

Kwahiyo kupambana nao ni kuwaua tu
 
Nchi yetu Ina katiba ,sheria za mienendo ya Makosa ya jinai ,PGO,Kanuni za Jumla za Adhabu sheria zote hizi zimeweka utaratibu wa kushughulikia makosa ya uhalifu .

Hakuna sehemu Polisi amepewa mamlaka ya kuuwa mtu kama njia ya kupambana na uhalifu , Polisi wamepewa wajibu wa kuchunguza na kupeleleza sio kuhukumu kwa kupiga mtu Risasi ni Mahakama tuu ndiyo yenye jukumu la kutoa adhabu iwe ni adhabu ya kifo ,kifungo Cha maisha au miaka yeyote hayo hufanywa na Mahakama. Mimi unanishambulia Nina taka Sheria tulizojiwekea tuzifuate na kuziheshimu ,kama hatuzitaki zimepitwa na wakati ktk kupambana na uhalifu tuzibadili, kwanini tuzivunje ???


Ndio maana tuna sheria,katiba , kanuni na taratibu zimeweka utaratibu wa namna ya kupambana na uhalifu .

Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi , ndio maana kuna Mahakama ,ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa.

Hata hao Panya Road wanaofanya uhalifu sheria zipo wakikutwa na hatia wanaadhibiwa sawa na sheria inavyosema kuna kifungo adhabu ya kifo , kifungu cha maisha ,miaka 30 na adhabu zingine . Kwanini wasishtakiwe kwa mujibu wa sheria wajibu wa Polisi ni kufanya upelelezi na uchunguzi kuisaidia Mahakama kufanya maamuzi sio kuuwa watuhumiwa.

Kama tunaona hakuna haja ya kuchunguza na kushtaki Polisi washinikize sheria zibadilishwe ili iwe rahisi wao kufanya wanachokifanya , hakuna mtu anatetea wahalifu ,ninachotaka utaratibu ufuatwe ktk kupambana na uhalifu na kama sheria zetu ni Butu basi tuzibadili na sio Polisi kuchukua hatua ya kuuwa Watuhumiwa bila kuwapeleka mahakamani.

Serikali imetangaza vita dhidi ya panya road kama kwa mfano serikali za Kenya na Somalia zilivyotangaza vita dhidi ya Al Shabaab au serikali ya Nigeria ilivyotangaza vita dhidi ya Boko Haram. Panya road wamewekwa kwenye kundi la maadui wa kivita (enemy combatant). Sheria zinazowalinda raia wa kawaida haziwalindi maadui wa kivita. Hapa ni Geneva convention ndiyo inasimamia.

Ni muhimu sana kufanya upelelezi na kujua walioko nyuma ya panya road. Na wakijulikana lazima wachukuliwe hatua maana wanahatarisha amani ya nchi kwa sababu za kisiasa. Nani anawafadhili, nani anawapa madawa ya kulevya ili kuwatayarisha kisaikolojia kufanya maovu. Ni muhimu kujua.
 
Kaka Adakiss , Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi , ndio maana kuna Mahakama ,ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa.

Hata hao Panya Road wanaofanya uhalifu sheria zipo wakikutwa na hatia wanaadhibiwa sawa na sheria inavyosema kuna kifungo adhabu ya kifo , kifungu cha maisha ,miaka 30 na adhabu zingine . Kwanini wasishtakiwe kwa mujibu wa sheria wajibu wa Polisi ni kufanya upelelezi na uchunguzi kuisaidia Mahakama kufanya maamuzi sio kuuwa watuhumiwa.

Kama tunaona hakuna haja ya kuchunguza na kushtaki Polisi washinikize sheria zibadilishwe ili iwe rahisi wao kufanya wanachokifanya , hakuna mtu anatetea wanalifu ,ninachotaka utaratibu ufuatwe ktk kupambana na uhalifu na kama sheria zetu ni Butu basi tuzibadili na sio Polisi kuchukua hatua ya kuuwa Watuhumiwa bila kuwapeleka mahakamani.
Inaelekea wewe hujui lolote kuhusu hawa vijana. mimi nimekuambia au kukushauri tembele familia zilizopatwa na majanga ya panya road au nenda polisi kaulizie rekodi za hawa vijana. nakuhakikishia kuwa utarudi kufuta hiki chote ukichokiandika hapa.
kifupi kufikia hatua hii polisi wamechoka kuzungushana na watu waewale na mbaya zaidi vijana wanarecruit vijana wengine. mtu anaiba mtaani anakamatwa, familia inamtoa kwa dhamana kwa maana ya kumbadili mienendo mtoto wao, polisi huwa wanakuachia kwa.dhamana sio kwa hela tu hata maneno. mama kaa na mwanao aache wizi. akitoka anakaa wiki anaendelea tena. unataka polisi waendelee kucheza hii michezo mpaka lini? huko mahakamani ni miezi 6 hadi miaka miewili anarudi tena mtaani na akirudi anakuwa kama amewekewa ndimu.
 
Back
Top Bottom