Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

Simbamteme kaususa uzi wake.

Hizi chuma za mdutch zina sarakasi zingi sana. Hizi ndinga mie naziitaga 'chuma ulete'.

-Kaveli-
Heheheh hapo kupigwa 1.5M ni uhakika tena kwa nchi zetu za kijima hizi. Ndio maana nawashaurigi watu wanunue Toyota tu uzoee gari ukijiingiza huko kwa Mdutch uwe ushajipanga kisaikolojia maana vipigo vikianza unaweza ukaikumbuka Toyota yako kwa ukali sana 😅😅😅
 
Wasalaam

Kwanza nianze kwa kusema kwamba maoni yangu sio sheria..haya ni maoni tu na mambo niliyoyaona baada ya kufanikiwa kumiliki gari ya mzungu

Mwanzoni nilikuwa na Toyota premio lkn niliichoka mapema baada ya kupata nayo ajali..bahati nzuri nikafanikiwa kuiuza kwa bei nzuri tu..nikawa najivuta kujichanga changa ili nivute ndinga nyingine kutoka ulaya

Nilipoingia humu kupata maoni khs hiyo gari(Volkswagen golf touran) kwa kweli negative comment zilikuwa nyng sana..nikapiga moyo konde nikaagiza hvyo hvyo..potelea pote,hela inatafutwa tu!!

Mwezi ulioisha nikafanikiwa kuikamata hii ndinga...nna kama mwezi mmoja hivi tangia niikamate na nishasafiri nayo mkoani nnapowajibika kikazi

Haya ni mambo machache sana nnayoweza kusema kuhusu gari ya mzungu:

Mosi,Kwa upande wa CONFORTABILITY,aisee toyota wameachwa mbali sana..Boss wangu ana Kluger,lkn majuzi alitaka aitest tu hii gari(maana kazini nnayo mwenyewe),aliivulia kofia

Pili,Kwa upande wa MAINTANANCE,kusema kweli vipuri vyake ni gharama kdg,ila ni GENUINE...ilinibidi nibadilishe plugs pamoja na break pads..plug moja nilinunua kwa tsh 35K..kwa upande wa break pads za mbele nilinunua kwa 160k na nyuma 95k

Tatu,kwa upande wa UPATIKANAJI WA SPARE,ilinibidi nitumie siku 1 nzima kuzunguka k/koo mpk posta kutafuta sehemu wanapouza spare za haya magari..nilifanikiwa kupata machimbo mengi,zaidi ya 5,lkn kuna chimbo moja lipo mtaa wa kisutu kuna muhindi mmoja ana kila aina ya spare ya magari ya MZUNGU..na kama hatakuwa nayo,ndani ya siku 5 anaagiza na unaipata...so kwa wale ambao ni waoga wa namna ya upatikanaji wa spare watoe shaka kbsa

Nne,kwa upande wa jinsi gari lilivyo..kwa kweli nimevutiwa na kila kitu...na kitu kizuri zaidi huitaji kuhangaika na chochote kwenye gari...muda wa service ukifika,taa ikiungua au jambo lolote ambalo sio normal kwenye gari basi DASHBOARD yako itakuonyesha,huna haja ya kuhangaika

Tano,Kwa wazee wa SPEED...hapa ndo mahali pake..niliyoichukua mm ina engine ya TSI,Speed 260..wakati nakuja nayo mkoani niliwatesa sana watu wenye ma prado yao/harrier waliokuwa wanataka ligi barabarani ...kuna jamaa mmoja alikuwa na crown aisee yule jamaa ni dereva,nilitoana nae jasho haswa ila mwishoni aliukubali mziki wangu ikabidi aniombe nisimame ili tu aijue hii gari..

Sita,Kwa upande wa kutulia barabarani(BALANCE)..aisee wazungu wazungu tu...kwenye mkeka wa njombe pale nilifanikiwa kufika spidi 250,lkn gari ndo kwanza inakamata chini..haiyumbi wala nn,imetulia balaa!!

Saba,Kwa uchunguzi wa haraka haraka nilioufanya(sina uhakika sana),brand rahisi ya magari ya ulaya kuimiliki moja wapo ni Volkswagen,hata maintenance yake ni ya kawaida tho ipo juu kidogo kulinganisha na Toyota..ila ipo chini sana kulinganisha na BMW au BENZI

Nane,Hii si gari ya kumpa kila mtu aiendeshe..madereva tunatofautiana..kama nilivyosema,hitilafu yeyote lzm DASHBOARD itakuonyesha...sasa ukiwa mtu wa kuazimisha sana,hii gari lazma uichukie!!

Tisa,Kwa upande wa SAFETY,hapa mzungu ndipo anàpompiga konzi la sikio mjapani..kwa hesabu za haraka hii gari ina AIRBEGS zaidi ya 4 ili tu kukuhakikishia usalama wako na familia pindi majanga yanapotokea

MWISHO...Unaenda mwezi wa 2 huu sasa sijapata tatizo lolote la kiufundi kwenye gari wala gari kusumbua au kuzimika au kugoma kuwaka...lipo freshi tu na linapiga kazi vizuri tu na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana kwa kweli..Tutoe uoga,kama unawish kumiliki gari ya mzungu miliki tu,acha kutishwa na maneno maneno ya watu

NB: Huku niliko hakuna hata duka moja linalouza spare za VW..ni mwendo wa Toyota,Subaru na Suzuki tu!!hata Mazda na Honda pia mtihani[emoji3][emoji3]

Adios!!
Mzee tupe mrejesho wengine vibubu viko tayari tunatafuta kitakachotufaa
 
High performance engine zinahitaji high octane petrol, ukizingua hapo lazima uvunje kibubu pia

Volkswagen 1.4 TSI Engine Reliability

As with many of Volkswagen's engines, if you follow the maintenance schedules religiously and use the correct fuel/oil, the1.4's are very reliable engines.
1625984772627.png

Volkswagen Tuning - Volkswagen Performance & Tuning Guides - Volkswagen Tuning and Performance Guides, Tuning News, and Videos › vw-1-4-tsi-eng...

The 5 Most Common VW 1.4 TSI Engine Problems - VW ...


Some problems include the piston ring land cracking over time which can be expedited by using the incorrect fuel. The CAVD engine must use 98 octane unleaded fuel as lower octane fuel will cause the engine to ping and result inprematurely cracked pistons. Another issue is the timing chain tensioner.28 Jun 2021
1625984818657.png

Car Parts Melbourne | New and Used Reconditioned Parts | Grant Walker Parts › v...

Volkswagen CAVD 1.4 Litre TSI Engine Problems - Grant Walker ...


Ni wajibu wako mmiliki/ derva wa gari kujua aina ya kiwese gari lako linahitaji, mhusika kwenye pump hana muda wa kuchunguza na inawezekana pia hajui hili swala kama ulivyo wewe.
 
European / American machine zimekaa kibabe sana na kila mtu anapenda kuwa na hizo machine.

Kwa mazingira yetu Mjapan kajua kutengeneza gari za kuendana na sisi kuanzia barabara, vipuri, oil, fuel.

Pesa zetu tunazipata kwa taabu sana, hata ukivimba ukaleta European car tayari ina Km za kutosha. Lazima ikupe stress tu.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
300kph kwa engine ipi....


Toyota tunazonunua ni za JDM hivo ziko limited to 180kph .... ukitoa limiter inazidi hapo ...mfano 1jz gte yenye 280hp inafika 250kph bila kupepesa macho ni swala la limiter tu
Watu huwa wanamchukulia poa sana Toyota, kwa sababu kajaa hapa Dodoma, ila production anazofanya kwa ajili ya soko la Europe na America usipime. Kwa jinsi watu wanavyolalamika ni ngumu kumantain gari za Mjerumani hapa Bongo kama mfuko wa shati sio mzuri, hivyo hivyo ni ngumu ku maintain gari za Toyota zinazouzwa kwenye soko la Europe na America
1640336777812.png
1640337097746.png
1640336802192.png

1640336854546.png
1640337134607.png

1640336919712.png
 
Hakuna watu wanajiskia kama wenye European Cars za bei chee kama BMW 1 na 3 series, Mercedes Benz C Class na AUDI A3 na 4 tena za miaka ya 2006 na 2007 huko[emoji28][emoji28].

Sema bana hizi ndinga zina muonekano flani hivi wa kuficha umaskini.

IMG_0426.jpg
 
Hakuna watu wanajiskia kama wenye European Cars za bei chee kama BMW 1 na 3 series, Mercedes Benz C Class na AUDI A3 na 4 tena za miaka ya 2006 na 2007 huko[emoji28][emoji28].

Sema bana hizi ndinga zina muonekano flani hivi wa kuficha umaskini.

View attachment 2081806

Huyu mleta Uzi sijuwi kapotelea wapi.

Aje atupe eksipirience kuhusu chuma ya mzungu.

Kama tayari ishamtoa kamasi, pia atueleze tu.

CC: Extrovert .

-Kaveli-
 
Chuma ya mzungu ni balaa. Haitaki mkwanja wa kuunga unga!

Huu ukimya wa Simbamteme unatupa mashaka wananzengo. Possibly kabisa tayari chuma ya mzungu dashboard ishawaka kama mti wa Xmas.

-Kaveli-
Kuna dogo m1 yuko mwanza bima maumeme yameifanya ikae juu ya mawe..namba DN....ukiiona inangaa inavutia balaa...sasa uliza anaiskuma ngap...7m....

Ile gar ikiwaka tu anaiuza haraka mno...mwanza tena..sasa mnunuaj namuonea huruma sana..gar ya 17m inauzwa 7m
 
Back
Top Bottom