Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

TATIZO wabongo wengi ni waoga(nikiwemo na Mimi) ndiyo maana tunakimbilia Kwenye matoyota Kwasabb kuna spare parts za bei rahisi(fake) na spare used pale mitaa ya shaurimoyo Kariakoo
Na tunaoishi mawilayani ikizingua hadi nije shaurimoyo?? sisi wa kipato cha chini mjapani yupo kila mahali yaani hata ikizingua saa4 usiku fundi anakutoa road
 
Waache wawe shamba darasa
Hhahahahaaaaaaaa kwakweli ngoja uone gari inauzwa 12M kisa Sensor tu imezingua mpaka uagize German.

Kuna BMW namba DK ilikuwa inauzwa bei ya kutupa kuuliza nkaambiwa ni mambo ya umeme na sensor. jamaa kapambana hadi akaamua alisukume. nlitakani nlinunue nihamishie injini ya 3S nitambe mjini. 🙂 🙂 🙂
 
Hhahahahaaaaaaaa kwakweli ngoja uone gari inauzwa 12M kisa Sensor tu imezingua mpaka uagize German.

Kuna BMW namba DK ilikuwa inauzwa bei ya kutupa kuuliza nkaambiwa ni mambo ya umeme na sensor. jamaa kapambana hadi akaamua alisukume. nlitakani nlinunue nihamishie injini ya 3S nitambe mjini. 🙂 🙂 🙂
Kama bei reasonable unaitupia tu 3S unainjoy kasha la BMW bila kero za ma sensor.
 
Mkuu hongera sana kwa kumiliki chuma cha ukweli,,,pitia na hapa ukutane na ndugu yako boss.

 
[emoji23][emoji23][emoji23] Acha mikwara [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mmiliki wa zamani wa vw Touran hapa,kaa nayo hata mwaka hivi ndio uje kupost tena hapa chief. Mimi ilinipa msiba mkubwa sana japo gari ilikua kali sana ,sunroof,8 airbags nk Ila dashboard ilikua inawaka taa kama mti wa Christmas.
 
Hhahahahaaaaaaaa kwakweli ngoja uone gari inauzwa 12M kisa Sensor tu imezingua mpaka uagize German.

Kuna BMW namba DK ilikuwa inauzwa bei ya kutupa kuuliza nkaambiwa ni mambo ya umeme na sensor. jamaa kapambana hadi akaamua alisukume. nlitakani nlinunue nihamishie injini ya 3S nitambe mjini. 🙂 🙂 🙂
Sasa gari kuzingua sensor haimaanishi zote zitazingua sensor...gari ni utunzaji bro..hizo toyota ngapi zimepaki garage na zinaoza!?

Kuna watu wapo rafu sana na gari!!lzma zitakusumbua tu
 
Na tunaoishi mawilayani ikizingua hadi nije shaurimoyo?? sisi wa kipato cha chini mjapani yupo kila mahali yaani hata ikizingua saa4 usiku fundi anakutoa road
Yes nashukuru umejua kuwa ni feki...nilitest kujua plugs OG za toyota premio nikaambiwa ni 45k..so ukitaka kujua toyota nayo ina gharama,tafuta spare zake OG uone!!
 
Wasalaam

Kwanza nianze kwa kusema kwamba maoni yangu sio sheria..haya ni maoni tu na mambo niliyoyaona baada ya kufanikiwa kumiliki gari ya mzungu

Mwanzoni nilikuwa na Toyota premio lkn niliichoka mapema baada ya kupata nayo ajali..bahati nzuri nikafanikiwa kuiuza kwa bei nzuri tu..nikawa najivuta kujichanga changa ili nivute ndinga nyingine kutoka ulaya

Nilipoingia humu kupata maoni khs hiyo gari(Volkswagen golf touran) kwa kweli negative comment zilikuwa nyng sana..nikapiga moyo konde nikaagiza hvyo hvyo..potelea pote,hela inatafutwa tu!!

Mwezi ulioisha nikafanikiwa kuikamata hii ndinga...nna kama mwezi mmoja hivi tangia niikamate na nishasafiri nayo mkoani nnapowajibika kikazi

Haya ni mambo machache sana nnayoweza kusema kuhusu gari ya mzungu:

Mosi,Kwa upande wa CONFORTABILITY,aisee toyota wameachwa mbali sana..Boss wangu ana Kluger,lkn majuzi alitaka aitest tu hii gari(maana kazini nnayo mwenyewe),aliivulia kofia

Pili,Kwa upande wa MAINTANANCE,kusema kweli vipuri vyake ni gharama kdg,ila ni GENUINE...ilinibidi nibadilishe plugs pamoja na break pads..plug moja nilinunua kwa tsh 35K..kwa upande wa break pads za mbele nilinunua kwa 160k na nyuma 95k

Tatu,kwa upande wa UPATIKANAJI WA SPARE,ilinibidi nitumie siku 1 nzima kuzunguka k/koo mpk posta kutafuta sehemu wanapouza spare za haya magari..nilifanikiwa kupata machimbo mengi,zaidi ya 5,lkn kuna chimbo moja lipo mtaa wa kisutu kuna muhindi mmoja ana kila aina ya spare ya magari ya MZUNGU..na kama hatakuwa nayo,ndani ya siku 5 anaagiza na unaipata...so kwa wale ambao ni waoga wa namna ya upatikanaji wa spare watoe shaka kbsa

Nne,kwa upande wa jinsi gari lilivyo..kwa kweli nimevutiwa na kila kitu...na kitu kizuri zaidi huitaji kuhangaika na chochote kwenye gari...muda wa service ukifika,taa ikiungua au jambo lolote ambalo sio normal kwenye gari basi DASHBOARD yako itakuonyesha,huna haja ya kuhangaika

Tano,Kwa wazee wa SPEED...hapa ndo mahali pake..niliyoichukua mm ina engine ya TSI,Speed 260..wakati nakuja nayo mkoani niliwatesa sana watu wenye ma prado yao/harrier waliokuwa wanataka ligi barabarani ...kuna jamaa mmoja alikuwa na crown aisee yule jamaa ni dereva,nilitoana nae jasho haswa ila mwishoni aliukubali mziki wangu ikabidi aniombe nisimame ili tu aijue hii gari..

Sita,Kwa upande wa kutulia barabarani(BALANCE)..aisee wazungu wazungu tu...kwenye mkeka wa njombe pale nilifanikiwa kufika spidi 250,lkn gari ndo kwanza inakamata chini..haiyumbi wala nn,imetulia balaa!!

Saba,Kwa uchunguzi wa haraka haraka nilioufanya(sina uhakika sana),brand rahisi ya magari ya ulaya kuimiliki moja wapo ni Volkswagen,hata maintenance yake ni ya kawaida tho ipo juu kidogo kulinganisha na Toyota..ila ipo chini sana kulinganisha na BMW au BENZI

Nane,Hii si gari ya kumpa kila mtu aiendeshe..madereva tunatofautiana..kama nilivyosema,hitilafu yeyote lzm DASHBOARD itakuonyesha...sasa ukiwa mtu wa kuazimisha sana,hii gari lazma uichukie!!

Tisa,Kwa upande wa SAFETY,hapa mzungu ndipo anàpompiga konzi la sikio mjapani..kwa hesabu za haraka hii gari ina AIRBEGS zaidi ya 4 ili tu kukuhakikishia usalama wako na familia pindi majanga yanapotokea

MWISHO...Unaenda mwezi wa 2 huu sasa sijapata tatizo lolote la kiufundi kwenye gari wala gari kusumbua au kuzimika au kugoma kuwaka...lipo freshi tu na linapiga kazi vizuri tu na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana kwa kweli..Tutoe uoga,kama unawish kumiliki gari ya mzungu miliki tu,acha kutishwa na maneno maneno ya watu

NB: Huku niliko hakuna hata duka moja linalouza spare za VW..ni mwendo wa Toyota,Subaru na Suzuki tu!!hata Mazda na Honda pia mtihani[emoji3][emoji3]

Adios!!
Tunayapenda magari ya wazungu ila mifuko yetu ndio shida wacha tuvimbe kwa mjapan tu
 
Back
Top Bottom