Niliyoyashuhudia Jeshini

🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Katika kazi ambazo zilishanishinda na sizitaki ni kazi zote Zenye nature ya Ulinzi.

Siko interested hata kidogo,zaidi ya kufundishwa matumizi ya silaha ila masuala mengine yote naweza pata mtaani.
 
Kweli kabisa. Wanazani utaanza mazoezi magumu bila kuandaa mwili.
Jeshi kwa hapo nawapa hongera ni kama wana mtaala kabisa na wanajua kabisa lazma mtu wakuandae kabla ya kukupa vitu vizito.

Ningetoka home na wakanianzishia six weeks moja kwa moja, lazma ningezima 😁😁

Ila phase ya uraia tu inakusaidia kuuweka mwili tayari kwa vitu vinavyokuja
 
Ukifungua moyo unatoboa sasa wewe jifanye umemkumbuka mama, wewe wakishua utajua hujui..
RSM wanaa sijapa kuona..
 
Ukifungua moyo unatoboa sasa wewe jifanye umemkumbuka mama, wewe wakishua utajua hujui..
RSM wanaa sijapa kuona..

mtoa mada ni wa kike ndio maana walimdekeza na kumpoza. Ingekuwa wa kiume unadhani kuna mtu anajali

Kwanza ukilia wanafurahia ili wakukolezee doso. Japo kuna wajeda wapo peace tu ingawa wengi ndo matatizo maana kuna huyo bakabaka toka niingie ile kambi, nilimuona katabasamu mara moja tu na ukikutana nae, unaona sura ya kukutamani kukuhenyesha tu😁😁😁
 
Kwa jinsi nilivyosoma uzi wake mpaka hapa unacomment huyu sio mwanaume ni mwanamke! Soma vizuri mkuu, hadi anasema Kuna mwanajeshi wa kike aliyemuonea huruma wanafanana majina.
JKT na JWTZ nk hawaangalii wanampokea kuwa Mwanamke au mwanaume mziki uko pale pale kupokelewa ni syllabus ya mafunzo ya Jeshi hupokelewi kienyeji uwe mwanajeshi wa kike au kiume wanazingatia syllabus sio matakwa ya mpokeaji au jinsia

Jeshi Wana syllabus kama ya primary au secondary au chuo kikuu kama zilikiukwa huyo aliyedharau hiyo syllabus aweza chukuliwa hatua za kisheria za kijeshii na Mahakama ya kijeshi yaani Court Martial ambayo Ina majaji mawakili waliosajiliwa mahakama ya kiraia na chama chama Cha mawakili Tanzania


ikiwemo kufukuzwa kazi akikukutwa na hatia ya kutozingatia military legal procedures za kuajiri
 
Umenikumbusha mbali bro..
Kukwepa ndege ni hatari, waweza haribu kiuno hivi hivi
Kuna boya mmoja alinipiga nua nika crawl kwenye matope akanipaka majivu mwili mzima alaf akanipigisha hilo tifu la kukwepa ndege akanizungusha kombania nzima masaa mawili

Jamaa alikua anatafuta kujengea jina kupitia mimi maana aliamua tu kunipiga tifu bila sababu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…