Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

Mbona wengi tu wanaagiza magari UK moja kwa moja? Na sijui kama kuna tofauti kubwa ya quality, ila tu mengi yanaouzwa Asia huko yanakuwa ni Petrol. Wengi walizoea huko Japan kwa sababu ndio soko lilikuwa accessible kirahisi na convenient zaidi toka miaka hiyo.
Mfano tu Australia, SA kuna viwanda vya TOYOTA na LR, Ford
Wewe unayo uliyoagiza kutoka huko ulaya direct..? Maana anaelaumiwa kutengeza magari ambayo hayana quality hao hao wanaolaumu wananunua magari ya ulaya yaliyotengenezwa Japan huo ndo msingi wa hoja...
 
Hayo magari ni mabovu sana, uza kwa ataejipendekeza nalo nakushauri, afu toyota chache ndo ziko stable, crown iko stable kwa gari za chini nizoziendesha
 
Mkuu kwanini uwe muoga wakati gari za kijerumani zinauzwa bei chee kuliko hata Toyota of the same years.

Nunua bana next time agiza used bmw kabisa ambayo ni kali sana kuliko Toyota interms of comfort na mbwembwe nyengine. Bado tunahitaji kujifunza kupitia mifano hai.

Naamini utakuwa balozi mzuri sana chief[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Atashika kichwa aisee
 
Hii inategemea, kama gari ni jipya au limetumika (umri). Mimi nina Mitsubishi Outlander (2016), tangu niinunue miaka mitano iliyopita sijaenda kwa fundi (haijahitaji matengenezo) isipokuwa regular service kila baada ya miezi sita. Of course mimi ni mzee, kwa mwaka ninaenda si zaidi ya kilomita elfu kumi. Ninyi vijana mna safari nyingi. Gari ni matunzo. Kama unaiendesha kama vile uko kwenye mashindano, wear and tear yake ipo juu na uwezekano wa kuharibika ni mkubwa kuliko yule anaye libembeleza gari lake kama mtoto
Ssaa hyo Mitsubishi si tayari ni mjapani, ukishasema mjapani tayari inadumu
 
Wasalaam

Kwanza nianze kwa kusema kwamba maoni yangu sio sheria..haya ni maoni tu na mambo niliyoyaona baada ya kufanikiwa kumiliki gari ya mzungu

Mwanzoni nilikuwa na Toyota premio lkn niliichoka mapema baada ya kupata nayo ajali..bahati nzuri nikafanikiwa kuiuza kwa bei nzuri tu..nikawa najivuta kujichanga changa ili nivute ndinga nyingine kutoka ulaya

Nilipoingia humu kupata maoni khs hiyo gari(Volkswagen golf touran) kwa kweli negative comment zilikuwa nyng sana..nikapiga moyo konde nikaagiza hvyo hvyo..potelea pote,hela inatafutwa tu!!

Mwezi ulioisha nikafanikiwa kuikamata hii ndinga...nna kama mwezi mmoja hivi tangia niikamate na nishasafiri nayo mkoani nnapowajibika kikazi


Haya ni mambo machache sana nnayoweza kusema kuhusu gari ya mzungu:

Mosi, kwa upande wa CONFORTABILITY,aisee toyota wameachwa mbali sana..Boss wangu ana Kluger,lkn majuzi alitaka aitest tu hii gari(maana kazini nnayo mwenyewe),aliivulia kofia

Pili,Kwa upande wa MAINTANANCE,kusema kweli vipuri vyake ni gharama kdg,ila ni GENUINE...ilinibidi nibadilishe plugs pamoja na break pads..plug moja nilinunua kwa tsh 35K..kwa upande wa break pads za mbele nilinunua kwa 160k na nyuma 95k

Tatu,kwa upande wa UPATIKANAJI WA SPARE,ilinibidi nitumie siku 1 nzima kuzunguka k/koo mpk posta kutafuta sehemu wanapouza spare za haya magari..nilifanikiwa kupata machimbo mengi,zaidi ya 5,lkn kuna chimbo moja lipo mtaa wa kisutu kuna muhindi mmoja ana kila aina ya spare ya magari ya MZUNGU..na kama hatakuwa nayo,ndani ya siku 5 anaagiza na unaipata...so kwa wale ambao ni waoga wa namna ya upatikanaji wa spare watoe shaka kbsa

Nne,kwa upande wa jinsi gari lilivyo..kwa kweli nimevutiwa na kila kitu...na kitu kizuri zaidi huitaji kuhangaika na chochote kwenye gari...muda wa service ukifika,taa ikiungua au jambo lolote ambalo sio normal kwenye gari basi DASHBOARD yako itakuonyesha,huna haja ya kuhangaika

Tano,Kwa wazee wa SPEED...hapa ndo mahali pake..niliyoichukua mm ina engine ya TSI,Speed 260..wakati nakuja nayo mkoani niliwatesa sana watu wenye ma prado yao/harrier waliokuwa wanataka ligi barabarani ...kuna jamaa mmoja alikuwa na crown aisee yule jamaa ni dereva,nilitoana nae jasho haswa ila mwishoni aliukubali mziki wangu ikabidi aniombe nisimame ili tu aijue hii gari..

Sita,Kwa upande wa kutulia barabarani(BALANCE)..aisee wazungu wazungu tu...kwenye mkeka wa njombe pale nilifanikiwa kufika spidi 250,lkn gari ndo kwanza inakamata chini..haiyumbi wala nn,imetulia balaa!!

Saba,Kwa uchunguzi wa haraka haraka nilioufanya(sina uhakika sana),brand rahisi ya magari ya ulaya kuimiliki moja wapo ni Volkswagen,hata maintenance yake ni ya kawaida tho ipo juu kidogo kulinganisha na Toyota..ila ipo chini sana kulinganisha na BMW au BENZI

Nane,Hii si gari ya kumpa kila mtu aiendeshe..madereva tunatofautiana..kama nilivyosema,hitilafu yeyote lzm DASHBOARD itakuonyesha...sasa ukiwa mtu wa kuazimisha sana,hii gari lazma uichukie!!

Tisa,Kwa upande wa SAFETY,hapa mzungu ndipo anàpompiga konzi la sikio mjapani..kwa hesabu za haraka hii gari ina AIRBEGS zaidi ya 4 ili tu kukuhakikishia usalama wako na familia pindi majanga yanapotokea

MWISHO...Unaenda mwezi wa 2 huu sasa sijapata tatizo lolote la kiufundi kwenye gari wala gari kusumbua au kuzimika au kugoma kuwaka...lipo freshi tu na linapiga kazi vizuri tu na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana kwa kweli..Tutoe uoga,kama unawish kumiliki gari ya mzungu miliki tu,acha kutishwa na maneno maneno ya watu

NB: Huku niliko hakuna hata duka moja linalouza spare za VW..ni mwendo wa Toyota,Subaru na Suzuki tu!!hata Mazda na Honda pia mtihani😀😀

Adios!!

======
Mzee vp gari yetu tupe mrejesho tupate hamasa ya kununua gari za mzungu

Share namba za fundi na duka la spairs.
 
VW si gari ya kukimbilia.inachachuka anytime. Na haliuziki kirahisi. Hapo lilizingua safarini xmass
gari yako chafu sana, unaitumia machombo ya mchanga au .. yani gari injini ina masizi kama unauza mkaa
 
Narudi tena...gari sasa ina mwaka na miezi 3..nimepiga nayo trip from nilipo to Arusha to DSM to huku nilipo...mwaka naaa...CV JOINT ndo zimeisha...sijabadili kitu kingine chochote

Ipo sokoni now...huku nnapokaa kipindi cha mvua barabara inaharibika na gari ipo chini..kupita ni changamoto ..nilishauriwa nisiinyanyue..nilipiga jiwe majuz kati nikatoboa sample...nashukuru ilichomelewa

View attachment 2118649View attachment 2118650View attachment 2118651View attachment 2118652View attachment 2118653

Mkuu, hii chuma ulifanikiwa kuuza?

-Kaveli-
 
magari yenye brand ya dunia,
magari yenye hadhi ya nyota 5+..
magari ya ndoto...
ni magari ya kizungu.
 
Back
Top Bottom