Tatizo letu Bongo ni feedback, unaenda kufanya interview unakosa kazi na jamaa hawakupi mrejesho wowote, hata simu hawapokei.
Ndiyo kama hili swala.
Kilichotakiwa, waandaaji wangeandika thread kuelezea nini kilichotokea, hata kama haikufanyika, kwa sababu nina uhakika hatukosi cha kujifunza.
Tuambieni changamoto ilikuwa ni nini, na wapi tungeweza kujirekebisha, bila hata kutupiana lawama.
Vinginevyo mnaendelea kuwapa sababu za kuongea watu kama hawa, wanawachafua mnaonekana matapeli kwa sababu tu hamtaki kutoa feedback. Let's face it, truth be told.