ipyax
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 4,247
- 6,578
Pole sanaVW si gari ya kukimbilia.inachachuka anytime. Na haliuziki kirahisi. Hapo lilizingua safarini xmass
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole sanaVW si gari ya kukimbilia.inachachuka anytime. Na haliuziki kirahisi. Hapo lilizingua safarini xmass
Narudi tena...gari sasa ina mwaka na miezi 3..nimepiga nayo trip from nilipo to Arusha to DSM to huku nilipo...mwaka naaa...CV JOINT ndo zimeisha...sijabadili kitu kingine chochoteMmiliki wa zamani wa vw Touran hapa,kaa nayo hata mwaka hivi ndio uje kupost tena hapa chief. Mimi ilinipa msiba mkubwa sana japo gari ilikua kali sana ,sunroof,8 airbags nk Ila dashboard ilikua inawaka taa kama mti wa Christmas.
Ndio Wabongo hao, wanasubiri bad news waburudike!Mwaka mzima upo unasubiri experience?
Nahamia Audi A8 before AprilWasalaam
Kwanza nianze kwa kusema kwamba maoni yangu sio sheria..haya ni maoni tu na mambo niliyoyaona baada ya kufanikiwa kumiliki gari ya mzungu
Mwanzoni nilikuwa na Toyota premio lkn niliichoka mapema baada ya kupata nayo ajali..bahati nzuri nikafanikiwa kuiuza kwa bei nzuri tu..nikawa najivuta kujichanga changa ili nivute ndinga nyingine kutoka ulaya
Nilipoingia humu kupata maoni khs hiyo gari(Volkswagen golf touran) kwa kweli negative comment zilikuwa nyng sana..nikapiga moyo konde nikaagiza hvyo hvyo..potelea pote,hela inatafutwa tu!!
Mwezi ulioisha nikafanikiwa kuikamata hii ndinga...nna kama mwezi mmoja hivi tangia niikamate na nishasafiri nayo mkoani nnapowajibika kikazi
Haya ni mambo machache sana nnayoweza kusema kuhusu gari ya mzungu:
Mosi,Kwa upande wa CONFORTABILITY,aisee toyota wameachwa mbali sana..Boss wangu ana Kluger,lkn majuzi alitaka aitest tu hii gari(maana kazini nnayo mwenyewe),aliivulia kofia
Pili,Kwa upande wa MAINTANANCE,kusema kweli vipuri vyake ni gharama kdg,ila ni GENUINE...ilinibidi nibadilishe plugs pamoja na break pads..plug moja nilinunua kwa tsh 35K..kwa upande wa break pads za mbele nilinunua kwa 160k na nyuma 95k
Tatu,kwa upande wa UPATIKANAJI WA SPARE,ilinibidi nitumie siku 1 nzima kuzunguka k/koo mpk posta kutafuta sehemu wanapouza spare za haya magari..nilifanikiwa kupata machimbo mengi,zaidi ya 5,lkn kuna chimbo moja lipo mtaa wa kisutu kuna muhindi mmoja ana kila aina ya spare ya magari ya MZUNGU..na kama hatakuwa nayo,ndani ya siku 5 anaagiza na unaipata...so kwa wale ambao ni waoga wa namna ya upatikanaji wa spare watoe shaka kbsa
Nne,kwa upande wa jinsi gari lilivyo..kwa kweli nimevutiwa na kila kitu...na kitu kizuri zaidi huitaji kuhangaika na chochote kwenye gari...muda wa service ukifika,taa ikiungua au jambo lolote ambalo sio normal kwenye gari basi DASHBOARD yako itakuonyesha,huna haja ya kuhangaika
Tano,Kwa wazee wa SPEED...hapa ndo mahali pake..niliyoichukua mm ina engine ya TSI,Speed 260..wakati nakuja nayo mkoani niliwatesa sana watu wenye ma prado yao/harrier waliokuwa wanataka ligi barabarani ...kuna jamaa mmoja alikuwa na crown aisee yule jamaa ni dereva,nilitoana nae jasho haswa ila mwishoni aliukubali mziki wangu ikabidi aniombe nisimame ili tu aijue hii gari..
Sita,Kwa upande wa kutulia barabarani(BALANCE)..aisee wazungu wazungu tu...kwenye mkeka wa njombe pale nilifanikiwa kufika spidi 250,lkn gari ndo kwanza inakamata chini..haiyumbi wala nn,imetulia balaa!!
Saba,Kwa uchunguzi wa haraka haraka nilioufanya(sina uhakika sana),brand rahisi ya magari ya ulaya kuimiliki moja wapo ni Volkswagen,hata maintenance yake ni ya kawaida tho ipo juu kidogo kulinganisha na Toyota..ila ipo chini sana kulinganisha na BMW au BENZI
Nane,Hii si gari ya kumpa kila mtu aiendeshe..madereva tunatofautiana..kama nilivyosema,hitilafu yeyote lzm DASHBOARD itakuonyesha...sasa ukiwa mtu wa kuazimisha sana,hii gari lazma uichukie!!
Tisa,Kwa upande wa SAFETY,hapa mzungu ndipo anàpompiga konzi la sikio mjapani..kwa hesabu za haraka hii gari ina AIRBEGS zaidi ya 4 ili tu kukuhakikishia usalama wako na familia pindi majanga yanapotokea
MWISHO...Unaenda mwezi wa 2 huu sasa sijapata tatizo lolote la kiufundi kwenye gari wala gari kusumbua au kuzimika au kugoma kuwaka...lipo freshi tu na linapiga kazi vizuri tu na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana kwa kweli..Tutoe uoga,kama unawish kumiliki gari ya mzungu miliki tu,acha kutishwa na maneno maneno ya watu
NB: Huku niliko hakuna hata duka moja linalouza spare za VW..ni mwendo wa Toyota,Subaru na Suzuki tu!!hata Mazda na Honda pia mtihani[emoji3][emoji3]
Adios!!
Nyamaume unaami upako kuliko mizimu yetu dah ..tumeusaliti utu wetuNgoja niende kwa Mwamposa nikanywe futa la upako na maji ya upako Kisha nishushie keki maridhawa, na Mimi ntakuja next week kushuhudia hapa
Hivi humu nani amenunua gari ya mzungu iliotoka ulaya? Maana 95% ya hayo magari ya kizungu yametengenezwa Japan na yamenunuliwa toka Japan...Ongea yote mkuu ila gari za mzungu huwezi fananisha na gari za mjapani. Japan katengeneza gari chache zenye hadhi ya kuitwa gari hayo mengine ni usafiri tu mkuu wanayaita makopo yanayotembea [emoji23][emoji23] bahatika kuendesha gari ya mzungu uione tofauti utaleta mrejesho hapa
Hivi humu nani amenunua gari ya mzungu iliotoka ulaya? Maana 95% ya hayo magari ya kizungu yametengenezwa Japan na yamenunuliwa toka Japan...
Kwaio mkuu unauza sh ngapi hii chuma? Na pia una mpango wa kurudi Japan...au unabaki huko huko kwa "The Bavarians" 😀😀😀Narudi tena...gari sasa ina mwaka na miezi 3..nimepiga nayo trip from nilipo to Arusha to DSM to huku nilipo...mwaka naaa...CV JOINT ndo zimeisha...sijabadili kitu kingine chochote
Ipo sokoni now...huku nnapokaa kipindi cha mvua barabara inaharibika na gari ipo chini..kupita ni changamoto ..nilishauriwa nisiinyanyue..nilipiga jiwe majuz kati nikatoboa sample...nashukuru ilichomelewa
View attachment 2118649View attachment 2118650View attachment 2118651View attachment 2118652View attachment 2118653
Hivi humu nani amenunua gari ya mzungu iliotoka ulaya? Maana 95% ya hayo magari ya kizungu yametengenezwa Japan na yamenunuliwa toka Japan...
Ngoja aje kutuambia hapa...sio wanajidai mjerumani mjerumani...wakati gari zinatoka Japan...😀😀😀 inakuaje Mjerumani anamuamini Mjapan amtengenezee gari ...1😂😂😂Swali zuri sana.
-Kaveli-
Kwaio mkuu unauza sh ngapi hii chuma? Na pia una mpango wa kurudi Japan...au unabaki huko huko kwa "The Bavarians" 😀😀😀
Naaam tena swali langu ni kwanini wananunua hayo magari ya kijerumani lakini yaliyotengenezwa Japan? Kwanini wasinunue huko huko ulaya i.e Uingereza maana ujerumani wao ni Left Hand Drive..kwaio alietoa gari ya kizungu direct ulaya ndo tunamtaka aje hapa...Kwamba wananunua mtumba wa Ulaya uliotumika Japan? Why wasinunue mitumba ya Ulaya directly kule kule Ulaya?
-Kaveli-
Unaweza kuta gari haijauzwa hadi leo...au kama imeuzwa ime depreciate mbaya...😂😂😂Mpaka hapo huyo mwamba anajuta kuzifahamu chuma za Ulaya.
-Kaveli-
Unaweza kuta gari haijauzwa hadi leo...au kama imeuzwa ime depreciate mbaya...😂😂😂
Naaam tena swali langu ni kwanini wananunua hayo magari ya kijerumani lakini yaliyotengenezwa Japan? Kwanini wasinunue huko huko ulaya i.e Uingereza maana ujerumani wao ni Left Hand Drive..kwaio alietoa gari ya kizungu direct ulaya ndo tunamtaka aje hapa...